Mke wangu ana wivu wa kuptiliza

Hapo unakuta mdau 'anayoosha miguu' huku anatumia gari. Lol.

Hii nanyoosha miguu hii...

we bwana wee!eti nanyoosha miguu!hiyo miguu si ukanyoshee kitandani?mi nije nikukande ala!ila jamani si muwe mnatoka na wake zenu siku moja moja,we toka nae tu akirudi home akakuta home hakueleweki siku ya kwanza,kesho akidai tena unamtoa akirudi anakuta nguo zilizoanikwa bado zipo kwenye kamba afa ni saa saba usiku,siku ya tatu karudi anakuta wageni wanawasubiri getini af nyie mko bwi!mwenyewe ataanza kudai kubaki home!tulikuwemo humo sa hizi tushajizoelea siye!we piga moja mbili tatu bar ukirudi siku ya kwanza unakuta nimenukia na uturi wangu na kipajama,unanicheki kwenye neti wee lakini ndo ushakuwa nyingi saa nyingine hata hufaidi vizuri!kesho ukirudi kutoka kunyosha miguu unakutana na bonge la menu mezani lakini ndo lishapoa,siku ya tatu we unatoka na mia nimejikalisha kwenye dressing table najiremba!kesho yake utaona kama hujamuuliza vipi leo huend kunyosha miguu!ahahahahahhahhahahha jamani ndoa ni kumjua tu mwenzio na kuendana nae accordingly!basi!
 
Na umtafutie kazi ya kufanya huyo mkeo! Manake wewe kakufanya ndo ajira yake. Wewe boss wako akikuona ofisini afu saa nne ukatoka 'kidogo' na kurudi saa saba atakubali?
Ukifa ghafla hapa utatuachia matatizo. Mtafutie walau kabiashara atoke ndani na yeye baba!
 
Yaani mbavu sina! Yaani raha ni kujipa mwenyewe na ukitaka stress unauziwa!

Hapo inaonyesha haumkuni kisawasawa ndio maana anaona unaenda kufanya nje lkn akiona unamsuuza kisawasawa hata ukiaga unaenda bar hatoona tatizo,kijana jitume mwanamme kaziiiiiii simamia kucha kijanaaaa wivu wote utaisha!!
 
ndo hivo vijana wa siku hizi mapenzi 0 wizi mtupu

kwa hiyo nyie mlikuwa mnatuibia kwa kukaa nyumbani?mi nadhani maisha yamebadilika na kusaidiana muhimu ili muishi maisha mazuri. pili mwanamke amesoma atakaa nyumbani tu kuosha vyombo?wengi hawatakubali n wivu kama hapo juu
 
Na umtafutie kazi ya kufanya huyo mkeo! Manake wewe kakufanya ndo ajira yake. Wewe boss wako akikuona ofisini afu saa nne ukatoka 'kidogo' na kurudi saa saba atakubali?
Ukifa ghafla hapa utatuachia matatizo. Mtafutie walau kabiashara atoke ndani na yeye baba!

halafu kuna familia wanahatarisha future za familia zao.....
Mke hana kazi basi tafuteni kibiashara afanye...
Maana hata kama mume unalipwa mamilioni kesho ukifumba macho inakuwaje? Si ndo mwanzo wa watoto kuacha shule kuuza maandazi? Au kugeuza mke na watoto ombaomba kutwa kwa ndugu kuomba msaada?
 
Hiyo inaitwaga abiria chunga mzigo wako,..habari za kuaga jioni jioni unaenda kunyoosha miguu na wakati anaona haijapinda peleka huko..
 
WAN JF naomba ushauri mke wangu ni mama wa nyumbani ,lakini cha ajabu nikirudi kazini nikimwambia natoka kidogo yeye anadhani naenda kwa wanawake nimejaribu kumweleza mke wangu nanyosha miguu ataki ,siku nyingine kama nataka nipate moja baridi nalszimika kupia moja baridi ndo niende home zaidi ya hapo nikifika home kutoka ni shida ,NAOMBA USHAURI

Duh! Mkubwa hiyo ndio wife material ya ukweli sasa........hivi sijui kwa nini aisee, tunaopenda wanawake wenye wivu hatuwapati, nyie msiowapenda mnawapata.....inakuaje lakini? Ila sikia mkuu unajua hawa watu bwana ni tofauti kidogo, kiukweli ni haki yake na nilazima awe na shauku ya kujua ukweli wa mambo yako bwana. Hivi kweli umeondoka kuanzia asubuhi mpaka jioni, halafu mtu wa watu maskini anakusubiri upumzike nae ukirudi then ghafla ukirudi unaondoka tena..............ina maana hapo kukutana nae tena lazima ni usiku tu, na kama kawaida ukirudi unakaa kidogo muda mfupi then unalala siku imeisha. Mpe nafasi bwana nae ajisikie mkuu, au la sivyo kama unajua ukirudi utatoka tena basi ukiwa unarudi mnunulie hata kazawadi basi ili hata ukitoka awe na amani...........unajua hawa watu wanathamini sana hivi vizawadi zawadi hivi. Au njia nyengine inayofaa ambayo haina mgogoro basi toka nae bwana ili asiwe na wasiwasi.

Maranyingi hawa watu sio vizuri kuwaweka katika wakati mgumu mkuu
 
Lazima ulikuwa kicheche hapo kabla ya kumuoa, sasa umeacha anakuhukumu kwa historia. Kabla ya kuoa na baada ya kuoa anafaa kwenda naye kunyoosha miguu. Pamoja na kumwambia umeacha, nahisi vitendo vyako havithibitishi kauli yako. hebu rekebisha ya fuatayo:
  • Acha usiri katika kuongea na simu na pia punguza mawasiliano yenye kuashilia kuongea na mwanamke mliyeshibana mbele yake. Pia usipende kuwa bussy na sms chating ukiwa nyumbani( hiyo inachukua nafasi yake ya kumjali na kupiga story}
  • Labda aina ya kazi yako inakuexpose sana kwa wanawake na mwishowe unaishia kukutana nao baada ya kazi katika kunyoosha miguu. Hata mkeo ulimpata namna hiyo. lazima awe na wasiwasi. Usiyaendekeze mazingira uliyotumia kumpata mkeo.
  • Wivu ni ishara ya upendo, so mkeo anakupenda
 
nashukuru ndugu yangu ushauri wako nitufanyia kzi alafu nitarudi kukupa feedback imekuaje
 
Naunga mkono hoja...Wanaume wengi wanapokuwa kwenye uBF na uGF outtings na wapenzi wao kibao mara wakishaoa tu basi outtings zinasepa...Mume yule ambaye alikuwa anapenda sana kutoka na GF wake kabla ya ndoa leo hii anapenda kuzuka mwenyewe mwenyewe sehemu nyingi. Hili husababisha mke kuanza kuwa na wasiwasi kuhusu mienendo ya mumewe....Kwani mke naye hataki kunyoosha miguu baada ya kukaa nyumbani siku nzima?

Mshirikishe kwenye mambo yako.

Ukitaka kwenda kunyoosha miguu nenda naye. Ukitaka kwenda kupata moja baridi muulize kama naye anataka muende wote.

Hata kama hataki, tendo la wewe kumuuliza/ kumwomba muende wote linajenga imani na kuimarisha imani yake kwako.

Ni hivyo tu.
 
kwa kweli wanajf naomba nitoe shukran kwa niaba yan mmempa mambo ambayo yatamsaidia mana mie nlitaka nmshaur kumbe mmeshayasema ni vyema nawe ndugu ye2 yazngatie hayo kwako kutabadilika hasa apate kazi. bt ucje ukawa unaenda kumcheat af uombe ushaur kwa great thnkers kama waliotoa maon utaumbuka ndugu yangu.
 
tuambiane tu ukweli wewe huna katabia ka kuchungulia mahali pengine? huenda kapata fununu mahali hivo wivu ni haki yake. kama huna tabia hiyo wewe usiache kutoka zidisha ila umwambie wenda wapi akitaka aweza naye akakufuata akapata japo vijisoda. kama wewe ni mpenzi wa mpira au unacheza "pulu tebo" basi akija siku mbili tu ataacha mwenyewe kukufuatafuata
 
Aiseh mimi niliamua kupumzika kidogo kidogo hii mitoko, Cku1 nimerud kama saa6 nkakuta chai ya Irik et lazma ninywe duh..wap na wap jaman Castle lite, Mara akawa hataki watt wafungue mlango nikirud fasta anaaamka mwnyw wakat smtym wtt hawajalala,anakuja full mausingz then ananyiosha makopa kopa kibao.......thn kila ukirud lazma upge full menu ata kama ni saa9,uspokula kesi....... nkaona bora nipumzike kwnza...Ila Snowhite Umetisha sana
 
Back
Top Bottom