Mke wa Rais ana madaraka gani hapa nchini?

Wakuu, leo (7/10/2011) mchana nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa marafiki zangu ambaye ana taasisi ndogo ambayo wiki chache kutoka sasa itakayosherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa. Akanijulisha kuwa kwa sababu inashughulika na masuala ya wanawake aliona vyema kumwalika Salma Kikwete kama mgeni rasmi.

Kilichonistaajabisha ni kwamba alipowasiliana na ofisi yake moja ya masharti aliyopewa ya mama huyu kuhudhuria ni kwamba lazima DC aalikwe pamoja na watu wengine wawili watatu wa kiserikali.

Swali ni je, katiba, sheria na itifaki zinasemaje kuhusu jambo la namna hii? Isitoshe huyu mama anaendeshwa kwenye msafara na gari yake ina ngao ya nchi wakati hana mamlaka yoyote yanayompa haki ya kutumia ngao.

Naomba kuwasilisha.

Swali hili linaweza kuulizwa na mtu mbumbumbu tu!
 
post yako ina chembe chembe za udini

Mkuu Mpuuzi wakati naandika hiyo post sikuwa na hisia zozote za kidini na sina chembechembe za kidini. Nimeandika hayo majina nikiwa na maana ya wafanya biashara wakubwa hapa TZ ambao hutoa misaada mbalimbali kwa watanzania wenzao.
 
Back
Top Bottom