Mke Ananigombeza Kisa Nilitafuta Kimada Mmoja Tuu

madaili

Member
Mar 6, 2014
32
27
Stori inaanzia miaka ya 80 huko, kipindi damu inachemka, nilijuana na dada mmoja mzuri, mwenye upeo na uzuri wa kimaumbile.
Baada ya kukutana mara kadhaa nilifall in love naye, na kwa kuwa nilikuwa na mke, nilijua itakuwa ni ngumu kuwa serious naye. Moyo ulikuwa unataka, ila nafsi ilinisuta. Lakini bado niliendelea na uhusiano wa kuiba iba naye. Siku moja akaniambia ana shida, kwamba nyumba yake inavunjwa muda si mrefu na hatakuwa na sehemu ya kuishi. Kwa kuwa nilikuwa na kiwanja maeneo ya boko ambacho mke wangu hajui, nikamwambia basi usihofu kwani ninajenga nyumba mitaa ya boko nikimaliza kwa muda ambao utakuwa unahama itakuwa tayari, nitakuachia uishi pale, akakubali na kwa muda huo nilikuwa najaribu kumsaidia tuu kama jirani wa chumba cha pili aliyekuja kuomba chumvi.
Baada ya nyumba kukamilika nilimkabidhi funguo na akaamia kwenye nyumba hiyo. Tokea siku hiyo mapenzi kati yangu na yeye yalikuwa kwa kasi kama kifaru aliyekoswa koswa kuuliwa na majangiri. Nilianza kulala nje na mke wangu akaanza kuhisi kuwa kuna tatizo katika ndoa yetu, nakumbuka mara kadhaa alikuwa akiniuliza tatizo ni nini, lakini nilikuwa naepuka kumjibu maana niliogopa kati kati ya maongezi naweza nikapitiwa nikamwaga sumu zote tukaishia kuachana.
Baada ya miaka kadhaa kimada huyo aliniambia kuwa anamimba, mimba tena? Kila siku nilikuwa makini sana kufuatilia upango wa uzazi na sijawahi kwenda naye kavu kavu, manake tayari nina watoto watatu na wananiendesha mno, siwezi kuongeza mwingine manake nitashindwa kumpatia maisha mazuri na mahitaji muhimu katika maisha yake. Baadaye akaniambia kuwa nisihofu kwani mtoto ana baba yake na hilo swala ameshashugulikia. Basi nikajifikiria sana nikaona hii sio vizuri na inabidi niachane na huu uhusiano, ili mwanamke huyo aendelee na huyo kidume cha mbegu na mimi nirudi kuwa mume mwema kwa mke wangu.
Nikaanza kuwa muadilifu katika ndoa yangu na mke akawa ananisifu kwa jinsi nilivyobadilika, manake kila siku nilikuwa nampa surprise na narudi nyumbani mapema. Mambo yalikuwa mazuri kila siku nikurudi nyumbani ni shangwe, watoto walianza kunenepa, mke akapendeza, na nyumbani kila siku ikawa ni burudani na sherehe.
Siku moja wakati naoga nikakuta maji ni ya moto kupita kiasi, niliungua, nikaenda kuchota maji ya baridi kupooza kidogo. Baada ya kumaliza kuoga nikaenda kula, tonge la kwanza nikagundua msosi una chumvi kupita kiasi. Nikamuuliza mamaa vipi mbona leo mambo yamekuwa hivi, akanijibu, hujui eh, basi ujue mi najua.
Sikufikiria sana, nilihisi atakuwa amepitiwa au anastress zinamsumbua. Lakini wakati najiandaa kulala nikaona nguo za kulala zote chafu, na sio mimi niliyechafua. Ni mtu amefanya makusudi kuzigaragaza kwenye mavumbi. Hapo ikabidi nimweke mamaa kitako, nikamuuliza "Mamaa, lipi ni tatizo?"
Kumbe alishagundua uhuni niliokuwa nafanya na kimada huyo, nikamwambia nilishaachana naye. Akasema hajali hicho, kama simjali kimada, basi inabidi nikamfukuze kwenye ile nyumba niliyomhonga, na nikimaliza basi nimpe hati za nyumba hiyo ili aiuze tupate pesa za kumpeleka mtoto wetu chuo.
Ilikuwa rahisi kumfukuza kimada kwa kuwa alishaolewa na kuhamia kwenye makazi ya mume wake. Baada ya kuomba hati za nyumba na kila kitu nilirudi nyumbani nikampa mke na kumwambia kuwa kila kitu kimemalizika na kama akitaka aangalie kwenye simu yangu kuhakikisha kuwa hakuna mawasiliano na yule kimada tena.
Kesho yake asubuhi wakati najaribu kujiandaa kwenda kazini nikakuta maji ya kuoga ni ya moto mno, na bomba za maji hazitoi maji, nikaamua kutooga, chakula cha asubuhi pia kilikuwa hakiliki, kwa hasira nikaamua kwenda tuu kazini bila ya kuoga wala kula breakfast.
Baada ya kufika ofisini nikapata ujumbe kwenye simu yangu unasema "Wewe jinga kabisa, kwa nini ulikuwa na kimada mmoja tuu, hivi hujui kama ungekuwa na vimada kumi tungekuwa mabilionea sasa hivi?"
Mpaka sasa hivi sijui hata nimjibu vipi huu ujumbe wake.
 
Muambie nisamehe mke wangu, nimeacha ujingaa ntatafuta hao vimada 9 kabla ya desemba. Sasa niambie na wewe una michepuko mingapi?

Kila la kheri na majibu yake
 
Jokes haziwi ndeeefu, mliosoma mtatuambia kama inachekesha kwa likes zenu hapo juu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom