Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

Download

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
344
126
DA,NDOA ZA MWENDOKASI


Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane. Kipato changu na chache hakitofautini sana, ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa. Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata SMS za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake, nikimuuliza ananijibu alikuwa anatongozwa tu. Nimeshagombana nae sana, nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.Last week pia karudia na nimemkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey, darling, love nimemuuliza, tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache, nichukue 50 zangu. Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu, tumeyajadili nikijua ataacha, tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake. Nimezaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba. Leo hii ananitaka niondoke,ninuache na watoto.Nikaanze maisha kimpango wangu.
Naambiwa kuwa anayaweza maisha bila hata ya uwepo wangu.
Nahisi kuna marafiki amewapata wana mshauri vibaya.

Naombeni ushauri.
............
Hatimaye nimefanikiwa kumfumania live akiwa guest na huyo Baba niliye zidaka sms zao,purukushani ilikuwa kubwa kwani nilijikuta nampiga sana mke wangu.
Leo tumetengana rasmi,naanza taratibu za talaka,ahsanteni sana kwa ushauri wenu...

Mungu awabariki...
 
Anzisha miradi pembeni ya kukupatia kipato cha ziada ili ujipange zaidi yake. But, hawa viumbe huwa wanamihemko tu. Utashangaa ukifanya hivyo...anarudisha mazima honey kibao, darling, love zinakuwa zako zote.
 
mkuu pole ila anza kufanya mchakato wa kuongeza kipato na akisisitiza kuachana ... lets her go me naamini mtu akishakuchoka amaekuchoka kurudisha mapenzi nyuma ni ngumu kwa kweli labda muuishi tu kwa ajili ya kuja kuzikana........... kaa chini anza kufikira mstakabali wa watoto wako.. ila baada ya kuachana soon or later atakukumbuka na kutaka mrudiane na itakuwa too late .. pole
 
ndoa ni msalaba cha muhimu ni kuvumiliana na kumtegemea Mungu sana, fanya biashara zako jiongezee kipato mbona atarudi mwenyew alafu usimuulize chochote wala usiguse simu yake we fanya tu yanayokuhusu ila msiachane atanyooka tuuu mkuu, msiachane watakaoumia ni watoto hasa wataumia kisaikolojia
 
Ameshakuwa pasua kichwa huyo..Nwei kama nyuma hakuwa hivyo basi jaribu kuchunguza sababu ya hayo mabadiliko ni nn..Watu wengine wakikerwa uwa hawaongei..Wanachofanya ni kulirevenge kimyakimya..Uende ww pia ndo chanzo cha yeye kubadilika..
 
Kama anataka muachane ni bora muachane kwa amani, ukiendelea kukomaa naye sio ajabu akaja kukudhuru, kuhusu nyumba usimwachie, angalia mfuko wako kama unaweza mpe staili yake aondoke. Lea wanao pambana na maisha. Maisha yenyewe ni mafupi hakuna sababu za kupeana stress.
 
Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane.
Kipato changu na chache hakitofautini sana,ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa.Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata sms za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake,nikimuuli ananijibu alikuwa ana tongozwa tu.
Nimesha gombana nae sana,nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.
Last week pia karudia na nime mkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey,darling,love.nime muuliza ,tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache,nichukue 50 zangu.Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu,tumeyajadili nikijua ataacha,tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake.
Nime zaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba.Leo hii ananitaka niondoke,nikaanze maisha kimpango wangu.
Naombeni ushauri.


naomba unitajie kwanza huyo mwanamke ni kabila gani
 
Kwani ni nani kichwa cha hiyo familia yenu? Iweje wewe ndiyo uwe wakuondoka hapo wakati aliyechoka na ndoa yenu ni mke wako?!
Labda kama hati au kiwanja ni cha mkeo vinginevyo utakuwa mwanaume wa ajabu sana duniani kama utawaachia nyumba yako wanaume wengine waje kuishi nyumba uliyoihangaikia hataka mchango wako ni mdogo kulinganisha na mkeo.
Mimi sikushauri muachane ingawa sijui ni aina gani ya ndoa mliyofunga, risk ni afya maana kwa maelezo yako jambo liko wazi kwamba shemeji ana 0% ya uaminifu cha kufanya muombe Mungu sana akupe hekima ya kuwezesha kufanya maamuzi sahihi.
Pole sana ndugu kwa majaribu haya unayopitia.
 
Pole, kaza moyo tu mkuu! Anza kumpuuza usimfwatilie kuwa busy na mambo yako ya kujiongezea kipato na rafiki zako pia jitahidi kukaa mbali nae kiufupi anza kumtenga maana ndivyo anavyotaka! Kama anakupenda ataanza kupata wivu kama hakupendi itakua ni suluhu ya kuepusha migogoro, muache yeye awe wa kwanza kudai talaka kama ni vikao aitishe yeye tena mwambie kabisaa kama unataka talaka itisha kikao udai talaka yako ili baadae asipate sababu ya kukushushia lawama kuwa wewe ulimfukuza na kumtelekeza na kwenye kikao kwa kuwa yeye ndo anahitaji kujitoa kwenye agano ng'ang'ana ubaki na wanao maana weka wazi tu huna uhakika na ubora wa maisha watakayoenda kuishi wanao chini ya mwanaume mwingine so ni bora upambane tu kuwalea watoto wajue mama yao ndio kawakimbia sio wewe ndio umewakimbia maana sumu ya maneno ya mama ni Kali sana kwenye saikolojia ya watoto, KUNA WANAWAKE Wana roho mbaya sana hasa wakipata bwana wa nje kama uyo wako yuko tayari kuvunja familia kwa ajili ya mjinga mmoja huko nje ila time will tell atakuja kukupigia kagoti ipo siku
 
anataka uondoke kwa maana ipi? wakat ni nyumban kwako kua mwanaume kama pamemshinda hapo nyumban mwambie aende zake na inavyoonyesha wewe ndio una uhitaj mkubwa zaid kuliko kuliko yeye
 
Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane. Kipato changu na chache hakitofautini sana, ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa. Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata SMS za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake, nikimuuliza ananijibu alikuwa anatongozwa tu. Nimeshagombana nae sana, nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.

Last week pia karudia na nimemkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey, darling, love nimemuuliza, tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache, nichukue 50 zangu. Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu, tumeyajadili nikijua ataacha, tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake. Nimezaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba. Leo hii ananitaka niondoke, nikaanze maisha kimpango wangu.

Naombeni ushauri.
Pole
 
Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane. Kipato changu na chache hakitofautini sana, ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa. Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata SMS za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake, nikimuuliza ananijibu alikuwa anatongozwa tu. Nimeshagombana nae sana, nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.

Last week pia karudia na nimemkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey, darling, love nimemuuliza, tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache, nichukue 50 zangu. Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu, tumeyajadili nikijua ataacha, tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake. Nimezaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba. Leo hii ananitaka niondoke, nikaanze maisha kimpango wangu.

Naombeni ushauri.
Sikia kaka, kama kweli hujamfanyia kitu chochote kibaya huyo mwanamke, na umeshatafuta ushauri kwa wazee mara kwa mara habadiliki, ACHANA NAE!
 
Back
Top Bottom