Mke wangu amezaa nje ya ndoa nimeamua tuachane .nisaidieni juu ya hili.

Maisha haya,wanaume wakizaa nje wanasameheka wengiwao.ila wanawake ni ngumu ndo nature.MSAMEHE.
Wanaume hawapati uja uzito, na hawaji na uchafu nyumbani wakifanya tendo la ndoa nje, kikubwa wakioga baaaaasi ni wasafi kurudi ndani ya ndoa yao

Hii topiki ninanikumbusha binti mmoja anayetaka kuzaa nje ya ndoa na kidumu (amepanga) wakati yeye bado ni mke halali na anaishi na kulala na mumewe.

Nakushauri usimuache huyo mkeo, leo wanao na huyo mtoto wa mkeo kwani kitanda hakizai haramu. Afadhali ya jana unaijua kuliko kuitegemea kesho ambayo hujaiona.

Duuh mkuu ulioa kihalali, yaani mkeo wa ndoa anakuwa na ujasiri wakukwambia kuwa mjamzito,
Kwani kuoa kihalali nikupi Mtalingolo
nyie hamjaoana kihalali mechukuna tuu kwani amepata wapi ujasiri wa kukuambia ushenzi huo? Huyo piga chini

Kihalali ni aje hebu nihabarisheni mwenzenu na amemwambia ushenzi huo nadhani kwa vile yuko mbali nae
kama mtu kishakaa nae na kuzaa nae watoto wawili huyo ni mkewe,,
Ingawa naona huyu mwanamke mwenzetu kicheche yaani kashindwa kumvumilia mmewe , kuna watu hawana hata mshipa wa aibu.
Pole sana nimekosa hata kusema

Wanaume hawapati uja uzito, na hawaji na uchafu nyumbani wakifanya tendo la ndoa nje, kikubwa wakioga baaaaasi ni wasafi kurudi ndani ya ndoa yao

umenikumbusha kuna jamaa yangu huwa anasema...yye huwa akienda kwa nyumba ndogo then baada ya shughui akioga huwa anasema anatakasika na anakuwa anajihisi hajafanya lolote..hahah

Wana,JF Naomba ushauri wenu.
Nilikuwa nimeoa na huyo mke nilikuwa nimezaa nae watoto wawili,nikapata nafasi ya kwenda kusoma hapahapa Tanzania,Mke wangu ni mwalimu wa shule ya Msingi,nilipokuwa chuo tulikuwa tunawasiliana vizuri,nilikuwa naendalikizo,lakini mara nyingi nilikuwa siendi likizo zote kwa sababu ya hali ya uchumi,na nilikuwa namwambia kwamba siendi likizo kwa sababu ya hali ya kiuchumi ambayo hata yeye alikuwa anaijua,nili kuwa namwambia ntabakia kwenye mkoa huu na kwa ndugu yetu ambaye na yeye anamfahamu,hadi namaliza chuo nikapata Temple ambayo ingeweza kutusaidia,kupata chakula,nikamwambia fanya utaratibu wa uhamisho,akasema sawa,badae siku hiyo hiyo usiku akanipigia simu akaniambia mimi ni sasa hivi ni MJAMZITO SI WEZI KUJA HUKO,Nikamuuliza umeolewa?akasema hapana,Tangu pale nikaona kuwa hatanifaa,watoto wako shule nina wahudumia mwenyewe nikimwambia changia shilingi elfu kumi,anakuwa mkali sana,tangu pale sikuwahi kumwambia chochote kuhusu watoto.
HADI HVI SASA HATUKO PAMOJA LAKINI YEYE ANATAKA TUSAMEHEANE NA TUISHI PAMOJA NIMEKATAA.
(NIMEONA NILILETE KWENU WADAU MNISAIDIE)

wewe umesema alikuwa ni mkeo!kivipi sasa? hebu cheki hapo kwenye red na jibu lake kwenye bluu! kwa hali hii unatakiwa kuchapwa viboko
kwanini ulikuwa unamtumia tu mama wa watu! na usikute hiyo ada kalipa yeye,,unapenda kumega tu ila kuoa hutakuti!

kama hujawahi toka nje ndoa toka ukiwa masomoni hustahili kumsamehe lakini kama ulikuwa na wewe unachovya chovya msamehe mkae muishi na kumlea mtoto wa kambo. Akianza kutembea mkabidhi baba ake.

Wanaume hawapati uja uzito, na hawaji na uchafu nyumbani wakifanya tendo la ndoa nje, kikubwa wakioga baaaaasi ni wasafi kurudi ndani ya ndoa yao
Inasemekana mwanamke hata akijisafisha namna gani; hata baanda ya masaa 3 akichuchmaa na kupiga chafya basi kuna vitu vitatoka!

Kuna mambo kadhaa ya kumpima huyo mkeo
Kwanza muulize akwambie mimba hiyo kalala na nani? Akikwambia ukweli yaweza kuwa dalili ya kutaka kusamehwa
Pili muulize sababu na mazingira ya kupata hiyo mimba -yawezekana alibakwa, au alikuwa amelewa au aliamua baada ya kuona wewe uko mballi
Tatu muulize sababu za kutotumia kinga ya aina yoyote na je usalama wake ukoje?
Nnne mpe swali gumu; mwambie akaishi kwa huyo mwanamume hadi ajifungue, alee mtoto na mtoto akishakua then arudi kwako. Jibu utakalopata hapo litakupa fursa nyingine ya kumpima anafikiri nini
Tano, jipime wewe mwenyewe uko safi kiasi gani? isije kuwa mkuki kwa nguruwe!
Mwisho: Ndugu yangu wako/tuko wanaume wengi tunaoishi na kulea watoto wasiokuwa wetu. Kumbuka kuna takwimu zilionyesha kuwa asilimia 59 za wananume wanalea watoto wasiokuwa wao (kipimo cha DNA); ila wengi huwa hatuulizi kwa sababu ya kuogopa athari kwa watoto.
Wakati nikiwa kijana kuna dada mmoja nilizaa nae mtoto mmoja halafu wa pili akachakachua - nilimwacha. Huyu nilifunga nae ndoa tuna watoto wanne sasa; sidhani kama ni rahisi kumuacha akichakachua wa tano.
Hivyo ukiamua kumuacha ni sawa na ukiamua kuendela kuwa nae ni sawa pia ali mradi akuonyeshe tabia zuri ili hilo lililotokea lionekane kuwa ni bahati mbaya.

Maskini.... Wanawake wengine wanapata waume wazuri wao wanageuka magodoro. Wanaume wanaopata wake wazuri waaminifu ni vise versa. Sijui Mungu ametuunganisha hasi na chanya ili tusaidianeje? Shukuruni kwa kila jambo. Ni msumari, lakini jipe muda wa kuumeza pengine utayeyuka. Duuuhhhhh!!!!

Maskini na wewe umeingia kwenye mtego one side story..lol

Alitakiwa kufanya juhudi zaidi ya kuzingizia hali ngumu ya uchumi kwenda kumpa huduma mamsap wake..

Tena usijaribu kumwacha mkeo, hata hao wanaokupa pole kwenye ndoa zao ni lazima kuna watoto wa nje kama si mmoja hata wawili kama unabisha kapime DNA, la maana wewe mlee huyo mtoto sawa na hao wengine, kwani wewe mimba ulizoziacha huko chuo ni nani anayezilea. Tulia mtoto wa kiume, tena hayo ni mambo ya siri sana kwenye kila nyumba. Utakuja kuoa mwingine ndo atakuletea makubwa zaidi ya hayo.

Wana,JF Naomba ushauri wenu.
Nilikuwa nimeoa na huyo mke nilikuwa nimezaa nae watoto wawili,nikapata nafasi ya kwenda kusoma hapahapa Tanzania,Mke wangu ni mwalimu wa shule ya Msingi,nilipokuwa chuo tulikuwa tunawasiliana vizuri,nilikuwa naendalikizo,lakini mara nyingi nilikuwa siendi likizo zote kwa sababu ya hali ya uchumi,na nilikuwa namwambia kwamba siendi likizo kwa sababu ya hali ya kiuchumi ambayo hata yeye alikuwa anaijua,nili kuwa namwambia ntabakia kwenye mkoa huu na kwa ndugu yetu ambaye na yeye anamfahamu,hadi namaliza chuo nikapata Temple ambayo ingeweza kutusaidia,kupata chakula,nikamwambia fanya utaratibu wa uhamisho,akasema sawa,badae siku hiyo hiyo usiku akanipigia simu akaniambia mimi ni sasa hivi ni MJAMZITO SI WEZI KUJA HUKO,Nikamuuliza umeolewa?akasema hapana,Tangu pale nikaona kuwa hatanifaa,watoto wako shule nina wahudumia mwenyewe nikimwambia changia shilingi elfu kumi,anakuwa mkali sana,tangu pale sikuwahi kumwambia chochote kuhusu watoto.
HADI HVI SASA HATUKO PAMOJA LAKINI YEYE ANATAKA TUSAMEHEANE NA TUISHI PAMOJA NIMEKATAA.
(NIMEONA NILILETE KWENU WADAU MNISAIDIE)

Mi nahisi hujatueleza ukweli wa hali halisi ilivyo, kuwa mkweli ili tukushauri vizuri! Hebu jibu maswali yafuatayo;
1. Mmefunga Ndoa ya aina ipi? (msikititini, kanisani,mkeka au bomani?)
2. Hujatembelea familia yako kwa mda gani kutokana na hilo tatizo la uchumi unalosema?
3. Sbb zipi zilikupelekea kushindwa kurud ilipo familia yako na kutafuta hiyo temple baada ya kuhitimuK?Kwa uzoefu wangu wanaume wanakuwa wepec sana kuwahukumu wake zao ili hali wanashindwa kuwahudumia ipasavyo.Haiwezekani kabisa umemaliza chuo bado unashindwa kuifuata familia yako ,huna uchungu kabisa na watoto wala mkeo, unategemea mwenzio aendelee kuishi pekeyake hadi lini?
Hebu jibu kwanza.

Pole sana bro but ktk upande mwingine ww ndie mwenye kosa uchumi ckigezo cha wewe kutorudi kwako! hapo akuna msaada zaid kutokana umeisha fanya uamuz wa kuachana.

Kwani kuoa kihalali nikupi Mtalingolo

Kihalali ni aje hebu nihabarisheni mwenzenu na amemwambia ushenzi huo nadhani kwa vile yuko mbali nae

kama mtu kishakaa nae na kuzaa nae watoto wawili huyo ni mkewe,,

Ingawa naona huyu mwanamke mwenzetu kicheche yaani kashindwa kumvumilia mmewe , kuna watu hawana hata mshipa wa aibu.

Pole sana nimekosa hata kusema
<br
aibu huwa sio kwenye kutenda,aibu huwa iko kwenye kujulikana.Hakuna binadamu ambaye hana siri yake,tatizo huwa linakuja siri inapojulikana.

Ni uzushi mtupu! hana ndoa huyo, walizashana tu, haiwezekani hata kidoogo

Back
Top Bottom