Mke wa Lowassa azindua kitabu

Wakulu tujihadhari na paka aliyevaa tasbii ya dagaa ili kutuzuga kwamba sasa hakamati panya!
Tunataka hao maaskofu watoe tamko juu ya kile kiwanja cha kanisa aichokipora muheshimiwa kule Mbezi Beach alipokuwa Ardhi!

hahahahaha hehehehehe bah hahahaha
tasbihi ya dagaa? imeniwehusha sana hiyo.
Nilipokuwa mdogo shuleni nilianza kusikia makashfa kibao ya huyu white head ila nilijua kuwa ukiwa kiongozi shurti ukashifiwe na wasiokupenda, nilivyopanda vidato nikaja kugundua kuwa si kashfa ni ukweli mtupu ila kwa kuwa TIS na idara zingine walikuwa bize na mambo mengine walishindwa kufanyia kazi suala la ubadhirifu wa huyu mtwana na washkaji wengine.
Sasa ameinunua idara karibu nusu nzima na usikute analindwa na hao hao kwa kuwa ni potential kiongozi (wa wizi)
 
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.[/COLOR]

Hongera kwa kumgeukia Mungu, lakini imeandikwa "Anayetaka kunifuata ajikane nafsi yake, abebe msalaba wake na kunifuata." usipofanya hivyo, unaweza kuwa umegeuka upande wa Mungu lakini haujamuona
 
Hongera kwa kumgeukia Mungu, lakini imeandikwa "Anayetaka kunifuata ajikane nafsi yake, abebe msalaba wake na kunifuata." usipofanya hivyo, unaweza kuwa umegeuka upande wa Mungu lakini haujamuona

Mkuu ayakane mabilioni hayo thubutu....mtamsubili sana mzee nywele nyeupe.
 
Unanikumbusha andiko jingine mkuu... 'Jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia mbinguni....'

Unajua mafisadi wanajua kuwa hata waibe vipi wakitoa zaka na matoleo mengine kanisani basi huweka hazina mbinguni.... Mungu hapokei fedha za wenye dhambi na ahongeki.
Kiama chao ki karibu kama si leo basi kesho
 
Kama kuoga ni usafi basi hakungekuwa na haja ya kufua taulo............,Pg 15 maaskofu nchi nzima kuisafisha familia chafu.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

Hii ni kauli ya hatari sana kutoka kwa kiongozi wa kidini. Kwa literal interpretation anatuambia mafisadi wakiiibia nchi tunyamaze. This is very dangerous!
 
Usema kweli mimi namepata hamasa na uandishi huo wa Mama Regina. Mwenye Kitabu hicho afanye scanning tuweze kukisoma! Mpaka nitakaposoma ndio nitatoa maoni yangu, lakini kwa sasa, nampa hongera mama kwa kuamua kuweka mawazo yake hadharani badala ya lowassa mwenyewe. I wonder weather it is a political strategy, or it simply a crying heart of a woman!
 
Kitu kinachosikitisha sana ni kwamba eti aliandika kitabu baada ya "kupata misukosuko"!! Misukosuko my a.. !!Aende kutembelea Mwananyamala hospitali akaone akina mama wamejifungua bila msaada wa nesi na kulala kwenye sakafu na vichanga vyao as a result of ufisadi wao, then atajua msukosuko ni nini!! Ushauri wa bure, ni dhahiri hamtafunguliwa mashitaka na serikali hii, mmeiba vya kutosha, go home enjoy your pension, and pls do not rub salts in our wounds !! As for our church leaders, credibility inashuka kila siku, hawa ni tabaka tawala lingine.
 
Kwani ajabu ni ipi hapa?

PENGUIN wanapenda PESA kama nini. Na wanajuwa kuzinusa vibaka wale? Wala vitu vya bure, utawaona na MAJOHO yao na kifuani meupe (Penguin) na mzinga wa li-blingbling wameninginiza kifuani na pete la nguvu.

Kama walimkaribisha hata Rostam Aziz, itakuwa Lowassa? Na kumbuka Arusha/Moshi huko pesa inapendwa kabla hata hawajazaliwa. Sasa akija kukua na kujua zaidi utamu wa hela na wapi zipo, hata kama atakuwa kazileta Marlin Manson au zungu la unga, watazipokea. Mbona Italy siyo big deal kabisa Penguin na Mafia ni DUGU MOJA.
 
Pg 15 maaskofu nchi nzima kuisafisha familia chafu.

Maajabu ati pg 15 kitabu,kwa nani anashindwa kuandika kitu cha page 15? Hata ukimwambia sasa hivi mtoto wa secondary akuandikie insha ya 15 pgs anaweza,nawashangaa sana hawa maaskofu kushabikia vitu visivyokuwa na maana,hivi si ni maaskofu hao hao walikua wanapinga ufisadi au? nashindwa kuwaelewa na pia siielewi misimamo yao naona kama vile wana sifa za kinyonga kubadili rangi kila wanapokua kwenye matukio,Na pia kidogo nawaona kama wanataka kuchanganya siasa na dini,maana wao si wanasiasa,unless otherwise wabadilishe fani wawe wanasiasa.
 
hata nakala za mwanakijiji ni zaidi ya page 15

labda huyu mwanamke angutueleza msimamo wake kuhusiana na ISRAEL's occupation of Palestine
 
labda huyu mwanamke angutueleza msimamo wake kuhusiana na ISRAEL's occupation of Palestine
Huu sasa ni uonevu! Unataka aandike pg 2? Kurasa 15, ndizo ameweza kuandika kutoka kwa hali halisi iliyomkumba! Ataandika kuhusu majengo na kanisa!
 
Hatuihitaji tuvijarida twa kujikosha kujifanya wanamjua Mungu saaaana, kama kweli walikuwa wana muogopa Mungu kwanini walitufisadi kiasi hicho?

Hata wewe Mama regina ulishindwa kumshauri darling wako kwamba alivyo kwisha tuibia vinatosha hadi akawa anataka tuletea mvua ya ndege??

TUNACHOTAKA NI TOBA YA KWELI, AREJESHE ALIVYO TUIBIA NA AOMBE MSAMAHA PERIOD!
MAMA REGINA, KAANDIKE KIJARIDA CHA KUOMBA MSAMAHA SI CHA KUJIFANYA UNAMJUA MUNGU.. HIYO SI TOBA NI DHIHAKA KWETU WALALA HOI!
 
Hawa viongozi wa dini Kina Kadinali Pengo, Mchungaji Mwakasege na Askofu Alex Malasusa hawana maana kabisa yaani kwa pamoja wameamua kwenda kujaribu kumsafisha Jambazi Lowassa na Mkewe. Kama walivyosema, msaidia Mafisadi nae ni Fisadi tu, kwa hiyo hapa naweza kusema kwamba hawa viongozi wa dini kwa pamoja wameenda kujaribu kubariki ufisadi na ujambazi Tanzania kwa kumsafisha na kumbariki Jambazi na Fisadi Mkuu Edward Lowassa, kwa Pamoja hawa viongozi wa Dini ni MAFISADI.
 
Last edited:
Breaking News.

Tuachane kidogo na habari hiyo. Kama kawaida mzee wa pangua pangua kapangua wakuu wa Mikoa. Monica Mbega anakwenda Kilimanjaro kutoka Ruvuma na Dr. Ishengoma anakwenda Ruvuma toka Pwani. Hajjat Amina M. Saidi Iringa to Pwani na Bw. Abulazizi from Tanga to Iringa.
 
Breaking News.

Tuachane kidogo na habari hiyo. Kama kawaida mzee wa pangua pangua kapangua wakuu wa Mikoa. Monica Mbega anakwenda Kilimanjaro kutoka Ruvuma na Dr. Ishengoma anakwenda Ruvuma toka Pwani. Hajjat Amina M. Saidi Iringa to Pwani na Bw. Abulazizi from Tanga to Iringa.

Nsaji asante kwa taarifa, ila hii ungeianzia thread yake, hapa tunamkoma nyani giledi, tuna changanua mbinu za fisadi kutaka kujisafisha kwa kutuandikia kijarida cha 15 pgs, kutueleza uongofu badala ya kutubu na kurudisha mara mbili ya chenji zetu alizo kwapua! walau zile milioni 152 daily za RICHMONDULI!
 
Breaking News.

Tuachane kidogo na habari hiyo. Kama kawaida mzee wa pangua pangua kapangua wakuu wa Mikoa. Monica Mbega anakwenda Kilimanjaro kutoka Ruvuma na Dr. Ishengoma anakwenda Ruvuma toka Pwani. Hajjat Amina M. Saidi Iringa to Pwani na Bw. Abulazizi from Tanga to Iringa.

anzisha thread mkuu hapa unatulisha pilipili kwenye chai
ila news uliyoleta ni kuntu. inabreak haswa.
Naogopa nisijekuteuliwa mkuu wa wilaya au mkoa maana sitajisamehe kuona watu wanafanya madudu ingawa ni wateule wa mzeee. (najipigia debe)
 
Ingekuwa vizuri Mama Regina Lowassa angeandika kitabu kinachoelezea jinsi mumewe alivyoanza ufisadi na ujambazi nchini Tanzania na ni kwa kiasi gani ameweza kuwaibia watanzania na kujitajirisha yeye binafsi na familia yake, nina uhakika hiko kitabu kingekuwa na kurasa zaidi ya 1000 lakini hii ya kusema sijui wamesulubiwa ndio maana hakuwa hata na maneno ya kujitetea akaishia na kurasa 15 ambazo freshman yeyote huandika kwenye term paper.

Muda umefika kwa Kadinali Pengo, Mchungaji Mwakasege na Askofu Makalasusa kubadilisha title zao na kuanza kujiita Fisadi Polycarp Pengo, Fisadi Christopher Mwakasege na Fisadi Alex Malasusa. Hizi titles zinawafaa kabisa hawa wachungaji kondoo wa kifisadi.
 
Rwabugiri.

Mkuu nimetekeleza kama ulivyoshauri. Ila nauliza hicho kitabu cha PG 15 ni kitabu au hotuba. Maana kinaanza na utangulizi na kuishia na utangulizi. Watanzania tumeamka mabo ya kuuziana hotuba kwa ajili ya kutafuta fedha za kampeni tumechoka nayo. Acha wachapishe wasome wenyewe. Ila kesho tutasikia mama rostam naye atatunga chake cha PG. nane the road from poverty to greatness
 
Back
Top Bottom