Mkapa: Kuna mtu kanizomea?

Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali
 
Wahaya wana msemo wa 'ki-utu uzima" unasema hivi: "Mwanamke akinajisiwa na asizungumze kwa mtu nani hatajua?" Hakuna. Habari za kunajisiwa zinasambazwa na yule aliyefanyiwa kitendo sio aliyetenda maana mtendaji anajua ana makosa hivyo hawezi kujichongea. Mzee Mkapa alishazomewa hapa Dar Es Salaam na wengi wetu tulisha sahau. Sasa anatukumbushia kuhusu Kuzomewa. Mkapa ameyakuza mwenyewe! Tutamzomea sasa.
 
Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali
Hizo ndio analysis za kijinga, Ok kafanya mazuri. Jee hiyo ndio ticket ya kufanya ufisadi wa mali za watanzania? Alikuwa na shida gani kuiba wakati katiba inatutaka tuwatunze Maraisi wastaafu maisha yao yote? Pamoja na aliyofanya,hapa katulazimisha tumwadhibu kama mhalifu. Labda afe tuu, lakini itakuja siku serikali makini na itamwadhibu. Kosa la jinai halina ukomo.
 
Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali

Hivi mkunga aliyeapa kufanyakazi yake kwa makini na maadili na kuifanya kweli kisha kuwa amelipwa alichostahili, lakini siku moja (ushetani/wivu/uroho) unampanda kichwani na kwenda kuua watoto wote aliozalisha utamhukumu kwa lipi baada ya kuwa amemaliza kazi yake??

Mkuu, hivi kuna kitu gani usichokielewa hapa? Hii thread inamwongelea yeye kama yeye kutokana na hotuba yake aliyotoa kwa wananchi. Threads za comparison kwenye performance zipo tele. Isitoshe tukianza kuongelea mambo ya performance inabidi ku-factor in mambo mengi - kuanzia hali ya kiuchumi duniani, population ya muda huo, uelewa wa jamii wakati huo na mengine mengi ambayo hayawezi kuwa sawa kila baada ya miaka 5 au 10 ya ngwe ya kiongozi.
 
Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali

Naona pay roll inafanya kazi kweli kweli. Yote unayoona kafanya mazuri ndo yalikuwa wajibu wake afanye, na si fadhila kawafanyia watanzania.
Tunachoangalia ni je alitimiza wajibu wake kikatiba?
 
Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali
1. Charles Keenja enzi za tume ya jiji la Dar.........
2. Mwaibula na madaladala .........
 
Tuache longolongo toa list ya watu unaowafahamu wamefanya Mazuri zaidi ya Mkapa ili tuchambue.Hata kama ni wewe pia weka Jina lako hapa. Lazima tuwapambanishe atakayeibuka mshindi basi tumkubali
Mkombozi,
Hawa watu wanaingia madarakani na wanaajiriwa kwa makubaliano ya kufanya KAZI ZAO kwa mujibu wa taratibu walizowekewa, hivyo kufanya mazuri tunzo lake ni mshahara na marupurupu mengine yaliyokuwemo ndani ya makubaliano. Wizi na Uhalifu mwingine wowote malipo yake ni JELA. Mkapa aeshalipwa kwa kazi zote nzuri alizofanya, tunachotaka kujua na kuhakikisha ni yeye atawalipa nini Watanzania kwa UOZA alioshiriki kuutenda kwa Taifa. sidhani kama tunahitaji Ligi na Point scoring table. Yeye aje clean kama alivyojiita na hili somo litafungwa.
 
He is the greatest Prezo ever, after mwalimu, no doubt about that, nobody is perfect bwana...bravo "ankal" Ben.....,
 
Tumezoea toka kwa viongozi wetu sisi na pia kuona kuwa ni lazima kuzomea kwa mkoa wa Iringa wana utamaduni wa kuwalaki viongozi wao toka siku nyingi hivyo sio ajabu
 
Cha msingi tusihukumu, mimi nimeangalia pamoja na mabaya aliyotenda lakini ametenda azuri mengi sana. Wengi waliopo madarakani hawawezi kuwa perfect 100%. Wewe mwenyewe jiangalie je uko perfect 100%? Mimi nawaeleza mkapa alifanya kazi yake vizuri sana. Kuzomewa sio tatizo hata malaika wanazomewaga na shetani. Sure I'm tell you guys, historia itahukumu, jamaa alichapa mzigo kweli kweli. Sasa tumezongumzia mabaya tu mbona mazuri hatuyasemi? Au dhamira yetu inatusuta? Unajua watu tusizungumze kwa kusikia vyombo vya habari tu, tuzungumzie pia vinavyoweza kuonekana kwa nacho pia. Tusidanganayane Mkapa alipiga mzigo sana, alikua hataki utani na kazi hata kidogo.
 
Jamani nimesoma maoni yote ya watu humu, kwa kusema kweli na pia tuache unafiki, Mkapa alifanya kazi kubwa sana ambayo huwezi kulinganisha. Mimi namkubali sana jamaa, ukianzia kuinua mapato ya serekali, hazina ya fedha za kigeni BOT, ubinafsishaji ambao umeongeza ajira, barabara, Uwanja mkuu wa Taifa, Daraja kubwa la Rufiji, utendaji kazi masaa mengi ofisini na safari chache za nje, alipambana na mfumuko wa bei (mkate haba Dar ulikua TShs 150,sasa zaidi ya 700, Unga wa sembe ulikua Tshs 250, sasa 900, Daladala ilikua 150 kwa 50 kwa muda mrefu. Amepunguza madeni ya nje
Tumwache apumzike jamaa alifanya kazi kubwa Sana, ila hamna mtu ambaye ni Mungu au Malaika asiye na makosa. Kama swala ni kufanya biashara je ni wangapi wanafanya kwa kupitia migongo ya ndugu zao? Si afadhali huyu alifanya mwenyewe? Mimi nakwambia Tanzania ni kubwa sana, kwa hiyo alifanya mambo mazuri sana jamaa.

Unajua performance ya mtu inabidi uipime kwa kulinganisha na tulikotoka, Mkapa alipokea nchi ikiwa katika hali mbaya sana, vijana walikua hawataki shule, serekali ilikua haina hela, shule ilikua haithaminiki, hospitali dawa kulikua hamna, yeye alipambana kufa na kupona. Vyote tunavyojivunia sasa vimetoka kwenye uongozi wake.
Swala hapa ni kuchambua kwa upeo wa mpana wa kiuchumi na sio kuleta siasa, unayesema mkapa hakufanya kitu je ni nani aliyefanya? Hamna aliyemsafi 100%

Wanaoamini biblia, Yesu aliletewa mwanamke moja mzinzi na watu wengi. Ila kwa sheria ya kiyahudi ilimpasa kupigwa mawe hadi kufa. Yesu akawaambia makutano, kwa yeyote anayejiona hana dhambi yeyote awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akainama chini akawa anachora kwa kidole chini, hapo alikua anandika amri za Mungu. Aliponyanyua kichwa hakumkuta mtu hata mmoja, na akamwamuru yule mama aende zake na asirudie tena dhambi. Kwa mfano huu, anayejiona hana dhami yeyote awe wa kwanza kumyooshea mkapa kidole.
Amefanya makubwa sana, tumwache apumzike

Well, kama unaongelea mambo aliyofanya, ni kweli amefanya mengi mazuri. Lakili hili halim exempt kwenye machafu aliyofanya. BW ni mwizi na anatakiwa awe ndani as we speak!!
 
Huyu anaonyesha alivyo na upungufu mkubwa wa kupambanua mambo. Yeye anasubiri Watanzania mpaka wamzomee ndiyo aamini kwamba utendaji wake ulijaa ufisadi wa kutisha.

Kahusika na kufanya biasha Ikulu hadi leo hajatwambia Watanzania biashara hiyo alifanya na nani na ilikuwa ni biashara ya nini. Alilazimisha kununua Rada ambayo sasa imejulikana kwamba ununuzi ule ulijaa ufisadi wa hali ya juu.

Alilazimisha kuwaingiza makaburu wa Net Group Problems pale TANESCO pamoja na Watanzania kuwapinga na hakuna chochote walichokifanya pamoja na kulipwa mabilioni.

Miezi michache kabla ya kumaliza muda wake mabilioni chungu nzima yalichotwa kupitia EPA, Meremeta na Mwananchi Gold. Alilazimisha kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa uamuzi ambao umeliingizia Taifa hasara ya shilingi bilioni 200.

Alilazimisha kununua ndege ya Rais kupitia yule yule wakala wa Rada akiwa amebakisha miezi mitatu tu kumaliza awamu yake na ndege yenyewe sasa hivi iko juu ya mawe.

Alisaini mikataba ya kuchimba dhahabu ambayo haina maslahi na nchi yetu ambayo tunaambulia 3% tu ya mapato yote. Aliiba Kiwira yenye thamani ya shilingi bilioni 7 na kujiuzia kwa shilingi milioni 700 na kulipa shilingi 70 milioni tu.

Kachukua mkopo NSSF wa shilingi bilioni 7 ambao hadi leo hii hajalipa hata senti. Sera zake uwazi na ukweli ilikuwa ni changa la macho tu. Sasa sijui anazungumzia utendaji gani alioufanya ambao unastahili sifa toka kwa Watanzania. Mtu mzima..........

Basi inatosha mkuu, utatutia hasira zaidi yewoooooomi, uuuuuuiiii. Huyu jamaa asisubiri kuzomewa, atapigwa mawe.
 
Cha msingi tusihukumu, mimi nimeangalia pamoja na mabaya aliyotenda lakini ametenda azuri mengi sana. Wengi waliopo madarakani hawawezi kuwa perfect 100%. Wewe mwenyewe jiangalie je uko perfect 100%? Mimi nawaeleza mkapa alifanya kazi yake vizuri sana. Kuzomewa sio tatizo hata malaika wanazomewaga na shetani. Sure I'm tell you guys, historia itahukumu, jamaa alichapa mzigo kweli kweli. Sasa tumezongumzia mabaya tu mbona mazuri hatuyasemi? Au dhamira yetu inatusuta? Unajua watu tusizungumze kwa kusikia vyombo vya habari tu, tuzungumzie pia vinavyoweza kuonekana kwa nacho pia. Tusidanganayane Mkapa alipiga mzigo sana, alikua hataki utani na kazi hata kidogo.

Mkombozi,

Unachokisema ni kweli lakini bado kama Rais aliyemaliza muda wake lazima awajibike kwa madudu aliyoyafanya akiwa madarakani.
 
He is the greatest Prezo ever, after mwalimu, no doubt about that, nobody is perfect bwana...bravo "ankal" Ben.....,
In the name of ''NOBODY IS PERFECT'' watu huwa wanafanya madudu hata ambayo wangeweza kuyaacha kwa kutoweka tamaa za kibinafsi mbele...............

In the name of ''NOBODY IS PERFECT'' then maraisi waliopita na aliyeko madarakani WOTE WAZURI.......WAMETUFANYIA MAZURI...........
 
He is the greatest Prezo ever, after mwalimu, no doubt about that, nobody is perfect bwana...bravo "ankal" Ben.....,

jana (kilolo) the guy was so confident in the media mpaka nikajiuliza what's the move?? he was talking and looking at Hon. Hawa Ghasia like someone with immense authority! ... huyu jamaa has a huge presidencial confidence jamani ... linajiamini sana!

Later nikamwangalia mkulu wangu huko turkey ... duh utafikiria mjumbe wa kamati fulani ya Lundenga (no offense meant pls!) ... mkulu inabidi ajiamini na awe mkali bwana .... too boring!!

He has the POWER but it seems he has no AUTHORITY!!

MDBD
 
Yaani umesema utafikiri umeusoma moyo wa Mkapa unafikiri nini. Ufisadi unamnyima raha, apende asipende. Rekodi yake kubwa ni wizi na ufisadi utamlindaje?

Halafu anajifanya yuko busy wakati ameweza kuhudhuria vikao vingi vinavyomuhusu vya chama chao, lakini hajawahi hata siku moja kuhudhuria sherehe za 9 December, Mapinduzi au Muungano tangu atoke madarakani. Naona huupanga ubusy wake uangukie sherehe hizo.

Wewe endelea kuwa busy tu lakini ujuwe hata kama Watanzania hatutakuzomea ukweli tunaujua kwamba wewe ni mwizi na kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hili na ulitumia muda mwingi wa madaraka yako kujitajirisha wewe, familia yako na ndugu na jamaa. Watanzania ni wastaarabu hivyo usijipige kifua kwa vile hujazomewa ukadhani tunafurahia utendaji wako ulipokuwa madarakani.
 
Back
Top Bottom