Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka (30)

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,892
31,091
MWANAMKE mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa Kibaoni mjini hapa, amewavunja mbavu wasikilizaji wa kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ipembe, baada ya kumjibu Hakimu kuwa kijana aliyemfikisha mahakamani hapo si mwanawe bali mumewe.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo Asha Abdallah anamshitaki mumewe, Kiemi Itambu (30), kwa kumwibia Sh 30,000 alizokuwa ameficha chini ya godoro.

Wawili hao wakiwa kizimbani jana, Hakimu Hosea Mkude alimwuliza mke: “Kwa nini wewe bibi unaolewa na kijana ambaye ana umri wa mwanao, huoni aibu?

Asha alijibu: “Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu.”

Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha’ hakimu: “Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?”

Majibu hayo yalisababisha watu waliojazana kwenye chumba hicho cha Mahakama, washindwe kujizuia na kuangua vicheko.

Ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa Kiemi alitenda kosa hilo Novemba 3, saa mbili asubuhi Kibaoni mjini hapa.

Asha alidai mahakamani hapo kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kumwibia Sh 100, 200 na 500, lakini safari hii alivuka mpaka kwa kuiba Sh 30,000 ndiyo maana akaamua kumfikisha mahakamani.

Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje baada ya kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya kutoa Sh 50,000 hadi Novemba 15 kesi hiyo itakapotajwa.

My take.

Hii ni hatari kubwa vipi hakuna sheria ya kulinda vijana dhidi ya ubakaji bila kujali jinsia.Sheria ya ubakaji inapendelea wanawake kwanini wanaume tusianadamane kupinga unyanyasaji wa aina hii kibibi kizee miaka 60 kuolewa na kijana wa miaka 30 ni uzalilishaji mkubwa.
 
Twende mbele turudi nyuma maneno ya Bibie AshaDii si huyu wa JF yana ukweli ndani yake.

Asha alijibu: "Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu."

Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha' hakimu: "Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?"
 
Kama kuna thread nyingine Mod waziunganishe hakuna kosa hata wewe ukikutana na uzi mzito kama huu lazima utapenda kuwashirikisha wenzako.

Hili lipost mbona likodublicated??!
 
kama wazee wenzake wameishiwa nguvu, na yeye bado mwili unadai mambo atafanyaje???
Si jambo la ajabu maana kuna wanaume wazee wa miaka kama 60 wanatoka na vibinti vya miaka 20
muhimu kama wamependana acha wale raha
 
Mwacheni bibi , kwa raha zake babuweee, sasa kesi ikiisha sijui wataendelea kuwa mume na mke?
 
Back
Top Bottom