Mke kagoma kujiita jina la Mumewe, mume afanyeje?

Mke wangu hatumii jina la ukoo wangu, na tuko very peaceful!
Huwezi kumlazimisha mtu kwa hilo, utaonekana una hila fulani!
 
Issue ya kubadili jina au kutobadili jina imekaa kidini zaidi. Kwa wanao fuata imani ya Kiislamu Uislam umekataza kubadilisha jina la baba na kutumia jina lolote jengine kama kutumia jina la mume.

Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu
Al-Ahzaab: 5

Na tabia ya mke kubadilisha jina kutumia jina la mume, mfano kuitwa Mrs Juma, ni tabia zisizolingana na maadili na mafundisho ya Kiislam kabisa!

Kufanya hivyo vile vile kuna madhara yake. Kwanza tabu ya kubadiisha pasipoti na vyeti vinginevyo kwa ajili ya utambulisho katika idara za serikali.

Pili, inapotokea kifo cha mume au talaka, inabidi mke arudie kubadilisha pasipoti na vyeti vyake vyote vingine kuweka jina la baba badala ya jina mume, hivyo ni usumbufu unaompotezea mtu fedha na wakati wake.

Kwa hiyo Muislamu ni bora kubakia katika amri na mafunzo ya dini yake ili kupata ridha ya Mola wake na pia kujiepusha na usumbufu mbali mbali.

Ila kwa wale wanao fuata kanuni za kimila na kikristo na kimagharibi ni jambo lililo zoeleka kwa mke kujiita kwa jina la ukoo wa mume wake.

...akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Matt 19:5-6
Kumbe kina Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Sitti Mwinyi ni waislamu jina tu wataishia motoni! Kina mama Salama Kikwete wana puuza dini! mmh!!?
 
Masaki I knew u will come up with answer... weye ni mwalimu wa kiswahili?
 
Masaki I knew u will come up with answer... weye ni mwalimu wa kiswahili?

Hapana, mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili, mwalimu wangu yupo hapa jamvini. Anaitwa Mwalimu bht.......!!!
icon10.gif
 
Usasa unatupoteza.. tatizo si wamam kuchukua majina.. tatizo ni kutaka kuwa 50kwa 50... bnafsi nahc mke kukubali jna la mume inamaanisha.. 1- upendo usio na mipaka wa mke kwa mumewe 2- ishara ya muunganiko wa asilimia 100 kwa mumewe na kuwa mwili mmoja 3- kwa mume.. kunamwongezea kujiaminisha kuwa mke ni wake na ni ubavu wake maisha..hivo kuithamini ndoa yao.
Ninadhani wanawake wanachelea kuchukua majina yao kwa kujihc watakuwa watumwa(si sahihi), kuogopa kubadili majina iwapo ndoa itakuwa ndoano na kuachana na waume zao!
Upendo, uaminifu, maridhiano vpo.. Na vnadhihirishwa na vtu vdogo(kama matumizi ya majina)!
I stand to be corrected wadau.. Thanks!!
 
Hapana, mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili, mwalimu wangu yupo hapa jamvini. Anaitwa Mwalimu bht.......!!!
icon10.gif
mwanafunzi ni kama unaelekea kumpiku mwalimu vile??
ntapunguza kasi sasa....
 
mwanafunzi ni kama unaelekea kumpiku mwalimu vile??
ntapunguza kasi sasa....

Mwalimu anatakiwa kuona fahari kutokana na mwanafunzi wake kufanya vizuri kwenye somo lake. Kitendo cha kupunguza kasi kutokana na mimi kufanya vizuri kwenye somo lako kutafanya watu watilie shaka wito wako!
 
hahaaa was just kidding
am proud of you
its only through you tha I realised I was called to be a teacher....
am proud of you Masaki...keep it up!!!
 
Kumbe kina Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Sitti Mwinyi ni waislamu jina tu wataishia motoni! Kina mama Salama Kikwete wana puuza dini! mmh!!?
Je wao binafsi wanajiita hivyo, kwa majina hayo ya Mama Fulani... Pia huwezi juwa maisha yao ya akhera yatakuwaje... wao ni waja wa M'Mungu wanaweza tubia kabla ya mwisho wa uhai wao.
 
Mrs - Mama fulani....say Mama Kikwete
Miss - Bi fulani......say Bi Mwenda
Ukimwita mtu kwa jina la Mama Fulani, una maanisha ana mtoto anaitwa Fulani.
Mf: Mama Kikwete, ina maanisha Mama mwenye mtoto anaitwa Kikwete (Mama yake na Kikwete).
 
ni jirani zangu na nimeisha wasuluhisha sana lakini kila upande unadai uko sahihi..
Jamaa kaoa mwaka watano huu lakini mkewe ambaye ni mfanyakazi serikalini amekataa kutumia jina la mumewe kama ilivyo zoeleka kwa kina mama wengi wakiolewa. K.m vile mama maria nyrere, magret sitta,hilary clinton, lwiza mbutu n.k
yaani mrs kang'ang'nia tu kutumia jina la baba yake kitendo ambacho mume kinamuumiza mno! Na anaona mkewe anampuuza eti kwa vile hana hadhi kubwa kama baba wa mke.
Jamani hii inakuwaje ni lazima mke abadili jina akiolewa na kujiita jina la mumewe?
sio muhimu kubadili jina cha muhimu ni maisha ya maelewano ya raha, amani,uendo,kuvumliana,kusameheana
 
Duh, kama ni hivyo wanaume tutafute "uwezo" jamani, lasivyo unaweza kupuuzwa ukakosa raha ya dunia.

Hakuna lolote; kama utamaduni unatuongoza kuwa ni muhimu kubadili basi lazima abadili; na ndoa zetu za kikristo ndio kabisa maandiko yanasema ataaachana na wazazi wake na ataambatana na mumewe! huko kuambatana ni pamoja na kubadili jina!

mwambie jamaa akomae kama ni kumwaga unga na umwagike usikute kuna vitu vingi vinendelea hapa zaidi yahii kitu!
 
Kumbe kina Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Sitti Mwinyi ni waislamu jina tu wataishia motoni! Kina mama Salama Kikwete wana puuza dini! mmh!!?

1. usimtilie x-pasta maneno kinywani.....hajasema wataingia motoni
2. inaweza kuwa wanapuuza dini ( si ajabu kwa kuwa wao sio viongozi wa uislam kama mkapa alivyokuwa si kiongozi wa Ukiristo )
3. Inawezekana kuwa wao hawajiiti, ila watu wanawaita. kwa maana ya kuwa yeye mwenyewe anapo jitambulisha hajisemi kuwa "mimi ni Siti Mwinyi"

tusipoteza muelekeo wa mada........mwaga data wewe unaonaje mke kutobadili jina?
upande wangu naona poa tu, whatever makes the lady happy ( isiwe tunafikiria whatever makes the guy happy pekee)
 
Well said Gaijin...!
 
Ukitaka aanze kuligombea jina lako kama vile amepagawa, tafuta mke mwingine tena awe mtangazaji wa redio za mipasho, kila kukicha anajitangaza kwa jina lako redioni kwa zile style za 'Dida wa Mchops'. Ataanza kutumia jina lako haraka sana.
 
1. usimtilie x-pasta maneno kinywani.....hajasema wataingia motoni
2. inaweza kuwa wanapuuza dini ( si ajabu kwa kuwa wao sio viongozi wa uislam kama mkapa alivyokuwa si kiongozi wa Ukiristo )
3. Inawezekana kuwa wao hawajiiti, ila watu wanawaita. kwa maana ya kuwa yeye mwenyewe anapo jitambulisha hajisemi kuwa "mimi ni Siti Mwinyi"

tusipoteza muelekeo wa mada........mwaga data wewe unaonaje mke kutobadili jina?
upande wangu naona poa tu, whatever makes the lady happy ( isiwe tunafikiria whatever makes the guy happy pekee)

Mkuu mimi naona wewe ni mgumu sana kuelewa! Mtu akiwa kipofu maana yake si haoni? tafadhali bwana, fikiri tena.
 
Nadhani hapa iko muneno, mke wake jamaa ni mtu wa majina sana hivyo anaona kwa sababu jina la kwao ni kubwa kuliko la mume basi asitumie la mume atumie la kwao. in short huyo mke ni opportunist tu hana lolote la maana linamfanya akatae kufanya hivyo!!
 
mwanamke kama mwanamke ukishaolewa inatakiwa utumie jina la mume wako si mr wako bwana lazima urinnge ningekua mimi ndiyo uyo mwanaume angenieleza tu,vinginevyo kwao
unajua wanaume some time lazima tusimame kama kichwa cha kila sehem
 
Back
Top Bottom