Elections 2010 Mkapa na kampeni za vitisho

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Haya ni maneno ya Benjamin Wiliam Mkapa, ambaye aliendesha kampeni za vitisho zilizowakatisha Wananchi tamaa ya kutokea mabadiliko ya uongozi.

Kwa sehemu kubwa sasa katitika kampeni ambazo zimeanza, naona pia kampeni za vitisho zinaweza kuwepo,kama hazijaanza.

Miongoni mwa kauli za vitisho alizo toa Mkapa ni hizi:

"Duniani kote hakuna hata siku moja utakuta chama tawala kinakubali kushindwa na kuwaachia wapinzani watawale. Naahidi kwamba nitatumia uwezo wangu, nguvu zangu zote na dola ili kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi…''
(Mwanachi, Mei 20, 2005)

"Mimi ni Amiri Jeshi Mkuu mpaka siku atakapopatikana rais mwingine. Kiongozi yoyote wa serikali ambae jimbo la mahala pake litachukuliwa na upinzani atashughulikiwa bila hata kusubiri vikao vya chama.'' (Tanzania Daima, Desemba 18, 2005)

Vipi kwa JK, atafuata nyayo za BWM au atatumia mbinu tofauti?

Nawakilisha
 
Nadhani atatumia mbinu tofauti.

Atauza ilani yenye ahadi tatanishi halafu baadaye akishindwa kuitekeleza atasema sikusoma hivyo sikujua kama wataalam wangu waliandika hili. Yaani atairuka kiunzi.!!!

 
Kutokana na hali halisi ya kisiasa ilivyo, hadi vyombo ya ulinzi na usalama kutoa matamko mbalimbali, imenikumbsha hii post kuhusu maneno ya BWK ambayo JK anataka kuyatumia.

SHIME WATANZANIA TUMPIGIE KURA KIONGOZI ATAKAYELETA UKOMBOZI NA MAENDELEO KWA TAIFA LETU.
 
Pamoja na vitisho kuzuia mafuriko ni shughuli nzito sana. Na bado ngoma inaendelea maana vita si ya CHADEMA AU CUF bali ya waTZ.
 
Back
Top Bottom