Wadau mama anaumwa na anataka kukaa na mimi,mke wangu anasema hana furaha kukaa na mama nyumba moja,nimechanganyikiwa nishaurini,nimuondoe mamam au nikae nae na mke wangu hatakuwa na furaha???
Nisaidieni wajameni.
Wadau mama anaumwa na anataka kukaa na mimi,mke wangu anasema hana furaha kukaa na mama nyumba moja,nimechanganyikiwa nishaurini,nimuondoe mamam au nikae nae na mke wangu hatakuwa na furaha???
Nisaidieni wajameni.
Mama yako anaumwa halafu unauliza watu wakushauri namna ya kumplz mkeo eti akubali ukae na mama yako ili apate matunzo na matibabu sahihi,...mimi naona haya mabo ya kutaka kuiga kila mambo ni ujinga_mama yako ana nafasi kubwa kuliko pengine hata ya mkeo ukweli ndio huo ingawa unaudhi,...
Acha kupoteza muda ku-uliza watu wakati mama yako anaumwa fanya fasta muite aje umpeleke hospital na umwambie huyo mkeo ambaye anaonekana ni jeuri asiye na huruma hata kwa mama yako ambaye anaumwa aachane na msimamo huo,...mama akipona ndio usuluhishe hizo tofauti kama zipo............
Igwe usikurupuke namna hiyo kaka. Ukijibiwa hiyo nyumba ni ya mke, utasemaje?
Busara zinahitajika zaidi kwenye hili kuliko povu. Kila nyumba inahitaji busara zake.
Kuombana ushauri ndio desturi za waungwana.
Duh, aisee kweli kuwa uyaone. Kwahiyo watu wakikushauri msikilize mkeo achana na mama yako mzazi utatekeleza ?
Inaonyesha behind the scene una mambo mengi sana, sitegemei katika hali ya kawaida kwa mtu wa kawaida na katika mazingira ya kawaida mama yako mzazi anaumwa eti unakuja kuuliza watu wakushauri kuwa ufanye nini ?
Nikuulize swali moja, una mtoto kwa huyo mkeo ?
Otherwise ukisikia una mke kimeo balaa ndiyo huyo uliyenaye.
Ni sawa mkuu,
Ila kwa mtazamo wangu kuna baadhi ya mambo ambayo nafikiri hayahitaji busara kuya-solve(inabidi kutumia nguvu)...mama anaumwa halafu mke wangu eti hataki nije nikae nae ili nimuuguze,...ooooooooooh no kaka,.....anayway watu tumetofautiana na kila mtu ana dunia yake kwenye hili kiongozi wangu.....mama kwa bahati mbaya akifa eti tunaongozana na mke wangu kwenda msibani..
Kwenye iman yangu ya dini kuna verse'baba ni kichwa cha nyumba'....na kama kichwa cha nyumba ni lazima ufanye maamuzi magumu ambayo pengine yatakera upande wa pili lakn yenye heri na baraka kwa familia
LOL,...nimekuelewa wapi unasimamia,...ila tatizo hapa si unaona lilivyo 'uchi wa mnyama?'
Huyu bwana amepungukiwa busara za kumshawishi mkewe waje kumuuguza mama hapo kwao.
Sasa ukimwambia atumie maguvu tu, nani atampikia huyo bi mkubwa, nani atamkogesha,
nani atakuwa akimvisha?...maana hatujajua huyo bi mkubwa anajiweza au la...
Binafsi wala sitopenda mama yangu aje kwangu kisha adhalilike na manyanyaso na masimango nikiwa sipo nyumbani.