Mkapa apanda kizimbani Kisutu

napendekeza katiba mpya waondoe kinga ya rais kutoshtakiwa
Katiba mpya chini ya mkuu wa nchi haitaingizwa kinga ya raisi, hiyo tukate tamaa, kuweka kipengele hicho ni sawa na kumwambia mkulo afanye suicide!!! Tuvumilie CDM tutakapo chukua nchi tutaiandika katiba ya kudumu na kipengele hicho tutakiingiza. Hii katiba ya sasa hivi ni ya viraka tu!!! Katiba gani ambayo hairuhusu kujadili Muungano!!!???
 
Fisadi Mkapa leo alikuwa anafanya Mazoezi ya kukaa Mahakani, muda utakapo wadia lazima tumburuze huyu Fisadi kwenye sheria na ikiwezekana afungwe Maisha mpaka afie huko huko Segerea. Mwizi mkubwa asiyekuwa na huruma na Rasilimali zetu.
 
Wana bodi naona hamtaki kujibu hii ni vyema tukajibu kwani pesa alizofuja Mahalu ni zetu wote(Kodi)

mtu unakuwa huna haki ya kugombea kama huna sifa za kupiga kura nina uhakika ipo kisheria na kikanuni kwa mujibu wa vyama vya siasa.
Hili la Mtu mwenye kinga ya kutoshtakiwa likoje. Kama yeye hashtakiwi ni kipi kinamfanya amtetee mtu mahakamani.
ninajua kuwa unapotoa ushahidi wa uongo mahakamani unaweza kufungwa! Je huyu Rais Mstaafu (kwa Mfano Mkapa leo dhidi ya Mahalu) ambaye ana kinga! akaongea uongo na mahakama ikaproove sheria inasemaje hapo! naomba mnijuze wandugu
 
Apande vyema kizimbani, mda si mrefu atapanda mahakani(kizimbani) mfururizo tu kujibu ufisadi wake
 
Kuna swali halijajibiwa hapa, hayo mambo ambayo Mkapa amesema ni Siri wakati anaulizwa na Wakili, Sheria ya ushahidi inasemaje kuhusu hili, na Mahakama inayachukuaje haya
 
Mkapa:
Kwangu issue ya kodi ya Italy ni yao, sisi tulitaka jengo na tulipata.
Hadi nsataafu hakukua na malalamiko toka Wizara ya nje wala yeyote, na nilienda kufungua jengo, sijaambiwa nisijihusishe na hilo jambo, ila imetokea baada ya mimi kustaafu!

Asingeweza kuona UFISADi wake mwenyewe wakati yeye yupo madarakani mpaka alipostaafu!
 
Mahalu ni rafiki yake mkapa sana,tangu udsm!huenda hili dili wamekula pamoja

Kuna mnyukano kati ya Kiwete na Mkapa, Kikwete anatamani sana Mahalu akanyee ndoo mkapa hataki ufitini wa JK lakini cha ajabu Mkapa hajamshtukia JK kwa ufitini akamtuma aende Alumeru akachafuke lakini Mkapa hakustukia.
 
Ah basi nilivyosoma mkapa kafikishwa kortini nikajua wamemfikisha pale kujibu shutuma zote anazodaiwa kipindi chake cha urais na hela alizozitafuna atasema atazirudishaje kwa wananchi kumbe sio hivyo...ni kuja kutoa ushahidi ooh :confused3: wishful thinking
 
Hivi ni nani alimshitaki Mahalu? Na kwa kosa lipi?

Nauliza maswali haya kwa sababu wanasema kahujumu Uchumi kvipi? maana Ushahidi wake unatuchanganya.. nakumbuka wakati ananunua hizo nyumba JK alikuwa Waziri wake.. Mkapa alikuwa Rais wake...

Wakati ule JK aliwahi kutetea Uamuzi ule akiwa Waziri.. Na Leo hii mkapa anamtetea kama Shahidi kuwa yote yaliyofanyika yalikuwa na Baraka za Serekali sana najiuliza ni nani alimshita Prof Mahalu kwani.

Kama ni uhujumu uchumi basi aliyekuwa Rais wakati huo na Waziri ndiyo wenye hii Kesi unless wanampinga kwa manunuzi aliyofanaya.

Swali langu la pili ni kwamba ni Nani atamlipa Prof Mahalu akifungua Kesi ya Madai baada yaKushinda au ni yale yale ya Zombe?????

CCM bwana..
 
Na kukubali kupigwa na kutembea na gongo miaka 2 kkisa .............
 
I applaud him for standing up to what he believes. He will never throw one of his own under the bus which I believe is his major quality.
 
Mkuu STEIN,

Chuki binafsi za JK ndizo zimepelekea kushitakiwa kwa Prof. Mahalu. Shahidi anayefuata kuitwa Mahakamani nimedokezwa kuwa ni JK mwenyewe (Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje). Kesi hii itatoa somo kwa viongozi wetu kwamba: "kama wamedhulumiana kwenye deals zao wasitumie Dola kukomeshana....wataishia kujiumbua wenyewe...ndo haya yanaelekea kutokea sasa."

Pamoja na Fedheha itakayopatikana, Wananchi wanyonge ndiyo watakamuliwa ili Serikali ipate Fedha za kulipa fidia.
 
dawa yake, ni kuanza maandamano kila mji,....kama akitoka, ili kushinikiza watu halisi wakamatwe kwa uchunguzi....nimeona serikali hii inaogopa sana ukisema 'tutaenda kwa wananchi..ikimaanisha maandamano'wanaona unataka kuleta kama maandamano yakiarabu kumng'oa rais...
 
Back
Top Bottom