Mkataba tata wa mteule wa Kikwete huu hapa

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
LGA/115/2010/1011/Non.c.

Ni kampuni ya PAVICO LTD, ya Mkuu wa Mkoa wa Singida iliyoanza kufanya kazi ya kuzoa taka 19/08/2011 katika Manispaa ya Singida. Mkuu wa Mkoa huyo akalipwa na Manispaa shilingi 7,500,000/- Niambieni Mshahara wa Mkuu wa Mkoa ni kiasi gani mpaka akaamua kuwa mjasiriamali.

Kazi za Mkuu wa Mkoa ni pamoja na kusimamia Halmashauri zilizopo Mkoani kwake, kazi hiyo inamnyima sifa ya kufanyakazi yoyote ile ya ukandarasi au hata ya kuwa mjasiriamali. Tunalazimika kuishi katika uchafu kwa sababu ya UFISADI, Je haya tusihoji?.

Jamani wananchi wa Singida hivi kweli mtu kama Mkuu wa Mkoa wa Singida anaweza kupewa tenda ya kuzoa takataka wakati hana rikwama,lori, toroli, hana uzoefu wa kuzoa takataka na hajasomea kazi ya kuzoa takataka halafu nani atakayemwuliza endapo hatafanyakazi hiyo, lakini fedha ni lazima alipwe na Manispaa? Hata aliposhindwa kazi ya kuzoa taka, mtoto wake akaenda kulazimisha ndugu zetu kwa kuwamwagia SUMU.

POLISI WANAENDELEA KUMLINDA MTOTO WA KIGOGO HUYU KWANINI? Kikwete sawa tu, endelea kumlinda atukandamize zaidi.
 
Nachangia kidogo, madoro nijuavyo mimi Mkuu wa Mkoa alikuwa analipwa 7,000,000/= Kwa Mwezi. Ila Mwanzoni walipoanza mkataba alikuwa anazoa kwa malipo ya 125,000/- Kwa kila trip ya Tani 10.

Kilichofanyika ni wizi tu wa pesa za manispaa ya Singida, lakini wananchi hawawezi kuhoji kwa sababu ya Uzoefu wa kulinda Mafisadi unaoendekezwa na serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

Sisi tunaohoji tunaonekana wabaya kweli. Ila Kama Kikwete alimwacha huyu jamaa ili watukomoe hivi tutajuta, maana naona wameamua kweli kuvunja hata sheria za nchi. Kikwete pamoja na kujua hili atamlinda tu......... INAUMA SANA!
 
Wakuu wa huko Singida,hamuwezi kumshtaki secretariat ya maadili ya utumishi wa umma au hata mahakama za kawaida?
 
Nachangia kidogo, madoro nijuavyo mimi Mkuu wa Mkoa alikuwa analipwa 7,000,000/= Kwa Mwezi. Ila Mwanzoni walipoanza mkataba alikuwa anazoa kwa malipo ya 125,000/- Kwa kila trip ya Tani 10.

Kilichofanyika ni wizi tu wa pesa za manispaa ya Singida, lakini wananchi hawawezi kuhoji kwa sababu ya Uzoefu wa kulinda Mafisadi unaoendekezwa na serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

Sisi tunaohoji tunaonekana wabaya kweli. Ila Kama Kikwete alimwacha huyu jamaa ili watukomoe hivi tutajuta, maana naona wameamua kweli kuvunja hata sheria za nchi. Kikwete pamoja na kujua hili atamlinda tu......... INAUMA SANA!

We Isango,si utafute kazi na wewe ufanye?Tofauti yako na Kone ni kuwa wewe unatumia muda mwingi kunywa pombe na kufanya ngono zembe wakati Kone anatumia maarifa yake kufanya kazi za kujiletea maendeleo!Pia nikusaidie uachane na akili mgando:mwenye mkataba na manispaa ni PAVICO LTD,siyo Kone you fat young man!
 
Back
Top Bottom