Mkapa should know better. Yeye alimsoma Shakespear ambaye alisema The good things men do get interred with their bones once they die but the bad ones live long after them. Yaani ukifa unazikwa na mazuri uliyofanya hapa duniani lakini mabaya uliyoyafanya hukumbukwa muda mrefu baada ya kifo chako.
Hivi inawezekana Mkapa wakati anaapishwa kuwa raisi hakuyajua haya? Na je ndiyo maana aliyafanya hayo yote? Nashindwa kuamini. Ila kinachokuja akilini mwangu ni kuwa Mkapa alifanya kwa kiburi kabisa akijua kwamba hakuna atakayeweza kumfikia wala kuuliza. Ubabe wa Chama aliutumia kwenye uraisi. Viongozi wa CCM wana hilo tatizo, wanapokuwa Mawaziri au Raisi wansaahau kuwa wakati huo ni viongozi wa nchi nzima wa hata wale wasiokuwa wanachama wa chama chochote.