Mkapa Appointed as a New Member of International Crisis Group

The Devil you know is better than the Angel you don't know! Kwangu mimi is an Angel I don't know, so namkubali Ben, pamoja na mapungufu yake lakini aliiacha TZ na uchumi wenye muelekeo! Thumb Up Ben!

Mwelekeo gani ambao Mkapa alituachia? Sekta ya Madini yote ilishaenda na maji kwa wazungu, mashirika ambayo yaliuzwa chini ya uongozi wake yote yalienda bure na kurekebisha TANESCO ilikuwa kasheshe. Bado akaona haitoshi akaamua kujipa KIWIRA na kujitengenezea mkataba wa kuzalisha umeme na kuuza TANESCO.

Ukiangalia figures kwenye vitabu utaambiwa uchumi wa Tanzania ulikuwa unakuwa sijui kwa wastani wa asilimia 6 au 7 wakati ya Mkapa, lakini ukijiuliza huo uchumi ulikuwa unasawaidia vipi wananchi wa kawaida? Hupati jibu la kueleweka, sana sana matajiri walizidi kuwa matajiri zaidi na walalahoi wakazidi kuwa hoi zaidi.

Ukichukua definition ya GDP ambayo ndio tunatumia kupima kukua kwa uchumi, wanaangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa ndani ya eneo la nchi bila kujali nani anamiliki. Ukiangalia kwenye sekta ya madini more than 80% ya kilichokuwa kinazalishwa kilikuwa kinaenda nje kwa wawekezaji, na hiyo kidogo ndo inabaki Tanzania kulipa mishahara ya wabongo ambayo ni midogo (hakuna multiplier effect), then mrahaba na bado kodi hawalipi na hata kodi ya mafuta mazito nayo hawalipi.

Ukija kwenye sekta ya utalii ndo balaa, huko wamejaa majambazi waliomilikishwa vitalu vya uwindaji kwa bei poa na hela zote wanazipleka nje. Over 50% ya wamiliki wa vitalu ni foreigners, hakuna kinachobaki. Njoo kwenye mahoteli ya kitalii, watalii wakija walishalipia kila kitu huko huko majuu, wakitua Tanzania wanaishia kununua vinyago vya dollar 20 ambazo hazina manufaa kwa mlalahoi. Hata vyakula vinavyouzwa kwenye hizo hoteli za kitalii vinaagizwa toka nje, tunaambiwa vyakula vyetu haviko kwenye viwango vinavyotakiwa! Matokeo yake sekta ya utalii haimsaidii mwananchi wa kawaida with exception of the employees ambao mishahara yao ni siri yao kwa jinsi ilivyo midogo.

Baada ya hapo unaenda kwenye sekta ya huduma za taasisi za fedha, nao wanachangia kiasi, lakini sehemu kubwa ya mapato wanapeleka kwenye makao makuu yao.

Viwanda angalau unaweza kusema vinatoa ajira, lakini angalia mishahara yake ilivyo midogo, mtu anafanyishwa kazi masaa 10 - 12 kwa siku na bado analipwa mshahara ambao uko less than kima cha chini, hapa ninawaongelea akina Urafiki.

Sekta pekee ya kumsaidia mwananchi wa kawaida ni Kilimo ambayo serikali imeitelekeza na kuwaachia wababaishaji wanaojiita makampuni ya kununua mazao. Pembejeo wanauza kwa bei mbaya, ikifika wakati wa kununua mazao wananunua kwa bei ya chini. Mfano ni kahawa, ukiwa Karagwe bei ni mbaya sana, ukivuka mpaka na kuingia Uganda unakutana na bei nzuri. Jiulize, waganda wanapata wapi soko zuri la Kahawa ambalo wanunuzi wa Tanzania hawawezi kwenda kuuza? Hali iko hivyo kwenye zao la tumbaku na mazao mengineyo. Hii sekta ndo ina ajiri zaidi ya 80% ya wananchi na inachangia pato la taifa kwa wastani wa 50%.

Sasa mkuu Kilembwe niambie huo mwelekeo wa uchumi aliotuachia Mkapa ni upi? Kutuachia EPA? Kutuachia Twin Towers? Kutuibia Kiwira na baadaye akairudisha na nina mashaka atafidiwa wakati haku-invest chochote. Kuuza nyumba za serikali ili Kikwete akija aanze kujenga nyumba nyingine ambayo ni burden nyingine. Mimi nilidhani walipouza nyumba walikuwa wanaachana na habari ya ku-provide nyumba kwa viongozi wa serikali. Last time tumelia hapa kwamba Sitta anakaa kwenye nyumba ya kupanga ambayo ni ya bei mbaya sana. Lakini ndiyo mavuno ya huyo mpendwa wenu Mkapa.

Hali mbaya tunayoiona kwenye hizi zama za Kikwete ni matokeo ya sera mbovu za Mkapa. Kikwete alipoingia aliahidi kubadilisha kila kitu, lakini yako wapi? Kila anapogusa anakuta pamefungwa. Alisema atarudisha nyumba zilizouzwa, ziko wapi? Alisema atapitia mikataba yote ya madini, kiko wapi? Alisema atadai chenji ya Radar, mpaka leo yuko kimya.

Mkapa alifanya damage kubwa sana kiuchumi na ndio maana mkwere amefika mahali anakosa majibu ya ahadi zake za kurekebisha kasoro zote alizokuwa anaziona kwamba zinaweza kurekebishika. Huyu Mkapa ndo unasema aliacha uchumi unamwelekeo? May be ulikuwa na mwelekeo kwa akina Karamagi, Malegesi, Chenge, RA, Patel na wengineo waliotafuna hela za EPA, Radar, Ndege ya Rais, na mikataba ya kifisadi kama TICTS, na kuiuza ATC kwa makaburu.

Hitimisho langu ni hili: Mkapa aliacha Tanzania ikiwa na uchumi wenyewe mwelekeo kwenye makaratasi na vitabu, lakini kwenye hali halisi aliacha damage kubwa na ndiyo maana sasa tunasema hali ni ngumu ni kwa sababu ya madudu aliyoyaacha Mkapa na hasa aliyoyafanya ngwe ya pili ya lala salama. Endeleeni kumsifia na kumpigia debe kwamba alirekebisha uchumi.
 
Ule wa Wajaluo na wakikiyu kule kenya!!
Noo mkuu wangu aliyesimamisha usuluhisho huo alikuwa Kofi Anan, Mkapa na JK walishiriki kama wajumbe tu kama walivyokuwa viongozi wengineo....

Genocide ya Rwanda ilianza mwishoni wa mwaka 1994..Kufikia 1995 Mkapa akiwa madarakani mauaji yalifikia peak na hakufanya kitu zaidi ya kutazama tu.. If he was than good angeweza kuyasimamisha mauaji ya Rwanda hata ikibidi kupeleka majeshi huko kama alivyofanya JK Comoro..Baada ya Rwanda tukaona Burundi na Kongo huyu kichwa chenu akitazama tu...
 
Mkandara

Ndungu yangu usipoteze muda wako kubishana na watu wanaomwona Mkapa ni kichwa. Mkapa ndio sababu leo hii ufisadi umekithiri kila kona ya nchi yetu. Watanzania tunaheshimu sana digrii bila hata ya kuangalia kama hizo degree zimemuwezesha nini mtu kupambana na maisha yake ya kila siku. Kichwa wanachokisifia kilikuwa kinafuata kila kitu kinachoambiwa na nchi za Magharibi kama vile hana akili. Watu walimwambia mikataba ya madini ni mibovu, yeye akawabeza watu kwa kusema Watanzania ni wagumu kufikiri. Sasa matokeo tumeyaona .
 
Mkandara said:
Noo mkuu wangu aliyesimamisha usuluhisho huo alikuwa Kofi Anan, Mkapa na JK walishiriki kama wajumbe tu kama walivyokuwa viongozi wengineo....

Genocide ya Rwanda ilianza mwishoni wa mwaka 1994..Kufikia 1995 Mkapa akiwa madarakani mauaji yalifikia peak na hakufanya kitu zaidi ya kutazama tu.. If he was than good angeweza kuyasimamisha mauaji ya Rwanda hata ikibidi kupeleka majeshi huko kama alivyofanya JK Comoro..Baada ya Rwanda tukaona Burundi na Kongo huyu kichwa chenu akitazama tu...

Mkandara,

..Mkapa alifanya kazi kubwa sana ya kusimamia mazungumzo ya Waganda kule Moshi na kupelekea kuundwa kwa serikali ya muda ya Uganda iliyoongozwa na Prof.Yussuf Kironde Lule.

..Genocide ya Rwanda ilianza April 1994 wakati huo Raisi akiwa Mwinyi, Waziri Mkuu John Malecela, na Waziri wa Mambo ya Nje Ahmed Hassan Diria. Genocide ilidumu kwa siku 100 na baada ya hapo RPF wakachukua madaraka. Ben Mkapa[waziri wa sayansi na teknolojia] wakati huo hakuwa ktk nafasi yoyote ile ya kuweza kuwasuluhisha na kuepusha genocide ile.

..infact, serikali ya Mzee Mwinyi ilifanya juhudi kubwa sana kutatua mgogoro Rwanda, na hata ule wa Burundi, tatizo ni kwamba wenye mgogoro wenyewe hawakuwa na nia ya dhati ya kupatana. mara nyingi walikuwa wanatumia mazungumzo ya amani kama nafasi ya kuvuta pumzi na kujipanga upya.

..ushiriki na mchango wa Mkapa ktk mazungumzo ya amani ulikuwa mkubwa kuliko wa Raisi Kikwete. muda wote wa mazungumzo Mkapa alikuwa bega kwa bega na Koffi Annan. it took a combination of Koffi Annan's international status ang gravitas, and Mkapa's knowledge about the background and "intricacies" of Kenyan politics, kuweza kusuluhisha mgogoro ule. Kenya wameanzisha nafasi ya Waziri Mkuu mwenye mamlaka kama ya Waziri Mkuu wa Tanzania na suala hili tunaweza kabisa ku-speculate kwamba inawezekana lilitokana na mapendekezo ya Mkapa.

..Mkapa ana mapungufu yake ya kimaadili na kiutendaji lakini haya masuala ya kimataifa-taifa ndiyo anayoyaweza haswa. kwa maoni yangu anastahili nafasi aliyoteuliwa.
 
Mwelekeo gani ambao Mkapa alituachia? Sekta ya Madini yote ilishaenda na maji kwa wazungu, mashirika ambayo yaliuzwa chini ya uongozi wake yote yalienda bure na kurekebisha TANESCO ilikuwa kasheshe. Bado akaona haitoshi akaamua kujipa KIWIRA na kujitengenezea mkataba wa kuzalisha umeme na kuuza TANESCO.

Ukiangalia figures kwenye vitabu utaambiwa uchumi wa Tanzania ulikuwa unakuwa sijui kwa wastani wa asilimia 6 au 7 wakati ya Mkapa, lakini ukijiuliza huo uchumi ulikuwa unasawaidia vipi wananchi wa kawaida? Hupati jibu la kueleweka, sana sana matajiri walizidi kuwa matajiri zaidi na walalahoi wakazidi kuwa hoi zaidi.

Ukichukua definition ya GDP ambayo ndio tunatumia kupima kukua kwa uchumi, wanaangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa ndani ya eneo la nchi bila kujali nani anamiliki. Ukiangalia kwenye sekta ya madini more than 80% ya kilichokuwa kinazalishwa kilikuwa kinaenda nje kwa wawekezaji, na hiyo kidogo ndo inabaki Tanzania kulipa mishahara ya wabongo ambayo ni midogo (hakuna multiplier effect), then mrahaba na bado kodi hawalipi na hata kodi ya mafuta mazito nayo hawalipi.

Ukija kwenye sekta ya utalii ndo balaa, huko wamejaa majambazi waliomilikishwa vitalu vya uwindaji kwa bei poa na hela zote wanazipleka nje. Over 50% ya wamiliki wa vitalu ni foreigners, hakuna kinachobaki. Njoo kwenye mahoteli ya kitalii, watalii wakija walishalipia kila kitu huko huko majuu, wakitua Tanzania wanaishia kununua vinyago vya dollar 20 ambazo hazina manufaa kwa mlalahoi. Hata vyakula vinavyouzwa kwenye hizo hoteli za kitalii vinaagizwa toka nje, tunaambiwa vyakula vyetu haviko kwenye viwango vinavyotakiwa! Matokeo yake sekta ya utalii haimsaidii mwananchi wa kawaida with exception of the employees ambao mishahara yao ni siri yao kwa jinsi ilivyo midogo.

Baada ya hapo unaenda kwenye sekta ya huduma za taasisi za fedha, nao wanachangia kiasi, lakini sehemu kubwa ya mapato wanapeleka kwenye makao makuu yao.

Viwanda angalau unaweza kusema vinatoa ajira, lakini angalia mishahara yake ilivyo midogo, mtu anafanyishwa kazi masaa 10 - 12 kwa siku na bado analipwa mshahara ambao uko less than kima cha chini, hapa ninawaongelea akina Urafiki.

Sekta pekee ya kumsaidia mwananchi wa kawaida ni Kilimo ambayo serikali imeitelekeza na kuwaachia wababaishaji wanaojiita makampuni ya kununua mazao. Pembejeo wanauza kwa bei mbaya, ikifika wakati wa kununua mazao wananunua kwa bei ya chini. Mfano ni kahawa, ukiwa Karagwe bei ni mbaya sana, ukivuka mpaka na kuingia Uganda unakutana na bei nzuri. Jiulize, waganda wanapata wapi soko zuri la Kahawa ambalo wanunuzi wa Tanzania hawawezi kwenda kuuza? Hali iko hivyo kwenye zao la tumbaku na mazao mengineyo. Hii sekta ndo ina ajiri zaidi ya 80% ya wananchi na inachangia pato la taifa kwa wastani wa 50%.

Sasa mkuu Kilembwe niambie huo mwelekeo wa uchumi aliotuachia Mkapa ni upi? Kutuachia EPA? Kutuachia Twin Towers? Kutuibia Kiwira na baadaye akairudisha na nina mashaka atafidiwa wakati haku-invest chochote. Kuuza nyumba za serikali ili Kikwete akija aanze kujenga nyumba nyingine ambayo ni burden nyingine. Mimi nilidhani walipouza nyumba walikuwa wanaachana na habari ya ku-provide nyumba kwa viongozi wa serikali. Last time tumelia hapa kwamba Sitta anakaa kwenye nyumba ya kupanga ambayo ni ya bei mbaya sana. Lakini ndiyo mavuno ya huyo mpendwa wenu Mkapa.

Hali mbaya tunayoiona kwenye hizi zama za Kikwete ni matokeo ya sera mbovu za Mkapa. Kikwete alipoingia aliahidi kubadilisha kila kitu, lakini yako wapi? Kila anapogusa anakuta pamefungwa. Alisema atarudisha nyumba zilizouzwa, ziko wapi? Alisema atapitia mikataba yote ya madini, kiko wapi? Alisema atadai chenji ya Radar, mpaka leo yuko kimya.

Mkapa alifanya damage kubwa sana kiuchumi na ndio maana mkwere amefika mahali anakosa majibu ya ahadi zake za kurekebisha kasoro zote alizokuwa anaziona kwamba zinaweza kurekebishika. Huyu Mkapa ndo unasema aliacha uchumi unamwelekeo? May be ulikuwa na mwelekeo kwa akina Karamagi, Malegesi, Chenge, RA, Patel na wengineo waliotafuna hela za EPA, Radar, Ndege ya Rais, na mikataba ya kifisadi kama TICTS, na kuiuza ATC kwa makaburu.

Hitimisho langu ni hili: Mkapa aliacha Tanzania ikiwa na uchumi wenyewe mwelekeo kwenye makaratasi na vitabu, lakini kwenye hali halisi aliacha damage kubwa na ndiyo maana sasa tunasema hali ni ngumu ni kwa sababu ya madudu aliyoyaacha Mkapa na hasa aliyoyafanya ngwe ya pili ya lala salama. Endeleeni kumsifia na kumpigia debe kwamba alirekebisha uchumi.

Ahsante sana Mkuu kwa uchambuzi wako mzuri kuhusu madudu aliyoyafanya Mkapa.
 
Wengi wetu hatufahamiani na Mkapa na familia yake kama Kiranga alivyosema anawafahamu. Lakini hata sisi, at least some of us, ambao hatumfahamu Mkapa tunajua kwamba Mkapa ni kichwa. Si mtupu kichwani kama viongozi wengi tulionao. Na si hivyo tu. Ni wazi kabisa kwamba Mkapa ni intellectual.

Whether you like him or not, there is no question that Mkapa is one of the most intellectual presidents Africa has ever had, along with a few others - Nyerere, Senghor, Nkrumah, Azikiwe, Obote, and Mbeki. He was also one of the most intellectual cabinet members Tanzania has ever had since independence, together with Abdulrahman Babu, Amir Jamal, and Kighoma Malima. Malima also would have been one of the most intellectual presidents in Africa had his quest for the presidency not been thwarted by his detractors, not just by his political opponents.

Unfortunately, intellectuals do not make good politicians with the exception of a few such as Nyerere or Pierre Trudeau of Canada who, coincidentally, was also Nyerere's friend.

Mkapa's weakness as a politician was his lack of charisma and mass appeal or ability to move the masses. Nyerere had that; so did Kawawa who was also one of the best politicians Tanzania and Africa as a whole has ever had. And even in terms of oratorical skills, Kawawa was on the same level with Nyerere.

The difference between the two leaders was that Nyerere was a combination of charisma and intellect. He was also scholarly while Kawawa was not. Also, Kawawa did not have the kind of charisma Nyerere and Kambona had.

But Kawawa was also highly intelligent, yet not intellectual. He was also a brilliant organiser, clearly demonstrated during his leadership before independence as the secretary-general of the Tanganyika Federation of Labour (TFL) when he mobilised forces in support of TANU during a period when some of us were just young boys in those days in the 1950s. So was Oscar Kambona whose organisational skills, combined with his great charisma, made him an excellent secretary-general of TANU. Kambona was also intelligent. But he was not an intellectual like Nyerere and Mkapa.

Not only is Mkapa highly intellectual; he is also highly articulate in both Kiswahili and English like Nyerere. Unfortunately, he is not a politician like Nyerere, Kawawa and Kambona, all of whom had the ability to move the masses.

But there was also a diference between Kambona and Nyerere as well as Kawawa. Kambona did not have the oratorical skills Nyerere and Kawawa had as politicians. But he was one of the most prominent leaders and cabinet members in the history of our country.

My assessment is based on experience, having seen, observed, listened to and lived under these leaders. Haitokani na hadithi za kusimuliwa. Nilikuwepo miaka hiyo tangu enzi ya ukoloni na wakati viongozi hawa walikuwa wanagombea uhuru. Many of you weren't even born when Kambona was one of our national leaders and cabinet member. Au mlikuwa watoto wadogo. Nakumbuka pia kwamba Kambona alikuwa anapenda sana kuvaa suti nyeupe ya kitaifa, lile vazi la taifa miake ile na baada ya hapo, wakati viongozi wengi walikuwa wanavaa suti nyeusi ambazo watu mbali mbali walikuwa wana ziita suti za Kimao au suti za Mao. And there is no question that Kambona was highly charismatic. But he was not a great public speaker like Nyerere and Kawawa. And as minister of foreign affairs, he was not articulate like Mkapa when the latter also served in that capacity.

Mkapa excelled as minister of foreign affairs, a ministerial post that does not require ability to move the masses. He was one of the most articulate foreign affairs ministers together with Malecela and Dr. Salim who also held that post at different times. And he didn't have to worry about appealing to the masses at the grassroots level in that capacity because the domestic arena is not the theatre of this ministerial post (of foreign affairs).

That is why even some of the most insular leaders, aloof and detached from the masses, for example Andrei Gromyko of the former Soviet Union, can serve as excellent minister of foreign affairs. It's said that Gromyko never set foot on the streets of Moscow when he was foreign affairs minister and went straight from his residence to the Kremlin and back in his chauffeur-driven limousine.

In the Tanzanian context, although Kambona had great charisma and mass appeal second only to Nyerere, he did not surpass Mkapa in the execution of his duties and responsibilities as minister of foreign affairs; a ministerial post which could have been handeld very well by other intellectual cabinet members such as Kighoma Malima, Abdulrahman Babu and Amir Jamal, besides Mkapa; and even by other great intellectuals such as Justinian Rweyemamu.

You don't need to have the ability to move the masses to be an effective foreign affairs minister. But you need that kind of ability ukiwa, kwa mfano, waziri wa kilimo au waziri wa elimu au waziri wa wizara zingine, because you deal with the masses at the grassroots level. That is the arena of domestic politics. Mkapa did not need that kind of ability, to move the masses, when he was minister of foreign affairs which is in the realm of international politics and diplomacy.

Mkapa's high standing in the international arena has to do with his intellect and his demonstrated ability as an intellectual leader, not with his charisma and mass appeal, neither of which he has. And he definitely knows what he's talking about just like Nyerere and other leaders such as Babu, Jamal and Malima did.

Simply because you disagree with his ideas or policies, or simply because you believe that he was wrong when he was president, does not mean that he is not an intellectual. And it does not mean that he was right simply because he is an intellectual. Intellectuals are not always right. And they all have their critics as well as admirers. Even some of Nyerere's most ardent critics in different parts of the world including the West who disagreed with his ideas and policies, and who believe he was wrong, acknowledged that he was a great intellectual. And they still do.

Mkapa's intellectual bent and scholarly approach would also have served him well as a professor just like Malima, Babu, Nyerere and Jamal, had the latter two decided to go into academia instead of going into politics. Babu became a professor after he left Tanzania, although he never left politics. Malima was a professor before he entered politics.

And you can see how articulate Mkapa is in international forums. He doesn't even need notes when he speaks. Nor does he need anyone to write speeches for him. Pia hana kugugumizi kinachotokana na kuwa mtupu kichwani.

Mkapa may not have succeeded in mobilising the masses in pursuit of his agenda the way Nyerere did. But he is unquestionably a man of high intellectual calibre who can serve well on the global stage where highly intellectual exchanges are the norm rather than the exception.

Who else? Mbeki, another highly intellectual former president.
 
Noo mkuu wangu aliyesimamisha usuluhisho huo alikuwa Kofi Anan, Mkapa na JK walishiriki kama wajumbe tu kama walivyokuwa viongozi wengineo....

...

Huyu kichaka anachomekwa tu .. Alikaa pembeni alivyoona suluhu inaelekea kupatikana akawahi ceremony ..
 
Acha upumbavu wewe! umetumwa hapa kuja kumpigia debe Mkapa? Tofauti ya Mwalimu na Mkapa, Mwalimu hakuwa mwizi wala mroho wa utajiri. Mkapa kafanya makosa mangapi? Hebu yahesabu kisha utwambie kama kweli aliingia madarakani ili kulinda maslahi ya nchi ama kujitajirisha

Mkuu unatukana badala ya kujibu hoja!!! unaanza sentensi kwa tusi!!
Sasa angalia wewe binafsi ulivyo jaa makosa, utayaona ya wenzio kweli???
Hata unatumia jina la bandia humu lakini nina uhakika 100% kabisa wewe siyo mzima, .......punguza kukurupuka ...kaa chini uwe unatafakari mambo kwa kina ndiyo uongee...
 
Mkandara,

..Mkapa alifanya kazi kubwa sana ya kusimamia mazungumzo ya Waganda kule Moshi na kupelekea kuundwa kwa serikali ya muda ya Uganda iliyoongozwa na Prof.Yussuf Kironde Lule.

..Genocide ya Rwanda ilianza April 1994 wakati huo Raisi akiwa Mwinyi, Waziri Mkuu John Malecela, na Waziri wa Mambo ya Nje Ahmed Hassan Diria. Genocide ilidumu kwa siku 100 na baada ya hapo RPF wakachukua madaraka. Ben Mkapa[waziri wa sayansi na teknolojia] wakati huo hakuwa ktk nafasi yoyote ile ya kuweza kuwasuluhisha na kuepusha genocide ile.

..infact, serikali ya Mzee Mwinyi ilifanya juhudi kubwa sana kutatua mgogoro Rwanda, na hata ule wa Burundi, tatizo ni kwamba wenye mgogoro wenyewe hawakuwa na nia ya dhati ya kupatana. mara nyingi walikuwa wanatumia mazungumzo ya amani kama nafasi ya kuvuta pumzi na kujipanga upya.

..ushiriki na mchango wa Mkapa ktk mazungumzo ya amani ulikuwa mkubwa kuliko wa Raisi Kikwete. muda wote wa mazungumzo Mkapa alikuwa bega kwa bega na Koffi Annan. it took a combination of Koffi Annan's international status ang gravitas, and Mkapa's knowledge about the background and "intricacies" of Kenyan politics, kuweza kusuluhisha mgogoro ule. Kenya wameanzisha nafasi ya Waziri Mkuu mwenye mamlaka kama ya Waziri Mkuu wa Tanzania na suala hili tunaweza kabisa ku-speculate kwamba inawezekana lilitokana na mapendekezo ya Mkapa.

..Mkapa ana mapungufu yake ya kimaadili na kiutendaji lakini haya masuala ya kimataifa-taifa ndiyo anayoyaweza haswa. kwa maoni yangu anastahili nafasi aliyoteuliwa.
Duh! yaani mkuu wangu tunarudia ubishi uleee tulokuwa nao miaka ileeeee..Mkapa hana kitu mkuu wangu Yusuph Lule aliwekwa na Nyerere kama alivyowekwa Bina Issa, Obote na hata Museveni. Kifupi binafsi naamini hata marais wa Rwanda, Burundi na Kongo wote ni wateule wa Mwalimu kama alivyomweka Mkapa mwenyewe madarakani Tanzania.

This mlugalula (Nkapa) couldn't buy his ticket to power hapa Tanzania pasipo Nyerere leo unambie ana uwezo wa kuzungumza? Mkapa alishindwa uchaguzi mkuu wangu alishindwa kabisa kujitetea iwe ndani ya chama au Kitaifa..Mkapa alibebwa sasa ujuzi wake upo ktk kitu gani maanake msuluhishaji bora anajua kuzungumza!

The guy kashindwa kabisa kusuluhisha mgogoro wetu na Zanzibar badala yake kutugawanisha zaidi leo unanambia ni mbora ktk swala hili..Sawa genocide, haya hakuwa rais lakini mwenye uwezo ange fanya mavitu yake, mbona wapo watu wengi tu ambao hawapo madarakani na wamefanya masuluhisho makubwa makubwa pasipo kukabidhiwa mamlaka hayo. Tunachoweza kuzungumzia ni yale aloweza kuyafanya kumpa sifa ama alikuwa na uwezo wa kuyafanya, hakufanya kutompa sifa..

Mkapa was inpower wakati wote wa vita ya Kongo, Rwanda, Burundi, matatizo ya Museveni Uganda na hata maswala madogo ya kisiasa yaliyotokea Malawi, Zambia lakini mkuu wetu alikuwa akifukanya John mtembezi na kutuibia tu.
Ya Kenya mkuu wangu Kofi Anan ndiye kichwa..Mkapa alikuwa ktk panel ya Anan ambayo hata mke wa Mandela alishiriki bega kwa bega ku chair mazungumzo...Hizi habari za nchi kuwa na Waziri mkuu hutokana na mamlaka ya Powersharing na sio kufuata utaratibu wa Tanzania. Ni gonjwa baya sana ambalo linajenga matabaka kwa sababu vyama hivi vya Kenya haviendeshwi na Itikadi isipokuwa UKABILA..Na unapoanzisha power sharing kwa kufuata misingi ya Ukabila, kesho hutaweza kubadilisha kurudisha Demokrasia kwani demokrasia haijengwi na matabaka ya Kabila au dini isipokuwa itikadi za Kisiasa..Ndiyo matokeo ya mgogoro wa Uongozi baina yetu na Zanzibar!..

Tutasema kila lugha kuhalalisha makosa haya lakini ukweli ni kwamba hatusuluhishi jambo isipokuwa tunapoza ukali wa moto kwa kuweka kuni mpya..Kifupi, sisi Tanzania kuwa na rais, makamu wa rais Waziri mkuu wote active serikalini ni mfumo ambao hakuna nchi wanaweza kuuelewa akilini labda ktk ukomunist.

Ya Kenya mkuu wangu ni Valcano iliyolala, hakuna suluhu iisipokuwa tuimepoza kwa kukokea kuni mpya juu ya moto wa Ukabila nchini humo, ipo siku itapamba moto na hakika sidhani kama itawezekana kuamlika, haiwezekani hata siku moja rais na waziri mkuu wakawa kabila moja, au pegine hata kabila nje ya Mkikuyu na Mjaluo..Ni swala la muda tu kama ilivyokuwa usuluhisho wa Rwanda na Burundi miaka yote ya nyuma..Ni swala la muda tu. Link
 
Kama kawaida ya Watanzania na upumbavu wao. Mitanzania ndivyo ilivyo! Mara tu wanampigia debe Mkapa pamoja na makosa yake chungu nzima aliyoyafanya. Mkapa kichwa! angekuwa kichwa angefanya upumbavu alioufanya akiwa Ikulu? Kweli Miafrika ndivyo ilivyo!

mbona huyu aliyepo anaendelea kufanya upumbavu kwani nini kimefanyika....
 
Ule wa Wajaluo na wakikiyu kule kenya!!

Na ule wa wapemba na waunguja kwa kuwatwanga risasi watu 30 na kupandisha vyeo waliowaua rai wasio na hatia, ule wa mwembe chai kwa kutwanga risasi waliokuwa wanatupa mawe n.k.
 
mbona huyu aliyepo anaendelea kufanya upumbavu kwani nini kimefanyika....
Mkuu hakuna mtu anayempima Mkapa kwa kumlinganisha na JK.. Hakuna mashindano baina ya JK na Mkapa, isipokupowa tunapinga sifa anazopewa Mkapa..
Huko nje hatujui wanamfikiria vipi kwa sababu kama nakumbuka vizuri Mkapa pia aliwahi kuchaguliwa ktk panel ya Tonny Blair kuhusiana na Corruption nchi maskini, wasijue kwamba Mkapa alikuwa mtu wa kuchunguzwa yeye mwenyewe.
 
Mkandara,

..Mwalimu alikuwa na influence yake ktk masuala ya Uganda kama Amiri Jeshi Mkuu na wasaidizi wake walikuwa na nafasi zao ktk operesheni ile. kwa kifupi tu Mkapa ndiye aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati ule. sasa huyu jukumu lake lilikuwa ni kuelezea na kutetea msimamo wa Tanzania wakati wa vita ile. yaani yeye alikuwa "askari" ktk medani ya kimataifa.

..baada ya kuanguka kwa serikali ya Amini, ilididi haraka haraka watafutwe Waganda wa kuunda serikali ili isione kama Tanzania inaikalia na kuitawala Uganda kijeshi. Waziri aliyepewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuunda serikali ya Uganda baada ya vita ile alikuwa Benjamin Mkapa. mchakato huo ambao ulifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro, ndiyo uliopelekea kuundwa kwa Uganda National Liberation Front[UNLF] iliyokuwa chini ya Prof.Yusuf Kironde Lule.

..ulidai Benjamin Mkapa hajawahi kusimamia mkataba wowote ule wa amani na ndiyo maana nikakutolea mfano huu. tunaposema hivyo haimaanishi kwamba tunapuuza mchango wa Baba wa Taifa, ila tunaweka bayana roles na michango ya watu mbalimbali ktk vita yetu na Amini. kwa mfano sijui kama unafahamu kwamba Musuguri ndiye alikuwa kamanda wa vikosi vyetu Uganda; au kuna kamanda kwa jina Lt.Col.Ben Msuya ambaye aliongoza vikosi vilivyoingia Kampala, na kusimamia shughuli nzima ya kuapishwa kwa Yusuf Lule etc etc. sasa hao, na wengine wengi, wanaweza kutajwa kwamba wali-play role fulani ktk kumuweka Prof.Yusuf Kironde Lule madarakani.

..kuhusu uwezo wa kujieleza, kuzungumza, au kupangilia hoja, nadhani hilo halina ubishi kwamba ktk Maraisi wetu wa Tanzania, baada ya Nyerere, basi anayemfuatia ni Mkapa. sasa kuwepo kwa Raisi mwenye kipaji hicho haimaanishi kwamba kutakuwa-translated na wananchi kuwa na maisha mazuri.

..kuhusu mgogoro wa Zanzibar, au mgogoro baina ya CCM na CUF, sidhani kama Mkapa was the right person kuushughulikia mgogoro ule. pamoja na kwamba hakuwa chanzo cha mgogoro ule, lakini kama mwenyekiti wa CCM, alikuwa sehemu ya mgogoro. kilichotakikana pale ni kutafutwa msuluhishi toka nje, au kama sasa hivi wenye magomvi yao waamue wenyewe kuweka tofauti zao pembeni.

Hofstede said:
Na ule wa wapemba na waunguja kwa kuwatwanga risasi watu 30 na kupandisha vyeo waliowaua rai wasio na hatia, ule wa mwembe chai kwa kutwanga risasi waliokuwa wanatupa mawe n.k.

Hofstede,

..Mkapa alikuwa safarini nje ya nchi wakati mauaji yanatokea Pemba. Raisi anapokuwa nje, nchi huongozwa na Kaimu Raisi. kwa kipindi kile inawezekana kabisa alikuwa ni Makamu wa Raisi marehemu Dr.Omar Ali Juma.kwa upande mwingine,Raisi wa Zanzibar ndiye mwenye mamlaka juu ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoko Zanzibar.

..si kweli kwamba Mkapa aliwapandisha vyeo askari baada ya mauaji kule Pemba. kama ungesoma habari ile kwa umakini zaidi ungekundua kwamba promotion hizo zilitoka kwenye government gazette muda mrefu kabla hazijadakwa na magazeti ya kawaida. sasa ktk goverment gazette huwa wanaelekeza kabisa kwamba promotion na cheo kipya kitakuwa effective as of when[date,month,year] na ilikuwa bayana kabisa kwamba ilikuwa ni kabla ya mauaji ya Pemba.

..tatizo ninaliona mimi kwa Mkapa ni kwamba hakuwawajibisha waliohusika na mauaji ya Mwembechai au Pemba. hii imekuwa ni tabia kwa karibu Maraisi wetu wote. kuna mauaji yalitokea Kilombero wakati wa Mzee Mwinyi na sikumbuki kusikia kuna askari yeyote aliyewajibishwa.

NB:

..wengi msioridhishwa na uteuzi huu mnakwazwa na rekodi ya ndani ya utawala wa Mkapa. nafasi hii imetolewa kwa kuzingatia ushiriki wa Mkapa ktk mijadala ya kimataifa.

..pamoja na kwamba Mkapa ana kashfa kibao za ufisadi na uhujumu uchumi ndani ya nchi, lakini kwenye majukwaa ya kimataifa huyu Mzee ni kiboko ktk kujenga na kupangilia hoja.
 
mwelekeo gani ambao mkapa alituachia? Sekta ya madini yote ilishaenda na maji kwa wazungu, mashirika ambayo yaliuzwa chini ya uongozi wake yote yalienda bure na kurekebisha tanesco ilikuwa kasheshe. Bado akaona haitoshi akaamua kujipa kiwira na kujitengenezea mkataba wa kuzalisha umeme na kuuza tanesco.

Ukiangalia figures kwenye vitabu utaambiwa uchumi wa tanzania ulikuwa unakuwa sijui kwa wastani wa asilimia 6 au 7 wakati ya mkapa, lakini ukijiuliza huo uchumi ulikuwa unasawaidia vipi wananchi wa kawaida? Hupati jibu la kueleweka, sana sana matajiri walizidi kuwa matajiri zaidi na walalahoi wakazidi kuwa hoi zaidi.

Ukichukua definition ya gdp ambayo ndio tunatumia kupima kukua kwa uchumi, wanaangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa ndani ya eneo la nchi bila kujali nani anamiliki. Ukiangalia kwenye sekta ya madini more than 80% ya kilichokuwa kinazalishwa kilikuwa kinaenda nje kwa wawekezaji, na hiyo kidogo ndo inabaki tanzania kulipa mishahara ya wabongo ambayo ni midogo (hakuna multiplier effect), then mrahaba na bado kodi hawalipi na hata kodi ya mafuta mazito nayo hawalipi.

Ukija kwenye sekta ya utalii ndo balaa, huko wamejaa majambazi waliomilikishwa vitalu vya uwindaji kwa bei poa na hela zote wanazipleka nje. Over 50% ya wamiliki wa vitalu ni foreigners, hakuna kinachobaki. Njoo kwenye mahoteli ya kitalii, watalii wakija walishalipia kila kitu huko huko majuu, wakitua tanzania wanaishia kununua vinyago vya dollar 20 ambazo hazina manufaa kwa mlalahoi. Hata vyakula vinavyouzwa kwenye hizo hoteli za kitalii vinaagizwa toka nje, tunaambiwa vyakula vyetu haviko kwenye viwango vinavyotakiwa! Matokeo yake sekta ya utalii haimsaidii mwananchi wa kawaida with exception of the employees ambao mishahara yao ni siri yao kwa jinsi ilivyo midogo.

Baada ya hapo unaenda kwenye sekta ya huduma za taasisi za fedha, nao wanachangia kiasi, lakini sehemu kubwa ya mapato wanapeleka kwenye makao makuu yao.

Viwanda angalau unaweza kusema vinatoa ajira, lakini angalia mishahara yake ilivyo midogo, mtu anafanyishwa kazi masaa 10 - 12 kwa siku na bado analipwa mshahara ambao uko less than kima cha chini, hapa ninawaongelea akina urafiki.

Sekta pekee ya kumsaidia mwananchi wa kawaida ni kilimo ambayo serikali imeitelekeza na kuwaachia wababaishaji wanaojiita makampuni ya kununua mazao. Pembejeo wanauza kwa bei mbaya, ikifika wakati wa kununua mazao wananunua kwa bei ya chini. Mfano ni kahawa, ukiwa karagwe bei ni mbaya sana, ukivuka mpaka na kuingia uganda unakutana na bei nzuri. Jiulize, waganda wanapata wapi soko zuri la kahawa ambalo wanunuzi wa tanzania hawawezi kwenda kuuza? Hali iko hivyo kwenye zao la tumbaku na mazao mengineyo. Hii sekta ndo ina ajiri zaidi ya 80% ya wananchi na inachangia pato la taifa kwa wastani wa 50%.

Sasa mkuu kilembwe niambie huo mwelekeo wa uchumi aliotuachia mkapa ni upi? Kutuachia epa? Kutuachia twin towers? Kutuibia kiwira na baadaye akairudisha na nina mashaka atafidiwa wakati haku-invest chochote. Kuuza nyumba za serikali ili kikwete akija aanze kujenga nyumba nyingine ambayo ni burden nyingine. Mimi nilidhani walipouza nyumba walikuwa wanaachana na habari ya ku-provide nyumba kwa viongozi wa serikali. Last time tumelia hapa kwamba sitta anakaa kwenye nyumba ya kupanga ambayo ni ya bei mbaya sana. Lakini ndiyo mavuno ya huyo mpendwa wenu mkapa.

Hali mbaya tunayoiona kwenye hizi zama za kikwete ni matokeo ya sera mbovu za mkapa. Kikwete alipoingia aliahidi kubadilisha kila kitu, lakini yako wapi? Kila anapogusa anakuta pamefungwa. Alisema atarudisha nyumba zilizouzwa, ziko wapi? Alisema atapitia mikataba yote ya madini, kiko wapi? Alisema atadai chenji ya radar, mpaka leo yuko kimya.

Mkapa alifanya damage kubwa sana kiuchumi na ndio maana mkwere amefika mahali anakosa majibu ya ahadi zake za kurekebisha kasoro zote alizokuwa anaziona kwamba zinaweza kurekebishika. Huyu mkapa ndo unasema aliacha uchumi unamwelekeo? May be ulikuwa na mwelekeo kwa akina karamagi, malegesi, chenge, ra, patel na wengineo waliotafuna hela za epa, radar, ndege ya rais, na mikataba ya kifisadi kama ticts, na kuiuza atc kwa makaburu.

Hitimisho langu ni hili: Mkapa aliacha tanzania ikiwa na uchumi wenyewe mwelekeo kwenye makaratasi na vitabu, lakini kwenye hali halisi aliacha damage kubwa na ndiyo maana sasa tunasema hali ni ngumu ni kwa sababu ya madudu aliyoyaacha mkapa na hasa aliyoyafanya ngwe ya pili ya lala salama. Endeleeni kumsifia na kumpigia debe kwamba alirekebisha uchumi.

hakuna safari isiyo na hatua, alifahamu uoga wetu, hofu yetu na kutokujiamini kwetu hivyo akaamua kustrategize mambo ili kesho awaachie fursa ya ku argue na hao investors, katika hili anathibitika kuwa yuko mbele kimaono, kama asingelifanya aliyoyafanya ujasiri huu wa akina zito, nyalali na hata tunaowaona watetezi wangetetea milima huko geita? Kiwira alitaka kuonyesha kuwa tukithubutu we can make changes ktk industry hii ya madini bahati njema kwa maadui zake wakafanikiwa kutotimilika njozi zake through kiwira.

Yote alofanya yanabaki kuwa big lessons kwetu na dira ya uongozi usiotawaliwa na uoga kukosa umaarufu.
 
Kiongozi ni yule aliye tayari kufanya maamuzi na kuyasimamiaa..Mkapa hiyoo ni sifa yake ya kwanza..na huo ndio uongozii.

hivii nchii hii tatizoo ni ukosefuu wa watu imaraa kuonyeshaa njia na sio personality..tunashuhudiaa upuuzii mwingii unaofanywaa na mfumo wa uongoziii uliopooo..
 
Back
Top Bottom