mukandarasi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 932
- 275
Watu kama Dr.Ulimboka lazima watokee katika jamii yoyote,na Dr.siyo wakwanza wala wamwisho kutokea.Watu wa aina yake huzalisha makundi yenye mitazamo isiyo fanana.Mitazamo hiyo hutafsiriwa kwa kadiri kila kundi lilivyoguswa na tukio lililompata Dr. bila kuwasahau wagonjwa ambao ndiyo msingi wa sinema nzima.Hao wanao mkejeli leo sijui watendelea kukejeli siku serikali itakapotekeleza madai ya madaktari na watoto wao watakapokuwa wanafaidi jitihada za Kina Dr.na wenzake.