Mke Mwizi!!!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,270
Ndugu yangu amekuja kuomba ushauri, mke wake ni mwizi, anamwibia pesa kila kukicha. Nguo zake pia huibiwa na mama watoto huyo.
Kibaya zaidi kilichomsikitisha ndugu yangu ni kuibiwa kwa mifuko ya saruji na mabati waliyotaka kuyapeleka saiti.
Mke huyo kila upotevu unapotikea, akiulizwa hajibu kitu zaidi ya kulia.
Jamaa anajiuliza amuache, awajulishe wazazi, ama ampeleke kwa wana saikoloji?
Tumshauri huyu mwenzetu nini afanye
 
Amrudishe kwao kwanza ajifunze kuishi na mme wake kama kitu kimoja
 
Kabla ya kumuacha hizo option zingine ni nzuri zaidi.
Kuna mashosti ni wezi kwa kweli.
 
Ukipenda Boga na ua lake, huyo ndio mke wako, mfundishe na kumuelimisha aache tabia ya wizi.
 
Amfungulie charge sheet hapo mahakamani atarudishwa vitu vyake!huyo si mke ni mlango wa saba!
 
Siku moja ale pweza,konyagi na karanga,halafu wafanye mapenzi na ajitahidi kufanya utundu wote wa kimapenzi na kumwamsha hisia za kimapenzi huku akimwuliza habari za uwizi,atajisahau na kueleza siri zote za uwizi.
 
Ana uhakika gani mke anaiba?unajua kuna mapepo yanatumwa kwa ajili ya kuharibu ndoa na ndo yanaweza yakawa yanaiba yeye anadhani mkewe,imeshatokea kwa ndugu yangu kabisa anaweka hela usiku asubuhi hamna na wako wawili tu,maombi yaliwaokoa na pengne mke analia coz haamini mume wake anaweza kumdhania mwizi?wakae pamoja waongee wajue tatizo,mi coni kwa nn mkeo aibie au haachi hela ya matumizi?
 
Mke anajenga huyo, kuna makabila hapa Tanzania ndio elimu ya unyago hiyo, nipo tayari kukosolewa katika hili!

Mfano watu wa Morogoro wakaguru, etc.... wengine walikuwa hawaibi ila wanasubiri ukimaza kujenga wanakupereka kule alipotangulia Shekh Yahya.

Ila uwe macho sana maana kama mkewe ni member wa JF kunasiku utapikiwa sumu maana wewe ndio unataka kumfukuzia njiwa wake.
 
ongea na TISS wamfuatilie sehemu atakayokwenda kuacha hivyo v2 na wao nao wawatume wezi waviibe
 
kuna wifi yangu naye alikuwa mwizi kweli, anaiba nguo za mamuwe anapelekea wadogo zake.
Kuna Xmas moja yeye na mumewe wakaenda kijijini kwa wazazi wa mwanamke. Wakakuta hizo nguo zimevaliwa, pia mwanamke alikuwa ameiba tv na kuihamishia huko kwao, yaani aliona aibu sana, akawa mnyonge hadi wazazi wake wakahoji sababu za unyonge huo, akawa mkweli akasema nimeumbuka leo, nilimdanganya mume wangu kuwa hivi vitu viliibiwa akiwa safari.
Wazee wakamuombea msamaha.
 
Ana uhakika gani mke anaiba?unajua kuna mapepo yanatumwa kwa ajili ya kuharibu ndoa na ndo yanaweza yakawa yanaiba yeye anadhani mkewe,imeshatokea kwa ndugu yangu kabisa anaweka hela usiku asubuhi hamna na wako wawili tu,maombi yaliwaokoa na pengne mke analia coz haamini mume wake anaweza kumdhania mwizi?wakae pamoja waongee wajue tatizo,mi coni kwa nn mkeo aibie au haachi hela ya matumizi?

kwa hiyo waliposali wakaliona pepo likiiba?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom