Mke wa mtu sumu, huyu nae vipi?

Buto

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
249
29
Habari zenu wana Jf: Kuna rafiki yangu alikuwa na mpenzi wake tangu mwaka 2007 na walipendana sana na walikuwa na mpango wa kufunga ndoa 2012. Ilipofika mwaka 2010 mpenzi wa rafiki yangu (shemeji) alianza mahusiano na mtu mwingine na kwa kuwa penzi halina halifichiki rafiki yangu akaja gundua kuwa mpenz wake anamchit na baada ya kumbana akakubali kuwa ametenda kosa ila jamaa ameahid kumuowa ila bado ana mapenz kwa boyfrnd wake wa zamani.

Ikafika kipind yule msichana akahamia kwa yule jamaa aliyemwambia kuwa atamuowa na wakati huo huo akawa bado anaendelea kutoka na rafiki yangu. Ijumaa ya tarehe 7/10/2011 rafiki yangu aliitwa na huyo mpenzi wake na kumwambia kuwa jpili ya tarehe 9/10/2011 ndio siku ambayo atakuwa anaolewa na huyo jamaa anaye kaa nae ila akamwambia rafiki yangu kuwa "JAPO KUWA NAOLEWA ILA BADO NAKUPENDA NA NAKUHITAJI" Naomba mnisaidie ili niweze kumshauri rafiki yangu maamuzi ya kuchukuwa katika hili jambo
 
Rafiki yako pamoja wewe sijui mnasubiri nini? Mnaendelea kujidhalilisha sana, hivi kweli nawewe unafurahia hiyo hali? Huoni ubaya wowote au jamaa kafika haambiliki? Msaidie rafiki yako mkuu, hapiness in love is not about forcing someone to be with you, its about something natural! kinakuja tu baada ya kuchambua pumba na mchele.
 
Rafiki yako ni bei poa......................kwa hivyo hashangazi............maana hajithamini hata chembe.........kwa namna hii hakuna atakayemthamini......
 
Rafiki kashushwa kutoka kuwa mpenzi hadi kuwa kidumu na akakubali....?
Nakataa kuamini kama kuna binadam wa aina hii.
 
Kama utani vile but haya mambo yapo... NASIKITIKA tu kwamba yupo kuomba ushauri ina maana ana consider kuendelea na huyo mtu hata baada ya ndoa... Kwamba anaweza jishusha thamani kiasi hicho?? Kweli anatia huruma.
 
Za style hizi mbona zipo nyingi tu, sio kwamba nazishabikia ila zipo na tunaziona, unakuta mwanamke/mwanaume anaoa/anaolewa na bado anaendelea kutoka na bf/gf wa zamani. Ni makubaliano tu na masuala ya kupenda kubadilisha mboga.
 
hivi mkuu hapo unahitaji ushauri wa nini??? kama mtu anakuambia ana mahusiano na mtu na ameahidiwa kuoelewa sasa hapo unashika pembe za nini au unataka ushauriwe nini?? maana hii ni jokes watu hatuwezi kushauri kwenye ujinga ...

kwa kifupi kamchape makofi aamke maana akili yake imelala
 
Hana haja ya kuendelea nae kwa kuiba. Atulie na atafute wake kuliko kung'ang'ania huyo anayeolewa.
 
hivi mkuu hapo unahitaji ushauri wa nini??? kama mtu anakuambia ana mahusiano na mtu na ameahidiwa kuoelewa sasa hapo unashika pembe za nini au unataka ushauriwe nini?? maana hii ni jokes watu hatuwezi kushauri kwenye ujinga ...

kwa kifupi kamchape makofi aamke maana akili yake imelala

Haya bwn!.
 
Sijaelewa au hiyo ndio inayoitwa 'love is blind'....huyo rafiki yako akapime afya ya akili kwanza
 
mwambie aendelee na huyo mtarajiwa wake, ungekuwa wa muhimu kwake asingekuacha shauri ya ndoa tu, sasa na ww ulipoona hivo si ungetangaza ndoa kama unampenda kiasi hicho?
 
Ni wazi kuwa huyo rafiki yako si mwaminifu na hana tena mapenzi ya dhati na huyo anayeishi naye! Ningelikuwa mimi ni wewe ningemshauri aendelee na Boy friend wake mpya kuliko kuolewa na kuendelea kutembea nje ya ndoa, hu ni uzinzi na kukosa adabu ndani ya ndoa! take care!
 
Safi sana! Mwambie aendelee kulazimisha hivohivo asiuache upendo wake kwa huyo mdada upotee bure bure na kadri siku zinavyokwenda ndivyo atakavyokuwa anazidi kuumia na ndipo ataanza kujiset mdogo mdogo then atajiengua mwenyewe!!
 
Kama utani vile but haya mambo yapo... NASIKITIKA tu kwamba yupo kuomba ushauri ina maana ana consider kuendelea na huyo mtu hata baada ya ndoa... Kwamba anaweza jishusha thamani kiasi hicho?? Kweli anatia huruma.

Za style hizi mbona zipo nyingi tu, sio kwamba nazishabikia ila zipo na tunaziona, unakuta mwanamke/mwanaume anaoa/anaolewa na bado anaendelea kutoka na bf/gf wa zamani. Ni makubaliano tu na masuala ya kupenda kubadilisha mboga.

nakubaliana na hizi hoja kuwa haya mambo yapo

sana sana yanatia nguvu hoja kwamba sio wote wanaolewa eti kwa mapenzi yao wenyewe...kuna vitu vingine ambavyo kwa bahati mbaya vinazidi msingi mkuu wa ndoa ambao ni mapenzi

huyu naona mapenzi yako kwa BF, ila ndoa ipo kwa mtu mwingine...what a mix but yapo na tunayaona

Mimi namsifu rafiki yako for hata baada ya kujua kuwa amemcheat, bado anaendelea naye. Owrst case scenario, huyo rafikio atakapokuwa na mpenzi mwingine.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom