Mke anashinda Kanisani !!

Too much of something is harmful!..
Anaiombeaje familia wakati hashindi nayo, mapepo yakipanda kichwani mtu haelewi hata anachokifanya!..Ukiwa na imani hata ukijifungia chumbani na kuomba, maombi hujibiwa na Muumba!!
 
na hiyo kurudi nyumbani na mapambio yake, hapo unakuta kelele mtindo mmoja kama anapunga mapepo vile, awe na kiac....wokovu nao ukiuingiza sana kwenye maisha unaleta shida jamani, sasa mama wa familia unashinda kanisani mbona hata kwako kunaweza kuwa kanisa tu na sala/maombi yako yakackika?

bora anayefanya hivyo kuliko yule anayeenda kwa waganga akuwekee libwata, kukuandika jina lako kwenye mihirizi, anayejenga nyumba kwao bila hata kukuambia, anayetafuta upate hela ili akumalize, anayekunywa mipombe na kulewa bar akishikwashikwa na wanaume wenzio. ni mara mia bora huyu anayeenda kanisani kumtafuta Mungu. unasemaje hapo?
 
Too much of something is harmful!..
Anaiombeaje familia wakati hashindi nayo, mapepo yakipanda kichwani mtu haelewi hata anachokifanya!..Ukiwa na imani hata ukijifungia chumbani na kuomba, maombi hujibiwa na Muumba!![/QUO

hapa haongei yeye, you must know that this is a third party hearsay message, angeongea yeye hapa pengine angetoa sababu kwanini anaenda kanisani, na anaiachaje fmailia yake. tungesikia upande wa pili ndo tungetoa hayo malalamiko mnayoandika, hakuna kesi ya kuhukumu upande mmoja. hivyo unavyoongea uwe unamfikiria na upande wa huyo mama. hakuna mwanamke anayeweza kuwaacha watoto wake bila kitu. lazima atakuwa anaacha mazingira mazuri kwa watoto kula na kupata kila kitu, isipokuwa dukuduku la huyu mwanaume ni kwasababu tu huyo mdada ameacha katoliki akajiunga na kanisa lingine ambalo yeye hapendi. this is the issue here kwa huyo jamaa, na wala si kushinda kanisani.
 
Hekima na kiasi tu vimekosekana.
Hakuna kanisa la kukufanya uwe mtumwa na usitekeleze wajibu wako kwa familia na taifa
Lazima kuna tatizo hapo la kiufahamu kwa mhusika
Mbarikiwe

nakushauri kuwa, hakuna kiasi katika kumtafuta Mungu. Mungu anasema, nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, hivyo ukimtafuta Mungu sana utamwona sana. hakuna kiasi hapa. acheni hekima za kibinadamu, fikirini na mambo ya rohoni pia. mwogopeni Mungu. mara nyingi ninyi watu mnayatukana sana makanisa ya kilokole, lakini mkishashindwa huko duniani mnakuja kwa hawahawa walokole wawaombeeee, pale mnapokuwa mmepigwa na dunia, pressure, strock, mnatembea ubavu mmoja juu mmoja chini, choka mbaya, ndo mnakuja kwa walokole, mkiwa wazima hivi mtatukana na kuwadharau wanaomtafuta Mungu. jueni ya kuwa ni Mungu tu aliyewasaidia hata leo hivi mkafika salama toka kazini, asingekuwa huyu Mungu mgegongwa hata na magari. NENO LA MUNGU LINASEMA, WEMA WA MUNGU UNAWAVUTA WAOVU ILI WAPATE KUTUBU, hivyo ukiona unaishi maisha mazuri, ujue Mungu anakusaidia akitarajia utamkumbuka na kumtafuta, ukamuweka yeye wakwanza kuliko vyote, lakini wapi, bado unaona unastahili tu kila kitu. jueni ya kuwa Mungu ndiye aliyeshika hiyo pumzi mnayooongea kwa kiburi, akiamua kuachia pua hiyo sasahivi unaenda kufukiwa. MKUMBUKENI MUNGU, MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO, KABLA HAZIJAJA SIKU MBAYA KWAKO.
 
kuna hao na wale wanaokuwa 'bize' kila waume zao wanapokuwepo nyumbani!,a sign your marriage is dead...simply she is avoiding you and the silenceness/strangeness that comes when the two of you are having a contact!!...home becomes uncomfortable place since theres no peace/harmony!...she 'turned' to church just like people would turn to alcohol/drugs to avoid problems!!!
 
Ubomoaji with horns raised high up!
Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!...Haiwezekani ukapotelea kanisani na kuacha majukumu ya kifamilia...Ndo shida ya kulimbukia dini hizi!...Mungu alijua wazi mambo hayo na ndo maana aliweka siku 6 za kazi na akastarehe siku ya saba, ambayo ndo hasa tunaitumia kuabudu na kujumuika, tofauti na siku zingine!
Hakuna jambo lisilokuwa na kiasi!...Mwambieni huyo mama kwamba hata kuhudumia familia ni ibada!

HIVI NINAVYOONGEA KUNA WATU WANATAMANI WANGEGUSA HATA UWANJA WA KANISA TU WAMBABUDU NA KUMSIFU MUNGU, lakini wamelala kitandani, wengine hata kuongea wanashinda hivyo wanaongelea kimoyomoyo tu. acha kiburi cha uzima, acha wale wanaomtafuta Mungu wamtafute. Bwana asipoujenga mji wake waujengao wanafanya kazi bure, Bwana asipoijenga nyumba yake waijengao wanafanya kazi bure, Bwana asipoulinda mji wake waulindao wakesha bure.....Bwana asipoilinda ndoa yako wewe unayefikiri kuwa unaacha kumtafuta Mungu ili umufurahishe mumewako/mwanadamu, unafanya kazi bure, sik uzote njia ambazo haziendani na mpango wa Mungu (kumtafuta na kumthamini Mungu kuliko vitu vyote na watu wote), huishia pabaya. mtumainini Mungu, acheni kutegemea wanadamu, acheni kuwafurahisha wanadamu, ACHENI KUTAFUTA KUWAFURAHISHA WANADAMU, DUNIA NA SHETANI, haita wasaidia.
 
kuna mama mmoja ndoa imevunjika kwa style hii ..yeye alikuwa ni kanisa ,mkesha na yeye..mme akamwambia ameamua kumuacha aendelee na kanisa na yeye kuoa mwanamke anayempenda na kumjari .
mama atakaejua amekula ameoga na amelala wapi ..sasa dada anatapatapa hana cha kufanya na mme ndo kishaoa mke mwingine

vyovyote itakavyokuwa, bora unatafuta uzima wa milele. itapona tu, Mungu huwa hamtupi mtu wake hata sikumoja, hata kama utaona kama mtu ndo huyoo anaenda kuangukia kwenye moto au kwenye maji marefu, Mungu amesema hata huko hautaangamia. nakuhakikishia kama utamtafuta Mungu, ukaacha kufanya vitu kwa kuwafurahisha wanadamu, utapata thawabu kubwa sana kwa Mungu, na Mungu hatakuacha kamwe.
 
Too much of something is harmful!..
Anaiombeaje familia wakati hashindi nayo, mapepo yakipanda kichwani mtu haelewi hata anachokifanya!..Ukiwa na imani hata ukijifungia chumbani na kuomba, maombi hujibiwa na Muumba!!

uwo mstari umeutoa wapi? au ni hekima tu iliyoko kwenye kicha chako? do you think your personal words and suggestions/opinions can override God's words?
 
Too much of something is harmful!..
Anaiombeaje familia wakati hashindi nayo, mapepo yakipanda kichwani mtu haelewi hata anachokifanya!..Ukiwa na imani hata ukijifungia chumbani na kuomba, maombi hujibiwa na Muumba!![/QUO

hapa haongei yeye, you must know that this is a third party hearsay message, angeongea yeye hapa pengine angetoa sababu kwanini anaenda kanisani, na anaiachaje fmailia yake. tungesikia upande wa pili ndo tungetoa hayo malalamiko mnayoandika, hakuna kesi ya kuhukumu upande mmoja. hivyo unavyoongea uwe unamfikiria na upande wa huyo mama. hakuna mwanamke anayeweza kuwaacha watoto wake bila kitu. lazima atakuwa anaacha mazingira mazuri kwa watoto kula na kupata kila kitu, isipokuwa dukuduku la huyu mwanaume ni kwasababu tu huyo mdada ameacha katoliki akajiunga na kanisa lingine ambalo yeye hapendi. this is the issue here kwa huyo jamaa, na wala si kushinda kanisani.

Nimechangia kutokana na upande mmoja wa stori,inawezekana ningesikia pande zote mbili comments zingekuwa tofauti. Ni hilo tu, vinginevyo siyo kila kitu ni kukubaliana na mtu!..kama nimekukwaza, nisamehe mana unashambulia!!..Usiandike kwa hisia nzito hivyo mkuu!!
 
ubungoubungo huwa unaimba naye mapambio nini??? lol

hapana, hata simfahamu. ila namwomba sana Mungu afungue macho ya kiroho ya watu humu jf, ili wajue kuwa, Mungu ni wa muhimu kuliko watu wote na vitu vyote. hii dunia ndugu yangu inapita na mambo yake yote, na watu wake wote. ukijenga nyumba yako juu ya mchanga, hakika siku mafuriko yatakapokuja utajuta, ila ukijenga nyumba yako juu ya mwamba ambao ni Yesu Kristo through his words, hata mvua, mafuriko yakija, hakuna shida. Mungu akusaidie ujue hili.
 
Nimechangia kutokana na upande mmoja wa stori,inawezekana ningesikia pande zote mbili comments zingekuwa tofauti. Ni hilo tu, vinginevyo siyo kila kitu ni kukubaliana na mtu!..kama nimekukwaza, nisamehe mana unashambulia!!..Usiandike kwa hisia nzito hivyo mkuu!!

Nashukuru mkuu, wala haujanikwaza, ndo ongea yangu. kama nimeongea kama nashambulia, naomba chukuliana nami tu, ndivyo nilivyo. Mungu akubariki.
 
You know, in the Bible, you have this story of the clay and the potter, God tells us that, he is the potter and we are the clay, we can never talk back to God, kwasababu yeye ni Mungu, hawezi kabisa kubishana na mwanadamu. chungu hakiwezi kubishana na mfinyanzi. LAZIMA UFANYE CHOCHOTE ANACHOSEMA MUNGU KTK NENO LAKE BILA KUULIZAULIZA MASWALI AU KUKOSOAKOSOA, haustahili hata kukosoa chochote kile Mungu alichokiweka kama foundation....so, kama Neno la Mungu linasema ya kwamba, nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, ina maana ya kwamba, unatakiwa kuchukua garama yoyote ile, lakini umpate Mungu. Ndiyo, unatakiwa kubalance kidogo kwaajili ya hekima ambayo Mungu amekupa, lakini katika yooote, ni lazima Mungu kwanza. God promises that, you will never be ashamed kama utakuwa mwaminifu kwake, that means, hatakuangusha ukaaibika kwa lolote hata kama dunia itaona kama ndo unaaibika au unaenda kuaibika. remember, kumbuka kina shedrack meshack na abednego, hadi walitupwa kwenye moto Mungu anaangalia tu hadi pale walipokuwa kwenye moto ndo akatokea, hivyo hata mtu yeyote hata akiwindwa na familia yake au na mtu yeyote kwasababu anamtafuta Mungu, kuna siku Mungu atatokea na maadui zake wote watanyamaza kimya.

makanisani wanafundisha sana kubalance, na watu wanabalance, isipokuwa, kuna iii kasumba watu wanachukia makanisa ya kuokoka, hata wakifanya mazuri kiasi gani wao kwao ni kibaya tu. ila wakipatwa na kiarusi au wakipigwa na ngoma, au uchawi na hirizi zao za kazini zikianza kuwarudi utakuta wameanza kutafuta walau mlokole mmoja awapige maombi, hapo ndo ajabu sasa.
 
Ni upepo tu wa mabadiliko ambao utapoa. Cha msingi awe kanisani kweli. Pia kuna gap ambalo mwanamke anajaribu kuliziba, tena bila ya wao kujua pengine. Pia keshajazwa hofu ya mchanganyiko wa maisha ya kiroho na kimwili kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi binafsi. Huyo mwanaume amchukulie aste aste kwani akiwa mkali mke atazidi kujitenga nae. Wanaume ishini na wake zenu kwa akili.
 
kuna hao na wale wanaokuwa 'bize' kila waume zao wanapokuwepo nyumbani!,a sign your marriage is dead...simply she is avoiding you and the silenceness/strangeness that comes when the two of you are having a contact!!...home becomes uncomfortable place since theres no peace/harmony!...she 'turned' to church just like people would turn to alcohol/drugs to avoid problems!!!

I could't agree with u more...she might have her reasons....but I am not with her when it comes to neglecting her kids... watoto wanataka malezi jamani ukisha kuwa na watoto lazima uache uselfish bana...
 
ubungox2 umesema yangu yote na ziada....! kuna wanawake kutwa wanashinda bar na jioni anataka kwenda club, weekend anataka rusha roho .....asubuhi supu bar na sio chai nyumbani kwake.......HERI HUYO MWANAMKE AMECHAGUA FUNGU JEMA.....!Je huyo mwanamume alitaka awe anasikia stori kuwa mke wake huwa anaenda gesti fulani? au anashinda bar? au taarabu ikipigwa yeye akiwa chakari ndo hunyesha mauno?TUMPE MUNGU NAFASI YETU.....!
 
Too much of something is harmful!..
Anaiombeaje familia wakati hashindi nayo, mapepo yakipanda kichwani mtu haelewi hata anachokifanya!..Ukiwa na imani hata ukijifungia chumbani na kuomba, maombi hujibiwa na Muumba!!


Kishapata mtu kule kanisani anayemrusha akili zake hata nyumba yake haitaki tena.
 
Rafiki yangu analalamika....,

Ndoa yake na mkewe haina muda mrefu sana , wote wana toka katika familia ya kikristu wa dhehebu la Kiroma na ndipo walipofungia ndoa yao.

Mungu kawajalia watoto na kazi nzuri pia.

Kwa takriban miezi saba sasa, Mkewe ambaye anaelimu na kazi nzuri amekuwa akisali katika moja ya haya makanisa ya "upendo/upako". Alianza kidogo kidogo kwa kuhamasishwa na wenzake sasa amebobea kuliko hata "mama mchungaji", imefikia kiasi cha kuwa kama amerogwa na "neno", kila siku anachelewa kurejea nyumbani toka kazini na mume akimuuliza anamjibu alikuwa kanisani...na akirudi nyumbani ni mapambio tu kwenda mbele,

Kwa siku za jumamosi na jumapili, inakuwa kama mama hayupo kabisa nyumbani na huwaacha watoto na msichana wa kazi akidai yeye yupo kanisani kuiombea familia yake.

Rafiki yangu anasema amejaribu kumsihi sana mkewe amunguze hiyo kasi ya kanisani ili pengine aangalie familia na asiache muda mwingi wa majukumu yake unachukulia na msichana wa kazi. Lakini sasa mke imefikia mahala anasema hawezi kamwe kuacha kanisani hata sekunde moja na ni heri aachike kuliko kupoteza ufalme wa mbingu...na anamweleza mumewe kuwa akizidi kumkera kwa hili la kushinda kanisani itabidi akaombe maombi maalumu ya kufunga kwa ajili yake kwani anaona yeye sasa ni kama ibilisi.....

Hivi hali inapofikia hivi, tunajenga au tunabomoa??...
Huyu jamaa inaonekana hata haki ya ndoa hapati tena siku hizi...hiyo ndoa yao inawalakini na iko njia panda ya sijui wapi....inabidi wakae waongeeee.....pole boss....
 
Back
Top Bottom