Elections 2010 Mke wa Dr.Slaa ajitoa CCM, Ajiunga na Chadema

KAribu uwanjani Rose KAmili.
Issue ni moja tu, kumtoa mkoloni mweusi ktk kongwa la watanzania
 
Ni uamuzi wa busara sana,ninampa hongeara toka moyoni mwangu.
Mama sasa ungana na mumeo kuendeleza mapambano mpaka kieleweke ikulu.Ushindi upo.
Tafuta watu kumi hapo ulipo siku ya kupiga kura hakikisha wanampigia Dr Slaa.
Sisi wafanyakazi Tumeshamua kwa pamoja kumpigia mumeo Dr Slaa kabla yeye hajatuomba kura.
Hii ni ishara ya unyenyekevu aliyotuonyesha wafanyakazi wote wa Tanzania.
 
nawasihi hawa wanaotaka kuwatumikia watanzania kwa kupitia vyama vya upinzani waje na hoja za matumaini na kujenga
 
mzee anapowania oval office mama lazima amsuport no matter what, so nashukuru mama kwa kulitambua hilo mapema
Hajalitambua hilo mapema, si kweli. Amepigwa chini kura za maoni huko kwao CCM ndio akakimbilia kwa mumewe CHADEMA. Angalia Makamba atakavyompiga madongo. Aibu!
 
MKE wa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Rose Kamili aliyekuwa akigombea ubunge Jimbo la Hanang kwa tiketi ya CCM, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho tayari kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.


kama alivyofanya mr...
 
Ni uamuzi wa busara, mzee anapogombea office kubwa ya nchi kama ikulu it doesn't make sense first lady kuwa mpinzani wake. Naamini amelitafakari hilo
 
hajalitambua hilo mapema, si kweli. Amepigwa chini kura za maoni huko kwao ccm ndio akakimbilia kwa mumewe chadema. Angalia makamba atakavyompiga madongo. Aibu!

makamba ni nani nchi hii au ni makamba "maprawn"
 
nawasihi hawa wanaotaka kuwatumikia watanzania kwa kupitia vyama vya upinzani waje na hoja za matumaini na kujenga

Mkuu kama sikusomi vizuri vile,
CCM ndo wanawatumikia watanzania vizuri?
 
Rose ungana na mzee katika vita vya ukombozi. Mbona Anna Mkapa aliungana na Ben katika kufisadi nchi, japo walishakuwa kila mtu na lwake longi timu!

Kwa wale wasiojua, Rose na Wilbroad ni wapambanaji kweli kweli...mtaona moto wake kwenye kampeni.
 
Kwani huyu Kamili alikuwa nani? ina maana asinge hama ange mpigia kikwete? Hata hivyo watakao mpigia kikwete nikiwahesabu naona ni kiduchu make
  1. Kura ya Baba mzazi
  2. Kura ya mama mzazi
  3. kaka zangu 4
  4. dada zangu 2
  5. mamdo 3, shangazi 2, mjomba 6.
  6. Kura ya mke wangu
Jumla kura 20 zote ni za Chadema ni za Dr. Slaa, na kaongeza moja ya mkewe!!!!! yaaani, we acha tu kikwete kama Chiluba! kazi thithiem mnayo. Nasema hivyo kwani ni mtumishi wa Serikali na hao wote huwa nawasaidia ki fedha. Tamko la Mkulu ndilo litampa balaa kwenye matokeo. HONGERENI WA TZ KWA MWAMKO MPYA.
 
amechanganyikiwa huyo naye si alikuwa diwani ccm? kwanza kamponza mwenzio akatoka upadri

Ha ha ha ni kwa vile hapa ni freedom of expression!!! Kwa taarifa ni kwamba Dr. Silaa aliacha upadri kwa sababu nyingine tofauti na hii unayofikiria wewe. Ninazo habari hizo kwa usahihi. Amemuoa Rose baadaye sana.

Hongera sana dada Rose, umefanya uamuzi wa busara sana. Ni vema kujenga umoja ndani ya nyumba yenu kisiasa ili pia muambatane katika kampeni. Mpe nguvu mume wako, ni chaguo la wengi only and only if hizi rough za chama tawala hazitakuwepo. Kweli hizi kura za maoni zimetia aibu na doa kubwa mno kwa chama kinachojinadi eti kinapinga rushwa na sheria ikaandaliwa na kuzinduliwa kwa mbwembwe, kumbe kiini macho kwa wafadhili tu. Ziba masikio na usisikilize yasemayo kwa sasa, songeni mbele na wanyonge watakuwa nyuma yenu.

 
kwa wanahanang huo ndo wakati wao wa ukombozi wa kweli baada ya ccm kuwabania haki yao kwenye kura za maoni ,huyo mama ni potential na wahanang na watanzania tupo nyuma yake daima......keep it up kamili tunauhitaji utendaji wako na uchapakazi wako kwa sasa na wakati ndio huu.kapachimbe kamili.
 
Has anyone confirmed this rumour?

Natamani majibu kwa hili jamani, isijeikawa ndo tunaanza kumshawishi hapa
MKE wa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Rose Kamili aliyekuwa akigombea ubunge Jimbo la Hanang kwa tiketi ya CCM, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho tayari kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Bi. Kamili ambaye alikuwa diwani wa CCM wa Kata ya Basuto, kabla ya Baraza la Madiwani la Hanang kuvunjwa, alitoa tamko hilo hadharani juzi baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za wagombea kupitia CCM.

Akizungumza juzi mbele ya viongozi wa CCM wa wilaya na waangalizi wa uchaguzi wa kura za maoni akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Frederick Sumaye na wanachama waliofika ndani ya ukumbi wa CCM kupokea matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dkt. Mary Nagu, Bi. Kamili alisema ameamua kujiengua kutokana na mizengwe iliyojitokeza wakati wa mchakato wa kura za maoni.
Dkt. Nagu alishinda kwa kura 20,042 wakati Bi. Kamili alipata kura 5,372.

"Nimeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uongozi wa CCM kunikataza kuwatembelea wapiga kura kwa madai kwamba kutangaza nia ni mara moja, vile vile wafuasi wangu kunyimwa kadi za CCM, na makatibu wa matawi kutakiwa kuhakikisha kuwa Mary Nangu anashinda katika uchaguzi huu," alisema.

Hata hivyo, Bi. Kamili hakuzungumza bayana kama anakusudia kwenda chama gani cha siasa, lakini baadaye alilieleza Majira kuwa anahamia kwenye chama cha mumewe, na alikuwa akabidhi kadi yake ya CCM kwa viongozi wa CHADEMA kwenye mkutano ulikuwa umeandaliwa jana katika eneo la Kateshi.

Mapema, akizungumza na gazeti hili kuhusiana na uamuzi huo, Bw. Sumaye, alisema ni kawaida ya mgombea yeyote anaposhindwa kuwa na hasira.
"Naamini hayo ni maneno ya hasira, na hasira yake ikiisha atabadilisha mawazo yake na atabaki kuwa mwanachama wa CCM," alisema Bw. Sumaye.

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Hanang, Bw. Michael Tsakhara alisema tuhuma hizo ni za uongo na kwamba walipokuwa kwenye mzunguko wa kuomba kura, kila asubuhi walikuwa wanafanya tathmini ya kuona kama kuna dosari
zilizojitokeza, ili wazifanyie kazi, lakini hata siku moja mgombea huyo hakutoa lalamiko lolote.

Dkt. Nagu baada ya kutangazwa mshindi aliwashukuru wananchi wa Hanang kwa kujitokeza kwa wingi na hatimaye kumpa kura nyingi, hali aliyosema ni ishara kuwa wananchi bado wanamhitaji.
 
amechanganyikiwa huyo naye si alikuwa diwani ccm? kwanza kamponza mwenzio akatoka upadri

Tayari siasa za "majitaka" zimeishaanza. Nadhani wewe mkuu ni CCM damudamu wasioweza kupembua mchele na pumba na bila shaka unaiga siasa za Makamba!
 
Back
Top Bottom