Mkapa ana kwa ana na Ulimwengu

Mpitagwa

JF-Expert Member
Feb 10, 2012
2,339
1,119
Ama kweli dunia hii ni ndogo sana, juzi na jana pale chuo kikuu kwenye tamasha la kigoda cha Mwl. Nyerere, wote wawili walihudhuria, kwakuwa na mie nilikuwepo nilisoma macho ya mkapa na kuona anahamu ya kuongea na Ulimwengu. Ikatokea wakagonga na kusalimia kiaina hiyo juzi, Jana Nkrumah pale baada ya Mkapa kuongea, ukafika muda wa wachangiaji akasimama Ulimwengu watu wakajua sasa hapa atawasha moto. Alivyomshule yule jamaa akasoma mawazo ya watu akachangia ile hoja kisomi bila kumgusia Mkapa, na hoja yake ikumkuna sana Mkapa binafsi pamoja na watu wengine na kuendelea kumtesa Mkapa moyoni. Kwani alidhihilisha uelewa wake wa tabia za watu zinavyoathiriwa na madalaka. Ikumbukwe kuwa walikuwa ni vijana wa Nyerere kwa muda mrefu wote wawili lakini Mkapa akiwa madarakani alitangaza kuwa Ulimwengu si raia. Na sasa uamuzi huo wa serikali yake unamtesa sana Mkapa kisaikolojia.
 
mkapa si alisema vicent si mmoja wa familia ya nyerere kwa hio ndio kawaida yake huyu mtu mfupi mla panya
 
Bila nukuu hata moja! mkuu tukisema umepiga porojo usikasirike.
 
Wasomi wetu watu wa ajabu sana. Madudu yote wanayoyaandika na kuyasemea pembeni juzi na jana mbele ya Mkapa wakashindwa kuyasema kwa uwazi. Binafsi nilitarajia mambo kama Kiwira, EPA, Ubinafsishaji wa NBC, uuzwaji wa nyumba za serikali,..., ungetajwa kiaina ili Mkapa ayatolee ufafanuzi. Wakamgwaya mwizi yule!
 
Mkapa alikomaa eti siyo juu yake kama alibinafsisha mashirika ya umma na walio yachukua kushindwa kuyaendesha! Yaani hapo ndo nilijuwa kumbe tulikuwa na mbwiga ikulu kwa miaka 10!
 
wewe ndiye mtu wa ajabu usiyejua kuwa kila jambo lina pahala pake...

kwa vile Mkapa aliacha mada na kuingiza siasa basi watu wengine nao wangetakiwa kuiga upumbavu wake...hatuwezi wote kuwa ni wapumbavu kuiga mifano ya watu wapumbavu.

samahani kama nitakuwa nimetumia lugha kali kidogo.
 
Mkapa alikomaa eti siyo juu yake kama alibinafsisha mashirika ya umma na walio yachukua kushindwa kuyaendesha! Yaani hapo ndo nilijuwa kumbe tulikuwa na mbwiga ikulu kwa miaka 10!

Anko sam wewe mwenyewe unapata jeuri ya kuongea kutokana na BMW kuwa makini kuhusu uchumi wa taifa hili na miundombinu aliyoimarisha. Mbwiga ni wewe ambaye huwezi ukachambua propaganda za magazeti na uhalisia
 
mi nashangaa sana mashirika yalionekana hayafanyi kazi ndo sbb ya kubinafsishwa leo unasema sio jukumu lako kuyaona yakifanya kazi non sense
 
Wasomi wetu watu wa ajabu sana. Madudu yote wanayoyaandika na kuyasemea pembeni juzi na jana mbele ya Mkapa wakashindwa kuyasema kwa uwazi. Binafsi nilitarajia mambo kama Kiwira, EPA, Ubinafsishaji wa NBC, uuzwaji wa nyumba za serikali,..., ungetajwa kiaina ili Mkapa ayatolee ufafanuzi. Wakamgwaya mwizi yule!

Mkuu kazi ya kuwasema mafisadi waziwazi wameachiwa Dr.Slaa na Tundu Lissu, kwa wengine imekuwa ni kama mzigo wa mwizi, wapi Zitto Kabwe
 
Mkapa alikomaa eti siyo juu yake kama alibinafsisha mashirika ya umma na walio yachukua kushindwa kuyaendesha! Yaani hapo ndo nilijuwa kumbe tulikuwa na mbwiga ikulu kwa miaka 10!

Kama aliyabinafsisha mashirika na hayakuwa yakipata ruzuku kutoka hazina, maana yake hayakuwa chini ya serikali, sasa ni kwa jinsi gani Mkapa anaweza kuhahakisha mashirika lazima yajiendeshe chini ya umiliki binafsi? Kwangu mimi naona ingekuwa kama vile anavuka mipaka ya kazi yake. Labda mtoa hoja aniambie kuwa serikali yake ilishindwa kuweka mazingira kwa mashirika haka kujiendesha baada ya kubinafsishwa, lakini hoja kuwa lilikuwa jukumu lake I doubt!!
 
Kwa wale walionunua mashirika ya umma, sharti moja ni kuwa ilikuwa lazima uendeleze kuzalisha bidhaa zili zile zilizokuwa zikizalishwa na kiwanda husika kabla ya kubinafsishwa; mfano mzuri ni Bakressa, yeye alinunua National Milling ambayo ilikuwa inajihusisha na usagaji wa nafaka na yeye anaendeleza usagaji wa nafaka!! Wengi walionunua viwanda wakati wa zoezi la ubinafsishaji hawakidhi sharti hilo kwa mfano :- walionunua Zana za kilimo hawazalishi tena zana hizo, walionunua kiwanda cha kushona viatu hawatengenezi viatu tena, walionunua kiwanda cha kusindika matunda hawasindiki matunda tena na kiwanda kimekuwa godown!! Na kulikuwa na kipengele kwenye makubaliano ya uuzaji kuwa kama masharti yaliyowekwa yangekiukwa viwanda hivyo vingerudishwa serikalini, lakini cha ajabu serikali haitaki kutekeleza wajibu wake huo na ndio maana Mkapa anasema eti sio wajibu wake; pengine kwa vile hayuko madarakani lakini ulikuwa ni wajibu wake alipokuwa madarakani na hakuutimiza na ni wajibu wa serikali kutimiza wajibu huo!!
 
Back to mada,

Kwani Ulimengu kesi yake ya uraia ilishaje?
 
Anko sam wewe mwenyewe unapata jeuri ya kuongea kutokana na BMW kuwa makini kuhusu uchumi wa taifa hili na miundombinu aliyoimarisha. Mbwiga ni wewe ambaye huwezi ukachambua propaganda za magazeti na uhalisia
wewe ndio tindi kwelikweli unathubutu kumtetea nguchiro huyo aliyeuza nyumba za serikali,viwanda. benki. migodi mashamba bado epa ndege ya raisi rada kweli we ndio ngoima hujui unachoögea toka humu jf
 
Mkapa bora aachane na siasa tu, maana Arumeru kwenye kampen alisema wanao hoji suala la ubinafsishaji ni wavivu wa kufikiri, then leo anasema ni tatizo la uongozi... sasa anatudhihirishia jinsi uongozi wake ulivyokuwa dhaifu wakati yeye akiwa kiongozi mwenye dhamana.......basi na ahukumiweee!!
 
walikuwa ni vijana wa Nyerere kwa muda mrefu wote wawili lakini Mkapa akiwa madarakani alitangaza kuwa Ulimwengu si raia. Na sasa uamuzi huo wa serikali yake unamtesa sana Mkapa kisaikolojia.
Wasomali wanakamatwa kila siku kwa kuwepo nchini isivyo halali. Serikali ya Mkapa ilibidi impendelee Ulimwengu na isimtangaze kuwa alikuwa illegal alien kwa vile yeye na Rais "walikuwa ni vijana wa Nyerere"?
 
Back
Top Bottom