Mke wangu anastahili adhabu?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Kwa kifupi nina familia ya mke mmoja ninayempenda sana na watoto wawili. Miezi kama tisa iliyopita nilipata matatizo ya kupunguzwa kazini baada ya Ka-NGO nilikokuwa nafanyia kazi kukosa wafadhili wa kutosha na kuamua ku-cut down costs za uendeshaji.

Hali ya kimaisha ilibadilika na kuwa mbaya, hivyo mama watoto wangu alichukua jukumu la kutafuta kazi kwa nia ya kusaidiana maisha hapo nyumbani. Baada ya kama miezi mitatu, nikiendelea na vibarua vya hapa na pale kwa sababu ya elimu yangu kuwa haitoshi, wife alifanikiwa kupata kazi kama Personal Assistant wa Boss fulani wa hapa Dodoma kwenye ofisi moja ya serikali.

Hali ya Maisha ikabilika na kuwa nzuri kama zamani. Kwa kweli tunapenda mno na hajawahi na wala mimi sijawahi kumuonyesha ubaya wowote wala kugombana.

Kama mwezi mmoja hivi uliopita, nilipata fununu kuwa wife anamahusiano na Boss wake. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina nikagundua kuwa ni kweli na nilipomuuliza alikiri kuwa alifanya hivyo mara moja tu ili apate kazi kunusuru hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa hapo nyumbani, lakini boss amekuwa akimsumbua sana waendelee na kitendo hicho angawa binafsi hafurahii na anajuta kwa yaliyotokea!

Naomba ushauri, nimfanyaje bimkubwa huyu? Anastahili adhabu???

*** Kisa hiki nimeletewa na rafiki yangu toka Dodoma akiniomba ushauri, hivyo hakina uhusiano na maisha yangu binafsi ***

HorsePower
 
Hivi Juma nature aliwahi kuimba wimbo gani vile?? Bosi kafanya nini nini.

Unadhani walifanya mara moja kweli? Unadhni wameacha?
Pima maji na unga kiume ndo utapata jibu
Pole sana lakini

Hiyo sentensi ya mwisho inaonekana wewe ni mwoga sana
Reputation ni thamani ya moyoni sio ya watazamaji labda kama ni mwanasiasa wa TZ
 
Naunga mkono hoja kwa 100%,.............aache uoga wa maisha_ndio maana hata mke wake anamegwa eti kwa kisingizio cha kupata kazi,..........pole yake
 
kwa kifupi nina familia ya mke mmoja ninayempenda sana na watoto wawili. Miezi kama tisa iliyopita nilipata matatizo ya kupunguzwa kazini baada ya ka-ngo nilikokuwa nafanyia kazi kukosa wafadhili wa kutosha na kuamua ku-cut down costs za uendeshaji.

Hali ya kimaisha ilibadilika na kuwa mbaya, hivyo mama watoto wangu alichukua jukumu la kutafuta kazi kwa nia ya kusaidiana maisha hapo nyumbani. Baada ya kama miezi mitatu, nikiendelea na vibarua vya hapa na pale kwa sababu ya elimu yangu kuwa haitoshi, wife alifanikiwa kupata kazi kama personal assistant wa boss fulani wa hapa dodoma kwenye ofisi moja ya serikali.

Hali ya maisha ikabilika na kuwa nzuri kama zamani. Kwa kweli tunapenda mno na hajawahi na wala mimi sijawahi kumuonyesha ubaya wowote wala kugombana.

Kama mwezi mmoja hivi uliopita, nilipata fununu kuwa wife anamahusiano na boss wake. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina nikagundua kuwa ni kweli na nilipomuuliza alikiri kuwa alifanya hivyo mara moja tu ili apate kazi kunusuru hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa hapo nyumbani, lakini boss amekuwa akimsumbua sana waendelee na kitendo hicho angawa binafsi hafurahii na anajuta kwa yaliyotokea!

Naomba ushauri, nimfanyaje bimkubwa huyu? Anastahili adhabu???

*** kisa hiki nimeletewa na rafiki yangu toka dodoma akiniomba ushauri, hivyo hakina uhusiano na maisha yangu binafsi ***

horsepower
hiyo mara moja inaweza kuigarimu familia ukimwi unapatikana kwa dakika moja.
Kwa kweli anastail adhabu kali sana
 
hivi vitu vya mapenzi vinashaurika kweli? ukishauriwa umuache utakubali? au uendelee nae utasema nakaa na wewe kwa sababu nilishauriwa?
kweli hata na feruzi aliimba huo wimbo na ushauri hakuupata.
kwa ushauri wangu mie sio adhabu tu, huyo ni wa kutupa kabisa. maisha ni kama bahari kuna dhoruba za mawimbi makali na wakati mwengine ni shwari, si angevumilia shida mpaka hapo yakikaa sawa, akamvulie nanii mtu mwengine kabisa, kisha aseme anakupenda? eti alivuwa kwa shida:lol: hiyo haiingii akilini mwangu mie.:hatari: ukimwi hauko mbali hapo.
 
Hivi ni Juma Nature au Ferooz!?

Ni Ferooz...@mtambuzi

..mmh,alichokosea ni kutokwambia kilichotokea tangu mwanzo..angekuwa hajapendezewa na kauli ya huyo boss kuomba rushwa ya ngono angesema. Kwakuwa hajasema mpaka tetesi zimezagaa mtaani,hadi unafahamishwa na watu baki....then ujue kuna possibility mambo hayakuishia hapo ka-movie kao kanaendelea...#Maamuzi ya busara yanahitajika hapo!
 
Haya mambo ya wanawake ni shida sana,mwambie jamaa yako ..,...aaaah....Ngoja nitarudi kwa ushauri zaidi!
 
kwa kifupi nina familia ya mke mmoja ninayempenda sana na watoto wawili. Miezi kama tisa iliyopita nilipata matatizo ya kupunguzwa kazini baada ya ka-ngo nilikokuwa nafanyia kazi kukosa wafadhili wa kutosha na kuamua ku-cut down costs za uendeshaji.

Hali ya kimaisha ilibadilika na kuwa mbaya, hivyo mama watoto wangu alichukua jukumu la kutafuta kazi kwa nia ya kusaidiana maisha hapo nyumbani. Baada ya kama miezi mitatu, nikiendelea na vibarua vya hapa na pale kwa sababu ya elimu yangu kuwa haitoshi, wife alifanikiwa kupata kazi kama personal assistant wa boss fulani wa hapa dodoma kwenye ofisi moja ya serikali.

Hali ya maisha ikabilika na kuwa nzuri kama zamani. Kwa kweli tunapenda mno na hajawahi na wala mimi sijawahi kumuonyesha ubaya wowote wala kugombana.

Kama mwezi mmoja hivi uliopita, nilipata fununu kuwa wife anamahusiano na boss wake. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina nikagundua kuwa ni kweli na nilipomuuliza alikiri kuwa alifanya hivyo mara moja tu ili apate kazi kunusuru hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa hapo nyumbani, lakini boss amekuwa akimsumbua sana waendelee na kitendo hicho angawa binafsi hafurahii na anajuta kwa yaliyotokea!

Naomba ushauri, nimfanyaje bimkubwa huyu? Anastahili adhabu???

*** kisa hiki nimeletewa na rafiki yangu toka dodoma akiniomba ushauri, hivyo hakina uhusiano na maisha yangu binafsi ***

horsepower

ushauri upi tena wakati ashavuliwa chupi ??labda tumshauri bosi wake kama akutumia kondom next time akumbuke basi
 
Ni Ferooz...@mtambuzi

..mmh,alichokosea ni kutokwambia kilichotokea tangu mwanzo..angekuwa hajapendezewa na kauli ya huyo boss kuomba rushwa ya ngono angesema. Kwakuwa hajasema mpaka tetesi zimezagaa mtaani,hadi unafahamishwa na watu baki....then ujue kuna possibility mambo hayakuishia hapo ka-movie kao kanaendelea...#Maamuzi ya busara yanahitajika hapo!

Mkuu hayo maamuzi ya busara ni yapi? Maana hayo ndiyo ninayoyahitaji kumshauri rafiki yangu huyu kutoka pande za mjengoni!
 
Mke wa jamaa na Boss wake, wote wanastahili kufunguliwa mashtaka na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa mke kutoa rushwa ya ngono na boss kuisasambua rushwa ya ngono. Kosa la pili ni la kutembea nje ya ndoa kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha kwa mke na kwa boss kutembea na mke wa mtu. Kosa la tatu ni kwa mke kurisk maisha ya mume kama itatokea boss kuwa amemuambukiza virus. Kidini Bible imeruhusu mtu kumuacha mke wake kwa kosa la uasherati kama amemfumania, hii ni kwa pande zote mbili.
 
yashatokea, asamehe na wasonge mbele, huku mtafute njia nyingine ya kuingiza kipato hapo kwa boss aache tu kazi
 
Piga chini mkuu, siitajigi ata kusikia mara, mbli napigaga chini faster
Kwann mwanamke akikosea anaonekana hafai na anatakiwa aachike,
Na iweje nyie wanaume mkikosea mnajiona mashujaa na linakuwa sio kosa?
wangapi wana nyumba ndogo tena szizokuwa na faida zozote na wake zao wanazijua na still wanaume wanaona ni haki yao?
Haya mambo sio ya kuwahukumu wanawake hivi bwana,huyo mwaume ndio anajua thaman ya mkewe na akiongea naye kulingana na mapenz na situation zao ataamua mwenyewe.
 
Ni kweli huyo mke kakosea tena sana,
Cha msingi kwa vile ameelewa kosa na kukuri asamehewe wakapime afya na aache hiyo kazi na watafute namna nyingine ya kupata kipato,
Naamin km mpaka amekiri mwenyewe ni kweli alishidwa tu kujitambua na kuendelea kutafuta kazi ya halali tofauti na alichofanya.
 
Back
Top Bottom