Mke wa Freeman Mbowe

Status
Not open for further replies.
Tunajua kuwa ni mtoto wa Kiongozi mwingine wa CHADEMA bwana Mtei

lakini mbona hatumwoni akifanya shughuli za kitaifa kama mkwe wa kiongozi wa upinzani ...yaani shughuli za akina mama?

Anajificha nini?

Mindhali Freeman ni public figure kama JK na mindhali anaweza kuwa rais wetu huko baadae si vibaya public na private life yake kuwa under scrutiny na bila kusahau what his wife has been up lately

Anajificha ili kisijulikane kuwa ni chama cha wanandugu! Hii ilishaongelewa sana siku za nyuma
 
Mimi sijali kuhus mke wa Mbowe (Lilian Mtei). Hata akiamua kuhama na nchi ili pia asionekane sioni tatizo.

Tatizo ninaloliona ni la kwa nini Mbowe hajitokezi kujibu mengi yanayoisulubu CHADEMA??

Inakuwaje watumishi na wanachama maarufu/muhimu (Kafulila & Danda Juju) wanahama chama lakini mwenyekiti hajitokezi kutoa angalau tamko au kujibu maswali ya waandishi wa habari?

Mbowe kama anaogopa waandishi leo hii kwa mambo madogo madogo kiasi hiki, je anategemea kumuongoza nani?

Kwani kuongea na waandishi si jambo la hiari ama?

Kama masuala ya CHADEMA si yamekuwa yanatolewa majibu na SLAA.Kumbuka CHADEMA si MBOWE.

Mtu kuama chama ni tatizo?Unapohama chama kisa matatizo yaliyopo kwenye chama husika utaama vyama vingapi?Kwanini usibaki na huwe sehemu ya kutafutia ufumbuzi matatizo.

Tubadilike!Tatizo wengi wetu tunadhani kwenye hivi vyama kuna wanachama daraja la kwanza/juu na wengine daraja la chini kwamba Kafulila & Danda Juju wakiondoka basi tamko lazima lotoke kwa MBOWE...kha!....Je,wale wanachama wapiga kura kadha wa kadha kule vijijini kwetu wanaoama chama nani ajitokeze kuongea na waandishi wa habari!

mwanamke ndo mshauri mkuu ma mume kwenye nyumba, sasa huyo anayeshauriwa akishaonekana kwenye public me nadhani inatosha, Mbowe akishachaguliwa kuwa raisi ndio hapo na huyo mke wake atakapo kabidhiwa majukumu ya kijamii kama First lady ndio mtamwona kwenye public vizuri...
fikiria mke wa kila kiongozi wa juu wa chama akijitokeza kwenye jamii.... kama wanamajukumu kwenye chama fine, kwa mtizamo wangu naona ni bora tumpe break huyo mke wa mbowe.
 
Tunajua kuwa ni mtoto wa Kiongozi mwingine wa CHADEMA bwana Mtei

lakini mbona hatumwoni akifanya shughuli za kitaifa kama mkwe wa kiongozi wa upinzani ...yaani shughuli za akina mama?

Anajificha nini?

Mindhali Freeman ni public figure kama JK na mindhali anaweza kuwa rais wetu huko baadae si vibaya public na private life yake kuwa under scrutiny na bila kusahau what his wife has been up lately
Hapo lipo jambo mkuu anataka kutuambia lakini kama kawaida anazunguka ukuta
 
Mimi sijali kuhus mke wa Mbowe (Lilian Mtei). Hata akiamua kuhama na nchi ili pia asionekane sioni tatizo.

Tatizo ninaloliona ni la kwa nini Mbowe hajitokezi kujibu mengi yanayoisulubu CHADEMA??

Inakuwaje watumishi na wanachama maarufu/muhimu (Kafulila & Danda Juju) wanahama chama lakini mwenyekiti hajitokezi kutoa angalau tamko au kujibu maswali ya waandishi wa habari?

Mbowe kama anaogopa waandishi leo hii kwa mambo madogo madogo kiasi hiki, je anategemea kumuongoza nani?

Mbona mtendaji mkuu wa CHADEMA, katibu mkuu ,Dr.W.Slaa alishatolea tamko kuhusu kutimuliwa kwa akina Kafulila & Danda Juju?????????????. Kwani lazima aseme Mbowe tu????????????
 
Mimi sijali kuhus mke wa Mbowe (Lilian Mtei). Hata akiamua kuhama na nchi ili pia asionekane sioni tatizo.

Tatizo ninaloliona ni la kwa nini Mbowe hajitokezi kujibu mengi yanayoisulubu CHADEMA??

Inakuwaje watumishi na wanachama maarufu/muhimu (Kafulila & Danda Juju) wanahama chama lakini mwenyekiti hajitokezi kutoa angalau tamko au kujibu maswali ya waandishi wa habari?

Mbowe kama anaogopa waandishi leo hii kwa mambo madogo madogo kiasi hiki, je anategemea kumuongoza nani?

Sio kila jambo la chama liongelewe kwenye public kama wamesharidhishana ndani ya vikao vyao. Hiyo nayo ni mbinu ya kumaliza mijadala isiyokua na manufaa kwa chama.
 
Mhhh jamani muacheni Dr Lilian Mtei Mbowe she is a very reserved lady, and very nice person, ukitaka msaada wake wewe mtafute tu atakusaidia she is cool. Kumbuka mumeo akiwa mwanasiasa siyo lazima na wewe upende siasa na hizo public life, watu wengine hawapendi siasa na public life. Na watu wengine kama mama Kikwete wanapenda sana nadhani mama Kikwete anaweza akainuka na yeye anataka kugombea kiti cha uraisi mwaka kesho au mwaka kesho kutwa haluuuuuuuuu!!!!
 
somi,
japo kwa upeo wako mdogo, nafuu umeona wazi kuwa, chadema ni ya wale wenye hisa kubwa (i.e. Wawekezaji wakubwa chamani), na pengine ndio maana zitto alizuiwa kuwa m'kiti.

wengine tulishasema haya siku nyingi kuwa, vijisenti vya mbowe na ndesamburo, wanayoipa chadema halafu wanarudi baadaye kinyume-nyume kukidai chadema wanapoona pesa ya ruzuku imeingia, inakifanya chadema kiwe chama cha kitumwa, kikabila na kisichoweza kujifanyia maamuzi binafsi billa ya hao, mbowe, mtei na ndesamburo, kuingiza pua zao. Sidhani kama hii ndiyo demokrasia na maendeleo watanzania wanayopigania.

chadema wanatakiwa wajikomboe kwanza kutoka kwenye huu ukabaila wa mbowe, mtei, ndesamburo & co., kabla ya kuomba watz rukhsa ya kutawala.

kubwa jinga hilo ni jina lako haswa au jina la utani? Nafikiri unauelewa wa kujua jema na baya.

Huyo anayesema chadema ina ukabila anaushahidi gani? Zito anatoka wapi?prof.baregu anatoka wapi?mwanasheria tundu lisu anatoka wapi?n.k.

Ukabila kwenye chama na ufanisi wa kuongoza nchi vina uhusiano gani?
Ni bora udanganywe miaka nenda rudi kuwa unaongozwa kwa usawa bila ukabila huku maendeleo hakuna kamwe na watu wanajirusha na pesa ya jasho lako wakati wewe unaogelea kwenye dimbwi la umasikini wa kutupwa au ni bora kuwe na uongozi bora na shupavu wakuleta maendeleo na mambo mengine yafuate baadae hata kama watawekana wote wa familia moja katika madaraka kama rwanda,uganda nk.
 
Mwacheni shemeji yangu jamani alikuwa Dr pale Muhimbili na ana mpango wa kuacha kazi pale, aliniambia business zao kwa sasa hazina msimamizi, so anaacha kazi asimamie business zao. Siasa ni Hobby, yeye hana hobby na siasa.
 
Mh Hii kali watu badala ya kujadili mambo ya maana na yenye tija kama swala la IPTL mnajadili mambo yasiyo na tija hata kidogo tena yamtu binafsi hii ni hatari sana (Ile thread ya "Umeme wa IPTL mafuta ndo yameshaisha..!" hakuna aliye tia pua limekuja hili la umbeaumbea watu ndo mmkimbilia haa haaaaa.
 
Tunajua kuwa ni mtoto wa Kiongozi mwingine wa CHADEMA bwana Mtei

lakini mbona hatumwoni akifanya shughuli za kitaifa kama mkwe wa kiongozi wa upinzani ...yaani shughuli za akina mama?

Anajificha nini?

Mindhali Freeman ni public figure kama JK na mindhali anaweza kuwa rais wetu huko baadae si vibaya public na private life yake kuwa under scrutiny na bila kusahau what his wife has been up lately

Mbona huulizi yuko wapi Mke wa Mtikila??hivi mna nini na CHADEMA nyie watu
 
Hoja zinapokosa, tunaanza kujadili maisha ya watu binafsi, nini hii!! Mbowe si rais kwamba tunantaka kumwona First Lady. Kama sio mtu wa public politics, kuna ubaya gani kuendelea na private life yake?!
 
watu mnampigia tarumbeta GT lakini angekuw amtu kauliza mke wa kiongozi fulani wa CCM yupo wapi wote mnganza kujadili ila kwa sababu majority ni chadema humu basi mnaona hatari kwa GT kuuliza swali hahahaha si bure ame watouch kiaina....kula 5 m2wangu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom