Mkapa Help This Guy

Status
Not open for further replies.
mnajua kuna wanafiki waliokuwa wanafanya kazi na nyerere lakini wezi wakuu kama CLEOPA DAVID MSUYA ..utajiri wake ni mkubwa sana ..jadi benki kuu ikachomwa..ufisadi haukuanza aleo..lakini masikini mwalimu alikuwa akimuamini msuya....

mtu mwingine aliyekuwa akiaminiwa na mwalimu ni mramba ...alimpenda kwa kuwa alikuwa kati ya vijana walioenda nje kusoma kuja kuanzisha SIDO na NDC....na kiukweli mramba kama ni wizi kaanza enzi hizi ..zamani hakuwa na ujanja....mwalimu alimshauri mkapa ampe uwaziri baada ya kusota sana mbeya as mkuu wa mkoa baada ya kuangushwa ubunge....
 
...mnamkumbuka waziri mgonja ..waziri wa kale wa elimu na waziri wa mambo ya nje ...juzi juzi nimemuona anaishi maisha ya kimasikini sana .....anapanda dala dala za huko kwao gonja ....amechoka kweli bora mwafongo alikuwa afisa tu wa ikulu...
 
Jamani Mwafongo hayuko peke yake katika watu waliotumikia taifa hili kwa uhadilifu na kisha kusahaulika.

Nani hamfahamu au hakuwahi kumsoma Daktari wa Kwanza wa tiba, muasisi wa TAA, TANU na Mdanganyika aliehudumia ofisi ya kwanza ya Danganyika huru New York? Namsema Dr. Vedasto Kyaruzi

Stori yake kwa ufupi ni sawa na Ayubu wa Biblia kwa wale wanaoifahamu. Mzee huyu hivi majuzi amepewa notice ya kuhami katika nyumba yake. Hii imeongeza pilipili kwenye kidonda kibichi. Kwa ufupi Mzee na muasisi huyu kwa wanaofahamu historia alipaswa kuenziwa hata zaidi ya kawawa. Kinyume chake katupwa hajifilie mbali.
 
".......wangechangamkia tenda vipi wakati enzi hizo kwa kiongozi, hata kufuga kuku ilikuwa ni makosa?..."

Nadhani hapa kidogo kuna chumvi imeongezeka, nafahamu wakuu wa wilaya,mkoa na wana TANU/CCM fulani wa ngazi za kati na juu ambao walikuwa wanafuga kuku ziadi ya elfu na nguruwe kwa wingi tu. Kipindi hicho hata mimi nilishawahi kufika kwao katika harakati za kucheze cheza utotoni.

Waliokuwa wanafuga nguruwe kwa wingi na bado walikuwa na Pick up ambayo ilikuwa iwasaidia kusambaza nyama na kuuza vitoto vya nguruwe kwa wafugaji wengine, halafu walikuwa na shamba kubwa mno. Pia hiyo familia baba alikuwa meneja mkuu wa shirika la serikali na mama alikuwa mkuu wa wilaya au mkoa, hayo nimeyaona kwa macho ingawa nilikuwa mdogo ki umri. Na kwa kifupi ni kuwa hadi leo hii sijawahi ona nguruwe wengi hivyo!
 
mi nasema matatizo yetu mengi lakini kila kitu analundikiwa Nyerere tu.

Nyerere ana sehemu yake ya lawama, lakini hata kama angekuwa Draco mwenyewe bado mtu mmoja hawezi kuwashinda mamilioni kama kweli hawataki.
 
Nadhani hapa kidogo kuna chumvi imeongezeka, nafahamu wakuu wa wilaya,mkoa na wana TANU/CCM fulani wa ngazi za kati na juu ambao walikuwa wanafuga kuku ziadi ya elfu na nguruwe kwa wingi tu. Kipindi hicho hata mimi nilishawahi kufika kwao katika harakati za kucheze cheza utotoni.

Waliokuwa wanafuga nguruwe kwa wingi na bado walikuwa na Pick up ambayo ilikuwa iwasaidia kusambaza nyama na kuuza vitoto vya nguruwe kwa wafugaji wengine, halafu walikuwa na shamba kubwa mno. Pia hiyo familia baba alikuwa meneja mkuu wa shirika la serikali na mama alikuwa mkuu wa wilaya au mkoa, hayo nimeyaona kwa macho ingawa nilikuwa mdogo ki umri. Na kwa kifupi ni kuwa hadi leo hii sijawahi ona nguruwe wengi hivyo!

Choveki,

Tuambie ilikuwa lini hiyo?

Katika miiko ya TANU ilikuwa ni marufuku kwa kiongozi wa serikali kuwa pia mfanyabiashara. Walikuwa wanaweza kuwa wakulima lakini sio wafanyabiashara.

Of course hiyo haina maana kama baba ni kiongozi basi mama naye alizuiwa kabisa kufanya biashara yoyote. Ulikuwa unaweza kufanya lakini pia jua ilikuwa lazima usalama wa taifa na watu wengine wa maadili wakupitie mara nyingi kujua umepataje hizo mali.

Hilo liliwafanya wengi waliokuwa na pesa za ziada kutokuziweka kwenye asset
yoyote kwa kuogopa kuulizwa kazipataje.

Mimi ni mpenzi na muumini wa mwalimu lakini pia naelewa hayo mambo yalikuwa yanatokea. Nikiangalia ufisadi wa sasa, wala simlaumu mwalimu kwa hilo.

Labda alichokosea Mwalimu ni kutokuwatengenezea pension viongozi wa siasa
sawa na wafanyakazi wengine wa serikali.

Tatizo lingine la TZ ni hii pride ambayo wasomi wanakuwa nayo hata pale ambapo hawana kitu. Naamini watu kama akina Mgonja au huyu Mwafongo kuna kazi nyingi sana wanaweza kufanya hata kwasasa, ni kuamua kujishusha na kukubali kazi zilizopo ambazo wana uwezo nazo.

Hata sasa bado serikali inaweza kutenga japo pesa chache kuwasaidia hawa ndugu zetu ambao walifanya kazi kwa uaminifu wote na sasa wanahangaika.

Tukishindwa kuwasaidia na badala yake kuwacheka, itakuwa ngumu sana kumshawishi mtu awe mwadilifu, watu wataona afadhali wawe mafisadi lakini wajihakikishie maisha bora uzeeni.

Hapa JF tuna watu wa magazeti, kama huyu mzee bado ana uwezo wake, msaidieni japo apate kibarua cha miezi kwenye hiyo sector ya habari.
 
Choveki, Tuambie ilikuwa lini hiyo?.
Kama nilivyosema miaka ya TANU/CCM yaani late 70's hadi mwanzoni mwa 80's.

Katika miiko ya TANU ilikuwa ni marufuku kwa kiongozi wa serikali kuwa pia mfanyabiashara. Walikuwa wanaweza kuwa wakulima lakini sio wafanyabiashara.

Sasa ukiwa mkulima hivyo vitu utapeleka wapi kama siyo kuviuza. Na kama nilivyosema hawa walikuwa wafugaji/wakulima. Na nimeeleza hivyo baada ya wachangiaji kusema ati wakati wa JKN viongozi walikuwa hawaruhusiwi kufuga hata kuku (si ndiyo ukulima huo??)

Of course hiyo haina maana kama baba ni kiongozi basi mama naye alizuiwa kabisa kufanya biashara yoyote. Ulikuwa unaweza kufanya lakini pia jua ilikuwa lazima usalama wa taifa na watu wengine wa maadili wakupitie mara nyingi kujua umepataje hizo mali.
Kama nilivyosema awali, katika familia mojawapo baba na mama wote walikuwa kwenye system!, Baba General Manager wa SU na mama Mkuu wa mkoa/ wilaya (sikumbuki vizuri)- Ila tetesi ni kuwa baba (mume) alikuwa mwanafunzi wa JKN kule tabora- hivyo alikuwa anagateway na vitu vingi tu, na ndo maana waote walipewa post)

Hilo liliwafanya wengi waliokuwa na pesa za ziada kutokuziweka kwenye asset yoyote kwa kuogopa kuulizwa kazipataje
Nakubaliana nawe, hususan wale waliokuwa na pesa za wizi au dhuluma. Ila wapo wale wachache ambao for some reason pia waliweza ku-gate away withit, na wale walioukuwa na bahati ya kuwa recyled eg: fuatilia mifano ya GAPEX, Kampuni za ushirika za mikoa/wilaya, Tanzania Elimu Supplies, Mawasilaino ya anga nk.
Mimi ni mpenzi na muumini wa mwalimu lakini pia naelewa hayo mambo yalikuwa yanatokea. Nikiangalia ufisadi wa sasa, wala simlaumu mwalimu kwa hilo
Hilo hata mimi nimeliona, na mwalimu yeye siyo wa kulamiwa, ila ninachotaka kusema ni kuwa hata enzi zake kulikuwa na makosa na kuna victims pia wa makosa yake
Labda alichokosea Mwalimu ni kutokuwatengenezea pension viongozi wa siasa sawa na wafanyakazi wengine wa serikali
Kwanini viongozi wa siasa tu, mimi nasema pensheni ni kwa kila mtz anayefikisha miaka fulani, mfano 65, siyo chosen few!
Tatizo lingine la TZ ni hii pride ambayo wasomi wanakuwa nayo hata pale ambapo hawana kitu. Naamini watu kama akina Mgonja au huyu Mwafongo kuna kazi nyingi sana wanaweza kufanya hata kwasasa, ni kuamua kujishusha na kukubali kazi zilizopo ambazo wana uwezo nazo.
Ndiyo maana baadhi yetu tumehoji jinsi ambavyo Ben Mkapa anavyolaumiwa ati hajamsaidia huyu bwana!, Au kwanini mbunge wake hamsaidii, Je mimi mzee wangu kijijini amkimbilie nani? Wengi wamesema huyu anaweza kufundisha shule nying tu je kwanini hafanyi hivyo?
Hata sasa bado serikali inaweza kutenga japo pesa chache kuwasaidia hawa ndugu zetu ambao walifanya kazi kwa uaminifu wote na sasa wanahangaika.
Pesa zitengwe kwa watanzania wote watakapoozeeka, kwani mimi bado naamini asilimia 99 ya waTz ni waaminifu, na ni wengi uzeeni wanahangaika.
Tukishindwa kuwasaidia na badala yake kuwacheka, itakuwa ngumu sana kumshawishi mtu awe mwadilifu, watu wataona afadhali wawe mafisadi lakini wajihakikishie maisha bora uzeeni
Kucheka mzee yeyote ni utovu mkubwa wa nidhamu na ukosefu wa maadili, ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa taifa la kesho wanakuwa na maadili tunayoweza kuringia.
Hapa JF tuna watu wa magazeti, kama huyu mzee bado ana uwezo wake, msaidieni japo apate kibarua cha miezi kwenye hiyo sector ya habari.
Nakubaliana nawe, ila wengi tumesema kuwa kuna kitu ambacho kimefichika hapo, hatuwezi kutoa maamuzi ya maana mpaka tupate picha kamili, na nakubaliana na kumsaidia ila wazee ni wengi wa kusaidiwa na ndiyo maana unatakiwa uwe mkakati wa taifa na siyo wana JF tu, kwa waTz wote siyo waliofanya kazi state house au serikalini tu.
 
Kama nilivyosema miaka ya TANU/CCM yaani late 70's hadi mwanzoni mwa 80's.

Sasa ukiwa mkulima hivyo vitu utapeleka wapi kama siyo kuviuza. Na kama nilivyosema hawa walikuwa wafugaji/wakulima. Na nimeeleza hivyo baada ya wachangiaji kusema ati wakati wa JKN viongozi walikuwa hawaruhusiwi kufuga hata kuku (si ndiyo ukulima huo??)

Kama nilivyosema awali, katika familia mojawapo baba na mama wote walikuwa kwenye system!, Baba General Manager wa SU na mama Mkuu wa mkoa/ wilaya (sikumbuki vizuri)- Ila tetesi ni kuwa baba (mume) alikuwa mwanafunzi wa JKN kule tabora- hivyo alikuwa anagateway na vitu vingi tu, na ndo maana waote walipewa post)

Nakubaliana nawe, hususan wale waliokuwa na pesa za wizi au dhuluma. Ila wapo wale wachache ambao for some reason pia waliweza ku-gate away withit, na wale walioukuwa na bahati ya kuwa recyled eg: fuatilia mifano ya GAPEX, Kampuni za ushirika za mikoa/wilaya, Tanzania Elimu Supplies, Mawasilaino ya anga nk.

Hilo hata mimi nimeliona, na mwalimu yeye siyo wa kulamiwa, ila ninachotaka kusema ni kuwa hata enzi zake kulikuwa na makosa na kuna victims pia wa makosa yake

Kwanini viongozi wa siasa tu, mimi nasema pensheni ni kwa kila mtz anayefikisha miaka fulani, mfano 65, siyo chosen few!

Ndiyo maana baadhi yetu tumehoji jinsi ambavyo Ben Mkapa anavyolaumiwa ati hajamsaidia huyu bwana!, Au kwanini mbunge wake hamsaidii, Je mimi mzee wangu kijijini amkimbilie nani? Wengi wamesema huyu anaweza kufundisha shule nying tu je kwanini hafanyi hivyo?

Pesa zitengwe kwa watanzania wote watakapoozeeka, kwani mimi bado naamini asilimia 99 ya waTz ni waaminifu, na ni wengi uzeeni wanahangaika.

Kucheka mzee yeyote ni utovu mkubwa wa nidhamu na ukosefu wa maadili, ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa taifa la kesho wanakuwa na maadili tunayoweza kuringia.

Nakubaliana nawe, ila wengi tumesema kuwa kuna kitu ambacho kimefichika hapo, hatuwezi kutoa maamuzi ya maana mpaka tupate picha kamili, na nakubaliana na kumsaidia ila wazee ni wengi wa kusaidiwa na ndiyo maana unatakiwa uwe mkakati wa taifa na siyo wana JF tu, kwa waTz wote siyo waliofanya kazi state house au serikalini tu.

Choveki,

Nafikiri hapa sio sahihi, miiko ya TANU ilikuwa haiwabani sana viongozi wa mashirika ya umma. Sehemu kubwa ilikuwa inawabana wanasiasa kama mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, nafikiri hata wakuu wa wilaya nk.

Mashirika ya umma walikuwa wanafuatiliwa lakini hawakuwa na miiko sawa na ya wanasiasa.

Mamanager wengi wa miaka ya 70, ni matajiri na waliiba au kutengeneza pesa zao. Tatizo kubwa ninaloliona mimi limewakumba zaidi waliokuwa wanasiasa au wasaidizi wa wanasiasa.

Serikali haina uwezo wa kumlipia kila mtu pension, kosa la Nyerere ni kwamba hakuwawekea wanasiasa pension, kwa maana kwamba wangekatwa kwenye mishahara yao ili iingizwe kwenye pension yao. Wafanyakazi wengi kwenye mashirika na serikalini walikuwa kwenye mifuko ya pension na hata kama pesa hazikutosha lakini angalau walikuwa na pension.

Pia muhimu kwa serikali kuwaelemisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya pension na kuweka pesa zao kwa faida ya uzeeni.

Huko tunakokwenda hali itakuwa mbaya zaidi, kuna haja ya kuanza kulipa kipaumbele hili suala ili tusije tukaadhirika huko mbele.

Najua kwasasa pension za wafanyakazi hasa serikalini zina unafuu sana ukilinganisha na miaka kama kumi iliyopita. Inabidi iwe hivyo hata kwenye kazi zingine na ikiwezekana hata kwa wakulima.
 
Nikirudi kwenye topic. Kwahiyo Mkapa amege utajiri wake amgawie huyu jamaa?! Just asking!
 
tatizo nadhani hawa watu walipokuwa madarakani hawakuchangamkia tenda.. Wangekuwa wajanja wangekuwa wanajitengenezea vitripu, viwarsha, na visemina vya hapa na pale... But I have an idea.. kuna mtu ana contact zake..?

Mzee ndio unataka kupata pa kutokea 2008 nini kama ilivyo kuwa issue ya Ukraine? au unataka umpe msada? Najua watu huwa wanatumia matatizo ya watu kunufaika kama vyombo vya habari na wapiga piacha wanavyofurahia kukamata matukio huko Kenya.
 
Darubini,

Asante sana kwa ujumbe mrefu lakini uliojaa maneno mengi ya maana.

Jamani tuangalie tunawezaje kumsaidia huyu mzee ili atoke kule kwenye umaskini na aanze kujitegemea.

Pili tunaposema Mkapa amsaidie, haina maana Mkapa atoe pesa zake. Kumpa ushauri tu na reference vinatosha kumwondoa huyu ndugu yetu kule kwenye umaskini wa kutupwa.

Kama kuna watu wako tayari kumsaidia, wengine tunaweza kumsaidia hata nauli na ikibidi mahali pa kufikia hata kwa mwezi mmoja.

Ndio maana mimi huwa nawalaumu sana baadhi ya wabunge wetu maana case kama hii ni moja kati ya mambo ambayo wanaweza kushughulikia na kusaidia mpaka mhusika anaanza kujitegemea.
 
Nikirudi kwenye topic. Kwahiyo Mkapa amege utajiri wake amgawie huyu jamaa?! Just asking!

FD hata mimi nimesoma ila sijaona hiyo kazi mnayotaka BWM aifanye?
Huyu mtu ni msomi....kwanini asiende tu hapo Mbeya mjini aombe kazi Mzumbe or Kisanji Univ.
He has to be proactive...matatizo yapo katika maisha lakini sidhani kama wamechukua akili yake. Maisha ni kugangamaa bwana..!
 
Mtanzania,

Kama umesoma msg ya Darubini kwa makini, nadhani huo msaada ambao wewe unapendekeza watu wampatie unaweza kuwa ni bure, if the old man (Mwafongo) is a marked person.

Kwanza tayari amesema alipoteza kazi katika mazingira ya kutatanisha na pia hakutaka kuingia kwenye undani wa hayo mazingira (hapo kuna alama kubwa sana ya kuuliza).

Pili, kwa miaka yote hiyo tangu alipofukuzwa kazi miaka hiyo ya 80s mpaka leo hii kwanini hajapata kazi nyingine tena? Kuna magazeti mengi sana ambayo yalianzishwa na kwa mtu kama yeye CV yake inatosha sana kumuuza kirahisi na kupata kazi, kwanini hana kazi mpaka leo hii? Kuna waandishi wa habari wengi sana ambao hawana hata diploma za uandishi wa habari, lakini wanapeta tu. Sasa iweje mtu mwenye diploma na uzoefu wa miaka hiyo ya waandishi waliobobea ashindwe kupata kazi??????

Hapo kuna mambo mawili:

Moja, inawezekana kwamba huyu Mzee aliachishwa kazi kwa sababu za kiusalama, aidha kwa kuchomewa ama kwa mambo ambayo hata yeye hataki kuyaelezea.

Mbili, baada ya kuachishwa kazi kuna watu walipewa jukumu la kumfuatilia kila anakokwenda ili kuhakikisha kwamba akiomba kazi ya aina yoyote ile hata kama ni ya umesenja hawezi kupewa kwa aidha mwajiri kuambiwa wazi na wana usalama kwamba huyo mtu hatakiwi kuajiriwa ama ukimwajiri basi unajipalia makaa.

Kutokana na hizo sababu 2, ndiyo maana Bwana Darubini amesema kwamba swala la kumsaidia huyu Mzee litafanikiwa iwapo tu viongozi wetu wa sasa watakuwa wako tayari kumfungulia kutoka kwenye hicho kifungo. Lakini kama hajafunguliwa kutoka kwenye hicho kifungo juhudi zetu zinaweza kuwa hazina maana. Sana sana inaweza kuwa ni msaada wa michango ambao hauwezi kuwa sustainable, lakini kama angepata ajira ingekuwa ni sustainable.

System ikitaka kukutesa itafanya kila iwezalo na maisha yako yatakuwa kama ya huyo Mwafongo. Wapo wengi waliopitia kwenye hilo tanuru na mpaka leo hii huwa hawasemi kitu, huwa wanabaki na machungu yao mioyoni mwao.
 
Anajua nini? Alisema nini? Tendo moja la uharamia linalofanywa na "usalama wa taifa" linaondoa mazuri mengi yanayofanywa.

Sasa kama mtu hawezi kuajiriwa katika nchi yake mwenyewe tunaweza kubisha kuwa Tanzania ni "police state"?
 
...................Pia inawezekana kuna watu ambao Mwafongo aliwaamini na wakamsaliti. Kama methali moja isemavyo: "Kikulacho kinguoni mwako."

Labda pia aliongopewa na wafanyakazi wenzake, pamoja na ndugu zetu wa usalama - wanaodhani wanaipenda nchi yetu kuliko wananchi wengine - waliotoa ushadi (perhaps concocted evidence against him) na kumharibia maisha....................

.....................Kuna sababu mbali mbali pamoja na wivu, na kupalilia unga - ngano! - zilizowafanya watu fulani kumwandama na kumtosa shimoni, kiasi cha kwamba imemlazimu aishi maisha hayo ya umasikini na taabu nyingi sana........................................

..............................Lakini wengi wao have been rehabilitated, includidng those who tried to overthrow the government. So why not him Mwafongo?

I wonder why.

Alifanya nini? Makosa gani? Na ni miaka mingi imepita tangu alipotupiliwa mbali, and he's still on the leash, like a dog, obviously allowed to go nowhere...................................

...........................................................................Pia napenda kusisitiza kwamba kila nchi inahitaji intelligence officers na security agencies. Case closed! Whether you like it or not. Tatizo ni wakati wanapoongopa kuwaharibia maisha watu fulani bila sababu.................................................................................................

...........................Sababu haikuwa ukabila. Marehemu Mdee hakuwa na ukabila hata kidogo. Hata Mwakipunda, alpoondolewa, hakulalamika na kusema kwamba ameachishwa au amefukuzwa kazi kwa sababu ya ukabila.....................................................

Duuhh Darubini kwa kweli unamfahamu vema huyu "Fong"
...............he "Fong" was "very outspoken".........................

Niliyo-highlight bold blue yana uzito sana.......

hii ni tabia ya kabila hili hata kwa wale wachache niliofanya nao kazi........................ni watu wenye misimamo yao husimamia wanachokisema wengi wao sio wanafiki (kumbuka Mama Thabitha Siwale)..........viongozi wengi waliofuata tabia ya Mwl Nyerere ya kutotaka kupingwa nao waliishia kuwatosa watu kama hawa walio kuw ahuru kimawazo/kifikra..............trust me.................no wonder hata BWM alipokuwa Rais alikuwa na nafasi kubwa ya kumrudisha "Fong".....hakufanya hivyo sababu zile zile za zamani za "Fong"

..................nafikiri kuna wachache sana walio-yield mmoja wao akiwa ni Mwakipunda (aliyesaidiwa na Mwangota) na Mar. Anangisye.

Kwa hiyo kumsaidia huyu mzee inabidi a-yield.................na mambo yake yatakuwa saafi
 
Darubini

Makala ndefu lakini hamna substance swali dogo la mstari mmoja lililoulizwa na MzalendoHalisi limebeba ujumbe mzito wa kuliko jamvi lako ulilotandika hapo juu.

Hivi mtu akirost lazima kuwe na mkono wa serikali? basi hata hao watoto wake wa kuzaa mwenyewe (naambiwa wapo Marekani) nao pia wanawekewa kazibe wasimsaidie baba yao?

Huyo itakuwa ulabu ndio umemfikisha hapo umeiona ile picha yake? look like someone in Ukhomboti Pub.

Si afadhali ya huyo alikuwa afisa mwandamizi kuna mawaziri kama Pfo Machunda,Tewa Said Tewa, Jaji Mwesiumo wapo hohe hahe nao pia wapo hivyo kwa sababu ya usalama wa taifa?
 
1. May be kapigwa 'kipapai' au ni laana ya wazazi- huenda yeye pia aliwatelekeza wazazi wake wakateseka yeye akiwa Ikulu. Sisi kuna jirani yetu kule kijijini wazazi walimsomesha hadi akapata kazi Uganda during EA- na akapata cheo kikubwa- sasa alipata mwanamke wa Kiganda kule na kusahau kabisa wazazi! wazazi waliishi maisha ya dhiki na baba yake akafa kwa njaa hatimaye- ila aliacha laana! Baada ya 5 years after kifo cha baba yake yule jamaa alifukuzwa kazi-na mke akamkimbia na watoto na yeye kurudi Tanzania.. na baada ya miaka mitano 5 pesa yote iliisha akaanza kunywa mataptap! Akawa fukara kuliko hata baba yake- nakumbuka aliomba kufundisha shule ya sekondari Physics jirani na mimi nilikuwa mwalimu pale siku zile- alipougua tukaenda kumwona-- ile hali niliyomkuta nayo alikuwa analala chini- nyumba mbavu za mbwa -hana chakula na alikuwa anajifunika na matambara! Tulimsaidia- tukampeleka hospitali na kumpa nguo- na pesa -sema zile pesa alikunywa nazo matap tap mara alipotoka hospitali!
Akilikuwa na kichwa kweli- ila yaonekana laana ya wazazi ndo ilimfikisha pale- naskia ameshakufa tayari- kwa kukosa lishe na kwa ufukara!

2. WanaJF nakumbushia tena kuna laana ya wazazi.. kwa wale wenye imani.. haya mambo yapo. Tusikae kusahau kuwangalia wazazi wetu! Naamini kati yetu hakuna ambaye amemtelekeza mzazi wake na kumwacha katika hali kama ya Mzee Mwafongo!

3. Tukumbuke pia tukiwatunnza wazazi- nasi tukiwa wazee- watoto watatuangalia na kututunza!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom