Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
Mnhhhh yangu masikio, mkipata taarifa ya muendeleo wa hii kesi mtujuze.
No,he means RA, Riz1, EL, Gabachoris
Kiongozi, unachozungumza ni kitu ambacho kweli kabisa na ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa.
Binafsi hili la kesi ya Mahalu naona kama maluweluwe tu.
Kuna ukakasi katika hili suala, nipingane na wewe kitu kimoja sio sahihi kwamba tunaweza kumuita Jk shujaa kwa hili, vile vile Mkapa!
Kama akweli Jk ni shujaa, kuna masuala mengi sana yanayofilisi nchi pamoja na ufisadi uliokubuu pia utendaji wa "kishkaji" wa utawala ameenda nayo mbali kiasi gani?
Jk kufikia ushujaa katika suala hili, angelifanya kama muendelezo wa kupigania hayo niliyoyasema.
Sasa Prof Mahalu anabeba ujiko wa "kuonewa huruma" sababu inaleta picha ya "Dr Msabaha na kisa cha bangusiro".... kondoo wa kafara.
Haiwezekani katika dimbwi la mfumo ulijivuruga katika ufisadi wa kupindukia mbele ya serikali iliyokoma kusimamia masuala muhimu na matatizo ya msingi ya WATU na ubunifu leo hii tumuone Rais wake ni shujaa kwa kukapeleka mahakamani kaprofessa kamoja kalikokuwa balozi huko nje, Mkuu Mbopo hii ni sawa???
Je mifumo ya balozi zetu ipoje? Tunauhakika hayajatokea kama haya ya Mahalu huko kwingine? Nini kinafanyika? Kuna maslahi ya nani?
Hata Mahalu akifungwa na hata kunyongwa na kupigwa risasi, katika namna yetu ya usimamizi wa mambo kwa ilivyosasa ni kazi bure na bado itaonekana ni uonevu tu.
Kwa ninavyowafahamu JK ( kama Rais wangu wa miaka 6) na Mkapa (kama rais wangu mstaafu) katika utendaji wao, kwa hili kila mtu kati ya hao mabwana wawili anamaslahi yake wala hamna maslahi ya taifa hapo, tusidanganyane.
Huhitaji akili nyingi kujua nani ni mkurupukaji kati yetu. Kama ulifuatilia kesi ile vizuri utajua kwamba kinachofanyika sasa hivi ni kuinyonga haki na dhana ya kwamba wakubwa hawastahili kwenda jela! Kama ungekuwepo pale IFM (mimi nilikuwepo)wakati wa video evidence ambayo Marando aliipinga sana (bila mafanikio) ungejua kwamba nchi hii ilipaswa kugeuka kuwa China kwa muda na kumtia adabu Mahalu. Yule muuzaji wa jengo lile alionyesha kushangazwa na Tanzania kuwa na maofisa ambao wanalazimisha kutengeneza mikataba miwili tean mmoja ambao una-inflate bei ya mauzo na huku Mahalu akikiri wazi kwamba alitaka kujipatia kitu. Na kwa nini ilielekezwa fedha hizo za malipo ziingie kwenye akaunti binafsi ya Mahalu. Fungua macho! Usiingie kwenye mkumbo wa watu ambao wana chuki binafsi na rais na kubeza hata yale ambayo yanafanyika kuwasaidia watanzania. Kwa mwenendo huu hakika kuna haja ya kutangaza wazi kwamba kila aliye na dhamana ya mali au rasilimali za umma sasa ajichukulie tu! Hivi mnadhani Mahalu ni malaika? Ulizeni mtaambiwa. Jiulize kwa nini imechukua miaka hataki kujitetea kama hana hatia na ana utetezi wa nguvu? Hivi tutabadilika lini na kuweka maslahi ya taifa mbele? Kama Kikwete ni mtu wa bifu basi angemwadhibu Prof. Mwandosya. Mbona wanapiga kazi pamoja tena bila matatizo? Acheni kulishwa sumu na huku mnachekelea!
You are better than this! Yaani badala ya nyie kushangazwa na kitendo cha Mkapa kujishushia hadhi yake kwa sababu tu ya urafiki, sasa mnamshutumu Kikwete kwa kufanya kitu ambacho asingefanya mngemlaumu. Sisi wengine tunajua kabisa juhudi ambazo Mkapa alizifanya kuhakikisha kwamba Mahalu hashitakiwi kwa sababu tu ya urafiki wao. Lakini ukweli ni kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani umemuumbua Mahalu na ndiyo Maana Marando na wenzake walihaha sana kukimbia kila mahakama ili Mahalu asijitetee wakati tayayri kuna uamuzi wa kwamba ana kesi ya kujibu.
Hii affidavit ya Mkapa ilikuwa itumike kuombe Nolle Prosequi lakini Mkurugenzi wa Mashitaka alipokataa ndo sasa wakaamua kuitoa hadharani ili kutafuta public sympathy, na huyu Marando akawa anatamba kwamba sasa wanaandika barua ya kuomba Kikwete akatoe ushahidi halafu wai-leak kwenye press na kweli wakafanya hivyo. Hivi mpaka hapo hamuoni kwamba kuna tatizo hapa. Tena wanaofanya hivyo ndiyo wale wanaojifanya kupambana na ufisadi (Marando akiwa Chadema) na huku akifanya mambo ambayo mengine ni kinyume na maadili ya taaluma yake. Nchi hii ni ya ajabu sana. Mtu akiwa mwizi wa mali ya umma watu wanamuona kama shujaa na kumpongeza. Hivi kuna nini cha kupongeza hapa wakati profesa mzima wa sheria anafanya forgery ya wazi na ya kitoto ili kukomba hazina ya nchi? Halafu nyie hao hao mnapigia kelele ufisadi mwingine wakati huu wa Mahalu mnauchekea!

Mimi nafikiri wewe ume-widen scope ya discussion na kwa namna hiyo huwezi kupata sense ya tunachuzungumza. Issue hapa ni whether Mahalu ameonewa au la kwa kumfungulia mashtaka. Kati ya wote waliotoa utetezi kwa Mahalu kwa kutumia hoja yao hiyo hawajaonyesha kwamba (a) kuna bifu kati ya Rais na Mahalu; (b) kwamba wizi huo haujafanyika na wala Mahalu hajahusika; (c) kwamba mashitaka hayo yamchochewa na chuki tu aliyonayo rais dhidi ya Mahalu. Lakini kilichojitokeza hapa ni kwamba eti kwa sababu Mkapa anakwenda kutoa ushahidi mahakamani, basi Mahalu ameshinda kesi na kwamba yeye Mahalu ameonewa.
Huu ni mtazamo finyu na hupati sababu yoyote ya kufikia conclusion hiyo zaidi ya chuki ambayo watu wanayo dhidi ya rais. Mahalu ana kesi ya kujibu and it doesn't matter who he brings as a witness lakini kudhani kwamba ushahidi wa Mkapa ndiyo ukweli wa mambo ni kutokuelewa mambo kwa hali ya juu kwa sababu kama inadhaniwa kwamba Mkapa ni msafi basi wangeangalia jinsi watu wote aliokuwa amewaamini wakati wa utawala wake walivyozalisha makashfa. Muangalie Ballali, Mramba, Yona, Mgonja, Mahalu, Kitine, Kigoda na wengine wengi na yuko tayari kuwatetea wote hao.
Mimi nafikiri tumejikita kudhani kwamba mafisadi ni wale tu waliotajwa Mwembe yanga na Tabora na kwamba wale ambao wanachukuliwa hatua kivingine basi hao si mafisadi bali ni maadui wa JK ambao ana bifu nao. Much as kuna safari ndefu katika kuchukua hatua dhidi ya hao waliotajwa, lakini ukweli ni kwamba hatua hizi zinatia moyo. Kwa mwenendo huu ni wazi kwamba very soon tutaambiwa kwamba hata Yona, Mramba na Mgonja tutaambiwa wanaonewa. This is unfair to the war against corruption.