Mke wangu anastahili adhabu?

Kwa kifupi nina familia ya mke mmoja ninayempenda sana na watoto wawili. Miezi kama tisa iliyopita nilipata matatizo ya kupunguzwa kazini baada ya Ka-NGO nilikokuwa nafanyia kazi kukosa wafadhili wa kutosha na kuamua ku-cut down costs za uendeshaji.

Hali ya kimaisha ilibadilika na kuwa mbaya, hivyo mama watoto wangu alichukua jukumu la kutafuta kazi kwa nia ya kusaidiana maisha hapo nyumbani. Baada ya kama miezi mitatu, nikiendelea na vibarua vya hapa na pale kwa sababu ya elimu yangu kuwa haitoshi, wife alifanikiwa kupata kazi kama Personal Assistant wa Boss fulani wa hapa Dodoma kwenye ofisi moja ya serikali.

Hali ya Maisha ikabilika na kuwa nzuri kama zamani. Kwa kweli tunapenda mno na hajawahi na wala mimi sijawahi kumuonyesha ubaya wowote wala kugombana.

Kama mwezi mmoja hivi uliopita, nilipata fununu kuwa wife anamahusiano na Boss wake. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina nikagundua kuwa ni kweli na nilipomuuliza alikiri kuwa alifanya hivyo mara moja tu ili apate kazi kunusuru hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa hapo nyumbani, lakini boss amekuwa akimsumbua sana waendelee na kitendo hicho angawa binafsi hafurahii na anajuta kwa yaliyotokea!

Naomba ushauri, nimfanyaje bimkubwa huyu? Anastahili adhabu???

*** Kisa hiki nimeletewa na rafiki yangu toka Dodoma akiniomba ushauri, hivyo hakina uhusiano na maisha yangu binafsi ***

HorsePower
Chunia tuu mbona hata RAISI yanamtokea hayo lakini anauchuna tuu.
 
Mwambie ampotezee huyo boc na kama ni ofc ya serikali maanake hawez kumfukuza kaz kwa kosa la kumnyima.wala usimfanye chochote maana amekuwa mkweli na kakueleza situation ilivokuwa.
 
Tatizo kuna hulka imejengeka mwanamke ili kupata ajira lazima afungue mapaja...hii ni mbaya zaidi kwa kuwa baadhi ya wanawake imewaingia akilini na kujaribu kuitumia kama kigezo cha kupata ajira. Mie kuna kadenti cha UDSM kalikuja kuomba kazi baada ya kufanyanae interview kakachukua namba yangu baadae kakanitumia msg huku kakiniita handsome. Nilikakanya na kukapa ajira ili kukabadili mawazo machafu ya kifedhuli aliyoyajenga. Hakika ni kitendo cha kinyama na kikatili kumdhalilisha mwanamke kwa ajili ya ajira hivi leo akifanyiwa mtoto wako, mkeo kama huyo jamaa utajisikiaje ?.
 
Du sipati picha huyo boss alimkunjaje huyo mkeo,mimi kama mimi kosa la wife kupigwa nao na mtu mwingine, huwa sisamei kabisa hata aje nani hiyo ndio inakuwa imetoka,hiyo ni dharau ya hali ya juu sana.


tuko wengi mkuu......ahahahaahhaaaaaaaaaaaaaaaaa_ni kama ka mfumo dume lakn ndio ukweli wenyewe.
 
Kwann mwanamke akikosea anaonekana hafai na anatakiwa aachike,
Na iweje nyie wanaume mkikosea mnajiona mashujaa na linakuwa sio kosa?
wangapi wana nyumba ndogo tena szizokuwa na faida zozote na wake zao wanazijua na still wanaume wanaona ni haki yao?
Haya mambo sio ya kuwahukumu wanawake hivi bwana,huyo mwaume ndio anajua thaman ya mkewe na akiongea naye kulingana na mapenz na situation zao ataamua mwenyewe.

Umeuliza swali zuri sana,...
Kuna mdada aliniuliza swali kama hilo nami nikamjibu kwa kumrudishia swali.....baba ama mama yako wakifumaniwa unaona aibu ama sema uchungu sana nani kati yao akifumwa ugoni_akasema kwa mama......sasa hapo ndipo ilipolalia human nature,.....

Mwanaume anaweza oa wanawake zaidi ya mmoja lakn mwanamke kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja ni haramu.period
 
Kwann mwanamke akikosea anaonekana hafai na anatakiwa aachike,
Na iweje nyie wanaume mkikosea mnajiona mashujaa na linakuwa sio kosa?
wangapi wana nyumba ndogo tena szizokuwa na faida zozote na wake zao wanazijua na still wanaume wanaona ni haki yao?
Haya mambo sio ya kuwahukumu wanawake hivi bwana,huyo mwaume ndio anajua thaman ya mkewe na akiongea naye kulingana na mapenz na situation zao ataamua mwenyewe.

Ameshindwa kuamua mwenyewe so anakuomba ushauri ampe adhabu gani?
 
Ila jamani naomba nisiwatoe povu wadada

Ila kuna kitu is not right with women na kazi zao
Sio shida tu kuna kitu kimeanza jengeka vichwani kwamba bila kuigawa kitu haupati kazi nzuri
Nimekutana na case tofauti lakini ya huyu dada iliniacha mdomo wazi

Ilikuwa conference
Yeye ni afisa serikalini wizara fulani TZ
Siku ya mwisho kuna cocktail part, baada ya kupata kinywaji na aibu kutoka kidogo
Anamfuata binti mwingine Mtz na kumwambia "unaringa nini?"
Wiki nzima umezubaa hapa wakenya wanachukua nafasi zote UN
Uza uc*** upate hela wewe
akaendelea " Mie nimeuza hadi nimepata kazi UN"
Utaishia kuwa maskini
Huyu ni mtu ambaye ana kazi yake na maisha yake nyumbani na isitoshe mke wa mtu

Swali lililonijia kichwani, anahakika gani huyu anayemwambia ana maisha duni huko atokako?
Je ni kweli sasa hivi mwanamke kupata cheo/kazi hadi amegwe?

I was so sad! kwamba wanawake wanaanza kulikubali hili kwa vitendo

Hii ndio imenihuzunisha kupita maelezo!
 
Makosa mengine kusamehe ni kujidanganya.Kama ni mimi na nimejiridhisha pasi na shaka kwamba jambo hilo limefanyika hatua nitakayochukua ni kuvunja ndoa FULL STOP!Kwani kitu gani bwana,ilisambaratika URUSI sembuse ndoa ya watu wawili!
 
Back
Top Bottom