nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,369
Pole sana dada. Na mara nyingi wanaopata laana za kuvunjika ndoa ni wanaume kwa sababu wao kama kichwa ndio chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika. In most cases women move on na maisha yanakuwa pouwa kuliko hapo awali. Mungu anawaadhibu hawa kaka zetu kwa tamaa zao za dogo dogo na kukubali kusambaratisha familia zao.
Kwa wanawake wengi waliotoka kwenye ndoa naona mambo yao si mabaya.
Kwa wanawake wengi waliotoka kwenye ndoa naona mambo yao si mabaya.
Yaani kaka ram unayosema ya dada yako yamewafika wengi mmoja wapo ni mimi hapa ninayeandika hapa. Yaani kuachana na mume /mke wa kwanza mara nyingi ni laana maana Mungu mwenyewe alisema kwenye BIBILIA nachukiia kuachana kwenu. Mimi niliolewa kwa ndoa ya Kanisani tumekaa kwa amani miaka 3 ule wa nne maneno yalianza tokea kwa ndugu wa mwanaume "hazai , hazai" nasikia alikuwa malaya. Mimi nikasikitika sana kwamba maisha yangu nilitulia na kufundishwa na wazazi kwamba nikiguswa guswa na wanaume nitpata ujauzito. Kwahiyo nikasoma nikamaliza bila kuguswa mpaka nikaolewa. Laajabu miaka 4 imepita hakuna mtoto, na mwenzangu kwa vile makabila ni tofauti akaanza kuletewa maneno ya uongo akayasikiliza mpaka mwaka wa 5 tukatengana hakuna chakula hakuna matumizi ni mimi kila kitu mpaka nikaanza kupigwa bila sababu basdaye nikajiondoa baada ya kipigo kikubwa cha mwisho. Kwa ufupi mwenzangu alikuwa na msichana mkerewe walikuwa naye siku tele zilizopita. Basi wakakaa sana wanafanikiwa tu mimi maisha yangu yalikuwa kawaida tu. Mpaka siku moja nikaamua kufungua case mahakani baada ya kugundua kwamba waliisha funga ndoa Bomani. Case ikanguruma akaulizwa umefungaje ndoa na huku una ndoa nyingine?. Akafanya mipango case ikahamishiwa ADR Kisutu yaani mimi through wakili wangu alihongwa hela akasaini case iende kuvunjwa.....
Case ikavunjwa bila hata kusikilizwa neno lolote nikalia mahakamani wenzangu walikuja wamekamatana kama kumbi kumbi mahakamani wananicheka. Basi nikaambiwa halali yako mama ni laki 5, mwenzako atapata wapi hela za kukupa?. Nikasema mimi sichukuwi hizo hela nikatoka mahakamani nikaacha hata kufuatilia tena talaka na wakili wangu alisaini kila kitu kwa niaba yangu.
Baada ya miaka 3, aliyekuwa mume wangu na mkewe wote waliachishwa kazi wakahama hapa mjini wakenda nje ya Dar karibu ma Moro huko wanalima na kuleta mazao kwa biashara hapa mjini. Mnamo mwaka 2004, aliyekuwa mume wangu alituma rafikye akiniomba nimsamehe maana kila anachofanya hakifanikiwi.......
Ndoa ni moja ila kuna zingine unashidwa inabidi uvunje ila ukivunja ndoa hakikisha huna makosa la sivyo utakiona cha mtemakuni.....