Mke na pombe, wanaume mnashauri nini????

Mmmmm,kama mtu unaweza afadhali usinywe pombe kabisa.
Hasa hasa ukiwa umeumbwa mwanamke,
Mwanamke ni mlinzi wa mwanaume,

Mwanamke kiongozi wa familia kwene swala zima la maadili, Mwanamke mlezi wa familia na mtekelezaji wa mipango yote.

Kama kweli unaweza kunywa kidogo kwa afya kunywa, kama huwezi acha tu.
Manake kiasi hichi ndugu yangu, baba unarudi chakari, Mama nae Chakari. Mmmm sipati picha!! Binti uko Chakari mmmh haipendizi bana!!

Wanaume walivyoumbwa bwana mambo yao mengi wala sio ya kuigwa na mwanamke. Ndo maana hata Mungu aliliona hilo akaumba msaidizi, na mlinzi ambaye ni Mwanamke.
 
Kiukweli familia ambayo baba na mama niwalevi hukosa staha na upendo wa ukweli.
Pombe hondoa utashi wa mtu na kujikuta anafanya mambo asiyoyatarajia.
pombe huleta umaskini
 
:suspicious:Inategemea nani, maana kuna wanaume nawafahamu, bia moja tu kama kanywa ndoo nzima. Lakini kuhusu wanawake kupombeka vilevile ni kwa sababu wanaume wengi wanyonge katika kuomba wanawapeleka wanawake kulewa ili waombe wote wakiwa chakali. Akikataliwa asingizie pombe. Waache wanawake wapombeke pia maana wanataka na wanaume wanaolewa hovyo nao wanahatarisha their behind wachokoaji wakiwaona wanawazengea vilevile
 
Pombe ni Pombe, kwa mwanamke au mwanaume yote sawa. Nakumbuka rafiki yangu mmoja ukienda naye ulevini, NGUMI mkononi!!!!!
Ataanzisha "War" ambapo hutakubali akiadhibiwa...........Hasara tuuuu!!!!!!!!!!!!
 
Sio heshima kusema Mwanamke huyu MLEVI itaonekana ana kasoro kidogo! Ila kwa mwanaume kusemwa ni mlevi sio issue, Utasikia wanasema "Mwanaume hasifiwi kula ni kulewa na wanawake.........." ambanyo vikisemwa kwa Mwanamke vinaleta tafsiri MBAYA. Hivyo kulewa kwa Mwanamke ni tabia mbaya sana katika jamii ya kibongo.........
 
Hapo chacha!

hapo nakubali.nilijionea njemba moja ilioacha ulevi forever baada ya kuvunjiwa yai kwenye makalio baada ya kunywa na kulala barabarani..je? Kama angelifanyiwa kweli? Wengine huishia kujitoa uhai kwa hicho kitendo...DRINK MILK SAVE BEER!!
 

Mpendwa Tabutupu, hebu nisaidie kidogo kwenye hii heading....

icon1.png
Mke na pombe, wanaume mnashauri nini????


Ulitaka uchaguzi kati ya Mke na Pombe au ulitaka maoni kuhusu wanawake wanywa pombe??

Please, kama hutajali....
 
ningekuwa mwanaume ningekaa mbali sana na mwanamke si tu anakunywa hata kama anaonja
 
Inategemea na sehemu, magomeni wakizimika m/ke na m/me anaweza salimika m/ke na m/me asisalimike.

Nasikia wanaume wengi siku hizi kwa sababu ya pombe huwa hawataki kushtuliwa ghafla maana habari yake kubwa:car:
 
Tunatosha shukrani nyingi sana kwa Dinnah. Hakika mwanamke kulewa na kusahau heshima yake kwa jamii ni jambo ambalo halivumiliki. Tunatoa ushauri wa bure kuwa wanapokwnda kwenye maeneo ya starehe na kupata kinywaji, wawe na uwezo wa kutawala nafsi zao kwa kunywa pombe wanazomudu ili kulinda heshima yao katika jamii
 

Mpendwa Tabutupu, hebu nisaidie kidogo kwenye hii heading....

icon1.png
Mke na pombe, wanaume mnashauri nini????


Ulitaka uchaguzi kati ya Mke na Pombe au ulitaka maoni kuhusu wanawake wanywa pombe??

Please, kama hutajali....

nataka maoni kwa ajili ya wanawake wanywa pombe.
 
Back
Top Bottom