Mke na mama mkwewe

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Tatizo la kina mama kutoelewana na mama wakwe zao ni tatizo sugu sana duniani. Hata siku moja hawawezi kuishi vizuri pamoja chini ya dari moja. Je kuna mtu ameshuhudia hawa watu wawili wakiishi vizuri! kama hakuna kabisa je ni kwamba ni laana za toka enzi hizo au ni nini. Kwanini inakuwa ngumu hawa watu kuelewana na kupendana. Kama ni wivu kwa mtoto/mume ni wivu gani huo mbona kila mmoja ana mapenzi tofauti kwa kijana/mtoto.
 
Kijana akishaoa, kama alikuwa anaprovide kwenye familia yake, basi ataacha au kupunguza frequency, sasa hii inatafsiriwa na Mama mkwe kuwa ni maagizo ya binti!
 
mama ana nafasi yake na mke vilevile. hao si wake wenza. mwanaume uwe imara ktk ndoa yako na usimame ktk haki.
 
Mbona akina baba hawakorofishani na baba wakwe zao, Ni akina mama tu. Hawa vipi!!. Ukweli ni kwamba ugomvi wa hawa watu wawili unakera sana, hata mwanaume ukijifanya una haki gani basi upande wa pili utakuwa shida tu, Wakati mwingine bora kukaa kimya uwaache wapambane. Suala ni kwanini lazima iwe hivi. Mke anasahau kabisa wajibu wa kumuona mama mkwe wake kama mama yake na mama mkwe naye anashindwa kumuona mkwe wake kama mwanae.
 
mimi nimeelewana na mama mkwe huwezi amini tena alishajua ili apate kitu kwa haraka anapitia kwangu yule mama nilimpenda tulikuwa zaidi ya rafiki bahati mbaya amefariki mungu amlaze mahala pema peponi
 
kuna mmoja alikuwa naelewana sana na mkwewe, lakini mashemeji walipiga jungu la nguvu hadi mama huyo hataki kumwona wala kumsikia huyo mke wa mwanae. Inategemea wote wawili na watu waliowazunguka wako objective kiasi gani, kuna familia wanaendekeza mambo ya kimbea, majungu, majivuno na mashindano na ushirikina pia maelewano lazima yapungue.
 
Hali hii inatokana na tabia za watu kutofanana. Ikitokea bahati ukapata mkwe mwenye tabia zinazofanana na wewe hali huwa shwari. Vinginevyo ndio hivyo tena ugonvi usio na sababu. Unajua, kuunga familia mbili zenye tabia na zilizotoka katika mazingira tofauti ni kazi kubwa.
 
Tatizo mama mkwe anataka kushindania mapenzi na mke wa mwanawe.
Lkn mama mkwe mstaarabu hana hizo anaamini kuwa yeye ni mama na hao ni watoto na
ni mke na mume.
 
Mkwe sikuzote anaona mapenzi yake yanahamia kwa mkwewe,niwachache sana walokua na mapenzi na kwaupande wangu naona ili muelewane msiwe nyumba moja, na ugomvi mwingi unatokea pale mume anapokua na visenti mkwe anaona yeye ana haki ya vyote na hasa familia ikiwa hana pesa tangu zamani ndio inakua mbaya zaidi.
 
mimi nimeelewana na mama mkwe huwezi amini tena alishajua ili apate kitu kwa haraka anapitia kwangu yule mama nilimpenda tulikuwa zaidi ya rafiki bahati mbaya amefariki mungu amlaze mahala pema peponi

Nimeipenda ID yako jinsi ilivyokaa kimatusimatusi, mie hoi hapa!
 
ndo maaa waitaliano hawaruhusu mwanao aishi nao hata aoe au awe mkubwa kiasi gani, watakaanaye hapo hapo home hadi mwisho wa maisha yao!
 
mh kweli hili ni tatizo jaman! hata mm linanisibu...mimi namchukulia km mama angu alienizaa lkn yeye ananichukulia tofauti kabisa da! vituko vituko vituko tele vinavyotokea baina yetu! inaniuma sana hiki kitu! mama mkwe km mke mwenzangu lol
 
ni bahat sana kumpata mamkwe anaekuona mkwewe kama bintiye!weng wanaona bint anafaidi!
 
Mbona akina baba hawakorofishani na baba wakwe zao, Ni akina mama tu. Hawa vipi!!. Ukweli ni kwamba ugomvi wa hawa watu wawili unakera sana, hata mwanaume ukijifanya una haki gani basi upande wa pili utakuwa shida tu, Wakati mwingine bora kukaa kimya uwaache wapambane. Suala ni kwanini lazima iwe hivi. Mke anasahau kabisa wajibu wa kumuona mama mkwe wake kama mama yake na mama mkwe naye anashindwa kumuona mkwe wake kama mwanae.

Mara nyingi mke hupenda kumfanya mama mkwe kama mama yake ila mama mkwe hushindwa kuwa mama kwake na ndio maana mke akilitanbua hilo na yeye anampotezea. Hakuna jipya kwa mama wakwe, tatizo ni maslahi tu!Mi mama mkwe wangu alinifanyia visa hadi alifanya ushirikina tuaachane ili kijana wake aoe mtoto wa dadake (anaaamini mwanae akifa basi mali ya mwanae haitatoka nje).
 
tatizo lipo kote kwa mtoto na mkwe. lkn pia ni vigumu kuuchukulia ukimwi kama malaria (ni ngumu kumchulia kama mamako au mtoto wako).
 
mh kweli hili ni tatizo jaman! hata mm linanisibu...mimi namchukulia km mama angu alienizaa lkn yeye ananichukulia tofauti kabisa da! vituko vituko vituko tele vinavyotokea baina yetu! inaniuma sana hiki kitu! mama mkwe km mke mwenzangu lol

hapana ilo c tatizo ila ni changamoto tu! ebu sister isome hii "greatness in life is measured by how well an individual respond to the happening in life that appears 2b totally UNFAIR, UNDESERVED AND CHALLENGABLE.
 
Mbona akina baba hawakorofishani na baba wakwe zao, Ni akina mama tu. Hawa vipi!!. Ukweli ni kwamba ugomvi wa hawa watu wawili unakera sana, hata mwanaume ukijifanya una haki gani basi upande wa pili utakuwa shida tu, Wakati mwingine bora kukaa kimya uwaache wapambane. Suala ni kwanini lazima iwe hivi. Mke anasahau kabisa wajibu wa kumuona mama mkwe wake kama mama yake na mama mkwe naye anashindwa kumuona mkwe wake kama mwanae.

Wamama majungu yamewazidi na kujifanya kila mmoja yupo juu ya mwenzie
 
mimi nimeelewana na mama mkwe huwezi amini tena alishajua ili apate kitu kwa haraka anapitia kwangu yule mama nilimpenda tulikuwa zaidi ya rafiki bahati mbaya amefariki mungu amlaze mahala pema peponi

Amen and RIP to har
 
Back
Top Bottom