Mkataba na Dhamana kwa Dereva wa....

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
habari zenu
Kuna gari ya mzigo nimetumiwa ya tonne 3, sasa nilikuwa nataka kumpa dereva afanyie kazi alete hesabu kwa wiki, nimesikia kuwa natakiwa niwe na mkataba naye, na pia awe na mtu wa kumdhamini, nilikuwa nauliza hivi vitu vina umuhimu gani? na nini hatari zake asipokuwa na mkataba na dhamana. naomba wenye ujuzi na hii kazi watoe darasa kidogo kwa faida ya wote
 
Mkuu sio mtaalamu sana kwa hili, lakini hilo gari lako la thamani pengine more than 10m kumpa mtu kienyeji bila mkataba sidhani kama ni busara. likija kutokea la kutokea huko mbele mkienda kwenye sheria mkataba ndio utakao ongea.
Nilikua na ka tax kangu nikampa dereva kienyeji kwa makubaliano ataniletea hesabu kwa mwezi, baada ya miezi 3 akagoma kuleta hesabu ya mwezi wa mwisho na akaniletea gari ameligonga. nilichukia sana nikaona ngoja nimpeleke kwa sheria, ilikua aibu hamna mkatba wala nini basi iliniwia ngumu nikaamua kuachana nae
 
habari zenu
Kuna gari ya mzigo nimetumiwa ya tonne 3, sasa nilikuwa nataka kumpa dereva afanyie kazi alete hesabu kwa wiki, nimesikia kuwa natakiwa niwe na mkataba naye, na pia awe na mtu wa kumdhamini, nilikuwa nauliza hivi vitu vina umuhimu gani? na nini hatari zake asipokuwa na mkataba na dhamana. naomba wenye ujuzi na hii kazi watoe darasa kidogo kwa faida ya wote

ungeanza kufanya research ya hiyo biashara kwanza na kikubwa ungekaa na wenye biashara kama hiyo na kusoma wanafanya nini, unakoelekea na kutokuja kwako hiyo biashara unaweza kulia kilio kikuu, nimeshashuhudia wastahafu wengi walijaribi kuingia kwenye hizo biashara+daladala na matokeo yalikuwa ni mabovu,
kama hilo gari limeshafika, lipaki vizuri na anza kuisoma hiyo biashara fizikali
 
habari zenu
Kuna gari ya mzigo nimetumiwa ya tonne 3, sasa nilikuwa nataka kumpa dereva afanyie kazi alete hesabu kwa wiki, nimesikia kuwa natakiwa niwe na mkataba naye, na pia awe na mtu wa kumdhamini, nilikuwa nauliza hivi vitu vina umuhimu gani? na nini hatari zake asipokuwa na mkataba na dhamana. naomba wenye ujuzi na hii kazi watoe darasa kidogo kwa faida ya wote

Mkataba ni muhimu Mkuu
  1. Mkatana ni Makubalinao baina yenu, iwe kwa maneo au kwa maandishi kuhusu yale ambayo kila moja wenu anawajibika kutekeleza.
  2. Mkataba ni kielelezo cha yale mliyoafikiana
  3. MKataba ni kelelezo cha kuthibitisha yale mliyokubaliana pindi litakapotokea lolote lile (ikiwemo gari kutumika bila madhumuni, dereva kudai alipwe zaidi, dereva kuleta makusanyo pungufu, dereva kutimka na gari nk)
  4. Mkataba utalinda haki zenu na pia kumwelekeza kila mmoja wenu nini anapaswa kufanya na nini anastaili katika hayo makubaliano.
  5. Mkataba ni msingi wa kuwafanya muonekane mlinuia kuwa na mahusiano ya kisheria na sio ya kirafiki, kindugu au jamaa iwapo mmoja wenu ataathirika kwa jinsi yeyote ile na makubalianao hayo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom