Mke wangu amenisaliti 'live', naombeni ushauri wenu tafadhali

pole sana mdau. Ila kwa mtazamo wangu naona haina haja ya kumpa talaka mkeo. Cha msingi tumia upole na umrudishe nyumbani. Mpaka akakubali kuolewa nawewe nikweli amekupenda, ila tamaa yawezekana zilimzidi, naye ni binaadamu. Usibadilike kwa chochote. Endelea na huduma zako na majukumu yako kama baba na muonyeshe upendo. Hapo atakuwa kapata fundisho
Na hiyo mashine iliyofumuliwa hadi imekuwa kama kopo na ku-expire ataifanyaje?? Hata hivyo huyo mfanyabiashara ana mtarimbo wa kutisha, hadi kufumua hiyo kitu!!!
 
Huyo ni mkeo kama kaomba msamaha msamehe ila mshauri mkapime afya(v.v.u), ni vyema ukafanya hivyo,pia ujaribu kufuatilia kama kaachana nae kweli asijie akawa ana kufariji.

ameshachovya peku,hivyo kama ilikuwa siku yake kaupata. From maternity leave mpaka kusaliti ndoa!! Huyo ni mzoefu yawezekana hata mtoto siyo wake. Umeshaibiwa in any way haitasaidia. Ukimuacha haisaidii, ukibaki naye haisaidii! Walimu wake wazuri sana lakini akirubuniwa na wajanja ni hatari sana.
 
pole sana mkuu.kwa sisi wanaume ni ngumu sana kusamehe na kusahau usaliti ,kwakweli kama huyo amekusaliti na ana mtoto mdogo wa miezi 6 hajaogopa hata kumuambukiza maradhi mtoto wako......kweli wahenga walisema "women are the weak creatures".mkuu hapo hata ukisamehe hamna ndoa kwakweli ,mwanaume haitakiwi kugundua mke wako amekusalit .....ikitokea umegundua ni kuachana tu ,kwasababu kumsamehe itakuwa ni kosa kubwa sana kwenye maisha yako.
 
Ndugu zangu wana JF,

Mke wangu ni mwalimu wa sec, ana mtoto mdogo wa miezi 6, toka ajifungue vituko vilikuwa haviishi....kuninunia daily sometimes hadi 3 weeks or mwezi. Nilipoona mambo yanazidi nilimrudisha kwao kwa muda kama wa mwezi mmoja hivi kwa sababu alikuwa ana maternity leave. Hata hivyo nilijua huenda postnatal period ndio inamfanya awe vile hivyo kwangu nikaona ni busara kuwa mpole ili kuepusha shari.

Aliporudi kutoka kwao tuliishi kwa maelewano mazuri kwa muda wa wiki moja tu, then yakarudi yale yale...ful mnuno kwangu lakini stori nyingi tu kwa mashost zake na majirani.

Mke wangu anafundisha kibaha, na tulikuwa tunaishi sote Dar sababu ndiko nilikojenga kibanda chetu cha kuishi na pia mimi ndiko ninakofanyia kazi. Mwezi uliopita nilishangaa mke wangu kuniambia kuwa yeye anataka kuhamia kibaha ili awe karibu na kituo cha kazi, pili ili aweze kupunguza gharama za usafiri za kila siku. Ikumbukwe kuwa ameanza kazi toka February 2011 na mimi siulizii mshahara wake anafanyia nini yeye ndiye ajuaye....but baada ya hoja yake hiyo nikajiuliza apunguze gharama za nauli....? je hela anafanyia nini? sikutaka ugomvi nikamruhusu lakini nikamuuliza vipi kuhusu maandalizi akasema kila kitu kipo sawa...chumba, kitanda+godoro na mahitaji mengine yote.

Ameondoka tarehe 04 June kuhamia kibaha, nikamwambia nitampeleka na gari hadi kibaha alikataa kata kata na kusema nimuache tu ubungo atapanda bus. Pia aka-haidi weekend atarudi lakini hakurudi na bila kutoa sababu. Ijumaa ya juzi amerudi home but still hakuwa mchangamfu, pia kuonekana kama ana chuki nami.

Kwa kuwa ni muda mrefu sijapata unyumba na yeye ndio mke wangu usiku wa kuamkia leo nikaomba haki yangu,.....WANA JF HAMUWEZI KUAMINI LAKINI NAWAAMBIA UKWELI....Nimekuta ikulu ya mke wangu imetumika kiasi cha kutosha saana hadi kiasi kwamba nilipatwa na mshangao wa ajabu....hiyo ilikuwa round ya kwanza, nilipojaribu ya pili...nilishindwa kumaliza game...coz sio K bali ni hatari. NILIUMIA SANA.

Toka saa 8.30 usiku sijalala hadi saa 10.30 usiku/alfajiri, niliamua kumuuliza tena kwa upole huku nimemkumbatia....kuwa huko kibaha ana wanaume ana-do nao!Alikataa kata kata....but alipoona naongea kwa upole sana akaingia kingi na kusena ndio anakiri ...lakini ni mwanaume mmoja tu ndio anatembea nae lakini sio wengi. Nikahoji ni nani huyo? nikaambiwa ni mfanyabiashara, anakaa kimara baruti, mmeanza toka lini mahusiano yenu....akasema toka...mwezi uliopita, mlifahamiana wapi.....tulifahamiana kwenye bus wakati naenda kazini.

Baada ya hapo akaanza kuliaaa.....na kusema anaomba nimsamehe!Nikamuuliza uliomba ruhusa ya kuhamia kibaha ili uwe huru? Je umekosa nini kwangu au mimi nilikuwa sikutoshelezi? akajibu hapana!

......WANA JF am so sorry kwa maelezo marefu but nimechanganyikiwa na simuelewi mke wangu. Anataka nimsamehe, but kabla sijachukua maamuzi nimeona ni vema niwashirikishe nyie ndugu zangu ili niweze kujiridhisha kwa uamuzi nitakao uchukua baada ya kupata maoni yenu.

NARUDIA TENA.....SAMAHANI KAMA MTAKWAZIKA KWA KUSOMA MAELEZO MAREFU...!

Ni mimi NGOSWE.120
Piga chini faster mkuu lol!
 
Hahahahaaa pole sana. Huyo mkeo wala hajakucheat bana. Toka lini wanawake wakacheat - hususan walioolewa? Wanawake walioolewa wanazithamini sana ndoa zao.

Tatizo unalo wewe mwenyewe. Hujiamini. Unawaza mabaya muda wote. Acha kuwa na mtazamo hasi na anza kuwa mtazamo chanya uone jinsi ambavyo mambo yatatengemaa.

Sidhani kama kama huyo mkeo anakucheat. Lakini hata kama akikucheat mara 2,000 wewe msamehe tu bana. Kwani akikucheat mara 2,000 ndo nini bana? Wewe samehe tu msonge mbele na maisha yenu.

Pole lakini.
 
Ndoa ngumu, ukiona mwanaume katulia basi mke wake anakuwa malaya mbwa, hivyo hivyo ukiona mwanamke katulia utaona mwanaume ana lundo lukuki la nyumba ndogo.
 
Pole sana kaka, tatizo hapa ni athari za uamuzi wowote utakaochukua-ukimsamehe na mkaendelea kuishi pamoja ikitokea kuna siku kakosea au headmaster kam-boa kazini karudi kanunu akili yako itakutuma kuwa ni jamaa wa kimara bado yupo! Ukimuacha, utaoa mwingine, huna guarantee atakuwa wa namna gani. Pima uzito wa Pros and Cons!
 
Don't give her 2nd chance. Just kick her out. Huyo jamaa yake anaweza kuwa alikuwa anapiga Tigo. She isn't worth any mercy.
 
[h=2]HEBU PITIA NA HAYA YATATUSAIDIA KUTAFAKARI KWA MAKINI, KUJUA WAPI TULIPOKOSEA NA KUCHUKUA UAMUZI SAHIHI.

Ndoa[/h] Je! Bibilia ya funza nini kuhusu ndoa?. Imeandikwa, Mathayo 19:5-6 "Asema kwasabu hiyo mtu atamwacha babye na mamaye ataambatana na mkewe na hao wawili watakua mwili mmoja? hata wamekua si wawili tena bali mwili mmoja basi aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe."


Je! waume wawatendeaje wake zao?. Imeandikwa, Waefeso 5:25-28 "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wal kunyazi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume na kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe anaipenda nafsi yake mewenyewe."


Waume wa waheshimu wake zao. Imeandikwa, 1Petro 3:7 "Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kupa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu, na kama waridhi pamoja wa neema ya uzima kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe."


Je wake nao wake na waume zao vipi?. Imeandikwa, Waefeso 5:22-24 "Enyi wake watiini waume zenu kama kutii Bwana wetu kwa maana mume ni kishwa cha mkewe kama Kristo naye nikichwa cha kanisa, naye nimwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo."


Je inamaanisha ya kuwa wake wafanye kila jambo? Asha!. Imeandikwa, Waefeso 5:21 "Hali mnanyenyekea katika kicho cha Kristo."


Je tumeagizwa kutoa kupigana kwa mke na mme. Imeandikwa, Wakolosai 3:19 "Ninyi waume, wapendeni waume zenu, msiwe na uchungu nao."


Kuwa na ndoa njema nivema kutatua mafaragano au kutoelewana mara moja. Imeandikwa, Waefeso 4:26 "Mwea na hasira ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka."


Fanya ndao yako ikuwe kwa umoja na kuelewana. Imeandikwa, Waefeso 4:2-3 "Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja kwa Roho katika kifungo cha amani."


Je! watu wapaswa kuiona vipi ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwa maana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu."
 
DUH aisee pole sana..
ninaweza kusema labda umri wake bado mdogo au ni tabia za ukahaba tu anaweza kuwa nazo..
tatizo may be linaweza kuwa linasababishwa na kuoana ili mtimize jukumu tu kwa kuwa umri ulikua umefika ila kimsingi wewe au yeye alikua hajakomaa kwa ndoa... inabdidi uvumilie kwa muda ila mambo yakiendelea kuwa hivi hivi ...akili ku mkichwa brother
 
mmh pole aisee!
lakin kwa haraka haraka ni wewe mwenyewe umepelekea mambo kuwa ivyo mkuu!
embu man up na ufanye mabo yako kiume zaidi jaman!
 
mmh pole aisee!
lakin kwa haraka haraka ni wewe mwenyewe umepelekea mambo kuwa ivyo mkuu!
embu man up na ufanye mabo yako kiume zaidi jaman!
Huyu bwana hajapelekea kutokea kwa hii kitu ila ni mwanamke mwnyw alijisia kufanya ivo. Hata ingekua mm siwez kaa na mwanamke afu haishi vituko kila kukicha asa itakua haina maana ya kukaa pamoja kama mke na mume. Na hiyo situation ya kumruhusu kwenda kukaa kibaha hata angemuacha Dar ila bado kama alikua amepania kucheat ingekua hivyo tu. So jamaa naona ni innocent kabisa na mwanamke inabd ajisepe.


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Pole sana ndugu yangu.Tukubali au tukatae,tuna tatizo kubwa sana la uhusiano,tusipokua siriaz yatatupata makubwa. . . . .
 
Mambo kama haya yanaumiza roho. Lakini mara kadhaa yanatokea kutokana na makosa yetu sisi wenyewe wanaume. Nafasi yetu ya uongozi katika familia hatuifanyii kazi ipasavyo. Kwa lugha nyingine hatumizi wajibu wetu inavyostahili.

Hata babu zetu adamu na eva waliingia kutenda dhambi inayotugharimu hadi leo kwa sababu ya kutengana tena kwa muda mfupi tu ndani ya bustani ya eden.

Ni kweli kwamba baadhi yetu tunaingia kwenye ndoa bila kupata mawaidha ya kutosha kutoka kwa wazee, dini zetu au watu mbalimbali wenye uzoefu wa kutosha juu ya namna ya kenenda katika maisha ya ndoa.

Ni vizuri kupitia semina kadhaa kabla ya kuanza maisha ya ndoa. Hata mawaidha ya baadhi ya wana jf yanafaa sana
 
Hahahahaaa pole sana. Huyo mkeo wala hajakucheat bana. Toka lini wanawake wakacheat - hususan walioolewa? Wanawake walioolewa wanazithamini sana ndoa zao.

Tatizo unalo wewe mwenyewe. Hujiamini. Unawaza mabaya muda wote. Acha kuwa na mtazamo hasi na anza kuwa mtazamo chanya uone jinsi ambavyo mambo yatatengemaa.

Sidhani kama kama huyo mkeo anakucheat. Lakini hata kama akikucheat mara 2,000 wewe msamehe tu bana. Kwani akikucheat mara 2,000 ndo nini bana? Wewe samehe tu msonge mbele na maisha yenu.

Pole lakini.
Angalau wewe umetoa ushauri wenye logic, personal mimi huwa siwazi haya mambo ya cheating, sometime the way you think is Problems.

Ila hapa mleta mada atakuwa ametenda haki kama atatueleza umri wake na umri wa mwanamke, au yatosha tu akitueleza umri wa mwanamke. Umri ni alama tosha sana kupata tafsiri ya mtu ni wa category gani, kwa sababu hata mimi binafsi kuna madudu niliyoyafanya miaka 10 iliyopita leo hii siwezi kuthubutu kufanya madudu hayo. am matured.
 
Angalau wewe umetoa ushauri wenye logic, personal mimi huwa siwazi haya mambo ya cheating, sometime the way you think is Problems.

Ila hapa mleta mada atakuwa ametenda haki kama atatueleza umri wake na umri wa mwanamke, au yatosha tu akitueleza umri wa mwanamke. Umri ni alama tosha sana kupata tafsiri ya mtu ni wa category gani, kwa sababu hata mimi binafsi kuna madudu niliyoyafanya miaka 10 iliyopita leo hii siwezi kuthubutu kufanya madudu hayo. am matured.

Vyovyote vile mimi siamini kama mwanamke mwenye ndoa anaweza akatoombesha nje. Haiwezekani kabisa. Na hata kama akitoombesha huko nje mpango mzima ni kusamehe tu kwa sababu ukimuacha utaacha wangapi sasa...? Dawa ni kusamehe saba mara mia saba.
 
Mkuu, pole sana. Photocopy ya yaliyowahi kunikuta. Ni PM nitakujulisha zaidi.

Solution:

1. Kama unampenda pata undani ujue ni nini kilipelekea hayo yatokee.
2. Ukiona yuko Genuine msamehe na pia saidianeni kuondoa hayo mapungufu
3. Mrudishe DSM. Distance kills relationship
4. Kapimeni HIV, rudieni after 3 months
5. Counter check loopholes za yeye kurudia tena kitendo hicho.
6. Forget the past Mpende, Mjali na Mtunze.
7. Jichunguzxe mapungufu yako katika ndoa, na jirekebishe

Anaweza akarudia, msamehe tena ila shirikisha mtu wake wa karibu. Akirudia tena, shirikisha tena mtu wake wa karibu.

Akiruduia bado mpe uhuru wa kuishi maisha atakayo. Atakuumiza kichwa. Ila Mwombee na Mjali maana ni Mzazi Mwenzako.

The thing is relationship za miaka ya siku hizi zina uzinzi sana. And am pretty sure hata wewe umeshafanya kama hujafanya kinachokosekana ni chance na opportunity tu. Sishabikii Unzinzi bali nazungumzia reality and I can give 100+ examples.

Huwezi kuacha mke kwa kosa moja la Uzinzi. Ni PM nitakushauri zaidi.

Meanwhile, cool off. Stay focused. Unaweza ukajitenga naye hata wiki ili upate muda wa kutafakari.
 
mmmmmh.....! how can u know kwamba K imetumika jamani?
pole kwa yaliyo kukuta, msamehe pia na ujenge familia
 
Vyovyote vile mimi siamini kama mwanamke mwenye ndoa anaweza akatoombesha nje. Haiwezekani kabisa. Na hata kama akitoombesha huko nje mpango mzima ni kusamehe tu kwa sababu ukimuacha utaacha wangapi sasa...? Dawa ni kusamehe saba mara mia saba.
Whatsoever mimi sina muda wa kumchunga na kumchunguza binadamu mwenye akili zake timamu, huu ndio msimamo wangu, i will play my part kama the head of the House, lakini mengineyo yapo ndani ya binadamu mwenyewe.

Lets say wewe ndio umemuoa Lulu, au Wema Sepetu, haya si ni matatizo ya kujitakia? hawa kina Lulu na Wema Sepetu wapo kila ngazi tofauti ni kwamba tulionao wengine si maarufu, jiulize na waulize wafugaji wote hadi wale wanaofuga Fisi je kuna aliyewahi kufanikiwa kumfuga kunguru!?....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom