Mke wangu ananitesa na kuninyanyasa sina raha na ndoa sijui nifanyaje

Neema, umeniacha hoi. eti akabebe vyuma gym, hahahaa!!! kazi kweli kweli... sijawahai kusikia mwanamme anakung'utwa na mkewe, its my first time. maybe wapo, lakini sidhani kama wana nguvu ya kuhadithia kwamba wanapata kipigo. kazi kweli kweli... huyu ni wa kumwacha tu. mapenzi yameisha kwako ndio maana kakugeuza house boy wake.
Kwa kifupi tu kaka, kwa mwanamke mapenzi yakiisha yameisha. hakuna kurudi nyuma. tofauti na mwanamme anaweza kumchukia mkewe akadhanimini nyumbani ndogo, lakini akarudi after sometimes anajirudi na kumwomba mwenzie msamaha na maisha yakaendelea kama kawaida. huyu alokugeuza house boy usitegemee kua eti kuna siku penzi litarudi. fikiria hatma ya watoto wako then fanya maamuzi ya busara.

1.usifanye kile unachodhani kitamuudhi na kukupiga,kisha man up na wewe akikupiga pigana mpaka atie adabu atiiii

2,tendo la ndoa la msimu inawezekana kuna mtu anamkuna,chunguza.......

3,kama bado unampenda,tafuta suluhu kwa kuongea na wazazi au watu unaowaheshimu....

4,tafuta nyumba ndogo isiyo na gharama,usimuulize kitu chochote mkeo,yeye kama ana akili atasense mabadiliko...na hivi ushamjengea kwao naona atatia jeuri,achana naye waone ustawi wa jamii na baadae mahakama ambayo itawatenganisha na kugawanisha mali mlizochuma nusu kwa nusu,mkishatengana wewe nenda kaipromote nyumba ndogo iwe kubwa ilaa angalia usifanye tena uzuzu wa kuijengea kwao

5,anza gym beba vyuma mwili wako ujengeke na uwe na stamina ya kupigana-hii itakupa confidence hata akikupiga utajidefence vizuri,na asikwambie mgtu ukimpiga mara moja tu kisawasawa huyo ataanza kukuheshimu/kukuogopa.
 
Kama nakuona vile wakati unapigwa na mkeo :photo:

Pole sana mkuu kaa chini na mkeo muongee maana hayo si maisha kabisa ikishindikana kabisa jaribu kuongea na pande zote mbili za familia yenu au kanisani. Ikishindikana na hapo mpe talaka ukae wewe na watoto wako tu!
 
Kaka nashukuru kwa ushauri wako lakini swala la kumuacha siwezi
 
1.usifanye kile unachodhani kitamuudhi na kukupiga,kisha man up na wewe akikupiga pigana mpaka atie adabu atiiii

2,tendo la ndoa la msimu inawezekana kuna mtu anamkuna,chunguza.......

3,kama bado unampenda,tafuta suluhu kwa kuongea na wazazi au watu unaowaheshimu....

4,tafuta nyumba ndogo isiyo na gharama,usimuulize kitu chochote mkeo,yeye kama ana akili atasense mabadiliko...na hivi ushamjengea kwao naona atatia jeuri,achana naye waone ustawi wa jamii na baadae mahakama ambayo itawatenganisha na kugawanisha mali mlizochuma nusu kwa nusu,mkishatengana wewe nenda kaipromote nyumba ndogo iwe kubwa ilaa angalia usifanye tena uzuzu wa kuijengea kwao

5,anza gym beba vyuma mwili wako ujengeke na uwe na stamina ya kupigana-hii itakupa confidence hata akikupiga utajidefence vizuri,na asikwambie mgtu ukimpiga mara moja tu kisawasawa huyo ataanza kukuheshimu/kukuogopa.

Taufanyia kazi huu ushauri nashukuru ndugu yangu
 
basi atumie kinga halafu ampe n'genyo la kufa mtu uone kama hata mwambia "....eeeh baba watoto ulikua wapi siku zoteee eeeeeh jamaani mmmh.....!!!?" na heshima itaanza siku hiyo hiyo...!

Badala ya kunipa ushauri unanijoke?
 
Hii sredi nina mashaka na ukweli wake! Hapo kwenye RED mwiko kwa kawaida hukaa jikoni iweje ukiomba tendo la ndoa upigwe mwiko? unataka kulifanyia jikoni? au mwiko unakaa chumba cha kulala?

Hapo kwenye bluu, Haiwezekani kila baada ya wiki 2 aende semina, Hakuna semina za jinsi hiyo kwa hapa BONGO.

Hapo kwenye kijani, Kwa kuwa una uwezo wa kujenga nyumba kwao, basi kipato chako si haba. Haiingii akilini kwa mwanaume mwenye kipato cha kujenga nyumba hadi ukweni usiheshimiwe, Haiwezekani.

La msingi Komaa, kwa hizo amri zake uone atakachokifanya.

Hivi wewe unadhani mapenzi lazima yafanyiwe kitandani? Kama unaona uwongo bora ungekaa pembeni watanisaidia watu wengine
 
Wana JF...

Naandika huku nafsi yangu ikiwa na majonzi makubwa.

Mke wangu wa ndoa tuna miaka 8 toka tufunge ndoa, tumejaliwa kupata watoto 2 mapacha wa kiume na kike.

Lakini taingia mwaka juzi kabadilika kaanza vituko nyumbani, sio kawaida yake ananipiga na vitu bila sababu.

Kaenda mbali zaidi ananiambia lazima nikitoka kazini niwahi kufika nyumbani nikae na watoto yeye yupo bize..

Kanilizimisha nimjengee nyumba kwao Same nimemjengea nyumba kubwa tu lakini hana shukurani..

Tendo la ndoa napewa mara moja kwa mwezi nikihoji napigwa na mwiko..

Kila baada ya wiki anasema anasafiri anakwenda kwenye semina nibaki na watoto.

Ndugu zangu nisaidieni nifanyeje??
hapo kwenye red kaka uache kukurupuka,hata kama ni mkeo witaji kufikiria na kupambanua sana,wanawake wetu awa siwo unaweza kumfanya kila kitu na ukajuta maisha yako yote,du ila pole sana
 
Looo ya bushoke kumbe ya kweli mweeeee, kaza ma..... kijana mbona unakuwa hivo sasa
mwanaume lazima ugangamale bwana
 
jamani kila siku naimba humu jf wanaume tunakung'utwa na wake zetu mnabisha,mnaona sasa?pole mchuzi,lakini sasa na wewe unatandikwa weeeeeee na we upo tu,kwa nini usijimuvuzishe ukaanza maisha kwingine? Au unasubiri kilema?
 
Back
Top Bottom