Elections 2010 Mkapa vipi??

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
77
Wana JF mnaichukulia vp kauli ya Mkapa aliyoitoa juzi kuwa "kwa vyovyote vile Uongozi wa Tanzania lazima utokane na CCM"
Kisha akaongeza "mimi sipingi Serikali ya umoja wa Kitaifa, ila nataka serikali ya umoja wa kitaifa inayotokana na CCM"

Binafsi naiona Statement hiyo kama inadumaza Demokrasia nchini maana tafsiri yake ni kuwa ccm lazima iwe madarakani kwa kuichagua au bila kuichagua. Na kama ndivyo it means what we did today for Dr.Slaa is meaningless.??

Je, Mkapa was serious au ndo wameshajipanga kuchakachua?? Je, kwa kauli hii nikimwita Mkapa Dikteta nitakuwa nimevunja kifungu gani cha katiba??
 
Ni dikteta tena mkubwa kabisa. Hiyo lugha yake haitoi nafasi kwa demokrasia. Yaani viongozi wa ccm bado wana mawazo ya kwamba bila wao tanzania haipo. Wanajiona wana hatimiliki ya kuitawala nchi milele. Ni ajabu sana, lakini ndicho wanachokiamini. Maskini wa mawazo!
 
soon or later watajua kwamba uongozi ni dhamana tu na sio haki ya kuzaliwa watapewa wengine
 
Wana JF mnaichukulia vp kauli ya Mkapa aliyoitoa juzi kuwa "kwa vyovyote vile Uongozi wa Tanzania lazima utokane na CCM"
Kisha akaongeza "mimi sipingi Serikali ya umoja wa Kitaifa, ila nataka serikali ya umoja wa kitaifa inayotokana na CCM"

Binafsi naiona Statement hiyo kama inadumaza Demokrasia nchini maana tafsiri yake ni kuwa ccm lazima iwe madarakani kwa kuichagua au bila kuichagua. Na kama ndivyo it means what we did today for Dr.Slaa is meaningless.??

Je, Mkapa was serious au ndo wameshajipanga kuchakachua?? Je, kwa kauli hii nikimwita Mkapa Dikteta nitakuwa nimevunja kifungu gani cha katiba??

Usiumize kichwa, angalia hiyo statement imetoka wakati gani.
 
Nadhani tuendelee kuhesabu kura zetu tu vinginevyo achaneni naye huyo mstaafu!
 
Msamehe mwenzenu alipitiwa na zigo zito alilotwishwa na Chadema. Chadema safari hii imewakoroga wengi adi walikuwa hawajielewi. Msamehe,namwombea msamaha mana tumewahukumu kwenye ballot box.
 
Mkapa bado analeta mambo ya udiktemokrasia. Tena hii kauli imeikosti CCM badala ya kuomba kura kwa adabu yeye anafosi, hakumbuki kuwa yeye mwenyewe hakuwa chaguo la wananchi sema tu kilichomsaidia bado waTZ walikuwaa na fikra za Unyerere na alikosekana mpinzani makini kama Slaa. Maana Slaa anajua waTZ wanataka nini. Nawaambieni jamaa Chanzo cha Umaskini watu ni UFISADI.
 
Your LAST statement is very true. Hata CHADEMA wakiingia jikoni, wasilewe na madaraka, pls, pls
 
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA. Waache kututisha. Hii nchi si yao ni ya Watanzania na ni Watanzania watakaoamua ni nani awaongoze. HATUTISHIKI, TZ BILA CCM INAWEZEKANA NA TZ YENYE NEEMA INAWEZEKANA TUKIWABWAGA MAFISADI
 
Mkapa alikua kimya Muda mrefu,kwa kua alizoea utawala wa kiimla,wa kimazoea..alipima kina cha maji kwa macho..alipogundua mambo ni mabaya kwenye chama chao akakurupuka..wee ngoja! kwanza uzee unamjia vibaya!
 
Back
Top Bottom