Mkapa 'Atoroka' Sherehe za muungano.

huh!? :confused:
Unatumia na matusi katika ukumbi wetu mwanana!? Moderators hebu mfungieni huyu kijana aliyekosa adabu.

Wewe mbona unakuwa na mtindio wa ubongo!Ukiambiwa utaje matusi utayaweka hayo.
Iwekwe wazi kama hapa ni mahala pa kuungana kwa jambo lolote kuhusu mtu fulani anaye dhaniwa kuwa mwovu bila kujali lina sound vipi.And you bubu sijui kiziwi don't be biased ,matusi na kuua lipi ni baya zaidi ya jingine ?unaweza kubadili maneno yawe matusi na kusema mutu afungiwe ,ila aliyetoa wazo la mimi kuning'inizwa jiwe kutoswa baharini hujamuona.By the way kwangu hajanishtua najua ni domo lake tu she can't get in my way.Ila wewe kwa kuwa uko baised hujaliona.

Sasa mtu anasema Mkapa atoroka sijuhi na pumba nyingine inahusu nini?Watu wanakuja mkuku na madongo eti waonekane eti wana uchungu,Damn !niambie jambo ambalo kweli ntaona baya kuhusu mtu sio kutoroka sherehe au kutokwenda ...inaingizia nini taifa au inapunguzia nini,wako watu ambao ni must go viongozi active kwa sasa.
Kwa kifupi hii thread "Mkapa 'Atoroka' Sherehe za muungano"ni pumba kama mnao penda kuongeza idadi ya post kazi kwenu.
 
Ufanisi wa kiutendaji wa Mkapa hakuna anayeweza kuutiliashaka, kwa kiasi kikubwa ni Rais ambaye naweza kusema ni mzuri kuliko wote ambao Tanzania iliwahi kuwapata, (this is debatable). Alikoitoa nchi na alipoifikisha wakati anaondoka anapaswa kushukuruwa sana. Hata jumuiya ya kimataifa (ndani na nje ya Afrika na kwa watanzania wenye akili) wanatambua wazi kuwa Ben alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wapya wa Afrika wenye kuletea matumaini. Aliweza kudhibiti mfumuko wa bei, aliweza kutoa leadership ambayo sasa haipo tena, alijaribu kuleta heshima kwenye Ikulu ya Tanzania ambayo iliezuliwa na Mwinyi, na kuondoa uswahiliswahili serikalini, at least Tanzania ikaonekana tena kuwa ni nchi, na sio kama genge la wajinga.
Lakini baada ya kusema haya inabidi tukubali ukweli kuwa yeye kama kiongozi mkuu wa nchi, alikalia kimya mambo mengi ambayo ninahakika yeye mwenyewe aliyajua kuwa ni uhalifu na wizi, ambayo ni kinyume na maadili ya Chama chake na conscience yake binafsi, na kinyume na kiapo alichotoa wakati anachukua urais mara mbili, kinyume na dini yake, na kinyume na aliyosema kuwa napaginaia, na baya zaidi alitumia vibaya cheo chake kujinufaisha (sio kuiba japo sina hakika). Haya yote na mengine mengi ambayo siwezi kuyasema na mengine ambayo siyafahamu yanamfanya asiwe kwenye kundi la watu waadilifu, he is equally liable kama mafisadi wengine.
NI kweli mimi ni-admirer wa Ben and i will keep on being so, lakini mazuri aliyotufanyia hayawezi kumfanya awe immune kwa ujinga aliousimamia, ambao angeweza kuusimamisha alipokuwa na uwezo kama Rais wa nchi na mwenyekiti wa Chama. Ni sawa na kusema mtu anakaa pembeni anaangalia jambazi linaua na anaweza kabisa kulishimamisha, halafu anasema mimi sikuhusika na uuaji huo, that is madness. Unless there is something we do not know! Ben is in for it and he must speak out, kwanini ametufanya hivyo.
The guy is more smart than many in the administration now, kwa hiyo kauli yake inaweza kuwa na mawili, kwanza inawezekana kabisa akisema tu watu wakakaa kimya na kuacha kupiga domo anajua sana kujenga hoja na kuzitetea hata kama ni za uongo, au anaweza kumwaga sumu ambayo ita-i palaralyze kabisa CCM na serikali. Inategemeana tumejiandaa kwa lipi!

Unaonekani hukurupuki kuongea una upeo and your not biased .Umeonyesha black and white sio kama wanaodai tu WANAUCHUNGU .
Hii nchi sijui itakuaje maana hawa wanaotawala sasa hawafai 'em weak very weak CMM na wapinzani wenyewe pia ndio mashaka matupu Nobody to trust.We need to change this!Either upinzani wenye nguvu na tuone wanamaanisha mabadiliko sio kwa kuwa hawako kwenye madaraka nop,OR mapinduzi yatokee ndani ya CMM .Ila hatuhitaji watu wanaojiita eti wanauchungu tu bila kutoa the way out,can't figure out the possible outcome ,no good approach just big mouth.Watu hawa inaonekana wapingaji tu kwa kuwa hawako kwenye channel.
Aksante Bongolander kwa mchango wako mzuri .
 
Mh. Mkapa sasa anakuwa kama hajaenda shule. He can't run away from this saga anymore, it is too late. He needs to manufacture his defence and face the public head on, no matter how weak is his case. For how long is he going to run away from his own home made mess??
 
Ufanisi wa kiutendaji wa Mkapa hakuna anayeweza kuutiliashaka, kwa kiasi kikubwa ni Rais ambaye naweza kusema ni mzuri kuliko wote ambao Tanzania iliwahi kuwapata, (this is debatable). Alikoitoa nchi na alipoifikisha wakati anaondoka anapaswa kushukuruwa sana. Hata jumuiya ya kimataifa (ndani na nje ya Afrika na kwa watanzania wenye akili) wanatambua wazi kuwa Ben alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wapya wa Afrika wenye kuletea matumaini.

Hapa naomba kutofautiana na wewe.

1. Ben hakujenga mashirika, bali alikuwa dalali mbovu wa mashirika ambayo aliyauza kwa kasi ya ajabu, ambayo hata katika nchi zinazoshabikia kuuza mashirika (Thatcherites) hakuna kasi hiyo. ni kweli mashirika yalikuwa na matatizo lakini ule uuzaji wake ulikuwa na matatizo makubwa zaidi, ambapo investment zote za miaka mingi na effort za hao walioyajenga mashirika hayo, zilipotea bure.

2. Uuzaji mkubwa wa mashirika ulimfanya awe na pesa nyingi katika serikali yake, japo zingeweza kuwa nyingi zaidi ya hapo. Ni sawa na mtoto anayerithi mashamba ya babaake (au viwanja ambavyo vilikuwa havifanyiwi kazi, lakini vinalazimka kulipiwa ada kila mwaka) na anaamua kuuza ovyo kwa bei yakutupa. kwa muda ataonekana ana pesa nyingi sana. Mkapa aliweza kufunika matatizo ya wakati wake in the short term.

3. Kuna project zilizokuwa na matatizo ya kimkakati, mfano NETGROUP Solutions. short term interests za NetGroup zilikinzana vikali na long term interests za TANESCO na taifa, na hapo taifa liliathirika sana na kuidhoofisha zaidi TANESCO. unless lengo lilikuwa kuidhoofisha TANESCO, kwa malengo kama tunayoyashuhudia sasa hivi, basi watakuwa walifaulu kwa kiasi kikubwa.

3. Investment alizozianzisha mwenyewe, mfano migodi, hazikuwa na maslahi yoyote kwa taifa. ila alianzisha mirija ambayo mashirika ya nje yaliweza na yanaendelea kufaidi uchumi wa Tanzania. kwa nini wasimpongeze? Asifuye mvua...

4. Eneo pekee ambalo namsifia mkapa (na luteni wake Pombe Kali) ni kwenye barabara. Hapo alikuna kipara na kuweka vitu chini. Hapo sina neno, unless nipate data zaidi...

The guy is more smart than many in the administration now, kwa hiyo kauli yake inaweza kuwa na mawili, kwanza inawezekana kabisa akisema tu watu wakakaa kimya na kuacha kupiga domo anajua sana kujenga hoja na kuzitetea hata kama ni za uongo, au anaweza kumwaga sumu ambayo ita-i palaralyze kabisa CCM na serikali. Inategemeana tumejiandaa kwa lipi!

1. Mkapa anaonekana smart kwa sababu mojawapo kwamba Kikwete katika kuonesha nia ya kupambana na rushwa za mkapa, naye katengeneza za kwake kwenye Richmond, kupitia Ngoyai. Hii inaondoa ka authority kokote ambako Kikwete angekuwa nako - No moral high ground there. Kama ulivyosema, kwa kuruhusu machafu yafanyike, na yeye pia kushiriki kuyafanya, ameondoa smartness yoyote ambayo ingeweza kuhusishwa naye

2. Hata hivyo, nguvu aliyo nayo Mkapa katika CCM ni kwamba ni baadhi ya pesa chafu alizozitengeneza ndio zimeiweka CCM madarakani katika uchaguzi uliopita. kaifunga kamba CCM kwamba hawawezi kum-ditch bila kujidhuru wenyewe. lakini hii haina maana kwamba kalifunga kamba taifa. ukifika wakati ikawa too hot kwa CCM, itabidi ihesabu gharama na kum-ditch. ni kama Kikwete alivyolazimika kum-ditch Ngoyai. si kwamba alipenda lakini ilibidi iwe hivyo. haya, chenge huyoo, kaenda zake, pamoja na nyodo zake. ukifika wakati Kikwete aamue ama anaondoka yeye au amshughulikie Mkapa, nadhani choice iko wazi
 
YOU CAN RUN BUT YOU CAN'T HIDE -- "You can try to escape from what you fear, but eventually you will have to face it.
 
..siku hizi amehama sea view...anaishi masaki na mostly lushoto....

tunaye rais mstaafu aliyefanya kazi kubwa kujenga uchumi...lakini yupo kati kati ya kashfa....

na tunaye rais anayetusaidia kujua upande wa pili wa shilingi wa mkapa tuliyemsifu sana ...lakini yeye akiwa hana analofanya kukuza uchumi zaidi ya kuudidimiza ...

historia itakuja kuwapa nafasi gani hawa wawili??

This is an interesting perspective...wanajf tumeng'ang'ania ufisadi ufisadi kama waandishi wa habari..kikwete akitoka...sijui tutamsifu kwa nini..au kazi ya raisi mpya ni kuonyesha maovu ya waliopita...usalama, polisi, mahakama, etc etc KAZI YAO NI NINI????
Kikwete should know that by putting mkapa's otherside in public..the same will happen to him when he goes...unless ataamua kung'ang'ania kama mugabe!!!
 
mkapa ana observe policy ya WAIT AND SEE..anasoma upepo unaendaji ....ukweli ni kuwa public critisism baada ya mafaili X yake kufunguliwa ni kubwa....lakini pia fact kuwa serikali ya kikwete perfomance yake ipo chini kabisa..pamoja na nia njema anayoweza kuwa nayo kikwete inamuharibia na inaweza kusababisha hata tuhuma za kifisadi zinazoibuliwa na awamu hii siku moja kugonga sikio la uziwi kwa watanzania ambao watakuwa hawaoni maendeleo aliyoleta kikwete anyway pamoja na nia yake...

juhudi za kupiga vita ufisadi za kikwete ziende sambamba na maendeleo katika sekta zote za kiuchumi.....ili asije onekana siku moja kuwa hizi kashfa zilikuwa zinaibuliwa ili ku divert attention ya wananchi kutoka critism kwa serikali yake!

Mkapa anacheka jinsi JK anavyo struggle kutawala Nchi .Maana anamjua kwamba ni Zero kabisa iifikia kwenye uongozi na utawala.Kwenye wizi kazi kubwa sina uhakika na wote 2
 
Mkapa anawaonea haya wananchi ambao mwanzo walimwamini sana na yeye aliwapa justification ya kumwamini. Sasa mambo yamegeuka na wananchi wamegundua kuwa waliyemwamini si mtu wa kuaminika kwani kawaibia saaaaaaaana tu na kuwaacha katika lindi la umaskini wakati yeye yu aponda raha kama vile hayuko tz. Lazima akimbie, he is a human being and he is guilty conscious as well.
 
Ufanisi wa kiutendaji wa Mkapa hakuna anayeweza kuutiliashaka, kwa kiasi kikubwa ni Rais ambaye naweza kusema ni mzuri kuliko wote ambao Tanzania iliwahi kuwapata

lakini mazuri aliyotufanyia hayawezi kumfanya awe immune kwa ujinga aliousimamia, ambao angeweza kuusimamisha alipokuwa na uwezo kama Rais wa nchi na mwenyekiti wa Chama.

Ben is in for it and he must speak out, kwanini ametufanya hivyo.

The guy is more smart than many in the administration now,

kwa hiyo kauli yake inaweza kuwa na mawili, kwanza inawezekana kabisa akisema tu watu wakakaa kimya na kuacha kupiga domo anajua sana kujenga hoja na kuzitetea hata kama ni za uongo, au anaweza kumwaga sumu ambayo ita-i palaralyze kabisa CCM na serikali. Inategemeana tumejiandaa kwa lipi!

Mkuu B, haya maneno yote yameandikwa na wewe mtu mmoja, either makapa ni mwizi au sio, lakini hawezi kuwa all this uliyoyasema, hawezi kuwa a smart leader halafu akanunua mgodi na waziri wake wakiwa Ikulu, angekuwa that smart leo tusingeweza kufukua uchafu wake kama karanga kila kona, angekuwa anajua kujenga hoja angeshinda ile zawadi ya MO, kui-paralyize CCM hawezi labda aji-paralyize mwenyewe binafsi kwa sababu hakuna kifungu chochote cha katiba kinachosema iba hela za wananchi halafu zipeleke CCM,

CCM haina hiyo katiba, wala jamhuri, angekuwa that smart asingewalazimisha bodi ya bandari kumpa Karamagi mkataba wa kihuni wa miaka 25 kuendesha bandari, mara ya mwisho ninajua in the private alikuwa akilalamika kuwa rafiki yake Mengi anam-betray kwenye magazeti yake, that does not sound like a smart fella!

Makapa ni mwizi kama wezi wengine kina Chenge na Lowassa, his right place ni jela Ukonga, na it is coming tena soon! Hizo hoja akazijengee huko, wananchi tumepania kwenye hili lazima aende kule Makonga!
 
Mkuu wangu uko right, na kama ukipitia mara ya pili niliyoandika nimeajiribu kuwa fair kwa Ben kwa mazuri aliyofanya, na nikasema hata hayo ninayoona mazuri ni debatable wengine wanaweza kuyaona mabaya. Ni vizuri kama it is clear kuwa aliiba, na fate ya wezi iwe moja tu regardless mwizi ni Bw Abdala aliyeiba kuku Manzese au Michael aliyeiba mbuzi vingunguti, au Ben aliyeiba akiwa ikulu.
Mimi kinancho ni kasirisha zaidi kuhusu Ben ni kuwa, pamoja na hayo mazuri aliyofanya, baya zaidi ni kuwa alikuwa kiranja wa ufisadi, yaani alisimamia wezi wakiiba na kukaa kimya, kwa hili namuweka kwenye kundi moja na wezi wengine.
He foresaw the plundering and lootin of our resources, he can not escape from this sin.
 
Hapa naomba kutofautiana na wewe.

1. Ben hakujenga mashirika, bali alikuwa dalali mbovu wa mashirika ambayo aliyauza kwa kasi ya ajabu, ambayo hata katika nchi zinazoshabikia kuuza mashirika (Thatcherites) hakuna kasi hiyo. ni kweli mashirika yalikuwa na matatizo lakini ule uuzaji wake ulikuwa na matatizo makubwa zaidi, ambapo investment zote za miaka mingi na effort za hao walioyajenga mashirika hayo, zilipotea bure.

2. Uuzaji mkubwa wa mashirika ulimfanya awe na pesa nyingi katika serikali yake, japo zingeweza kuwa nyingi zaidi ya hapo. Ni sawa na mtoto anayerithi mashamba ya babaake (au viwanja ambavyo vilikuwa havifanyiwi kazi, lakini vinalazimka kulipiwa ada kila mwaka) na anaamua kuuza ovyo kwa bei yakutupa. kwa muda ataonekana ana pesa nyingi sana. Mkapa aliweza kufunika matatizo ya wakati wake in the short term.

3. Kuna project zilizokuwa na matatizo ya kimkakati, mfano NETGROUP Solutions. short term interests za NetGroup zilikinzana vikali na long term interests za TANESCO na taifa, na hapo taifa liliathirika sana na kuidhoofisha zaidi TANESCO. unless lengo lilikuwa kuidhoofisha TANESCO, kwa malengo kama tunayoyashuhudia sasa hivi, basi watakuwa walifaulu kwa kiasi kikubwa.

3. Investment alizozianzisha mwenyewe, mfano migodi, hazikuwa na maslahi yoyote kwa taifa. ila alianzisha mirija ambayo mashirika ya nje yaliweza na yanaendelea kufaidi uchumi wa Tanzania. kwa nini wasimpongeze? Asifuye mvua...

4. Eneo pekee ambalo namsifia mkapa (na luteni wake Pombe Kali) ni kwenye barabara. Hapo alikuna kipara na kuweka vitu chini. Hapo sina neno, unless nipate data zaidi...

1. Mkapa anaonekana smart kwa sababu mojawapo kwamba Kikwete katika kuonesha nia ya kupambana na rushwa za mkapa, naye katengeneza za kwake kwenye Richmond, kupitia Ngoyai. Hii inaondoa ka authority kokote ambako Kikwete angekuwa nako - No moral high ground there. Kama ulivyosema, kwa kuruhusu machafu yafanyike, na yeye pia kushiriki kuyafanya, ameondoa smartness yoyote ambayo ingeweza kuhusishwa naye

2. Hata hivyo, nguvu aliyo nayo Mkapa katika CCM ni kwamba ni baadhi ya pesa chafu alizozitengeneza ndio zimeiweka CCM madarakani katika uchaguzi uliopita. kaifunga kamba CCM kwamba hawawezi kum-ditch bila kujidhuru wenyewe. lakini hii haina maana kwamba kalifunga kamba taifa. ukifika wakati ikawa too hot kwa CCM, itabidi ihesabu gharama na kum-ditch. ni kama Kikwete alivyolazimika kum-ditch Ngoyai. si kwamba alipenda lakini ilibidi iwe hivyo. haya, chenge huyoo, kaenda zake, pamoja na nyodo zake. ukifika wakati Kikwete aamue ama anaondoka yeye au amshughulikie Mkapa, nadhani choice iko wazi

Nakubaliana na wewe mzee, ndio maana nimesema nam-admire lakini kuna mambo mengi ni debatable, kuuza makampuni ilikuwa idea nzuri, lakini utekelezaji wake ulikuwa mbaya sana. Tatizo tulilonalo ni kuwa, kila kazi inapotaka kufanyika Tanzania, viongozi wetu wanaangalia window of opportunity ya kufanya ufisadi, ndio maana kazi nzima ya ubinafsishaji ilienda na bado inaendelea ovyo!
 
Mzee ES..kula tano kwa nukta hapo juu.Bongolander Huna RABA ya kumsafisha MKAPA. Wabunge sasa wanakuja kuhoji Majumba waliouziana kama Njugu. Hata hizo barabara zote zipo under standard hazijapitiwa tu!!! tunasubiri CAG aje aseme UFISADI wa TANROAD....ila kichwa cha Habari ya Hii mada hakijatulia
 
Ndugu yangu hakuna fisadi anayesafishika, kuwasafisha ni pale watakapoingia kutumikia adhabu kutokana na vitendo vyao. Kwa hiyo Rubber ya kumsafisha huyo ndugu ipo ukonga, let us hope atasafishika.
 
Ina maana Bongo imekuwa ndogo mara hii,ana bahati mbaya Zimbabwe wamekataa kupigana,labda angeenda huko kusuluhisha ugomvi,lakini yaani ameamua kuuchuna pale sea view sio, poa ipo siku ambayo haiko mbali sana.Hawakawii kupandisha BP ili wasiende kwa pilato.BWM ni mmakonde hana kwa kwenda, ni lazima atajibu hoja.

Siku hizi hakai Sea View naishi Lushoto sehemu inaitwa Mkizu Creeks, Mkimtaka nendeni mtamkuta kapiga pensi anakula hali ya hewa nzuri ya Lushoto.

Mwacheni mzee wa watu "ajipumzikie" hehehehe sihasa bwana eti ajipumzikie! hata akifa hatapumzika kaburini huyu! Mungu atamwadhibu kwa kuwataabisha watu wake na kujinufaisha yeye na family yake.

Huo ndio dume la mbegu a.k.a dume la nyani a.k.a nduli, a.k.a genda heka sir bwm
 
Mkuu wangu uko right, na kama ukipitia mara ya pili niliyoandika nimeajiribu kuwa fair kwa Ben kwa mazuri aliyofanya, na nikasema hata hayo ninayoona mazuri ni debatable wengine wanaweza kuyaona mabaya.

Unajua mkuu wangu, mpaka sasa wa-Tanzania wengi hatujui how much damage huyu Makapa, ametuachia as a nation lakini one of this days tutakapokuja kuamka na kuelewa jina lake litafutwa kila mahali lilipo,

kwa sababu mind you kuwa ni huyu jamaa ndiye aliyetuletea mtandao kwenye power, na huyu ndiye hasa chanzo cha ufisadi unajua leo ninapomuangalia Chenge, na hela zote alizonazo nje ambazo sio siri kuwa amezipata under utawala wa makapa, halafu ninamuangalia mstaafu wa idara ambaye pia utajiri wake ameupata under makapa, Yona, Kigoda, Ruhinda, Rostam, Maramba, Lowassa, Karamagi and the list goes on and on and on,

Guys tunasema Mwalimu ametufanyia mazuri as a nation na kuna mapungufu yake pia, sasa I find it very hard kusema the same kuhusu makapa, kwa sababu nikisema the same, ina maana ninamuweka makapa na Mwalimu kwenye level moja, that to me amounts to insanity kama sio insane!

Makapa to me is just a thief, kwa maneno mengine ni mwizi period, there is no any other way around it kuanzia intellectualism, mpaka politicalism the man is just a thug!
 
Vigogo kitanzini (Tanzania Daima)

na Ratifa Baranyikwa na Kulwa Karedia

SASA ni dhahiri kuwa Rais Jakaya Kikwete amedhamiria kuandika historia mpya kwa kuwa rais wa kwanza wa Tanzania kumfikisha mahakamani mtangulizi wake.

Ingawa hatua hiyo inaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa inaweza kuwa na athari mbaya kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na serikali anayoiongoza, inabaki kuwa nguzo yake kuu ya kurejesha imani kwa wananchi wanaotaka kuona akitekeleza ahadi zake kama ambavyo amekuwa akiahidi mara kwa mara.

Tamko la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Alhamisi, Aprili 24, bungeni Dodoma, kuwa inafuatilia taarifa za tuhuma kuhusu matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu, na iwapo ikithibitika kuwa walitenda makosa, watachukuliwa hatua zinazostahili, linaonyesha kuwa sasa Mkapa anaweza kufikishwa mahakamani.

Katika kuonyesha dhamira ya dhati ya serikali yake kuhakikisha inatekeleza matakwa ya wananchi ya kutaka kuwepo uchunguzi kwa viongozi wa juu serikalini wanaotuhumiwa kutumia madaraka yao vibaya, Rais Kikwete jana aliwaambia waandishi wa habari kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, kuwa juhudi za kupambana na vitendo vya rushwa zinaendelezwa bila ajizi.

Rais Jakaya Kikwete, ambaye jana aliongoza mamia ya Watanzania kuadhimisha miaka 44 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, sherehe zilizofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam bila kuwepo kwa mtangulizi wake, Mkapa, aliwaomba wananchi kushirikiana na serikali yake katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa Ikulu, alisema mafanikio ya mapambano yanayoonekana hivi sasa yanategemea zaidi ushirikiano wa wafanyakazi na akawataka kuwa mstari wa mbele katika harakati hizo.

Aidha, aliwataka kuzingatia kujiepusha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa, kwa sababu nao wananung’unikiwa na umma kujihusisha navyo.

Taarifa hiyo ambayo Kikwete anaeleza kuwa hatakuwepo katika maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi, ilieleza kuwa wafanyakazi wakiipiga vita rushwa, vigogo wanaodaiwa kupokea rushwa watapata wakati mgumu wa kufanikisha vitendo vyao viovu.

“Rais amewaomba wafanyakazi wafanye mambo matatu, kwanza, wajiepushe wao wenyewe na vitendo vya rushwa….wakatae kutumika katika vitendo vya rushwa…na wasaidie kutoa taarifa za rushwa ili zifanyiwe kazi na wahusika wabanwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ya Rais Kikwete.

Tamko hili la Rais Kikwete ambaye jana alitangaza kutohudhuria sherehe za Mei Mosi kutokana na kuwa safarini katika nchi za Uganda na Ethiopia, limetafsiriwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa hatua yake ya kwanza ya kuuthibitishia umma wa wafanyakazi kuwa hakuna kiongozi atakayesalimika kama atabainika kuhusishwa na rushwa.

Aidha, walieleza kuwa Rais Kikwete amelazimika kutoa tamko hilo ili kupoza dukuduku la wafanyakazi kuonyesha hasira yao kwa serikali katika maadhimisho hayo, jambo linaloweza kuzidi kujenga taswira mbaya kwa serikali yake.

Pamoja na Mkapa, tamko la Waziri Mkuu Pinda, sambamba na lililotolewa jana na Rais Kikwete, yanonyesha kuwa viongozi wengine waandamizi walio katika hatari ya kufikishwa mahakamani iwapo tuhuma zinazoelekezwa kwao zitathibitika kuwa kweli, ni pamoja na Andrew Chenge na Basil Mramba, ambao walikuwa mihimili na washauri wa karibu wa Mkapa wakati wa utawala wake.

Tayari Chenge ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri hivi karibuni ameanza kuchunguzwa kwa tuhuma za kuhusika na kashfa za rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo Tanzania iliuziwa na Kampuni ya BAE ya nchini Uingereza.

Wachambuzi wameeleza kuwa iwapo Mkapa na Chenge watathibitika kuhusika na makosa ya jinai, basi haitakuwa rahisi kwa Mramba kuachwa pembeni kwa sababu alikuwa mshauri mkuu wa masuala ya fedha wa Mkapa.

Katika hatua nyingine, kutoonekana na ukimya wa sasa wa Mkapa umeanza kuzusha hisia tofauti miongoni mwa jamii.

Mkapa jana pia hakuonekana katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya Muungano huku viongozi wengine wastaafu wakihudhuria sherehe hizo.

Ukiacha Mkapa, viongozi wastatafu waliohudhuria ni Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Haikufahamika hasa sababu za kutohudhuria kwa Mkapa katika sherehe hizo, ikiwa ni mara ya pili kukosekana katika matukio makubwa ya kitaifa na yale yanayokihusu chama chake, ambacho alikuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka kumi.

Mkapa hakuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika Butiama, mkoani Mara mwishoni mwa Machi, mwaka huu.

Wadadisi na wachambuzi waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili walieleza kushangazwa kwao na kutoonekana kwa Mkapa katika matukio hayo makubwa ya kitaifa na kichama na kudai kuwa huenda kunasababishwa na uzito wa tuhuma zinazomkabili.

Baadhi ya tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkapa ni pamoja na kumiliki Kampuni ya kuzalisha umeme ya Tanpower Resources Ltd, ambayo ilishinda zabuni ya kununua mradi wa kuzalisha umeme kutoka mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ulioko Mbeya.

Madai hayo ambayo ni miongoni mwa yale yaliyoelezwa kuchunguzwa na Serikali, yanaelezwa kuwa huenda ni moja kati ya mambo yanayomkosesha raha kiongozi huyo na kumfanya ashindwe kujumuika na viongozi wenzake hata katika masuala muhimu.

Aidha, sherehe hizo za muungano ambazo jana zilifanyika kwa mbwembwe za aina yake, hazikuhudhuriwa pia na viongozi wengine wa vyama vya siasa.

Watu wengine mashuhuri ambao hawakuhudhuria sherehe hizo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Andrew Chenge.

Matukio ya jana yalivuta hisia za wengi katika sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 4:05 asubuhi, baada ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo akiwa katika gari la wazi pamoja na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange.

Wakati akiingia uwanjani, rais aliweza kuvumilia mvua iliyokuwa ikinyesha.

Sherehe hizo pia zilipambwa na mbwembwe za helikopta za jeshi pamoja na ndege za usafirishaji zilizopita uwanjani hapo zikitokea upande wa kaskazini mwa uwanja huo.

Katika kuadhimisha sherehe hizo, Rais Kikwete jana alitoa msamaha kwa wafungwa 3,300.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, kwa vyombo vya habari, ilisema msamaha huo utahusu wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya miaka mitano.

Alisema msamaha huo utawahusu wafungwa wazee na wenye umri zaidi ya miaka 40, lakini hauwagusi wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, waliokamatwa na dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, wanaotumikia kifungo cha maisha, kujamiana na wenye makosa ya kuwapa mimba wanafunzi.
 
Aisee, lakini on one note...hhawa jamaa wamemruka kabisa mzee wetu mkapa, Ule ufisadi ulimsaidia Kikwete aingie madarakani...sasa anamgeuka...yatamrudia huyu rais wetu JK
 
Magazeti haya yana habari kweli ama yanapamba na hasa kwa vile Mkapa hakuwepo kiwanjani ?Maana JK hawezi kuchukua hatua kwa kuanza na Mkapa kuna mengi nyuma hakuwahi kuwa mfano hata mara moja hili ataliweza ?
 
Mkapa yeye kwakweli ameshikwa na butwa, kwani siku zote alijua Watanzania ni mabubu hawajui kusema sasa anashangaa, na bado
 
Back
Top Bottom