Mkapa ni Sawa na Ungo Kwa Majirani, Kibeku Kwa Watanzania

Ben Mkapa,kwangu mimi ni mmoja wa viongozi imara na wenye upeo katika kuleta maendeleo kwa watu..

Ubora wake kadiri siku zinavyosonga utajitokeza zaidi hasa pale anapolinganishwa na viongozi wa nafasi yake...
 
Mkapa kavurugiwa tu na mkewe na familia yake. Mama Mkapa na tamaa zake ndizo zinamfanya Mkapa wetu aonekane hivyo alivyo. Tatizo jingine lilikuwa kuwaamini mno WAZUNGU.
 
viongozi wazuri hawazaliwi wanatengenezwa na mfumo, ndio maana viongozi wa miaka ii ni wezi tupu ule mfumo wa JKN ushatupwa, hatutakaa tupate viongozi wazuri waafrica tusimsingizie mungu kwamba TZ imebahatika kupewa viongozi wazuri, mkapa aliyoyafanya hayajustify wizi wake thats is the point!
 
Kwangu mimi Mkapa ni kama fumbo. Miaka yake minne ya mwanzo alifanya kazi makini na ya kitaaluma ambayo hatuwezi kuikana. Kwa kifupi aliirejesha nchi toka kwenye "wild west" ya uchumi na kuiwezesha kukopesheka. Lakini baadaye, hasa mara baada ya kumzika JKN, alianza mwenendo ambao unadalili za mtu aliyekuwa na kisirani na nchi hii.

Kauli zake katika hotuba zilikuwa zimejaa vitisho na kejeli. Akiulizwa kitu majibu ni ya kijeuri. Mara "wavivu wa kufikiri", "mtu mzima hatishiwi nyau", "mwenye bilioni 15 ajitokeze nimkabidhi NMB", n.k. Halafu, hujuma za uchumi alizoendesha na/au kuruhusu zitekelezwe BOT, TANESCO, sekta ya madini, jeshini, n.k. (Netgroup Solutions, EPA, IPTL, Meremeta, rada, n.k.) zilikuwa ni za kuvuruga mpangilio mzima wa uchumi na kufanya ufisadi kuwa taasisi rasmi ya dola. Hata Usalama wa Taifa hivi sasa unaonekana kazi yao kuu ni kulinda mfumo huo tu.

Kijijini kwangu mpaka leo Mkapa anasifiwa kwa kuimarisha thamani ya shilingi na kufanya maisha ya watu wa kawaida kuwa nafuu. Hawamfurahii kabisa Muungwana; wanatamani BWM angerejea tena. Lakini najiuliza, kwa vurugu mechi iliyochezwa nusu ya pili ya BWM, huo uimara wa uchumi ungeweza kuendelea?
 
Back
Top Bottom