Mke wa rafiki yangu anasumbuliwa na mumu wa mtu

Zambavuni

Senior Member
May 24, 2012
118
26
Hello wana JF.
Nina rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nchi ya jirani anasoma. Amemuacha nyumbani mke wake na watoto wao watatu. Mke wake ni mama wa nyumbani na anashughuli zake za kujiongezea kipato. Ni familia yenye upendo na wote mme na mke wanapendana sana. Tatizo kwa sasa ni jirani yao mmoja, mme wa mtu anayemnyemelea huyo mke wa rafiki yangu. Anakaa standby akichungulia dirishani, mke wa rafiki yangu akienda dukani hilo jamaa linamfuata nyuma na kumtongoza, akielekea sokoni, jamaa hilo linawasha gari haraka lina pretend kumpa lift. Mke wa rafiki yangu a.k.a shemeji hamfichi mme wake anamwambia kila kitu maana anapatikana kwenye simu. Hilo dume limekuwa kero kwa shemeji. Sasa rafiki yangu kaniomba ushauri afanye nini? Nilichomshauri ni ampigie huyo jemba aache kumfuata mke wake maana ana namba yake ya simu. Sasa ninaileta issue hii kwenu wana JF nikiomba maboresho ya nini kifanyike kumstopisha huyo fara.
 
dah
huwa nawa admire sana wanaume ambao hata akijua unamtongoza mkewe
hakwambii kitu kabisa
ni kimyaa mpaka unajiuliza kuna nini?

with women usipeleke kimbelembele kumuonya kidume
ukaja kurahisisha kazi kabisaa
 
Kwa hiyo unashauri jamaa akae kimya?
 
Mambo ya kutongozwa yanamhusu mke.Mke nae si binadamu?Si anaweza kujiongoza?Sasa huyo mume yanamhusu nini?Amwache mkewe adeal na ishu hiyo.Mwanamke sio gogo mpaka aamuliwe cha kufanya,ebo!
 
Mambo ya kutongozwa yanamhusu mke.Mke nae si binadamu?Si anaweza kujiongoza?Sasa huyo mume yanamhusu nini?Amwache mkewe adeal na ishu hiyo.Mwanamke sio gogo mpaka aamuliwe cha kufanya,ebo!

Mume yanamhusu kwa sababu ni mke wake. Pia inategemea aina ya wanawake. Yule shem shari haziwezi.
 
Inaonyesha huyu mwanamke hajui kumkatalia mwanaume! Hivi wanaume wote wanaomtongozaga huwa anamwambie mumewe awakanye? au tangu aolewe huyo ndo mwanaume wa kwanza kumtongoza?
 
Pamoja na wasiwasi wangu nilioonyesha hapo juu, ngoja nikwambie rafiki yangu alivyofanyaga miaka hiyo and it worked out, kwani tukio ni exactly the same.

Baada ya mkewe kumwambia taarifa hizo, jamaa (mwenye mke) aliamua kumpigia boss wake kazini na kumwambia mwanzo mwisho, halafu akamuomba huyo boss ndo amuonye huyo 'mbaya wake'. Ilikuwa bonge la aibu na jamaa akatia heshima hadi leo! Bahati nzuri wote walikuwa wanafanya kazi sehemu moja so it worked out easily!

Kwahiyo na yeye anaweza akafanya the same, Au kama vipi amtumie mtu mwenye heshima zake ndo amuonye huyo mwizi wake.
 
Sijaelewa kitu hapa .......Huyo mama hana mdomo, mke wa rafiki yako naye huwa anakubali lift?angeweka sura ya nguchiro mara mbili tu asingerudia kumfuata .....:wacko:mulika!

Hii ni dozi tosha kabisa umemalliza, vinginevyo huyo mwanamke anafurahia kunesa kwenye gari
 
Nimekupata mito. Vipi mwenye mali akiamua kumstopisha huyo jamaa kwa simu itakuwa na madhara?
 
wanamme wengine mabushoke!!

Mkeo anatongozwa anakuja simulia? Na akikubali aje asimulie.

Yeye huyo mke hajui la kufanya? Kabla hajaolewa alikuwa haotngozwi?

Ina maana aliwakubali wote walomtongoza kabla hajaolewa? Nani alikuwa anamjibia maana hakuzaliwa na mme?

Kilaza tu huyo shemejio
 
Hii ni dozi tosha kabisa umemalliza, vinginevyo huyo mwanamke anafurahia kunesa kwenye gari

Kuvaa sura ya nguchiro hilo nimelikubali laweza leta mabadiliko. In fact hajakubali kupanda gari lake ila jamaa ndilo analombambaisha nalo. Jingine dada?
 
Kilaza fine! Nini kifanyike katika ulaza huohuo?
wanamme wengine mabushoke!!

Mkeo anatongozwa anakuja simulia? Na akikubali aje asimulie.

Yeye huyo mke hajui la kufanya? Kabla hajaolewa alikuwa haotngozwi?

Ina maana aliwakubali wote walomtongoza kabla hajaolewa? Nani alikuwa anamjibia maana hakuzaliwa na mme?

Kilaza tu huyo shemejio
 
Mume yanamhusu kwa sababu ni mke wake. Pia inategemea aina ya wanawake. Yule shem shari haziwezi.

Yanamhusu kwani katongozwa yeye?Mwanamke ni binadamu kamili anajua cha kuamua sio mpaka mumewe amuamulie!
 
Amfundishe mkewe kukataa na trick za kutimua watu kama hao..Nachelea kusema huyo mwanamke ni wa aina yake...Kama yeye mwenyewe mtu mzima hajuhi kutimua mtu basi kazi ipo...

Na nataka kuangalia upande wa pili wa shilingi... sawa jamaa hajatulia..ndio...lakini mi navyowajua watu wasiojua kutimua wanaume atakuwa anampa signals ambazo zina read nataka... ndio maana anamfata bila kuchoka.

Nakumbuka those days nikiwa kijana mtu akinifata mara ya kwanza namjibu vizuri tu kuwa asante kwa kunipenda (maana kupendwa ni heri) lakini samahani siko interested. Kesho akinifuata tena akyanani siongei kitu wala kumwangalia simwangalii mwenyewe atajiona chizi harudi tena...Wanaume ukianza kujibishana nao mbona watakushinda... ooh mimi mke wa mtu... ataanza... hata mimi mbona nina mke. Hakuna discussion kuna watu wana 'A' za ku argue. Ni kujifanya bubu na kumfanya watu wamuone chizi anaongea peke yake. Ina work sana.

Inaonyesha huyu mwanamke hajui kumkatalia mwanaume! Hivi wanaume wote wanaomtongozaga huwa anamwambie mumewe awakanye? au tangu aolewe huyo ndo mwanaume wa kwanza kumtongoza?
 
Hello wana JF.
Nina rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nchi ya jirani anasoma. Amemuacha nyumbani mke wake na watoto wao watatu. Mke wake ni mama wa nyumbani na anashughuli zake za kujiongezea kipato. Ni familia yenye upendo na wote mme na mke wanapendana sana. Tatizo kwa sasa ni jirani yao mmoja, mme wa mtu anayemnyemelea huyo mke wa rafiki yangu. Anakaa standby akichungulia dirishani, mke wa rafiki yangu akienda dukani hilo jamaa linamfuata nyuma na kumtongoza, akielekea sokoni, jamaa hilo linawasha gari haraka lina pretend kumpa lift. Mke wa rafiki yangu a.k.a shemeji hamfichi mme wake anamwambia kila kitu maana anapatikana kwenye simu. Hilo dume limekuwa kero kwa shemeji. Sasa rafiki yangu kaniomba ushauri afanye nini? Nilichomshauri ni ampigie huyo jemba aache kumfuata mke wake maana ana namba yake ya simu. Sasa ninaileta issue hii kwenu wana JF nikiomba maboresho ya nini kifanyike kumstopisha huyo fara.

" Na atakayekuwa hajawahi kufanya tukio hilo awe wa kwanza kumpiga mawe "
 
Back
Top Bottom