Mke anakwepa sana tendo la ndoa, nini kifanyike?

Hivi wakulu hapa hamjambo kwanza?

maandishi madogoooo
......
 
mweke chini mkeo ongea nae kwa LUGHA NZURI LAINI ILA ISIYOTUMIA TAFSIDA KABISAA MWAMBIE MAMA NATAKA HIVI NA HIVI NA HIVI NA UNAVOFANYA HIVI NA VILE NAKOSA RAHA KABISA SINA AMANI KABISA NYUMBA NAIONA CHUNGU KABISA...YANI MUELEZE YE MWENYE WE ATBADIRIKA COZ TIS IS NOT SERIOUS....KHA...MUME HANYIMWI UNYUMBA JAMNI.....
 
Charity hii post yako nimeisoma kwa umakini sana hivi kweli hawa Jini mahaba wapo???

1. Wapo FL1.. Tena akikushika hutaki hata kusikia habari ya mume. Na anakuwa mlinzi wako kusudi usifanye na mtu mwingine.

2. Kitu kingine, Wanawake wa hivi, ndio chanzo cha waume zao kwenda nje ya ndoa. Huyu Mama ajaribu kukaa na Mashangazi wamshauri jinsi ya kumlinda mwanamme. Maana Biblia inasema, Mwanamke atamlinda mume wake. Ukimnyima tenda la ndoa, hujamlinda.
 
Haya ni masuala ya kiimani zaidi my dear.Mimi naamini yapo haya majini na yanaharibu ndoa za watu na mnabaki mnalaumiana.

Hata wachawi pia nao huwa wanachangia sana kuharibu ndoa na kutoa vizazi vya watu.Kama umewahi soma kitabu cha 'mama yangu anakula nyama za watu'kinaelezea haya matendo yao ya kuwavuruga wana ndoa.

Pia ujue jambo moja,siku hizi dunia imejaa mambo mabaya sana tena ya kuua wengine.Laiti kama Mungu angetufunua macho yetu tuone kinachoendelea kwenye ulimwengu wa kiroho nadhani tungekuwa makreze.

Nishawahi sikia pia kuhus ndoa zilizopztz misukosuko kama hivi baada tu ya harusi kwa vile walipewa zawadi zilizokuwa za kichawi,na waliteseka mpaka walipofanya maombezi.

Kwa case ya huyu yote yanawezekana.inaweza kuwa ni masuala ya kisaikolojia.kibailojia na zaidi sana kiroho(asi-neglect hili jambo)

mmmmmmmmmmmmmmmmmh haya Charity tuombeana kwa mungu
 
asante Dreamliner hapo kwako nimekosa kidude cha thanx wala cha ku-quote sijui kimeenda wapi:D
 
Hivi mtu utapataje usingizi wakati husband yupo polisi?

Hawa watu hawalingani kwa shepu zao na siajabu wana mapenzi ya kudanganyana. Mke ana uzito wa kilo 90 (Ngoma nzito) na mume kilo 70 tu. Mke ana kipato mara 4 kumzidi mmewe(Maji marefu). Kwa hali hiyo nyendo za mke haziwezi kufanana na huyo bwana wake/mme. Ushauri: Wanawake wako wengi, atafute mwingine Saizi yake kwa umbile na ikiwezekana kwa kipato pia. Uaminifu wake kabla ya ndoa umemfanya awe *****/mshamba wa mapenzi.
 
Mhh,Mume sasa ingebidi ajue vizuri background ya mkewe kwa kweli

Katika mazingira kama haya,si kawaida sana kwa mwanamke kufanyiwa yoote hayo halafu bado anakua jeuri namna hiyo.Aidha background ya mkewe ina mashaka au si muaminifu.pia inawezekana mambo mengine kama mkewe katokea katika family inayoendekeza mila za ukeketaji pia,inaezekana alifanyiwa hivo akiwa mdogo

Pia inawezekana mkewe alificha rangi zake halisi.

Ila mshauri huyo jamaa asiseme sana nje hayo mambo ya ndoa yake coz ataishia hata kupoteza heshima yake kwa jamii,afanye hivyo tu kama kuna ulazima
 
Vile ninaelewa wanawake,being one myself.Hatupendi mwanaume anaye beg.Hatu pendi mwanaume ambaye anaonyesha hamu sana.tunapenda mwanume proud,mgumu,dont care and hata kama yeye ana earn centi chache awe yeye ndiye mwanaume-asinyenyeke ! The problem here is that huyu mtu amekuwa intimidated by the wife's business acumen.Its tym he mans up!

The second thing is that women wanataka seduction,yaani unamleta juu mpaka yeye mwenyewe ndiye anaitisha,kama arrangement yenu ni ile routine boring sana ya kumake love is as exciting to her as kupiga mwaki meno its obvious huyu mama amesha mzoea huyu bwana tena anaona sex ikiwa kazi ya ziyada ambayo haoni manufa kwake so ana avoid kuifanya since there is nothing in it for her.

This guy needs to flip the script, iwe sasa ni mama anamtafuta,anatakikana a withdraw kabisa,hata awe haongei ili yule mama ababaike kidogo,halafu bwana huyu afanye sex iwe exciting for the wife yaani ile naughty seduction halafu ana ignore so that pia bibi ajue she also needs it,na hata yeye anaweza akanyimwa ;-)
 
Kona Kali,
Huu ni ushauri mzuri sana.
Akifanya haya hasa la kwanza na la pili basi ajue hakuna tatizo.
Ajaribu haya hapa;

1. Aangalie kwanza upande wake kwa kutafuta mapungufu yake mwenyewe; kama vile lack of polite language, kuwa na affair nje, kutomwandaa mwenzake ipasavyo nk. then arekebishe kabla ya yote.

2. Akae na mkewe chini na kujaribu kumweleza (in a serious intention) yanayomsibu na madhara ambayo yanaweza kutokea katika ndoa kwa ajili hiyo.

3. Atambue tu kwamba life has no a fixed fomula to apply, sometimes force is fruitful and sometimes freedom, so let him try to apply whichever is seem to be so and available by the time and situations. Too much freedom might be harmful also.

4. Inaonekana mahusiano yao hayakuwa na background imara, alipaswa kuwa na walau consultant juu ya mahusiano yao tofauti na mchungaji, paroko nk.

5. Asisahau haya katika maombi yake ya kila siku, hivyo ajaribu kuyakabidhi kwa Mola wake atie marekebisho kwa mkewe.

6. Ajaribu kuchunguza kwa undani na taratibu sana, huenda mwenzake anawajibika huko nje; hii ni feeling niliyoipata kwa kiwango kikubwa sana.....!

7. Kama anaweza kuongea na mama mkwe wake basi ayaeleze haya, kama hawezi amtume hata mtu wa kuongea naye ili ajaribu kuzungumza na bintiye na kumuelewesha kuwa hakuja kuimba kwaya, bali yupo kwenye ndoa. Mara nyingi wake zetu wanareflect wanachoshauriwa na mama zao.....!

8. Aache mara moja kufua na kupasi nguo, kudeki, kupika, na kumpakua chakula; provided mkewe yupo na ni mzima wa afya kabisa. Akiweza kufanya hivi mkewe atafanya maamuzi yatakayoashiria alichojiandaa nayo; kama vile kumleta mwanaume ndani, kuondoka na kurudi kwao, nk.

9. Ampunguzie haosegirl kazi na kumwekea mipaka ndani ya nyumba; kama vile kutofika chumbani kwao, kupika siku za weekend, kufua nguo zao, nk. Abaki tu kufua nguo za watoto, kudeki sehemu zingine za nyumba (with exception of master bedroom yao).
 
Mwanaume ana options zifuatazo:

1. Aanze utaratibu wa kupiga punyeto. Watu wengi wana mtazamo kuwa punyeto si kitu kizuri ila inabidi wafahamu kuwa punyeto ni sehemu ya maisha na ni muhimu kufanya kuliko kukosa uaminifu kwenye ndoa. Sisi tuliosomea psychology hasa ya wanawake na ngono tunawashauri wanaume kufanya punyeto.

2. Asiwaze kuwa na affair kama anampenda mkewe maana akienda nje na hana experience ajue hatarudi ndani. Nje ya ndoa jamani kuna kasheshe zake. Kama huyo hajawahi kucheat its not very advisable anaweza kutorudi na akakosa mke na kupoteza hata hamu na watoto.

3. Asikubali kuwa weak kwa mke. Kama anaweza amtimue mke kwa kumrudisha kwa wazazi au kuseparate kwa muda. Kama anaweza atafute kazi nje ya mji au ampeleke nje ya mji. Distance makes the heart grow fonder or colder but its worth the try.

4. Lazima atambue kuwa sisi wanawake ni watu selfish (i am sorry my female colleagues). hatukuumbwa kwa ajili ya kuwafurahisha nyie. Tuna commitment nyingi. Kwa huyu dada kwa hela aliyonayo ambayo ni 4times ya mwanaume sex kutoka hata mara moja kwa miezi 6 yenyewe ni ya kushukuru.

Sijui wenzangu wanaonaje lakini hayo ni maoni yangu.
 
Inaonekana NDOA inakasoro - Mume alimpenda mkewe kwa dhati na akafunga naye ndoa - lakini mkewe HANA MAPENZI NAYE - no chemistry - na inaonekana alitaka kufunga ndoa mradi tu nayeye kafunga ndoa ila - its obvious hakuna mapenzi hapo -

Ushauri:

1) amwombee mkewe Mungu aweke upendo ndani ya moyo wake
2) ajieleze kwa mkewe madhara yanayompata - labda mkewe haelewi kuwa anateseka
3) avumilie - labda alioa bila kumshirikisha Mungu kuwa ndoa hiyo ni Mpango wa Mungu kweli au alikurupuka
4) atulie kwani kila chenye mwanzo kina mwisho - mwisho wa taabu yake utafika tu siku moja
 
Uwanja wa suala hili ni mpana sana (prosperity93):

1.Inawezekana Mke ana matatizo ya kisaikolojia yanayomfanya asijisikie askhi na mumuwe, na mambo kama hayo yanahitaji ushauri nasaa (hivyo nawaachia wataalamu)

2. Inawezekana kuna vitu ambavyo mume anakosea kimwili ambavyo vinamfanya mke asiwe na ashki kwa mfano usafi (hapigi mswaki vizuri hivyo ananuka mdomo, ana jasho lenye harufu kali, usafi wa sehemu zake husika n.k) vitu kama hivi vinaweza kumfanya mke akuepuke kwani kuibusu midomo itoayo harufu mbaya yataka moyo wana JF

3.Yawezekana mume ana pupa mno kiasi cha kumuumiza au kuwa kero wakati wa tendo, ikumbukwe kuwa mwili wa mwanamke si gogo la mti au jiwe,sasa kama ndugu yetu akikwea anatandika raundi tatu kwa vurugu kiasi kwamba mmke anaugua siku mbili zinazofuata basi si la ajabu akawa anatafuta njia ya kumuepuka mume.

4. Yawezekana mapenzi yameisha, inapaswa ikumbukwe kuwa mwanamke ataendelea kumpenda mumu wake mpaka pale sababu iliyomfanya ampende huyo mwanaume itakapopotea...je ndugu yetu anaijua sababu iliyomfanya huyo mwanamke akubali kuolewa na yeye.Kama mwanamke alimpenda jamaa kwa ajili ya fedha alizokuwa nazo na sasa mwanamke ana mshahara mkubwa kuliko yeye asishangae kuona nyoka halambi unga

5. Jamaa kawa mnyenyekevu kupita kiasi....ikumbukwe mungu mwenyewe ametupa sisi wanaume nafasi ya kuwa vichwa kwenye nyumba zetu...na ni jukumu letu kuwapenda wake zetu na wao ni jukumu lao kututii....sasa inapotokea mwanaume ukawa unajilegeza kupita kiasi a.k.a ndio mama, kwa kila jambo usishangae mkeo kuanza kuleta dharau.Hata mtoto uliemzaa ukiwa unamuitikia kila kitu ataanza kukuletea mbwembwe. Kwa kuwa jamaa ameshamueleza mkewe kuwa ana ashki ya kutisha ya unyumba sishangai mke kumtingishia kibiriti kwa kuwa tayari anajua jamaa hachomoi...(naheshimu haki za kina mama ila tu zisi athiri haki za kina baba)

6. Je, ndugu yetu amejijengea mazingira ya kuzunguza kwa uwazi nini chanzo cha tatizo hili na mkewe?....wakati mwengine sisi wanaume tunawaweka wake zetu katika mazingira ambayo hata kama hawafurahii tendo la ndoa wanaogopa kutueleza kwa hofu ya kutukasirisha....sasa ukute kwa kuwa huyu mke anaogopa kuongea yale yanayomkwaza ndo mana anaona suluhisho ni kuepuka tendo

Ushauri wangu, ni kwa jamaa atafute namna ya kumdodosa mkewe ajua tatizo linatokea wapi,ikishindikana ashirikishe wazee wa familia au kidini...ikishindikan basi kila mtu atafute yule anaeona atamfaa zaidi...maisha haya ni magumu na si vizuri yule umpendae awe anayafanya yawe magumu zaidi.....
 
Kona Kali,
Huu ni ushauri mzuri sana.
Akifanya haya hasa la kwanza na la pili basi ajue hakuna tatizo.

YES Caren......!

Haya ndio madhara ya kutomegana hadi ndoa......! Jamaa angeyaona haya mapema na angeweza kuwa na uwanja mpana wa kufanya maamuzi yake na kuwa huru. Lakini huwa "nge" ikishatumika basi ujue hilo haliwezekani tena...! Hivyo, ajaribu tu hayo, huenda yakamsaidia.
 
Mhh,

Hapa nakosa maneno ya kusema.

Hili ni suala zito ila kama huyu jamaa ni dume kweli basi unaweza kuwa mchezo rahisi kama kumsukuma mlevi. Kuna wakati inabidi jamaa asimame kama mume. No sex no life in a marriage. Kama mwanamke anataka waendelee kuishi pamoja basi aache ubinafasi. Hawa watu wanahitaji kuongea kwa kauli za mamlaka zinazoweka conditions ambazo lazima zifikiwe ili waishi pamoja. Jamaa akiendelea kulia lia na kuona huruma sana atajuta. Ikifikia mahala mama na baba hawaelewani basi ni muhimu wakubali kufanyaa maamuzi ya busara ili kutunza watoto. Hii itamwezesha kila mtu ashike hamsini zake. I can't imagine my life without that delicious meal at least twice a week!
 
Tendo la ndoa ni muhimu sana kwenye ndoa yoyote ile. Kama mama mwenye nyumba hawezi kumridhisha mwenzie katika dept hii basi hii ndoa haina future. Kama wanandoa wote hawana tatizo la kiafya na juhudi za jamaa ili kurekebisha halii hii hazizai matunda yoyote basi asiendelee kupoteza muda wake katika ndoa ambayo haina uhai.
 
Tendo la ndoa ni muhimu sana kwenye ndoa yoyote ile. Kama mama mwenye nyumba hawezi kumridhisha mwenzie katika dept hii basi hii ndoa haina future. Kama wanandoa wote hawana tatizo la kiafya na juhudi za jamaa ili kurekebisha halii hii hazizai matunda yoyote basi asiendelee kupoteza muda wake katika ndoa ambayo haina uhai.

BAK ushauri wako ni atoe talaka ili aoe mke atakeyemtimizia hitaji la ndoa au???
 
me naona wakae na kuzungumza kusolve issue yao maana kunyimwa tunda duh ni kaaaazi kweli kweli
 
BAK unamshauri wako ni atoe talaka ili aoe mke atakeyemtimizia hitaji la ndoa au???

1st lady, afanye juhudi za kutafuta suluhisho la tatizo hili kwa kupitia nyanja mbali mbali kama juhudi zake zote zikishindikana na hakuna matumaini ya hali kuwa nzuri basi ndoa hii ni mfu, jamaa hastahili kupoteza muda wake.
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom