Mkataba wa TRL (TRC)

I don't believe this................yaani aliyekuwa mshauri kiufundi baadaye anakuja pewa tenda ya ku-run the same company!!!.......yaani hatuna viongozi kabisa wa kuprotect interest za nchi.......damn!!

na viongozi waliopo inabidi wapelekwe/warudishwe ktk darasa la RISK ANALYSIS
 
What the @#$%? Yesu nisamehe leo ni Jumapili napaswa ongoza misa na si kutukana, lakini inabidi, msamehe mtumishi wako!

Hivi Serikali yetu inaendelea kujimomonyoa namna hii? Are we standing on quick sand and we are sinking?

What I want to know is what is our president do about this!

Infact I urge all Watanzania that are affected with this (Wafanyakazi, Abiria Wafanyabiashara) along the rail line to resist more Pilau and vote someone else in 2010.

We need to push for another special Parliamentary commision that will review ALL contracts entered by our government from 1992! These should be uuzaji mashirika, uwekezaji ans such!

Gademuit, these people think we are just going to sit down and say hewala? Hivi sasa let me ask, ikiwa treni haifiki Uvinza (assume) na hakuna barabara imara kufika Uvinza (assume), je Mha na Mmanyema wanaopigiwa kelele walime mawese, wavune chumvi na dagaa wengi watawasafirisha vipi? what about revenues kutoka Congo ambao ni land locked na wanategemea Makontena yao yabebwe kuingia melini na Karamagi?

I have said before, It is time Kikwete starts packing the boxes and prepare to go back to Bagamoyo or Chalinze and enjoy mafao in 2010!
 
This happens only in India!!

india1.jpg


india2.jpg


wahariri PICHA NZURI SANA HIZI..caption inayofaa...'" MOJA YA MAGARI MOSHI YA KAMPUNI MAMA YA RITES [INDIA]...AMABAYO NDIO MWEKEZAJI ALIYEPEWA NA SERIKALI KUENDESHA SHIRIKA LETU LA RELI....BAADA YA KUONEKANA ANAYO TEKNELOJIA NA MTAJI UNAOTOSHA KUENDESHA SHIRIKA HILO..."
 
Jamani inabidi tuwe waangalifu maana huu mradi wa Bwana Mkubwa na Ag wetu wa zamani ni mradi ambao umesainiwa huku JF na blogs zote zikiwepo wakati wa mchakato mzima.

Rites wanaown I believe 51% ya TRL na swali la msingi ni je wameinvest kiasi gani kupata hiyo ownership???

Wanapochukua kila kitu kutoka Rites India kwa bei za ajabu wizara iko wapi?? Oh samahani waziri anashare hapa!!

TRL wamepata mikopo ya almost $100 million guarantor akiwa wetu mtiifu BOT.

Sasa swali la msingi ni je Mbunge wetu kijana Zitto atatusaidia sababu ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge ambako TRL iko??

Zitto mkuu tunakutegemea sana maana TRL< Kiwira< Bandari na hata Tanesco i believe ukiwa makini unaweza kuleta changamoto.


Pinda jamani nimepata habari mbaya kuhusu yeye. Nasikia huyu mtu hawezi kabisa kuchanganua mambo na vioja vyake vitaanza rasmi kwenye issue ya Richmond bungeni soon.
 
Philemon, you are not serious Mkulu...... Ina maana walikuwa washauri wa TRC na kisha wakashiriki mchakato wa kutafuta muzimwaji (inaitwa kuwekeza ee) shirika hilo hilo.....

Halafu tunasema Madiwani wenye makampuni hawaruhusiwi ku tenda kwa kazi za halmashauri?? Duh, kaazi kweli kweli.....

Yaani jamaa walitayarisha mkataba/vigezo vya mwekezaji pale TRC, kisha wakaomba kazi na kisha wakaishauri TRC (technical advisor, usisahau hii cheo hapa) kujipa pasi........ Kweli hujafa hujaumbika....

On top of that wale bidders wengine wakaliona hili wakaamua kujitoa (walisema why?) and yet we proceeded with the whole process and gave the mighty TRC to Rites......

I rest my case, this is too much for my small head....

Ndivyo ilivyokuwa na kuna watu walishatoa tahadhari kuhusu suala hilo wakati PSRC wapo kwenye mchakato wa kumpata mwekezaji/mwendeshaji huyo. Wakaonya kabisa kuwa Rites ilikuwa inaifahamu TRC inside out na hivyo isingekuwa busara nayo ikaruhusiwa kuomba tenda hiyo.
kumbe andy chande ndiye alikuwa mchonga deal mkuu na onyo hilo halikupewa fikra zozote, kufumba na kufumbua, Rites ikashinda na leo tunayaona!
 
serikali imesema itawalipA mishahara wafanyakazi kama mujibu mkataba wao wanyongeza unavyosema.


sasa hapa vp?

nimesikia toka bbc dira ya dunia
 
MUHINDI ALIYEKUWA AKISIMAMIA HUO MRADI WA KUKARABATI MABEHEWA NA KUISHAURI MANAGEMENT KUPITIA HUO MKOPO WA BANK YA DUNIA KATI YA MWAKA 2002 HADI 2006 KUTOKA KAMPUNI YA RITES ..ANAITWA ENGNEER MUKESH..NA NDIE ALIYEHUSIKA KUANDAA SOME TECHNICALITIES...NA BAADAYE KWA KUSHIRIKIANA NA SUBASH PATEL NA CHANDE ..WAKAISHAURI RITES INUNUE TRC....

KWA SASA ENGENEER MUKESH AMERUDI TENA BAADA YA ZOEZI KUKAMILIKA AKIWA SASA NDIYE MKURUGENZI WA UFUNDI WA TRL...[CHIEF MECHANICAL ENGNEER...]WA TRL...

KWA KIASI KIKUBWA HUJUMA ZA KULIFANYA HILI SHIRIKA LA UMA KIYUMBE NA HATIMAYE KUWA MZIGO KWA SERIKALI HADI KUAMUA LIUZWE ZILIFANYWA NA HAWA WAHINDI WAKISHIRIKIANA NA SUBASH NA ANDY KAMA MWENYEKITI WA BODI NA HAWA KINA MBOMA KWA KUJUA AU KUTOJUA ..HASA PALE WALIPOKATIZA SAFARI ZA RELI ZIISHIE DODOMA ...MZIGO UKAWA MKUBWA KWA SHIRIKA KULIPIA WASAFIRI..NA MIZIGO MABASI HADI DODOMA...WASWAHILI WENZETU WAO WALIFAIDIKA KWA KUPEWA COMMISSION NA MAKAMPUNI YA USAFIRI AMBAYO YALIPATA KAZI KUPELEKA WASAFIRI NA MIZIGO DODOMA....NA HAPO SHIRIKA LIKAZIDI KUYUMBA KWA NAKISI YAO KUWA KUBWA...KUTOKANA NA KULIPA GHARAMA KUBWA HIZO NA ZILE ZA MAFUTA AMBAZO WALIKUWA WAKINUNUA KWA PESA TASLIM[BANKERS CHEQUE]..KUTOKA GAPCO AMBAYO NI KAMPINI YA MWENYEKITI WAO WA BODI ANDY CHANDE.....IKAWA HOOI KIPESA ...IKABIDI SERIKALI YA AWAMU YA NNE ILIPOINGIA IKAKUBALI MKATABA UANZE KAZI..UKISAINIWA NA CHENGE AMBAYE NDIYE PIA ALIYEDRAFT MKATABA UPANDE WA SERIKALI WAKATI AKIWA MWANASHERIA MKUU AWAMU YA TATU...

MKITAKA KUJUA RITES WALIFANYA HUJUMA MAKUSUDI WAKISHIRIKIANA NA MA ENGENEER WAZALENDO KUSHAURI NJIA YA RELI YA DODOMA TO DAR ILIKUWA MBOVU..SHANGAA KUWA NI HAO HAO TENA WIKI MBILI TU BAADA YA KUINGIA TENA BILA UKARABATI WA AINA YEYOTE ..WALIANZISHA SAFARI ZA RELI KUANZIA DAR [MABEHEWA NA ABIRIA].......

TENA MASIKINI RAIS WETU JK NA MAWAZIRI WAANDAMIZI BILA KUJUA AU WAKIJUA WAKAKARIRIWA WAKISIFIA WAHINDI WA RITES ETI ">>>wamefanikiwa kuanzisha safari za treni kutoka dar es salaam kwa abiria na mizigo ndani ya wiki mbili tu......bila hata kujiuliza ...."

phillemon michael:

Hata kama mtu angetaka asikubaliane na 'conspiracy theory' kama ilikuwepo; itakuwa vigumu sana kuyapuuza haya unayoyasema hapa:

" Mkitaka kujua RITES walifanya hujuma maksudi wakishirikiana na ma-engineer wazalendo kushauri njia ya reli ya Dodoma to Dar ilikuwa mbovu.. shangaa kuwa ni hao hao tena wiki mbili tu baada ya kuingia,tena bila ukarabati wa aina yoyote.. walianzisha safari za reli kuanzia Dar...."

This is absolute criminal! Watu kama hawa wanafaa kupigwa risasi kwa kuhujumu taifa!

Taarifa kama hizi ndio zinazofaa wabunge wetu wawe wanazijadili ili wananchi nao waweze kujua jinsi wanavyohujumiwa na wananchi wenzao.
 
Kuhusu TRC wakuu tulizungumza humu JF hata kabla ya contact kukabidhiwa hii kampuni ya wahindi...

Habari mpya toka ndani....
Nasikia kutokana na kashfa nyingi zinazokuja siku za usoni ndio maana PSRC ilivunjwa, hivyo ushahidi mwingi wa makabrasha umesha pigwa kiberiti.. wanavyodai wao kazi ya PSRC imekwisha!...
Ili kupata uhakika zaidi hivi ni kweli PSRC imeshavunjwa?..
 
Pinda jamani nimepata habari mbaya kuhusu yeye. Nasikia huyu mtu hawezi kabisa kuchanganua mambo na vioja vyake vitaanza rasmi kwenye issue ya Richmond bungeni soon.[/QUOTE]

KWELI PINDA HAWEZI KUCHANGANUA MAMBO ..BREAKING NEWS NI KUWA PAMOJA NA KUJUA RITES HAWAJAWEKA PESA ZA MTAJI....LEO AMEAMUA KULIPA SHILINGI BILIONI 3.5 KUGHARAMIA NYONGEZA ZA MISHAHARA KWA MIEZI MITANO..AMBAZO RITES NDIO WALITAKIWA WAZILIPE....NA WAO WENYEWE NDIO WALIOAHIDI HIYO NYONGEZA...PESA ZETU ZA KODI ZINAENDA KUGHARAMIA WAHINDI

..MWEKEZAJI GANI AMBAYE HATA KUGHARAMIA NYONGEZA NDOGO YA MSHAHARA WALIYOAHIDI HAWAWEZI..WAKATI TUNAJUA KUWA WAMEPEWA DOLA MILIONI 100 MKOPO NA BENKI YA DUNIA KWA KUDHJAMINIWA NA SERIKALI YETU..
 
Pillemon Mikael,
BREAKING NEWS NI KUWA PAMOJA NA KUJUA RITES HAWAJAWEKA PESA ZA MTAJI....LEO AMEAMUA KULIPA SHILINGI BILIONI 3.5 KUGHARAMIA NYONGEZA ZA MISHAHARA KWA MIEZI MITANO..AMBAZO RITES NDIO WALITAKIWA WAZILIPE....NA WAO WENYEWE NDIO WALIOAHIDI HIYO NYONGEZA...PESA ZETU ZA KODI ZINAENDA KUGHARAMIA WAHINDI
Whaat????..
Wait a minute..Je sii kweli kuwa RITES wako under contract ku run mradi huu na TRL inamilikiwa na serikali 100%!....
Kuna mtu mwenye mkataba wa hii kampuni auweke hapa?
 
serikali ina hisa za 49% na rites 51% kama niko sawa.

huenda serikali ikafidiwa hizo pesa baadae ila tusubiri wambeya watupashe
 
Pinda amesema kuwa huo ni mkpo kwa mwekezaji/mwendehsji huyo na atapaswa kuurejesha. lakini sijui kama kweli ataurejesha. nadhani wameshaanza delaying tactic, wanataka kuanza kuwachezea wafanyakaza wa TRL. Wamewapa hicho wanachokitaka ili wasahau huku serikali cun TRL ikijipanga vema na itakapofika hiyo Julai, watakuwa wameshapanga mikakati ya kukabiliana na wafanyakazi.
 
Pillemon Mikael,

Whaat????..
Wait a minute..Je sii kweli kuwa RITES wako under contract ku run mradi huu na TRL inamilikiwa na serikali 100%!....
Kuna mtu mwenye mkataba wa hii kampuni auweke hapa?

BREAKING NEWS.....

GET YOURSELF A COPY OF CONSESSION AGREEMENT BWT GOVERNMENT AND TRL ON TUESDAY-

PATA NAKALA YAKO (BINAFSI)YA MKATABA ULIOSAINIWA KATI YA SERIKALI NA TRL... JUMANNE
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameushtukia mkataba baina ya Serikali ya Kampuni ya Rites ya India kuhusu ukodishwaji wa lililokuwa Shirika la Reli nchini (TRC).

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli (TRL), iliyoundwa baaya ya kukodishwa kwa TRC, Pinda alisema mkataba huo una mushkeli, kwani kuna mambo ambayo hayaelewi jinsi yanavyoendeshwa.

Akitoa mfano, alisema kuwa wakati TRC ikikaribia kumaliza shughuli zake, ilieleza kuwa ina injini zaidi ya 90, lakini mara baada ya TRL kuanza kazi, ilieleza kuwa kuna injini takriban 50 tu.

Pia, wafanyakazi wa TRL wamesema kuwa mwekezaji huyo hakujali kukarabati vifaa hivyo vilivyopo, badala yake alikwenda kukodi injini nyingine kwenye kampuni yake ya Rites na tayari zimeshaingia injini saba ambazo zinalipiwa ‘capacity charge’ ya sh 600,000 kila siku hata kama hazifanyi kazi.

Jambo hilo limemfanya Pinda auone mkataka huo kama ile ya umeme ambayop inalikamua Tanesco. Wafanyakazi wa TRL wameshamuomba Pinda kuwa mkataba huo nao upelekwe Bungeni ukachunguzwe.

HATUTAENDELEA KWA SABABU HATUJUI KINACHOENDELEA

Hiki kihabari hapo juu ni mfano wa tatizo kubwa la nchi yetu: vyombo vya habari mdosho!

Siwezi kusema lolote kuhusu huu mkataba na kudokeza ni vipi mambo yangetakiwa yaende kwa sababu sielewi mambo yanavyotakiwa yaende sasa hivi, na yalikwendaje.

Pinda alikuwa anatembelea ofisi za TRL wakamuonyesha mafaili au kila mkataba unapita kwa Pinda? Na nini kinafuata, Pinda kaagiza nini, kuna watu watatemwa, au mkataba ufutwe? Pinda, au Kamati za Bunge zina nguvu gani hapa? (Leo tumelipa dola laki moja na elfu hamsini kwa mkataba wa Richmond ambao haukufutika!)

Wafanyakazi wa TRL nao wameulalamikia huu mkataba. Lakini, wafanyakazi wa ngazi za juu wemesema nini kuhusu huu mkataba? Nataka kujua TRL imejibu nini baada ya Pinda kuukosoa huu mkataba. Kampuni nyingine zilizoleta tenda zilikuwa bora kuliko TRL?

Waziri Mkuu katoa mfano kwamba TRL waliwaeleza wana injini 90 halafu baadae wakawaeleza wana injini 50. Lakini hivyo walivyo ambiana kwa nini hawakuviandika? Mkataba unawataka wawe na injini ngapi? Mfano wa Pinda nao una mushkeli.

Hii habari hapa kwanza hatujui inatoka wapi, bahati mbaya Mpita Njia hakuonyesha ni chanzo gani. Nikiisoma naona ni kama ya Tanzania Daima na majarida ya IPP, ambayo yanaandika habari nusu nusu na kishabiki shabiki, wakati watu tunataka pande zote. Huwezi kuchukia ufisadi kishabiki shabiki tu.

Vyombo vya habari ndio kiungo dhaifu kuliko vyote katika mnyororo wa kuvuta gurudumu la maendeleo. Na hatuwezi kufanya mabadiliko kama hatujui kinachoendelea. Tudai ukweli.

Mwana JF mmoja ana saini inasema:"Huwezi kuwa na ufahamu kama hujaasi, na huwezi kuasi kama huna ufahamu."
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameushtukia mkataba baina ya Serikali ya Kampuni ya Rites ya India kuhusu ukodishwaji wa lililokuwa Shirika la Reli nchini (TRC).

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli (TRL), iliyoundwa baaya ya kukodishwa kwa TRC, Pinda alisema mkataba huo una mushkeli, kwani kuna mambo ambayo hayaelewi jinsi yanavyoendeshwa.

Akitoa mfano, alisema kuwa wakati TRC ikikaribia kumaliza shughuli zake, ilieleza kuwa ina injini zaidi ya 90, lakini mara baada ya TRL kuanza kazi, ilieleza kuwa kuna injini takriban 50 tu.

Pia, wafanyakazi wa TRL wamesema kuwa mwekezaji huyo hakujali kukarabati vifaa hivyo vilivyopo, badala yake alikwenda kukodi injini nyingine kwenye kampuni yake ya Rites na tayari zimeshaingia injini saba ambazo zinalipiwa &#8216;capacity charge' ya sh 600,000 kila siku hata kama hazifanyi kazi.

Jambo hilo limemfanya Pinda auone mkataka huo kama ile ya umeme ambayop inalikamua Tanesco. Wafanyakazi wa TRL wameshamuomba Pinda kuwa mkataba huo nao upelekwe Bungeni ukachunguzwe.

Kwa maana nyingine hao wahindi walitoa info za uwongo ili kuweza kuupata mkataba huo wa kuendesha shirika la Reli. Hivyo siri kali ina kila sababu ya kuuvunja kwa kuwa hao wahindi hawakuwa wakweli na hivyo kuepuka hayo malipo ya shilingi 18,000,000 kwa mwezi za hizo injini saba, malipo ambayo yanafanywa hata kama injini hazifanyi kazi. Pia inabidi siri kali iyasimamishe malipo hayo mara moja.
 
Hivi mtu unawezaje kuliamini kampuni ambalo hata huko kwao watokako hawawezi kupata udhamini kwa ajili ya kupata mkopo toka World Bank!!!!
 
Sidhani kama Pinda anaelewa exactly TRL ni kitu gani. Serikali inahisa humo ndani almost 50%, sasa yeye anadhani ametoa mkopo kumbe mlipaji wa hizo hela bado ni serikali yenyewe, wenzake walimzungumka kabla TRL kila investment au mkopo lazima itoke TZ govt, hao Rites ni jina tu la wazee wa shughuli wa mjini.

Sasa imagine kulipa tu mshahara kidogo wanasema hawawezi, je rehabilitation wataweza vipi?? Hicho ni kitendawili ili ujue namna unavyoweza kuwa majority owner in TZ lakini watoaji mtaji ni wananchi wa TZ.

Hii tendency ya kuwa owner wakati mwenye kutoa investment ni Govt of TZ inabidi ipewe jina rasmi yaani KUCHENGE kwa sababu yeye ndiye architect wa deal zote za IPTL< SONGAS<KIWIRA<ATC<TRL<NBC<BARRICK<TANZANIAONE<
 
Pillemon Mikael,

Whaat????..
Wait a minute..Je sii kweli kuwa RITES wako under contract ku run mradi huu na TRL inamilikiwa na serikali 100%!....
Kuna mtu mwenye mkataba wa hii kampuni auweke hapa?

Mkuu Mkandara, Rites wanaown 51% lakini serikali ya TZ minority owner wako responsible kwa funding zote 100% together with Tax exemption on everything mpaka hata vinywaji vya soda, bia, petrol blah blah.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom