Mkapa aomba suluhu kwa Nyerere

tumia neno lolote unaloona linakufaa kuondosha heshima yangu ila tetea hoja! Tatizo lenu mnatumia fimbo kuwachapa wenzenu kwa makosa fulani, fimbo hiyo hiyo ikitumika kuwachapa nyie kwa makosa yale yale, mnaona mwaonewa na maneno meeengi!

acha kulia lia, jibu hoja. Kama huna hoja tulia tuliiiii!
 
Niliishawahi kusema hapa janvini hakuna kiongozi yeyote wa MAGAMBA akaongea kitu cha maana ni ***** mtupu yaani BMW ndio wanamwamini eti ni msafi wakati ni mchafu zaidi ya jalala
 
MUNGU AMEAMUA KUFUNUA YALIYOFUNIKWA. mwenye macho na atazame na mwenye maskio na asikie.
 
tumia neno lolote unaloona linakufaa kuondosha heshima yangu ila tetea hoja! Tatizo lenu mnatumia fimbo kuwachapa wenzenu kwa makosa fulani, fimbo hiyo hiyo ikitumika kuwachapa nyie kwa makosa yale yale, mnaona mwaonewa na maneno meeengi!

Nyerere ni shujaa wangu.Kama ulifurahia kifo chake nakuona wewe ni sawa na Kibwetere
 
Mpendwa Mnyisanzu, nakubaliana na wewe kwa kila ulilosema lakini hapo kwenye red hapana. Anyway that's your opinion! Ila inaonesha chuki ya kupindukia kwa Mkapa ilhali alikuwa Raisi bora kuliko tuliye naye sasa.
Ubora wake haumtoi kwenye kashfa ya kuua watu Zanzibar, Kupiga waislam Mwembe Chai, Kunyang'anya Kiwira, Kuasisi na Kuikamilisha EPA, Kuuza mashirika ya Umma kwa bei chee, Kuuziana wenyewe kwa wenyewe nyumba za serikali na janga kubwa kuliko yote ni kumsaidia rais wa Sasa awe rais wetu. Tungemsamehe yote lakini sio hili la kumfanya Mkwerre awe Rais.
 
Mpendwa Mnyisanzu, nakubaliana na wewe kwa kila ulilosema lakini hapo kwenye red hapana. Anyway that's your opinion! Ila inaonesha chuki ya kupindukia kwa Mkapa ilhali alikuwa Raisi bora kuliko tuliye naye sasa.
mkapa ndo aliyeanza kuiingiza nchi shimoni.
 
cdm cdm cdm!kule ameguswa slaa na mbowe mumekuwa mbogo sana,halfu mnakurupuka tu,kwl watu kama nyie mpewe nchi,dr slaa angekuwa na akil finyu kama zenu leo hii cdm isingekuwa hapo.Jaribuni kujheshmu muwe fair pia
Ninaona unaongea kama usiyehambua vitu usihame mada stay on course!!!!
 
kama NYERERE angekuwepo nchi isingeliwa na wachache kama sasa, we Ben Mkapa kwanini ulimuua mtetezi wetu?
 
kama NYERERE angekuwepo nchi isingeliwa na wachache kama sasa, we Ben Mkapa ulimuua mtetezi wetu ili mtutese watanzania! Dhambi hii itakutafuna milele
 
Usinikasirishe hapa na wewe;

Mkapa akalipwe mara ngapi hapa duniani wewe? Inamaana umesahau lile sakata la kutolewa panya anayehema kwenye goti lake ndipo akapata kutembea tena?

Nakuuliza Mkapa akalipwe hapa duniani mara ngapi wewe; umesahau kwamba pale karibu na Agha Khani Mzee mzima anaishi kisera?

Mbona unatafuta kuniudhi hivi; inamaana umesahau kwamba pamoja na lile tofali la dhahabu toka Kahama, Mzee wa watu bado tu analazimika kuchagua kitu gani ale maana vyakula vingi vimemkataa?

Na huko Butiama akiend shauri yake huko!!!


Yani huyu mkapa ni gamba la kobe full!
Kweli nimekubaliana na maoni ya wadau!

Hana hata aibu mbele ya Watanzania??
Kamwondoa Mkongwe wa Nchi yetu kwa tamaa ya fedha tu?
Ama kweli fedha mwana haramu!

Na bila shaka malipo ni hapa hapa, tusubirie na kumwona yeye ataishije.

Halafu anaomba msamaha!
 
sina tatzo na cdm kubeba nchi ila nina tatizo na nyie wanajf-cdm hamko fair kwnye kujenga hoja!kwa mfano hoja ya ubadhilifu wa pesa za msaada alzotoa sabodo!hakna alyejenga hoja mnakurupuka tu,mara mnalazimisha mod afute thread,hoo lete ushaidi.Mnaharibu chama mna ushahabiki usio na maana,let us be fair in decision making

Thread ya sabodo na mkapa wapinawapi mkuu unataka kupoteza mada kiaina moto kauwasha mwenyewe mwanakijiji alitahazalisha mapema mkapa ni sikio la kufaa yeye kafanikisha kumuuwa nyelele hajuwi yeye atakufa kifo gani mkapa anaanza kujificha kwenye shamba la mahalage anaonekana
 
Mpendwa Mnyisanzu, nakubaliana na wewe kwa kila ulilosema lakini hapo kwenye red hapana. Anyway that's your opinion! Ila inaonesha chuki ya kupindukia kwa Mkapa ilhali alikuwa Raisi bora kuliko tuliye naye sasa.
Je unadhani mazuri yake yanafunika mabaya yake? Na kwanini aligeuka papa na kummeza BABA WA TAIFA?
 
cdm cdm cdm!kule ameguswa slaa na mbowe mumekuwa mbogo sana,halfu mnakurupuka tu,kwl watu kama nyie mpewe nchi,dr slaa angekuwa na akil finyu kama zenu leo hii cdm isingekuwa hapo.Jaribuni kujheshmu muwe fair pia

Wee endelea kujifunika kwenye blanketi la babu yako ukifikiri bado usiku; wenzako tuko nje huku tumeshaamka endelea WE kulaza brain utakapozinduka unaweza ukajikuta unarudi usingizini for good
 
Ajibu Kwanza tuhuma ya KUMUUA Mwalimu Nyerere in cold-blood, na si kuomba mapatano ya kificho!

Nadhani kuna watu wamemshitua kujibu tuhuma hizo maana ni kama ange expose kila kitu na kuufanya umma wa watanzania umuone ni fisadi la kutupwa lisilo na shukrani.
 
MADARAKA Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ameibuka na kuthibitisha kuwa Mbunge wa sasa wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere ni mdogo wao na mwanafamilia hiyo, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, Josephat Kiboko Nyerere.

Kauli ya Madaraka imekuja siku chache baada ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, kudai kwamba hamtambui mbunge huyo kuwa ni miongoni mwa familia ya Mwalimu Nyerere kwani katika kipindi chote alichofanya kazi na Mwalimu, hakusikia jina hilo.

Jumatatu ya wiki, akizindua kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Mkapa aliuambia umati uliohudhuria kwamba hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mtoto wa familia hiyo aliyekuwa akiitwa Vincent Nyerere.

Kauli hiyo ilipingwa vikali juzi na Vincent akisema si jambo la ajabu Mkapa kutomfahamu yeye kwasababu Mkapa si sehemu ya ukoo wao huku akimrushia kombora kwamba akiwa madarakani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa Hospitali ya St Thomas, Uingereza, kinyume na matakwa ya familia yao na wakati huo huo, daktari wake Profesa David Mwakyusa alijua maradhi ya mwasisi huyo wa taifa.

Vincent alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mkapa kwa kuongoza ubinafsishaji holela enzi za utawala wake huku akimtuhumu kuuza viwanda na rasilimali za nchi kwa kisingizio cha ubinafasishaji.

Jana gazeti hili liliwasiliana na Madaraka kutaka kupata ukweli wa kauli hiyo ya Mkapa. Katika jibu lake fupi, Madaraka alithibitisha kuwa Vincent ambaye sasa ni Meneja Mwenza wa Chadema katika kampeni za Arumeru Mashariki, ni mmoja wanafamilia ya Mwalimu Nyerere ambayo chimbuko lao ni Kijiji cha Butiama mkoani Mara.

Katika jibu lake alilolituma kwa barua pepe Madaraka alisema; "Naomba kutoa maelezo yafuatayo kuhusu yanayozungumzwa kwenye kampeni za uchaguzi wa Arumeru; Ili kuepuka kujiingiza kwenye masuala ya kampeni, nitajibu sehemu ndogo sana ya maswali yako".

Aliongeza "Nataka kuthibitisha tu kuwa Mhe. Vincent Nyerere ni ndugu yetu, mtoto wa marehemu baba yetu mdogo, Mzee Josephat Kiboko Nyerere. Hayo maswali mengine naomba yaelekezwe kwa Mhe. Benjamin Mkapa au Mhe.Vincent Nyerere".

Maswali mengine ambayo Madaraka aliulizwa na Mwananchi ni pamoja na kwamba; Nani alishinikiza Mwalimu Nyerere kupelekwa St Thomas, Uingereza na kama familia hiyo iliridhia apelekwe Uingereza au nchi nyingine za Kijamaa.

Madaraka pia aliulizwa anamtambuaje Vincent Nyerere, Ni mmoja wa familia hiyo ama la?

Akizindua kampeni za CCM kwenye uwanja wa michezo wa Ngaresero, Usa River Jumatatu wiki hii, Mkapa alisema:
"Nimefanya kazi na Mwalimu kwa miaka 25, nikiwa mwandishi wake, Waziri na katika muda huo, nimemzika yeye, kaka yake na mama yake mzazi, sijawahi kusikia jina la mtu kama huyo katika familia ya hiyo".

Vicent alimtaka pia Mkapa kuacha kujiingiza katika masuala ya familia yasiyomuhusu na kwamba akiwa Rais mstaafu, ana kashfa nyingi zinazougusa utawala wake wa awamu ya tatu.
 
Vincent Nyerere kama ndivyo hivi basi hii si blow tu kwa Mkapa bali hata kampeni zimekwisha waendea vibaya CCM. NAKUOMA SANA KAMA UTAAMUA KUFANYA SULUHU USIFANYE KABLA YA UCHAGUZI KUMALIZIKA kwa sababu CCM wanaharibu halafu wanataka wakwepe matokeo. Usiwe na haraka kufanya suluhu maliza kwanza kampeni ili ngoma inoge. Tumia dirisha la udhaifu wa Mkapa alioonyesha arumeru mbele ya wapiga kura kuifukia CCM.
 
Back
Top Bottom