Mke wa pili kisirani.

promiseme

JF-Expert Member
Mar 15, 2010
2,707
931
Mambo waungwana?
Mwenzenu nna ka mtihani,nna shoga yangu nikonae kama ndugu,alipata bwana kwenye FB
Mapenzi yaka dumu kwa miezi 5 wakamua kufunga kutaka kufunga ndoa shost wangu ndio
Mara ya kwanza anaolewa,alipokuja kuni shauri nikawanamjua bwana anaetaka kumuoa
Nikamwambia bora asubiri ili amsome vizuri huyo jamaa kwani huyo bwana yeye atakua mke
wa 5 kuolewa nahuyo bwana anapenda sana wanawake wanaojitegemea ili na yeye ajipatie
mteremko,shosti wangu kumwambia hivyo alinisomea nakunambia simtaki mema huyu bwana
watu wanamtia ila tuu mimi nilikua najua wewe mwenzangu nakuelezea dhiki na raha zangu
kumbe ni adui yangu lohh amakweli mfadhili mbuzi binadamu atakuudhi na maneno kibao,

akaenda kuolewa, na huyo bwana akamwambia kama mie namtaka yeye nilisha wahi kumtongoza
akaanza kunitumia sms za mafumbo nikamuona kama chizi sikumjibu,leo kaja nakilio bwana kamla
senti alokua nazo nyumba amepewa siku 7 inapigwa mnada gari kaenda kuichukulia mil 20 bank
biashara anawakopesha wanawake zake wamegombana mume kwambia sikutaki kampata mwengine
nimemwambia alale kwanza manake kachafuka kamasi uso mzima na hata lakumwambia sijui nianzie
wapi tangu awena huyu bwana ni miezi 18 alikua akiniona sehemu anatema mate mwisho saloon
nikimkuta aampigia cm mume baby ebu njoo unichukue upesi kuna kituko hapa ntatapi sasaivi,
leo hii waungwana nauliza hajaona pakwenda? au akikakwangu hatotapika? ebu naombeni ushauri wenu
sijui nianzie wapi manake kama asira sasa zamu yangu...
 
msamehe amejifunza,ila kuwa careful naye asije akakutapeli na wewe,mpe sehemu ya kupumzika kwa sasa kula naye,lala naye, zaidi ya hapo akikuomba hela usimpe lol,kaa naye kimachale anaweza akawa hajaachana na huyo bwana au kalizwa na yeye roho ya ubinadamu imemtoka..akakuliza na wewe,lol
 
hamna nukta wala mkato, imeniwia vigumu kuifuatilia hii habari
 
Sidhani kama hapa ni sawa kuyaleta hayo, usimsimbulie mwenzako, mapenzi ni upofu.

Gari aliyoikopea millioni 20 ni ya aina gani?
 
Aisee, hii inatisha. Pole na msamehe, hadi kuja kwako maana yake anakutegemea maana kwa aliyokutenda, wewe ungekuwa mtu wa mwisho kukuletea kilio chake!

Men men men, nasi wadada tunapaswa kuwa careful sana na hawa wanaume wa siku hizi!
 
hapo ndiyo FB inapowatoa watu ushamba... na kwa ulimbukeni huu wataendelea kulizwa sana
 
mwambie aende kwa ndugu zake akalie huko as wewe huna cha kumsaidia. sio nduguyo huyo badae atakuaribia maisha kwa wivu, achana nae.
 
Aisee, hii inatisha. Pole na msamehe, hadi kuja kwako maana yake anakutegemea maana kwa aliyokutenda, wewe ungekuwa mtu wa mwisho kukuletea kilio chake!

Men men men, nasi wadada tunapaswa kuwa careful sana na hawa wanaume wa siku hizi!

kaunga shost upo? nimekumic
 
mmhh hatari. huyo shosti wako saivi ndo kaja kuomba ushauri pale mwanzo alikuja kukualika harusi tu mamuzi ya kuolewa alikuwa tayari anayokichwani mwake..
duniani kuna watu wa ajabu lkn, unawezaje kumtukana rafiki au ndugu yako hivi hivi
 
Back
Top Bottom