Mkapa + Wassira = CCM dhaifu

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
WIKI hii nzima nimeitumia kuwaza lakini sikupata majibu ya

kuniridhisha. Wazo langu kuu ni nani ndani ya Chama cha Mapinduzi

(CCM), alipanga na kuidhinisha wazee wawili yaani Rais mstaafu

Benjamin Mkapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano wa

jamii), Stephen Wassira, waende kumpigia kampeni mgombea wa

chama hicho jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari?


Pasipo kumng'unya maneno kama walilazimishwa kwenda huko basi

aliyewalazimisha na alaaniwe kwa ubabe huo na kama

walijipendekeza wao bila kujali kuwa zama zao zimepita na kukubali

kwenda kujipaka matope, basi aibu yao ya chama chao dhaifu.


Niliwahi kuandika huko nyuma nikisema kuwa CCM ni dhaifu lakini

watu hawaichukii kwa hilo bali kwa matendo ya baadhi ya viongozi

wao wanaofikia maamuzi pasipo kujali madhara yake na mustakabali

wa chama mbeleni.


Ni aibu kubwa sana kwa chama kikongwe chenye umri wa miaka 35

na makada chungu nzima, kumtegemea rais mstaafu kwenda

kuwazindulia na kuwafanyia kampeni ya kugombea nafasi ndogo ya

ubunge.


Nilivyosikia Halmashauri Kuu ya CCM mwaka jana ikimteua mzee

huyo kuzindua kampeni katika Jimbo la Igunga, nilipigwa butwaa

nikidhani pengine ni hadaa ya kuwababaisha wapinzani wao lakini

mwisho wa siku nikajua Mkapa atakuwepo pale kama mwalikwa tu

na mshauri wa wenzake.


Lakini Mkapa alipopanda jukwaani mara mbili Igunga kwa kufungua

na kufunga kampeni za CCM, niliamini kuwa chama hicho sasa basi,

kama hakiwezi kuwatumia makada wake wasafi kimatendo na hoja

kuomba ubunge hadi wakimbilie kwa Rais mstaafu na magamba

mengine basi ni hatari.


Sasa Mkapa amenogewa jukwaa, akaona ni sehemu ya kupitishia

mashambulizi yake kwa kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake miaka

mingi lakini akawa kimya kuzijibu na kujijengea heshima ya kaulimbiu

yake ya uwazi na ukweli.


Badala yake mzee wetu anadhani Watanzania wa leo ni wale wa

miaka 10 iliyopita, kumbe hawa hawadanganyiki tena, hawaogopi

mikwara yake, wanataka kujua aliwezaje kufanya biashara kwa

kutumia rasilimali zao akiwa Ikulu.


Mzee Mkapa bila kutambua hilo na kwa ushauri dhaifu wa chama

chake legelege akakubali kudanganyika kwenda Arumeru kumnadi

Sioi ili atumie mwanya huo kuendelea kufunika ukweli wa tuhuma za

ufisadi zinazomkabili.


Hata hivyo, kwa udhaifu wa hoja, akajikuta ameishiwa maneno ya

kuwapumbaza wananchi wa Arumeru na badala yake shetani

akampitia akaamua kuikashifu familia ya Baba wa Taifa hayati

Mwalimu Julius Nyerere.


Ni Mkapa huyu huyu aliyejitapa kwenye mazishi ya Nyerere mwaka

1999 kule Butiama kuwa yeye, CCM na serikali wangemuenzi muasisi
huyo kwa kila jinsi, lakini akageuka muasi wa kudai kwamba Mbunge

wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA) si mmoja wa

wanafamilia ya Nyerere.


Haijulikani shetani huyo alitokea wapi hadi Mkapa kuacha kumnadi

Sioi na kurukia kumshambulia mbunge huyo kijana ambaye anajua

fika ni mtoto wa mdogo wake Nyerere, Kiboko Nyerere, akidai si

mmoja wa wanafamilia.


Akaenda mbele na kujinasibu kuwa Nyerere alimtambulisha wana

ndugu wote kwa muda waliofanya kazi naye lakini Vincent hayumo.

Hivi ni kweli Mkapa alikuwa akifanya kazi ya kukariri wanafamilia wa

Nyerere kujua nani anazaliwa, ameolewa, ameoana na nani?


Yeye ndoa yake iko safi, familia aliyonayo haina kasoro hadi apate

muda wa kuhama hoja ya kampeni na kurukia kumdhalilisha hayati

Baba wa Taifa kwa kumzushia uongo? Na hata kama ingekuwa ni

kweli, Vincent si mmoja wa wanafamilia ya Nyerere, watu wa

Arumeru ilikuwa inawasaidia nini?


Lakini kama wasemavyo wahenga kuwa siku za mwizi ni arobaini au

muosha huoshwa, Mkapa alipata aibu ya mwaka baada ya mtoto wa
Nyerere, Madaraka Nyerere, kukanusha uongo wake na kukiri kuwa

Vincent ni mwanafamilia wao akiwa mtoto wa baba mdogo wao.


Hapa utapima mwenyewe, kuwa hiyo ndiyo CCM ambayo tegemeo

lao ni Mkapa anayekosa hoja jukwaaani na kuamua kusema uongo

pasipo kujali kuwa wananchi wanataka kufahamu mengi na ya msingi
kutoka kwake.


Kwa mantiki kama hiyo, unadhani nani anaweza kuisemea CCM ili

watu waelewe kuwa chama bado ni makini ikiwa vijana wamewekwa
kando na kufanywa mtaji wa kutumika kurubuniwa kufanikisha

ushindi wa hila na ghiriba?


Kama kawaida CCM bila kukaa chini na kutathmini aibu na madhara

aliyowaletea Mkapa, wakakurupuka na kumpeleka mkongwe

mwingine, Waziri Wassira huko Arumeru kunusuru jahazi.


CCM ama kwa kutojua kuwa enzi za Wassira zimeisha na amechoka

hadi anapigwa picha akiwa ameuchapa usingizi bungeni,

walimpandisha jukwaani, naye kama Mkapa akatumia muda wote


kulidhalisha Kanisa Katoliki na Katibu Mkuu wa CHADEMA badala ya

kumnadi Sioi.


Wassira kwa makusudi aliwadanganya wananchi wa Arumeru kuwa

Dk. Willibrod Slaa alifukuzwa upadri baada ya kuiba fedha za ujio wa
Papa Yohane Paul II, alipokuja nchini mwaka 1990, wakati huo

akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).


Lakini kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu kuwa Mungu

hamfichi mnafiki, siku moja baada ya uongo huo wa kumdhalilisha

Dk. Slaa na kanisa kwa ujumla, Rais wa TEC, Askofu Mkuu Juda

Thaddeus Ruwa'ichi, alimjibu akimtaka kutoa ushahidi kuthibitisha

kama kweli.
Ruwai'chi ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Kuu la

Mwanza, alisema Wassira athibitishe tuhuma zake kwani kanisa hilo

halijawahi kumtuhumu Dk. Slaa kwa tuhuma za wizi.
“Kanisa

halijawahi kumshutumu Dk. Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira).

Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi

ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha

madai yake,” alisema Ruwaichi.
Kwa mwendo huu wa wakongwe wa

CCM kuamua kujivua nguo hadharani kwa kusema uongo, nini hatima
ya chama hicho mbeleni, je, vijana na watoto wajao wanaweza

kujifunza nini katika maadili ya viongozi ikiwa watu wenyewe ni

kama hawa wanaosema lolote linalowajia mdomoni.
Safu hii ya Fikra

Mpya katika kutafakari, imekuja na njia nyepesi kwa wale

wanaoiwaza CCM kwa sasa kuwa wachukue kanuni hii ya hesabu;

Mkapa+Wassira=CCM dhaifu, kama huamini tupe hoja yako maana

hawa ndio walikuwa tegemeo huko Arumeru Mashariki wakaishia

kuwadhalilisha watu na taasisi za imani za dini. Tafakari

 
Ccm c dhaifu ni CHAFU. Uchafu ambao ni vigumu mno kutakasika na waloichafua wao humohumo ndani hawajatokana hawawezi kuwatoa, hata lile gamba tuliloshangilia sana lilipotangaza kujivua bado lipo na haziwezi kutoka kabisa kamwe ni kiini macho tu kile.
 
"Msiwazomee wale waliovaa uniform za CCM kwasababu hawana nguo nyingine za kujisitiri."
By Mh God Bless Lema.
 
Wassira zimemruka...mara aseme nassari anatembea na mama wa kizungu...kwani sheria za nchi haziruhusu au anamuonea wivu.
 
ccm ni sawa na makahaba wao wale wanaohamia bungeni kipindi cha mikutano... wameathirika........wewe huoni hata Ane makinda naye an import kijana wake wakumfyonza wakati wa mikutano ya bunge kule dom? sasa wote hawa wamekwisha kama walivyo ambukizwa maradhi na hao machangu..........
 
Back
Top Bottom