Mke wangu ana HIV nifanyeje?

huyo ni Mkeo? mlioana lini?, mbona katika maelezo yako sijaona hata sehemu moja mnayosema mlioana, mbona tangu mwanzo mmekuwa mkiishi kwa mikwara na fujo tu?

ndugu yangu Mungu ni mkubwa, hapa hapa hakuna wa kukushauri, uhamuzi unao wewe mwenyewe, we kaa chini na futa hisia zako na jipe uhuru binafsi wa kujudge, na mwisho wa yote utapata jibu zuri tu
 
Nimeanza kuishi na huyu mwanamke toka mwaka 2007 wakati huo tulikuwa tunaishi kama wapenzi na tulikuwa tunatembeleana tu yeye akiwa Dar na mimi nikiwa nafanyakazi Mbamba Bay lkn ilipofika mwezi Desemba 2009 niliamua nipeleke barua kwao ili nioe,jambo la ajaabu lililotokea nilitajiwa mahali kubwa sana yaani Tshs 4,500,000/= mimi nilkawa nimeshindwa kuilipa na ndoa ikashindikana na yeye akarudi kwao Arusha, niliumia sana kwa kukosa kumuoa ilipofika mwezi Machi 2010 yeye alinipigia simu na kunieleza kuwa yuko tayari kuja kuishi na mimi Mbamba Bay ingawa wazazi wake walinitajia mahali kubwa,nilikubali kumpokea na kweli alifika.
Maisha yetu yalikuwa mazuri sana na kila mmoja wetu alisahau tofauti zilizotokea, lkn baada ya kama mwezi mmoja alianzisha ugomvi ambao tulishindwa kuusuluhisha na aliomba nauli ya kurudi kwao na nilimpa.
Ilipofika mwezi Juni 2010 aliomba radhi na akaniomba tuishi tena na mimi bila kinyongo nilikubali ila moyo wangu ulikuwa na wasiwasi kidogo nikaona kuwa safari hii atakapokuja basi ni lazima tucheki HIV.Nikikwenda kumpokea Mbeya na alipofika tu nilimweleza kusudio langu la kupima HIV mimi na yeye .Tarehe 6 Julai tukaenda kupima pale Hospitali ya Rufaa matokeo yake yeye akawa amekutwa na Virusi vya UKIMWI na mimi nikawa sina! Tulipewa maelekezo ya jinsi gani ya kuishi katika mahusiano yetu.Mwenzangu aliipokea hali yake kwa majonzi na mimi nikawa na kazi ya ziada kumtuliza,tukarudi wote Mbamba Bay ila baada ya kurudi tu kama wiki mbili akanywa sumu ili afe,tulimuwahisha Hospitali na tukafanikiwa kuokoa maisha yake,lkn ghafla akanijengea chuki ambayo haina mfano na aliahidi mbele yangu kuwa ni lazima aniue! Niliwaelezea wazazi wangu na wazazi wake pia,wazazi wangu wakanishauri nimrudishe kwao na mke wangu akawa hataki kurudi kwao na tuliendelea kuishi hivyo hadi mwezi Oktoba tarehe 16 alipoamua kuondoka mwenyewe.Ingawa mke wangu ameondoka bado nampenda ila nilipokuja kufanya uchunguzi zaidi nimekuja kufahamu kuwa maisha yake yalikuwa ni ya kutangatanga sana na hivi sasa yupo Dar! Nifanyeje?

You are not serious! Maelezo yako yana utata sana. Lakini kama ni kweli sikiliza nafsi yako inakwambia nini, mimi binafsi ninavyoogopa HIV sijui hata kama ningejiuliza mara mbili ktk hili!
 
aaahhh bwana kashaondoka mwenywe sasa start new life ushauri unao wewe au wataka mrudia akumalizeeeeeeeeeeee
 
Nimeanza kuishi na huyu mwanamke toka mwaka 2007 wakati huo tulikuwa tunaishi kama wapenzi na tulikuwa tunatembeleana tu yeye akiwa Dar na mimi nikiwa nafanyakazi Mbamba Bay lkn ilipofika mwezi Desemba 2009 niliamua nipeleke barua kwao ili nioe,jambo la ajaabu lililotokea nilitajiwa mahali kubwa sana yaani Tshs 4,500,000/= mimi nilkawa nimeshindwa kuilipa na ndoa ikashindikana na yeye akarudi kwao Arusha, niliumia sana kwa kukosa kumuoa ilipofika mwezi Machi 2010 yeye alinipigia simu na kunieleza kuwa yuko tayari kuja kuishi na mimi Mbamba Bay ingawa wazazi wake walinitajia mahali kubwa,nilikubali kumpokea na kweli alifika.
Maisha yetu yalikuwa mazuri sana na kila mmoja wetu alisahau tofauti zilizotokea, lkn baada ya kama mwezi mmoja alianzisha ugomvi ambao tulishindwa kuusuluhisha na aliomba nauli ya kurudi kwao na nilimpa.
Ilipofika mwezi Juni 2010 aliomba radhi na akaniomba tuishi tena na mimi bila kinyongo nilikubali ila moyo wangu ulikuwa na wasiwasi kidogo nikaona kuwa safari hii atakapokuja basi ni lazima tucheki HIV.Nikikwenda kumpokea Mbeya na alipofika tu nilimweleza kusudio langu la kupima HIV mimi na yeye .Tarehe 6 Julai tukaenda kupima pale Hospitali ya Rufaa matokeo yake yeye akawa amekutwa na Virusi vya UKIMWI na mimi nikawa sina! Tulipewa maelekezo ya jinsi gani ya kuishi katika mahusiano yetu.Mwenzangu aliipokea hali yake kwa majonzi na mimi nikawa na kazi ya ziada kumtuliza,tukarudi wote Mbamba Bay ila baada ya kurudi tu kama wiki mbili akanywa sumu ili afe,tulimuwahisha Hospitali na tukafanikiwa kuokoa maisha yake,lkn ghafla akanijengea chuki ambayo haina mfano na aliahidi mbele yangu kuwa ni lazima aniue! Niliwaelezea wazazi wangu na wazazi wake pia,wazazi wangu wakanishauri nimrudishe kwao na mke wangu akawa hataki kurudi kwao na tuliendelea kuishi hivyo hadi mwezi Oktoba tarehe 16 alipoamua kuondoka mwenyewe.Ingawa mke wangu ameondoka bado nampenda ila nilipokuja kufanya uchunguzi zaidi nimekuja kufahamu kuwa maisha yake yalikuwa ni ya kutangatanga sana na hivi sasa yupo Dar! Nifanyeje?

Duuhhh pole sana mzee... lakini Mungu anamakusudi na kila mtu hapa duniani .... kwa hiyo usikate tamaa kabisa ya maisha ... cha kumshukuru Mungu ni kwamba we u mzima. .... Na ninaamini Mwenyezi Mungu alikukutanisha na huyo demu kwa makusudi yake..... kwa sasa nafikiri you need to take care of your self 1st mentally, emotional and physical..
 
Hi Hemed Maronda:

Vipimo vya siku hizi vya HIV viko very sensitive kutokana na maendeleo ya ki-technologia. Ukipima wiki nane toka ufanye tendo la mwisho la ndoa na majibu yakawa negative, basi uwezekano wa wewe kutokuwa na HIV ni mkubwa sana.

Tukija kwenye uhusiano wako na huyo mkeo, uamuzi huko juu yako. Lakini pamoja na hayo yote kumbuka yeye ni binadamu mwenzio, hivyo uungwana ni kitu cha maana kutendeana. Kuna kipindi mlifurahia maisha pamoja. Yeye kukutukana ni kitu kinachoweza kusababishwa na yeye kuchanganyikiwa na hali aliyonayo sasa. Kijana yoyote mwenye afya akipata HIV, anaweza kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi yasio ya kawaida.

Kama una uwezo msaidie hili aweze kuishi productive life. Kuwa na HIV sio tiketi ya kifo.
 
Maronda pole kama ni kweli inaelekea umekufa umeoza kwa mpenzio. Pamoja na kuwa hadithi ulotoa ina mapungufu mengi lakini ninachowezakukuomba kwa sasa ni kutuliza moyo na kuomba MUNGU sana. As for your "wife" all I can say ni kuwa pengine yuko kwenye "denial" stage hajaamini na hataki kuamini kuwa ameathirika na ndio maana anaact kimiujiza. So tulia ikiwezekana tafuta watu wamshauri akapate ushauri nasaha .........anaweza akarudiwa na akili zake na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Pole sana.
 
Ninapata faraja kubwa kwa haya yote mnayonishauri,kumbe mtu ukiwa na tatizo uka-share na wenzako kwa namna moja unapata unafuu moyo unatulia na akili pia inatulia nawashukuru wote tena kwa moyo mmoja,ila kwa muda huu sina mpango wa kutafuta mwanamke wa kuoa ni mapema mno na nimepata funzo kuwa ndoa siyo jambo la kukurupuka!

...Nadhani hakuna ushauri utaozidi hayo ambayo tayari ushatahadharishwa nayo.
Kubwa, uwe na msimamo thabiti kusimamia uamuzi wako wa kuachana nae ingawa bado unampenda.
Hii ni kwa faida yako mwenyewe, wema usizidi uwezo, na usipende ukawa kama mtumwa/mpofu.
Ngumu kwetu sie kuelewa kwanini bado ana chuki mbaya sana kwako na anaendelea kukutukana.
Kama alikutamkia dhamira ya kukuua, nakushauri jiepushe nae kabisa.

Pole sana kwa yote yaliyokukumba na kila la kheri kwenye kusimamia maamuzi na maisha yako..
 
Kama ni mkeo, basi jitahidi kusaidiana naye ili mwisho wa siku ajirudi na akuone wewe kama ni mwenzi wake kuliko mpinzani wake. Kwa bahati mbaya mara nyingi kuelewana inakuwa ni ngumu. Ila ukweli ni kuwa sote ni binadamu na tunafanya makosa. Hakuna aliye bora kuliko mwingine na mwisho wetu sooote ni futi sita chini. Yes, ndio maana nilimlilia sana super coach maana alikuwa mtundu sana na dunia hii.
 
Ndugu yangu kama mkristo katoe sada au kam muislamu sijui wenzangu huwa mnatoa zaka ............na umshukuru mungu kwa yote. Kama mwenzio anahitaji msaada na una uwezo, msaidi maana haya magonjwa wakati mwingine unaletewa bila kujijua. Matatizo yanndoa na familia/wazazi ni kitu cha kawaida tu, kila mzazi huwa anaona mtoto wake ni bora, haswa kama nyie wenyewe hamko strong kiuchumi. Mungu akusaidie, jaribu kupata ushauri kwa wataalamu wakuelekeze nini cha kufanya.
 
Wana JF ninawashukuru kwa mawazo yenu na ushauri,ni kweli ndoa kati yangu na huyo dada wa KINYIRAMBA haikuwahi kufungwa kwa kuwa mimi nilishindwa kulipa MAHALI ya Tshs 4,500,000/= labda wakwe zangu hawakutaka kunioza mtoto wao,mimi kwa Kabila ni MMAKUA,ila tukija kwenye utaratibu mwinginene ni kuwa tumeishi pamoja zaidi ya miaka miwili hivyo naweza kusema ni mke kwa kuzingatia jambo hilo.Waungwana napenda ni washukuru tena na msichoke kuniombea ili nibaki NEGATIVE,kwa upande wa dini mi ni Muislamu na tayari nilishaweka ahadi kuwa nikipima mara ya pili na kuonekana niko salama nimtolee MWENYEZI MUNGU SWADAKA,na tayari nimeshafanya hivyo.
 
Kapime mara tatu kila baada ya miezi mitatu. Halafu ukiwa fresh tafuta mwingine. Realationship is just a predestiny.
 
Wana JF ninawashukuru kwa mawazo yenu na ushauri,ni kweli ndoa kati yangu na huyo dada wa KINYIRAMBA haikuwahi kufungwa kwa kuwa mimi nilishindwa kulipa MAHALI ya Tshs 4,500,000/= labda wakwe zangu hawakutaka kunioza mtoto wao,mimi kwa Kabila ni MMAKUA,ila tukija kwenye utaratibu mwinginene ni kuwa tumeishi pamoja zaidi ya miaka miwili hivyo naweza kusema ni mke kwa kuzingatia jambo hilo.Waungwana napenda ni washukuru tena na msichoke kuniombea ili nibaki NEGATIVE,kwa upande wa dini mi ni Muislamu na tayari nilishaweka ahadi kuwa nikipima mara ya pili na kuonekana niko salama nimtolee MWENYEZI MUNGU SWADAKA,na tayari nimeshafanya hivyo.
mkuu kumbe wa kunyumba kabisa "CHIMKO"
 
osijali Mungu atakusaidia tu,unachotakiwa ni kuakaa chini na kuweka mikakati yako ya baadaye,na kujiweka bussy itakusaidia kidogo kumsahau huyo mwenzi wako,kwani najua kuwa sio rahisi kumsahau mwezi wako hata kama anamatatizo gani.
Mungu akutie nguvu na ujasiri zaidi.
Lakini mimi ninahisi kuna uwezekano kuwa wazazi wake (familia yake) walikuwa wanajua ndio maana hawakutaka wewe umuoe( naanisha kukwambia utoe mahali/posa ya milion 4 na nusu) na kumbuka akutukanaye hakuchagulii tusu,kuna uwezekano hawakutaka kukueleza hali halizi ila walivyotoa hiyo mahali walijua kabisa utashindwa na kumwacha mwanamke.:doh:
 
@mbogodume.

lol najaribu kutafakari Avatar yako inamaaninsha nini?? ndo wamekutana au ndo wanachana it look very funny..lol:smile:
 
Ninapata faraja kubwa kwa haya yote mnayonishauri,kumbe mtu ukiwa na tatizo uka-share na wenzako kwa namna moja unapata unafuu moyo unatulia na akili pia inatulia nawashukuru wote tena kwa moyo mmoja,ila kwa muda huu sina mpango wa kutafuta mwanamke wa kuoa ni mapema mno na nimepata funzo kuwa ndoa siyo jambo la kukurupuka!

Great... kuwa makini zaidi next time..
 
Bwana Hemedi me wanchanganya kidogo.Huyo mwanamke si mke wako kwani sijaona mahala kwenye hiyo post panapoonesha mlifunga ndoa,ila ulisema mahari ilikuwa kubwa ukashindwa na mke akakufuata Mbambabay.Kaka bado hujaoa acha ZINAA tafuta mke uoe.Zidisha ibada na umshukuru MUNGU kwa kukuepusha na maradhi hayo,ila usimtenge huyo mwenzio kimisaada.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom