MKAPA na INFLATION

Tutafika

JF-Expert Member
Nov 4, 2009
1,443
631
Pamoja na tuhuma na maovu mengi ya awamu ya tatu ya uongozi Tanzania, Mzee Mkapa, nitaendelea kumkubali nikilinganisha na wengine. Hebu ona takwimu hizi za mfumuko wa bei jinsi alivyorekebisha madudu ya Mwinyi na jinsi aliekabidhiwa anavyoendelea na yale yale ya Mwinyi. Nyerere simuongelei sana kwasababu naona jinsi alivyokua anajitahidi kuziba pengo kubwa lililosababishwa na IDD AMIN

1980- 30.205
1981- 30.3
1982- 25.7
1983- 28.9
1984- 27.1
1985- 36.1
1986 -33.3
1987 -32.4
1988 -47.702
1989 -20.602
1990 -22.562
1991 -28.037
1992 -21.935
1993 -23.619
1994 -37.146
1995 -23.969
1996 - 20.496
1997 -15.443
1998 -13.161
1999 -8.996
2000 -4.589
2001 -5.147
2002 -4.555
2003 -4.429
2004 -4.138
2005 -4.359
2006 -5.612
2007 -6.251
2008 -8.405
2009 -11.826
2010 -10.496

[TH]Year[/TH]
[TH]Inflation, average consumer prices[/TH]
2011 - 19.8
2012 March - 19
 
Mfumuko wa bei kwa sasa haupukiki maana wakati ule tulikusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi zikawa za serikali ikasaidia kupunguza mfumuko. Sasa baada ya lile zoezi kufanikiwa tukanunua ndege ya rais, rada , tukajenga nyumba za viongozi kwa bei kubwa baada ya kuuza zile za awali kwa bei poa, nk

Hii ndio akili ya serikali yako ndugu mwananchi
 
Tufanyeje sasa ili kuepukana na kupanda kwa mfumuko wa bei?

Ongeza uzalishaji wa kilimo baba ili upunguze maumivu kwa mwananchi wa kawaida

Ki "kibasket" kinachotumika kupiga hesabu za mfumuko wa bei kinaangalia sana bei za chakula na mafuta. Hizi bei ndio zinasababisha kila kitu kingine kinakuwa bei juu.

Angalia mchele ulivyoruka kutoka 1500 hadi 2500 ongezeko la asilimia 66.67% na angalia mafuta yalivyokurupuka hadi sasa 2200 kutoka 1600 ni 37.5%. Angalia Dollar tulikuwa tunanunua 1200 ghafla imeruka sasa 1600 hili ongezeko la 33.33% . Hapa tu ukiangalia wastani tayari tupo huko juu kwenye 30% na kuendelea! na hivi ndio vyenye impact kubwa.
 
Tufanyeje sasa ili kuepukana na kupanda kwa mfumuko wa bei?
Wizi tu...Tukiacha wizi mbona kila kitu shwari....nchi ita nawiri we mwenyewe utashangaa !!!!
nafikiri idadi ya Watanzania wanoamini kuwa "maisha bila rushwa hayawezekani" inazidi kuongezeka kwa kasi na hasa hii outputs ya shule na vyuo vyetu vya kata na yeyote anayejaribu kufundisha maadili anaonekana mwendawazimu.
Ili kuwa na ule uwezo wa kuelewa ni kwa nini nchi/jamii zote zilizopiga hatua zinachukia rushwa na hata kufikia hatua ya kuwanyonga wahusika, ni lazima tuanze na kufundisha kuwa binadamu yeyote alivyo na uwezo wa kufanya mambo makubwa pale anapowekewa taratibu nzuri na zilizo wazi za maisha yake ya kila siku.

Tutampata wapi mwingine kama Mkapa? Tutampata wapi mwingine mwenye vision ya kumaliza umasikini wa Tanzania ifikapo 2025? Atatoka wapi, ndani ya CCM au nje?
 
Tutampata wapi mwingine kama Mkapa? Tutampata wapi mwingine mwenye vision ya kumaliza umasikini wa Tanzania ifikapo 2025? Atatoka wapi, ndani ya CCM au nje?

Lazima wananchi waoneshe mfano kwa kuingia mtaani na kudai haki, bila kulazimishana huu mfumo uliopo utazidi kutumaliza.
 
Mfumuko wa bei kwa sasa haupukiki maana wakati ule tulikusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi zikawa za serikali ikasaidia kupunguza mfumuko. Sasa baada ya lile zoezi kufanikiwa tukanunua ndege ya rais, rada , tukajenga nyumba za viongozi kwa bei kubwa baada ya kuuza zile za awali kwa bei poa, nk

Hii ndio akili ya serikali yako ndugu mwananchi

Na zile kidogo zilizobaki Bank tukagawana kupitia EPA, Twin Towers, na Richmond
 
Lazima wananchi waoneshe mfano kwa kuingia mtaani na kudai haki, bila kulazimishana huu mfumo uliopo utazidi kutumaliza.
Unguja wameingia mtaani tayari lakini cha kusikitisha sio kuunganisha nguvu bali kutenganisha na wameanza na kuchoma mMakanisa. Nchi inaongeza matatizo badala ya kupunguza. Asante JK

Similar Discussions

Back
Top Bottom