Mke wangu hajawahi kuniambia ananipenda

Unajua hiyo 'I LOVE YOU' ni kama hiki kitufe cha kugongea 'like' hapa JF. Ukigonga like kadhaa kwa siku kanatoweka. Sasa huyu jamaa kila siku wenzie wanamuwahi kwa kuchelewa kwake kurudi nyumbani. Hajui kuwa kuna watu huwa wanatembelea boma yake in his absence

Mkuu una uhakika?uusije ukasababisha ndoa kuvunjika
 
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne..

Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi..

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..

Duh! Pole sana sioni hata kinamchomsababisha akununie...Yaani kumwambia mumeo kwamba unampenda imeshakuwa shida kiasi hicho!!!?
 
Duh! Pole sana sioni hata kinamchomsababisha akununie...Yaani kumwambia mumeo kwamba unampenda imeshakuwa shida kiasi hicho!!!?

Huu ni ukweli wa mleta mada
Bado ukweli wa mkewe
Na ukweli halisi!

Hatutaweza kujua kamwe!
 
Pole sana amani anakupenda tena sana
Labda anaona neno gumu kulitamka mwambie awe anakwambia hata kwa Kingereza au kabila yoyote kama
Nene nakutogagwa
 
Jamaa yangu usijiumize bure kwa mambo ya kufikirika,
unajua kila mtu ana njia yake ya kuonyesha upendo anaweza akawa anakupeti dear,baby baby za kumwaga lakini akawa
hakupendi kwa dhati.Na pia anaweza kuwa mzito kusema nakupenda still akawa anakupenda.
Tumia akili kama anakuichukia utajua tu !!
 
Matendo yake wee ubayaonaje? Kwani matendo hukidhi haja kuliko maneno. Mtu anaweza akawa anakwambia kila Siku nakupenda bab kumbe hakupendi. Mwangalie matendo yake, utajua tu ka anakupenda.
 
siku hizi unaweza kupata mpnz na i love you za kuzidi,ila hakuna mapenzi bali kuna anachotafuta,huko unakotaka kwenda i lov u utazipata sana ila utajuta
 
shida hapo hua humfikishi kwenye mavituuuz,
amini usiamini kuna anaemwambia,kumtamkia na anamaanisha,endelea kumlazimisha siku atatamka nakupenda ..........(jina la huyo anaemfikisha)
 
Ebu nishaurini,nina mke ambaye tumeona kama miezi sita hivi imepita..katika hari ya uchumba wetu tulikuwa na mapenzi ya kawaida,si ya moto wala baridi katika kipindi cha miaka minne..

Tulikubaliana tuoane ..lakini katika kipindi chote cha ndoa sijawahi kusikia mke wangu akinitamkia kuwa ananipenda japo tunafanyia mambo mbalimbali kama wanandoa,kila nikimuuliza kwa nini huwa usijawahi ukisema kuwa unanipenda hata siku moja toka tuoane basi huwa ananuna mpaka basi..

Jana nimemwambia siku nikipata mtu anayeniambia ananipenda na kunijari kuliko wewe..utakuja kujuta na huku ukiwa umekwisha chelewa..basi kanununa usiku kucha mpaka naondoka nyumbani..

Nishaulini nichukue hatua gani kwa huyu bibie..
Ha ha ha ha ndoa kaaazi kweli kweli
 
Mi ni bora nionyeshwe mapenzi kwa vitendo kuliko maneno. Nishaambiwa sana hayo maneno 'i love u, i miss u, cant live without u, ur thr best thing anf most important person in my life' lakini leo hii hata hayupo na mie so wewe mradi mkeo anaonyesha mapenzi ya kweli anakuheshimu na kukujali hilo ndo la maana, wanakuambia maneno hayavunji mfupa.
 
Hataki kuwa mnafiki! Mpe pongezi kwa kutokukudanganya na mfanye akupende kama ndio unachotaka!
 
hapa naona unalazimisha kupendwa kwa maneno wewe.........kwa upande mwingine naona kama umemchoka mkeo ila unamtafutia sababu ya kumletea mwingine.......na kama ungekuwa unampenda pia sidhani ungejitangazia kwamba umemwacha amenuna mpaka unaondoka nyumbani.......unatarajia ukirudi umkute anatabasamu akwambie "anakupenda" kwa upande wangu nadhani huyo mkeo anakupenda kwa dhati labda kununa kwake ni jinsi gani wewe unashindwa kuona na kufahamu anavyokupenda kutoka moyoni na sio kutoka mdomoni........na ukiendelea ivi hakika nakwambia mtaparanganya......suluhisho mwite mkae mueleweshane...........
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom