Mke wangu habebeki...

embu kata huduma ya kutuma hela, sema umepigwa panga la punguzo la kazi. Kwa hiyo huna hela ya kuishi na kama vipi akutumie paund chache kwa mwezi, hapo utajua Muabudu hela na muabudu penzi.
 
Jaman me nataman kumpata mke mwenye IQ ndogo kama huyo,naamini atarekebishika tu make me mwenyewe nishachanganyikiwa kitambo!
 
Kweni mnajenga? Kwa matumiza ya chakula cha nyumbani tu bila ada yeye na mwanae ni more than enough! Hiyo hela atakuwa anamhonga mtu, haki ya nani vile!
 
yuko kimaslahi achana nae. Hata angekuwa anakaa london na mwanaye 1000us inatosha. Labda anajenga kwao timua huyo mnyonyaji
 
Niko nasoma nje ya Tanzania huku nifanya kazi katika company fulani nikilipwa mshahara dollar 1,800 kwa mwezi,najigharamia mwenyewe masomo yangu kwa 50% nyingine ni sholarship na gharama nyingine za maisha.
Nimeacha mke na mtoto mmoja nyumbani.mke wangu najitahidi kumtumia dollar 1,000 kila mwezi.yeye anafanya kazi katika shirika fulani Tanzania na anapokea mshahara kiasi fulani mara zote analalamika pesa ninayomtumia haitoshi imagine juzi nimetuma kwa exchange rate ya Tanzania alipokea kama Tsh,1,800,000 bado ananipigia cim na kunigombeza pesa haitoshi kwenye matumizi yake ya maisha na mtoto sasa jamani huyu ni mke au mzigo?nimemweleza hari halisi ya maisha ya huku haelewi naishi kwa kujibana ili kile kinachopatikana tukiserve lakini wapi.nahisi kama nilikosea kwenye uchaguzi au anafanyia nini hiyo pesa ya kila mwezi au anaamua kunifanyia ushenzi tu.nimemwambia kuna watu wanalia mchana na usiku wanakosa bahati kama hiyo lakini haelewi.ila ninafikiria kumchukua mtoto wangu akalelewe na mama yangu mzazi au nimchukue nihishi naye ..nahisi huyu mwanamke nimzigo tena haubebeki..nasiyo kwamba kuna assets za ndani ananunua nyumba hiko full hadi usafiri nilimpatia wa kutumia.

Jamani mke wa namna hii nimfanyeje?

Kakangu kama hiyo story ni kweli, i feel unavyopata uchungu, huyo mwanamke ni mpumbavu kuliko wanawake wote.

Nakuomba kaa ujifikirie mara mbili, huyo mwanamke siyo kabisa. Najua maisha ya ughaibuni yalivyo, yeye ni limbukeni na anawashauri wabaya nahisi, watu wengi ambao hawajafika ama kuishi ulaya na marekani huwa wanadhani huko kunahela za bure za kuokota tu, kumbe hela ni ngumu kuliko bongo.

Kama yeye anafanya kazi hata ungemtumia dala 500 bado ni nyingi sana.
 
Niko nasoma nje ya Tanzania huku nifanya kazi katika company fulani nikilipwa mshahara dollar 1,800 kwa mwezi,najigharamia mwenyewe masomo yangu kwa 50% nyingine ni sholarship na gharama nyingine za maisha.
Nimeacha mke na mtoto mmoja nyumbani.mke wangu najitahidi kumtumia dollar 1,000 kila mwezi.yeye anafanya kazi katika shirika fulani Tanzania na anapokea mshahara kiasi fulani mara zote analalamika pesa ninayomtumia haitoshi imagine juzi nimetuma kwa exchange rate ya Tanzania alipokea kama Tsh,1,800,000 bado ananipigia cim na kunigombeza pesa haitoshi kwenye matumizi yake ya maisha na mtoto sasa jamani huyu ni mke au mzigo?nimemweleza hari halisi ya maisha ya huku haelewi naishi kwa kujibana ili kile kinachopatikana tukiserve lakini wapi.nahisi kama nilikosea kwenye uchaguzi au anafanyia nini hiyo pesa ya kila mwezi au anaamua kunifanyia ushenzi tu.nimemwambia kuna watu wanalia mchana na usiku wanakosa bahati kama hiyo lakini haelewi.ila ninafikiria kumchukua mtoto wangu akalelewe na mama yangu mzazi au nimchukue nihishi naye ..nahisi huyu mwanamke nimzigo tena haubebeki..nasiyo kwamba kuna assets za ndani ananunua nyumba hiko full hadi usafiri nilimpatia wa kutumia.

Jamani mke wa namna hii nimfanyeje?

Funga safari mchukue mtoto muweke na mama yako mzazi (ikiwezekana). Kama mtoto ni mkubwa mweke boarding. Kikubwa kabla ya kumtema fikiria namna ya kuangalia mwanao hatima yake ni nini. Hapa unapigana vita na watu waliojificha nyuma ya mkeo. You do have a virtual war pressured by peer group mkuu. Some thing is very wrong with your family and something must happen too, fanya maamuzi magumu majibu unaendele kuyapata hapa hapa JF. Heko JF
 
Pooole wee! mwanamke ni kama mtoto anayejifunza kutembea yan ukimpa gari ya miguu 3 ajifunzie kutembea basi ujue atataka tu kutumia gari muda wote. Ukimwacha atembee kwa miguu yake basi atatembea bila wasiwasi! WANAITWA WATU WA WHOLE WEATHER BANA! Mwanamke anaweza kuishi kwa 1000 kwa siku na anaweza kuishi kwa 100,000 kwa siku (there are flexible bana, na wapo makini sana kwenye matumizi ya pesa kama wakijua ni chache na visa versa is true)
Mi nachoona wewe ndiyo umemzoesha, labda kila akisema pesa hazitoshi unamtumia nyingine na kawaida binadamu hatosheki. Inawezekana pia haamini kabwa unapokea hizo $ 1,800 na anafikiri akiendelea kupiga vuvuzela unamwongezea nyingine. Kumwacha sio suluhisho, be a man and plya your part. Kuwa mkali maelezo ya matumizi ya pesa unazomtumia, kama akishindwa cut off remittance bana for sometimes usikilizie! Najua ATAKUA NA AKIBA YA KUTOSHA SASA, KAMA ATAKUA SIYO MFUJAJI. Naamini unaweza kumbadilisha kwa kuanza kudai mchanganuo wa fedha anazotumia kila mwezi

Jamani wewe usinichekeshe yaani kuna mtu anashindwa kutoa mchanganuo!? Hiyo sio solution hata kidogo, nakawambia anaweza kuleta mchanganuo hadi akaona na hela anazomtumia ni cha mtoto. Bwana kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba apigwe deshi mwezi mmoja au hata miwili kabisa tuone atafanyanini, nakwambia baada ya hapo hata akiletewa $ 500 atashukuru...

Yaani wanawake wengine bwana sijui vipi, kuna wenzao waume zao wako hapa hapa hawaachiwi hata senti tano, yeye mume wake yuko mbali anamkumbuka halafu analeta useless poses, ameniudhi kweli...
 
Funga safari mchukue mtoto muweke na mama yako mzazi (ikiwezekana). Kama mtoto ni mkubwa mweke boarding. Kikubwa kabla ya kumtema fikiria namna ya kuangalia mwanao hatima yake ni nini. Hapa unapigana vita na watu waliojificha nyuma ya mkeo. You do have a virtual war pressured by peer group mkuu. Some thing is very wrong with your family and something must happen too, fanya maamuzi magumu majibu unaendele kuyapata hapa hapa JF. Heko JF

Malezi ya wazazi kwa watoto ni muhimu lol, asipelekwe boarding wala nini, tusiige tu vitu, unakuja kushangaa mtoto akiwa mtu mzima anakuwa mkatili, kumbe hakupata mapenzi ya wazazi toka mdogo, tuache bahati mbaya kama uyatima ndio ulete hizi habari. Huyo baba amshikishe tu adabu huyo mke wake kwa kutomtumia pesa japo 2 months, nina uhakika atasurvive kwa sababu ana akiba ya kutosha mwaka mzima..
 
kaka, ujue ndoa ni kushibana yaani tendo lile la ndoa ni la msingi sana. unaweza usimpe hata hela bado ile hela kidogo anayopata yeye akakutumia tena wewe. unaweza mpa gari na kila kitu lakini bado hayuko sambamba na wewe. hivyo inaonekana wazi kwamba kuna mtu anayecheza mechi vizuri baada ya wewe kutokuwepo na ndiye pengine hata anayekula pesa yako. Ushauri wangu, jaribu kumbwambia aje huko akutembelee huko likizo fulani kama inawezekana halafu muone atasemaje. Akikataa hitimisha kwamba kuna sub akikubali fanya uchunguzi wa kina wakati uko nae huko na baada ya yeye kurudi huku. Halafu utaujua ukweli. POLE SANA MWANAUME MWENZANGU
 
heri ajenge nyumba hata kwao kuliko ukute kuna kibuzi kingine ndo kinachotumia hiyo mihela yote. Mkuu hapo sio bure hadi anakuforce, kuna namna
 
mmmmh hi thread ina uwalikini hivi kwa maisha yetu bongo milioni moja unafanyia nini hata kama foleni ya dar?Tufanye count down ndogo,petrol 300,000 sokoni 120,000 housemaid 100,000,miscelleneous 200,000 laki nane roughly sasa huyo milioni 2 tena ana mshahara?either anajenga kwao au ana mwanaume tena miundombinu almaarufu marioo.halafu kumbe nie wanaume mnajua kuna umuhimu wa kuangalia kabilae?ushauri embu acha kumtumia matumizi mwezi mmja mweleze chochote either umelipa ada or whatever uone reaction yake hata kama uko mbali hisia zitakugusa.pole all the best.
 
Unajua bei ya kiatu CL, ni $ 1000+, pochi ya LV, sijataja nguo na vipodozi kwa mwezi inaweza kuwa $ 1000 pia. Mnaishi dunia gani ndugu.

Ukiwa nacho tumia, ukikosa jutia...... na mkumbuke kuwa landcruser mkonga hainunuliwi show room/yard, hadi kwa order.
 
kama kiatu ni dollar 1000 sio kwao kwa sababu mume wake amesema ndo anayomtumia kwa hiyo unataka kusema ye amenunua kiatu tubila kufanya mengineyo?thread ya mtoa mada sio wa class hiyo na majibu yangu yalimlenga yeye hayakukulenga wewe na matajiri wengine wenye kununua kiau cha milioni na laki sita
 
Back
Top Bottom