Mke wa balozi Daraja auawa; Mfanyakazi wa nyumbani atafutwa

Na sijui hapo nyumbani kwa balozi walikuwa wakiishi watu watatu tu yaani marehemu mama balozi, balozi mwenyewe, na huyo msaidizi ama....

that is the implication; kama kuanzia J'mosi ile akiwa Muheza alipiga simu na hakumpata mtu ina maana hana mtu yeyote katika Dar ambaye angeweza kumuagiza kwenda kuangalia pale nyumbani?
 
that is the implication; kama kuanzia J'mosi ile akiwa Muheza alipiga simu na hakumpata mtu ina maana hana mtu yeyote katika Dar ambaye angeweza kumuagiza kwenda kuangalia pale nyumbani?

You know..I was wondering the same thing...yaani hata ndugu, jamaa, ama rafiki au hata jirani? Kuna kitu hakijakaa sawa hapa...
 
Ninavyosikia mimi ni kwamba it was robbery. Some money was stolen and a few things taken from the ambassadors bedroom. The ambassador had been in Muheza, apparently he is campaigning for Ubunge and he had talked to his wife earlier in the day. He called back in the evening and the phone went unanswered. After a few more unanswered calls he decided to drive back to Dar to find his wife dead with a knife still in her chest. The "house help" is missing.
 
The "house help" is missing.

You mean the "house aide"

Lakini kwa nini kama huyo msaidizi wa nyumbani hapatikani moja kwa moja atajwe kama ndio mshukiwa? Nadhani kama bado yu hai sehemu basi awe ni 'person of interest'...lakini kwa wakati huo huo wasi rule out anything until they have solid evidence....
 
Ninavyosikia mimi ni kwamba it was robbery. Some money was stolen and a few things taken from the ambassadors bedroom. The ambassador had been in Muheza, apparently he is campaigning for Ubunge and he had talked to his wife earlier in the day. He called back in the evening and the phone went unanswered. After a few more unanswered calls he decided to drive back to Dar to find his wife dead with a knife still in her chest. The "house help" is missing.
Habari haijakaa vizuri hii....aendeshe toka Muheza wakati angeweza tu waambia majirani hata ndugu wakamchecki mamsapu maana hapatikani! Balozi nashawishika anahusika kwa njia moja ya kifo cha huyu mama. Ni uchunguzi wa kina utaondoa utata. Huyo kijana anauziwa mbuzi kwenye gunia.
 
So sad jamani....aaaaaaargh!!!!...R.I.P mama Anna Daraja,pole sana kwa familia ya mzee Daraja,mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu mno kwenu
 
duuh unyama mkubwa sana huu.poleni sana wafiwa.

hapa utata mkubwa sana na mtu anayeweza kuisadia polisi ni huyu house boy ambaye hatujui kakimbia kwa ajili ya ku-panic au kakimbia kwa vile yeye ndio muhusika?

na je huyu kijana alikuwa anafanya kazi kwa mda gani kwenye nyumba hii? siku aliopewa ajira alitambulishwa na nani ? huyo mtu aliomtambulisha house boy ni vizuri akaulizwa labda anaweza kuwafahamu ndugu wa huyu house boy hili kujaribu kumtafuta zaidi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
hapa utata mkubwa sana na mtu anayeweza kuisadia polisi ni huyu house boy ambaye hatujui kakimbia kwa ajili ya ku-panic au kakimbia kwa vile yeye ndio muhusika?

Sasa wewe unakimbilia kuhitimisha kuwa huyo msaidizi "kakimbia". Unakosea kusema hivyo. Kama na yeye ni victim?
 
Jasusi,
Hili swala bado halijakaa vizuri mno, Bill ameandika vizuri saana je hapo nyumbani walikuwa wanakaa wangapi? kingine hakuna mtu atakuja kuiba nyumbani kutafuta pesa kama hana taarifa nzuri kuwa mna pesa mle, hapo ndo naona kijana au jamaa wa watu anaingina kwenye equation. Polisi wambane vizuri tu balozi aeeleze kama alikuwa anafanya shughuri yeyote ya kufanya muda wote awe na kiasi kikubwa cha pesa nyumbani. Baada ya hapo mengi yatafunguka tu, tatizo vyombo vya habari na kauri yake tayari ni kama wanamhukumu kijana wa kazi kitu ambacho si haki kwa nini aseme hivyo? Je akikuta na yeye ni victi ndo ataenda kuiomba familia ya kijana samahani?
 
Habari haijakaa vizuri hii....aendeshe toka Muheza wakati angeweza tu waambia majirani hata ndugu wakamchecki mamsapu maana hapatikani! Balozi nashawishika anahusika kwa njia moja ya kifo cha huyu mama. Ni uchunguzi wa kina utaondoa utata. Huyo kijana anauziwa mbuzi kwenye gunia.

Ukweli ni kwamba habari haijakaa sawa kabisa,labda tusubiri na tusikie taarifa rasmi ya polisi(kama itakuwepo)....Haiwezekani Balozi ampigia simu mkewe hampati kisha anaamua kudrive kutoka Muheza mpaka Dar na kumkuta mkewe kafa?,je hana ndugu au hata majirani ambao angeweza kuwaomba waangalie kitu gani kimempata mkewe?,au hata polisi tu angeweza kuwafahamisha...Kwa mtu mwenye hadhi ya ubalozi hivi ni vitu ambavyo vingemijia akilini mara tu baada ya kujaribu kumtafuta mkewe hewani(kwa simu) na kumkosa....Kunani???????
 
Ninavyosikia mimi ni kwamba it was robbery. Some money was stolen and a few things taken from the ambassadors bedroom. The ambassador had been in Muheza, apparently he is campaigning for Ubunge and he had talked to his wife earlier in the day. He called back in the evening and the phone went unanswered. After a few more unanswered calls he decided to drive back to Dar to find his wife dead with a knife still in her chest. The "house help" is missing.

Jasusi.. that is the story we have been told; but in a situation like this there is a story behind the story. Ngoja nioneshe matundu machache kwenye stori ilivyo sasa.

a. The Story:
The former ambassador, who has served in public office in various capacities, told the 'Daily News' today that he last contacted his wife on Saturday afternoon to inform her that he would be travelling back the next day (yesterday).

“When I tried to call again later in the evening, the call could not go through. I tried again later several times and still it didn’t go through,” he explained his eyes welling up with tears.

Kwa hiyo.. timeline yetu ni kuwa lolote lililotokea lilitokea siku ya Jumamosi kati ya mchana na jioni. Halikutokea usiku. Kama lilikuwa ni tukio la ujambazi na matumizi ya nguvu kiasi hicho hao majambazi watakuwa ni watu wa karibu sana kiasi cha kutokusababisha shuku toka kwa majirani mchana kweupe; na hiyo ina maana wapo mashahidi walioona kilichotokea, gari, watu n.k

Balozi alilala salama usiku ule bila kutoa taarifa polisi, kwa ndugu, jamaa na marafiki huku akiwa hana mawasiliano na mke wake na hajasema kama alijaribu kuwasiliana na msaidizi huyo wa nyumbani. (this is important to keep in mind)

b. The Story:
When he arrived at his home, his driver hooted but there was no response from inside.

“I tried calling again, and got no answer. I was then beside myself with worry, I knew something was definitely wrong. I asked my driver to climb over the fence and open the gate,”

Sasa tunajua kuwa Balozi alilala salama usiku wote ule na hakufanya juhudi ya kupiga simu nyumbani siku ya pili wala kutoa taarifa kwa mtu mwingine yeyote. Muda huo unatoa nafasi ya mtu yeyote kutoweka na kuchelewesha uchunguzi.

Lakini pia tunaona jambo jingine muhimu kwa upelelezi. Malango ya nyumba ya Balozi yalikuwa yamefungwa kwa ndani. Sasa hapa hatuna budi kujiuliza huyo msaidizi wa nyumbani alitokaje na vitu vya kuiba halafu akafunga mlango kwa ndani kiasi kwamba mtu aliye nje anashindwa kuufungua?

La pili ni kuwa Balozi hana ufunguo wa mlango wa nyumba yake akiwa nje?

c. The Story:
They saw her shoes and bags strewn on the ground close to the gate, propelling ambassador Daraja to rush into the house to check on his wife.

Hapa kuna tatizo kidogo. Kwenye upelelezi tunaweza kusema ni kutokubaliana kwa eneo la tukio (inconsinstence of crime area). Viatu vya mhanga na mabegi yake yamekutwa karibu na geti. Vilifikaje hapo? Je mhanga aliuawa nje, aliwafukuza wahusika, hapa ni clue nzuri.. kulikuwa na damu karibu na geti?

d. The story:
I looked everywhere in the whole house but I couldn’t find her. My driver and I looked around the compound but did not find her either

So far.. tunachosikia hapa ni kwamba ndani ya nyumba na eneo zima hakukuwa na ushahidi wa foul play! Ina maana huyo mama hakuuawa ndani ya nyumba au nje ya nyumba kwani kama kungekuwa na damu au aina yoyote ya ushahidi kuwa amedhurika wangeita polisi mara moja. Kama walikuta ushahidi wa kitendo kibaya walipoingia ndani (hasa baada ya kukuta viatu vyake nje na mabegi) walitakiwa kutoa taarifa polisi mara moja, itakuwaje kama wabaya walikuwa bado wako ndani wanasubiri? especially baada ya kujua kuwa geti lilifungwa kwa ndani?

d. The story:
[Just when he was about to give up, he remembered to look inside his garage and…there she was, laying on the floor with a knife sticking out on her chest.

“We unlocked the garage which was padlocked from outside but she was already dead. We reported the matter to the police and they are investigating,” he whispered, tears streaming down his face. /QUOTE]

Hapa kuna mambo ya kutugusa fikra zetu kidogo. Baada ya kumkosa huko kwingine kote akaamua kuangalia kwenye gereji na wakaona mwili wa marehemu ukiwa na kisu kifuani. Wakafungua hilo lango la gereji (na hivyo kupoteza kwa kiasi kikubwa ushahidi wa nani aliufunga!) na siwezi kushangaa walipofika ndani mmoja wao akakichomoa kile kisu, na hivyo kufuta ushahidi wa nani alikichomeka (I hope thats not the case).

e. The story:
Nothing of value was stolen, but the former ambassador suspects the assailants were looking for cash.

“I think the assailants were looking for cash, because they didn’t take anything of value and the bedroom was in a mess with things strewn all over,”

Tunaambiwa kuwa hili halikuwa tukio la ujambazi kwani hakuna kitu cha thamani kilichoibiwa, kuna kitu hawa watu walikuwa wanatafuta au kulikuwa na sababu binafsi ya kufanya tukio hilo zaidi ya kuiba. kama hao jamaa walikuwa wanatafuta fedha na ndani ya nyumba kuna vitu vya thamani why not take the valuables and liquidate them later?

So.. in short ni kuwa it is not what it seems..
 
Habari haijakaa vizuri hii....aendeshe toka Muheza wakati angeweza tu waambia majirani hata ndugu wakamchecki mamsapu maana hapatikani!
mkuu hili hapa ndio lilo nichanganya mimi.kwanini usubiri mpaka ufike dar wakati unaweza kuomba ndugu au jirani wamuangalie mkeo kama yuko salama?

lakini tusijaribu kumhukumu mtu yoyote kwa sasa japo kuwa kuna maswali mwengi ya kujiuliza.uchunguzi utapata majibu.
 
Mwanakijiji,

Analysis yako umeweka boriti la mwisho kwenye sanduku la upelelzi naona kamanda Kova itabidi akutafute uwe mshauri wake ha ha ha ha very good aanlysis
 
Sasa wewe unakimbilia kuhitimisha kuwa huyo msaidizi "kakimbia". Unakosea kusema hivyo. Kama na yeye ni victim?
sasa kama wahusika walitaka kufuta ushahidi na yeye si angeuliwa angeachwa hapo hapo? nahisi kakimbia labda kutaka kuokoa maisha lakini pia kama alikimbia kutaka kuokoa maisha yake kwanini asingeomba msaada wa majirani ?

labda walimteka hapo naweza kukubaliana lakini kwanini wamteke wakati wameshafanya unyama mkubwa wakuua tayari kwa mama mwenye nyumba kitu gani kiwape huruma kwa house boy ?
 
You are just making assumptions and I'm glad you acknowledged it. Kusema "kakimbia" ni statement of fact ambayo hadi hivi sasa bado haijathibitishwa. Unless wewe unajua kwa uhakika kuwa "kakimbia" huwezi kusema hivyo.

labda walimteka hapo naweza kukubaliana lakini kwanini wamteke wakati wameshafanya unyama mkubwa wakuua tayari kwa mama mwenye nyumba kitu gani kiwape huruma kwa house boy ?

Afadhali umerekebisha lugha yako....sasa tuendelee na mjadala.
 
sasa kama wahusika walitaka kufuta ushahidi na yeye si angeuliwa angeachwa hapo hapo? nahisi kakimbia labda kutaka kuokoa maisha lakini pia kama alikimbia kutaka kuokoa maisha yake kwanini asingeomba msaada wa majirani ?

labda walimteka hapo naweza kukubaliana lakini kwanini wamteke wakati wameshafanya unyama mkubwa wakuua tayari kwa mama mwenye nyumba kitu gani kiwape huruma kwa house boy ?

alikimbiaje halafu akafunga mlango kwa ndani?
 
alikimbiaje halafu akafunga mlango kwa ndani?
labda aliruka ukuta manake kama viatu vya mama vilikuwa karibu na getini labda purukushani imeanzia hapo.

tatizo kubwa hapa kwanini hakuomba msaada wa majirani? ndio maana najiuliza alikuwa anafanya kazi hapa mda gani? na walimpata wapi au walitambulishwa na nani kwake mpaka wakaweza kumuamini kuwa mtumishi wao wa ndani?

na pia inawezekana alifanya njama, manake kama issue ya wezi wamevamia sidhani kama wangepoteza mda hata wa kumfungia huyu mama garage na kufuli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom