Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

na nyie mmezidi kuoa mijanamke yenye tabia za ajabu ajabu......wanawake wote hawa duniani hapa we unaenda kuoa watu walio na akili za ajabu ajabu.

Uko kwenye ndoa kweli au bado? Kama bado uscheke wakunga, na ukiona mwenzio ananyolewa tia maji mdogomdogo. Na kama uko kwa ndoa huna uwezo wa kujua baada ya sekunde moja nini kinaweza tokea na kugeuza mlolongo mzima wa maisha yako. Think big.
 
Acha ligi wewe, kataja kabila tu hakumaanisha wanawake wote wakichaga, pengine asingetaja watu wangemuuliza chakwanza, huyo mama ni kabila gani.
unaweza kuita ligi au namna yoyote, lakini huwezi kubisha kuwa kuna watu ambao wanapoona tatizo katika mahusiano, wanashindwa kuwa objective bila kuhusisha dini au kabila.
Ni kweli kuwa utamaduni unaweza kumshape mtu, ni muhimu kujua mtu wako amekuwa shaped na vitu gani, ili uweze kusaidia kufany amaamuzi.

Huyu jamaa anakwazwa na kabila, kabila ni kitu mtu hawezi kubadili, ushauri ni kuwa amuache. na kwa kuwa kabila ni ishu kwake, asioe tena kabila la tofauti, atajikosesha raha bureee,
hakuna haja ya kumficha, mie kama mchaga nimeishi maisha yangu yote nikiwa na makabila mengine na neiona hio attitude haina DAWA.
 
Kwa ndugu yake mbona hakujadili na bado hakuongea chochote....kifupi jamaa anatakiwa asimamie maamzi yake kama kicho cha familia na akileta msimamo wake wa kuto wataka ndugu za mme amtimue....

Asimtimue, ila akizidi asishiriki chochote cha upande wa mke.
 
Uko kwenye ndoa kweli au bado? Kama bado uscheke wakunga, na ukiona mwenzio ananyolewa tia maji mdogomdogo. Na kama uko kwa ndoa huna uwezo wa kujua baada ya sekunde moja nini kinaweza tokea na kugeuza mlolongo mzima wa maisha yako. Think big.

Mamshika asante manake, nilijizuia kumjibu huyu mheshimiwa,
Lakini afadhali umemwambia inavyopasa.
 
Mkuu kama maelewano hakuna... hata angekuwa mchina dawa ni moja tu.... timua akakae kwao, miaka mi3 yote bado hajaona umuhimu wa kumhudumia huyo mtoto yatima....:twitch:
 
Yaani sijui inakuwaje watu wanashindwa kusaidia ndugu zao kama hivyo mimi sioni shida kabisa kukaa na ndugu wala mtoto wa mume ilimradi heshima yangu ipo na kila kitu napata
 
Huyu mwanamke anakosa huruma kabisa kwa huyo mtoto anasahau kama na yeye amezaa. Leo yupo kesho hatakuwepo atapenda watoto wake warushwe dana dana kama anavyomfanya huyu mtoto? Ushauri wangu kwake ni kuwa aende pale walifunga ndoa huyu mama anahitaji mafundisho makubwa ya kiroho. Biblia inasema tuwaangalie yatima na wajane, tuwasaidie wenye shida... nadhani ataelewa na atabadili msimamo.
 
Hapendi ndugu wa mume au hapendi tabia ya huyo kijana ndugu wa mume anayesema ni mtundu kashindikana?hilo la kutoshirikishwa laweza kuwa sababu tu ya kujazia ila kama kijana ana tabia zisizovumilika huyo mama nae ni binadamu yawezekana hawezi.....huyo nduguye pengine si mtundu na hajashindikana......:coffee:
 
Mkuu ChiefmTz, mimi siyo mchaga! Ila kwa sababu umetutajia kabila ya huyo mama, hebu tutajie na kabila ya huyo mume ili tukupe maushauri yaliyoenda shule.. Kabila ya mbaba please...
 
DAWA NI RAHISI SANA.
Nimeshuhudia kwa jirani yangu nae alioa huko huko uchagani mke hataki ndugu zake. Dawa ni rahisi. Jino kwa jino. Akimkataa ndugu yako kataa wake, ukifanya hivyo atakuelewa na atakubali ndugu zako. Ukiwaruhusu tu ndugu zake utakuwa umewasaliti ndugu zako. ACHA UJINGA fukuza tu.
 
OK, Thanks. Msg delivered: Nafikiri tunapo-post tuwe makini ili kutoumiza feelings za watu. Mtoa hoja nafikiri ange-edit kidogo ili isiwe kama ilivyo.
Ahsante kwa ushauri. Nimeshaedit. Pole dada Haika kwa usumbufu hakukuwa na nia yoyote mbaya ya kutaja kabila bali ilikuwa ni kujibu in advance maswali juu ya kabila.
 
unaweza kuita ligi au namna yoyote, lakini huwezi kubisha kuwa kuna watu ambao wanapoona tatizo katika mahusiano, wanashindwa kuwa objective bila kuhusisha dini au kabila.
Ni kweli kuwa utamaduni unaweza kumshape mtu, ni muhimu kujua mtu wako amekuwa shaped na vitu gani, ili uweze kusaidia kufany amaamuzi.

Huyu jamaa anakwazwa na kabila, kabila ni kitu mtu hawezi kubadili, ushauri ni kuwa amuache. na kwa kuwa kabila ni ishu kwake, asioe tena kabila la tofauti, atajikosesha raha bureee,
hakuna haja ya kumficha, mie kama mchaga nimeishi maisha yangu yote nikiwa na makabila mengine na neiona hio attitude haina DAWA.

Haya bwana, lakini hilo ni tatizo la malezi wala sio kabila.
 
Roho MBAYA,mimi cwez shangaa mwanamke wangu awe ivo lazma aende kwao,kwa nin awachukie ndugu zangu? Sasa anakua anamaana gan? Uyo jamaa yako kashkwa masikio na usikute KAPULIZWA ndo mana anashndwa kua na maamuz kama baba.
 
Mimi namshauri akae na mke wake amuulize msimamo juu ya kuishi na ndugu ukoje, kama wanakubaliana no ndugu basi kila mtu asilete ndugu, sio wewe unakataa ndugu wa mwenzio halafu wewe unaleta wa kwako. Na amwambie huyo kaka (denti) akija kukaa hapo na yeye anaenda kukafuata kale katoto, sometimes application ya jino kwa jino inafaa kwa watu kama hao.
 
DAWA NI RAHISI SANA.
Nimeshuhudia kwa jirani yangu nae alioa huko huko uchagani mke hataki ndugu zake. Dawa ni rahisi. Jino kwa jino. Akimkataa ndugu yako kataa wake, ukifanya hivyo atakuelewa na atakubali ndugu zako. Ukiwaruhusu tu ndugu zake utakuwa umewasaliti ndugu zako. ACHA UJINGA fukuza tu.

Mh hii inanipa tabu kidogo, sipendi kusema ukabila ila nadhani kuna tatizo kwa akina dada wa kichaga. Ninamfahamu rafiki yangu sana nae alioa mke uchagani, huko maeneo ya rombo, nae ni hivyo hivyo hataki kabisa ndugu wa mume wala hataki mume asaidie chochote kwa ndugu zake. Huyu kaka alikuwa anakaa na mtoto wa dada yake, huyu dada na mume wake wote sasa ni marehemu na huyu mke alimkuta huyu mtoto . Ila mke wa huyu kaka kakataa kukaa na mtoto huyu (yatima) na imelazimika mtoto achukuliwe na mama yake mkubwa. MM nilidhani labda itakuwa ni tatizo la huyu dada tu, ila ninaposoma hii michango, nadhani kuna tatizo kubwa.
 
Hapendi ndugu wa mume au hapendi tabia ya huyo kijana ndugu wa mume anayesema ni mtundu kashindikana?hilo la kutoshirikishwa laweza kuwa sababu tu ya kujazia ila kama kijana ana tabia zisizovumilika huyo mama nae ni binadamu yawezekana hawezi.....huyo nduguye pengine si mtundu na hajashindikana......:coffee:
The boy at the time analetwa he was just 7yrs. Kwa hy suala la kushindikana halipo kwa sbb bado alikuwa kwenye age ya kufundishika. Kama ilivyotokea kwani amechange sana utadhani sio yule. Hoja ya utundu haina mashko
 
hahaha!sawa crash lkn je,,amewahi kuongea nae mara ngapi juu ya hilo kabla ya kumtimua?
Jamaa anadai kuwa alishaongea mara nyingi sana kuhusu hilo na iliwahi kutokea mke akatishia kuondoka kwa sababu ya mtoto huyo. Jamaa pia alimuelewesha mkewe kuwa kwa nature ya kwao hakuna atakayemuelewa iwapo atamrudisha nyumbani kwao na lau kama wazazi wa mtoto wangekuwepo isingekuwa issue. Lakini mke hataki kuelewa
 
Bila sababu tu hataki kuelewa? Mwambieni aje aonane na mimi tuzungumze, aniambie anawaza nini juu ya huyo mtoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom