Mkapa - zawadi ya ngombe zizini mwake kwa wamisionari

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
1.jpg
3.JPG

RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa ametoa zawadi ya ng'ombe wawili wenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 1.4 kwa ajili ya kitoweo cha wajumbe 15 kutoka nchi 60 duniani ambao watashiriki Mkutano wa Dunia wa Shirika la Roho Mtakatifu (Congregation of the Holy Ghosty), unaotarajiwa kuanza Juni 24 mjini Bagamoyo.

Akizungumza shambani kwake eneo la Vikawe, Bagamoyo mkoa wa Pwani mara baada ya kukabidhi ng'ombe hao kwa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambayo inaongozwa na Padri Joseph Shio, Rais huyo mstaaafu alisema ameguswa kutoa msaada huo kutokana na kulelewa na wamisionari wa shirika hilo. "Nimekulia katika mikono ya wamisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu ambalo lilikuwa linamiliki Shule ya Sekondari Pugu wakati huo ikiitwa St. Francis College kabla haijataifishwa na serikali na sioni kwanini nisitoe kidogo nilicho nacho kufanikisha mkutano huu muhimu" alisema Mkapa.

Alisema Rais huyo mstaafu kuwa licha ya yeye pia kuna wanafunzi wengine ambao walipita Pugu Sekondari ambao nao wamejitolea walicho nacho kuhakikisha mkutano huo wa kwanza kufanyika barani Afrika unafanikiwa. Mkapa alisema kuwa ng'ombe hao wawili ambao ametoa ni shemu ya zawadi ambazo alipewa na watanzania wakati anastaafu hivyo haoni kwanini asiwatoe zawadi kwa ajili ya shughuli hhiyo.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mkuu wa shirika hilo Padri Shio alisema Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndie ambaye ataufungua rasmi mkutano huo wa mwezi mmoja hapo Juni 29 mwaka huu. Alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili lilipotoka shirika, lilipo na litakapokwenda sanjari na changamoto ambazo zinalikabili na kutengeneza dira ya miaka nane hadi 10 ijayo.

Mkuu huyo alisema watendaji wakuu wa shirika hilo wangeweza kuufanya mkutano huo popote lakini wameona umuhimu wa Tanzania na historia ya mji wa Bagamoyo ambako ndipo shirika hilo lilipoingilia mwaka 1868. "Wamisionari wa shirika waliingia Bagamoyo wakitokea Zanzibar na kuasisi mbegu ya ukatoliki nchini" alisema Shio na kuongeza kuwa shirika hilo linatambulika vema ulimwenguni kutokana na huduma zake kwa wanajamii .

Alisema shirika hilo linatambulika kutoka na jitihada zake za kupiga vita biashara ya utumwa wakati huo kwa kuwanunua na kuwapatia elimu na matibabu wahanga wa biashara hiyo na toka wakati huo shirika hilo limezidi kupanuka nchini na duniani kwa ujuma likitoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya na masuala ya uchumi.​
 
Nimeipenda hii ranchi yake, wengi tujifunze kwani huko unapata faraja kubwa na pumziko la akili baada ya mikiki mikiki ya hapa na pale.
 
Nimeipenda hii ranchi yake, wengi tujifunze kwani huko unapata faraja kubwa na pumziko la akili baada ya mikiki mikiki ya hapa na pale.

mkuu inafurahisha unatuliza akili ukimaliza kufanya kazi,ila tatizo hiyo kutuliza akili wakati wa kumpunzika ndo wanawaza ufisadi
 
wazanzibar ndio walioleta ukatoliki huku bara kumbe ..ulianzia kwao huko visiwani ..sasa kwa nini shule kama pugu hazikujengwa huko visiwani? ama walizichoma moto???
shirika hilo lilipoingilia mwaka 1868. "Wamisionari wa shirika waliingia Bagamoyo wakitokea Zanzibar na kuasisi mbegu ya ukatoliki nchini
 
wazanzibar ndio walioleta ukatoliki huku bara kumbe ..ulianzia kwao huko visiwani ..sasa kwa nini shule kama pugu hazikujengwa huko visiwani? ama walizichoma moto???

Zanzibar walitangulia Waanglikana, hao RC wakaamua kuja bara
 
Hawa Mapadre ndo wanamiliki shule za Marian Girls and boys pamoja na Tengeru boys iliyopo Arusha.
Wamefanya maendeleo makubwa sana hasa katika upande wa elim.
 
Zanzibar walitangulia Waanglikana, hao RC wakaamua kuja bara

waangalicana walijengwa mashule kama shule ya minaki ilikuwa inaitwa st andrew high school..sasa kwa nini hawakujenga huko visiwani wakaja kujena bara? ...visiwani walizichoma ama kilitokea nini
 
waangalicana walijengwa mashule kama shule ya minaki ilikuwa inaitwa st andrew high school..sasa kwa nini hawakujenga huko visiwani wakaja kujena bara? ...visiwani walizichoma ama kilitokea nini

Wamisionari wote walianzia Zanzibar, ninachoshangaa wakakimbilia bara nini kilitokea wasifanye maendeleo kama ya bara kwa kuanzisha shule na vituo vya afya?
 
Wamisionari wote walianzia Zanzibar, ninachoshangaa wakakimbilia bara nini kilitokea wasifanye maendeleo kama ya bara kwa kuanzisha shule na vituo vya afya?

kijana unaonaje kwa jibu la haraka haraka? inawezekana kuchoma makanisa ni hulka kuanzia miaka ya 1800's ..kwa hiyo vyoe vilivyoanzishwa vilichomwa ..ama wewe unaonaje
 
kijana unaonaje kwa jibu la haraka haraka? inawezekana kuchoma makanisa ni hulka kuanzia miaka ya 1800's ..kwa hiyo vyoe vilivyoanzishwa vilichomwa ..ama wewe unaonaje

Inawezekana sababu hapo awali hakukuwa na kumbukumbu ya matukio kama hayo kama ilivyo siku hizi za dot com
 
Hongera mstaafu kwa kujiwekea hazina mbiguni ambayo haitaliwa na nondo wala mchwa.Safi sana mkuu BMW
 
wazanzibar ndio walioleta ukatoliki huku bara kumbe ..ulianzia kwao huko visiwani ..sasa kwa nini shule kama pugu hazikujengwa huko visiwani? ama walizichoma moto???

Wakatoli...sijui wanaogopewa nini,lol! Dunia hii kuna schemes nyingi sana za kuubomolea mbali, kwa siri siri au wazi wazi. Mhhh!
 
Naona kaamua apunguze madhambi yake kwa kuwagaia kile alichokiiba tehe tehe.Kama diamond tungeita blood diamond ila kwa sababu cow, tuite blood cow
 
Hawa Mapadre ndo wanamiliki shule za Marian Girls and boys pamoja na Tengeru boys iliyopo Arusha.
Wamefanya maendeleo makubwa sana hasa katika upande wa elim.

Dah umenikumbusha academic master wa Tengeru Boys yule father mwenye kisauti..nimemkumbukaje!
 
Angetugawia na sisi hivi vitu vyake ingekuwa powa sana maana hata sisi si tulimchagua kuwa mkuu wa kaya.Tugawane hiyo keki yake bana
 
Back
Top Bottom