Mke mwema hutoka kwa BWANA?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
black%20bride..jpg

Ukiuliza Biblia jibu ni "ndiyo"! Sasa nimejiuliza.. kwanini hayo maandiko hayasemi

Mke mzuri

Mke mrembo
Mke mwenye figure ya namba 8
Mke msomi
Mke mwenye sura ya umodo
Mke mkamilifu
Mke mtulivu
Mke mpole
Mke mwenye mapozi
n.k

Anatoka kwa Bwana!?


Maana wengine katika maisha yetu tumewatafuta "wake" wenye sifa nyingine kibao na kushindwa kuitafuta ile ambayo ni prerequisite ya sifa nyingine zote yaani "wema". Ndio maana ikaulizwa mahali fulani (msiniulize wapi).. "mke mwema ni nani awezaye kumpata"? ..


Well.. I'm still searching!!! Wakati mwingine nafikiria nimempata and I get all elated and euphoric to find out.. she has everything else but 'THAT' ..


Umeshampata, bado unatafuta, wewe ni mmojawapo, unajitahidi uwe.. au ndiyo inabidi "to settle" na kile ulichonacho?
 
Kwa sababu mke mwema hufanya mambo yaliyoorodheshwa katika Mithali 31!
 
Mke mwema atokaye kwa bwana lazima ataendana na sifa zako uzitakazo au niseme tu kama kweli anatoka kwa bwana basi utaridhika nae!
 
Mkuu MM, ukishampata Mke mwema hayo mengine yote yanakuwepo. MUNGU ni mwema hawezi kukupa mke mwema halafu hakakosa hayo mengine yote.
 
Mkuu MM, ukishampata Mke mwema hayo mengine yote yanakuwepo. MUNGU ni mwema hawezi kukupa mke mwema halafu hakakosa hayo mengine yote.

mmh.. kwa hiyo mke mwenye sura ya utata hawezi kuwa mwema?
 
mmh.. kwa hiyo mke mwenye sura ya utata hawezi kuwa mwema?

MM, vyote ulivyovitaja ni subjective. vinategemeana na kila mmoja apendavyo lakini 'wema' hakuna wa aina nyingi. sura haisababishi wema lakini wema unafunika vyote ulivyovitaja ndiyo maana biblia inazungumzia mke mwema na siyo sifa ulizotaja.
 
nafikiri lazima na wewe uwe mume mwema kwanza ndo upate mke mwema........si dhani kama Mungu anaweza kumpa mwanamme muovu mke mwema.
 
Ndio ukweli wenyewe hatuwezi kupingana na maandiko ya mungu wala kuongeza ..
Ndio ukweli wenyewe mke mwema hutoka kwa mungu
 
Mwema - ikimaanisha anatenda wema - wema unatoka ndani ya moyo - sio mavazi, urembo, sauti etc. - wema ni matendo ya mke huyo ya kila siku - Mumewe humwita mwema lakini hata watu wengine (familia etc) humwita mwema kwa matendo yake.
Wakati wa shida na matatizo ndio kipindi cha kujua wema hasa wa mtu - mke aliye tayari kukosa chakula lakini watu wengine wakipate - mumewe, watoto, ndugu etc.
 
Mwema imetulia mno na umeielezea vizuri Mzee Mwanakijiji I hope vijana wasiooa watazingatia hilo.
 
Mtu akikuambia mke mwema anatoka Ruvuma, na wewe uko Dsm, itakuwaje? Tatizo langu mimi ni mume mwema anatoka wapi? Manake tunajitafutia kwa kutumia checklist na ku-certify lakini .....!
 
Mtu akikuambia mke mwema anatoka Ruvuma, na wewe uko Dsm, itakuwaje? Tatizo langu mimi ni mume mwema anatoka wapi? Manake tunajitafutia kwa kutumia checklist na ku-certify lakini .....!


hapa nimesmile tu .no comment
 
Duh,kutafuta Mme kwa kutumia check list unaweza end up kupata jambazi au mme wa kichina(fake)
 
..hao wengine sio mungu huyo huyo amewaumba???
...mke mwema na sie mwema wote wanatoka kwa BWANA...lol

kiukweli mnasahau hio check-list inatwakiwa iwe na vitu vyote...wema included!..mapozi,sura nzuri na wema pia...lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom