Mkapa akingiwa kifua na Sekretarieti ya Maadili

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imemkingia kifua Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, kuwa alitaja mali zake wakati akitoka madarakani.

Kwa mujibu wa sekretarieti hiyo, Mkapa ambaye alikuwa Rais kati ya mwaka 1995 hadi 2005, aliwasilisha tamko la mali zake baada ya kumaliza awamu yake ya uongozi.

Sekretarieti hiyo ilisema Mkapa alifanya hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 9(1) D cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995. Tamko la sekretarieti hiyo linafuatia taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kuwa Mkapa alitangaza mali zake wakati anaingia madarakani mwaka 1995 lakini alipoondoka mwaka 2005 hakufanya hivyo.

“Sekretarieti inakanusha taarifa kwamba Mkapa hakutangaza mali zake, ni uongo na huenda imetolewa kwa nia mbaya,” ilisema sehemu ya taarifa ya sekretarieti hiyo.

Hata hivyo, sekretarieti hiyo imeshindwa kuweka wazi iwapo ilienda kuhakiki mali za Mkapa ili kujiridhisha kuwa kile alichojaza kwenye fomu kinalingana na hali halisi ya mali zake.

“Sheria inasema sekretarieti itahakiki mali za kiongozi wa umma lakini hairuhusu kutangaza mtu anayeenda kuhakikiwa mali zake, mfano hatuwezi kusema leo tunaenda kuhakiki mali za mtu fulani…Vile vile hatuwezi kusema kuwa tulihakiki mali za Mkapa au la,” alisema Mataula.


CHANZO: NIPASHE
 
Yaleyaleee..
Lakini ni kipi kipya?? System iliopo inatengeza, kulea na kukingia kifua waizi na mafisadi. So this was expected.
 
Kabla ya kuwahukumu nenda pale tume kajipatie taarifa hizo ili hata sisi tuweze kufanya milinganyo na si kulalama na kubeza.
 
NI jambo la busara kwa Tume ya maadili kuwaalifu wananchi kuwa tofauti na vyombo vya habari kuandika kuwa Rais mtaaafu Mkapa hakutangaza mali zake alipostaafu, ukweli ni kwamba aliorodhesha mali zake kwa mujibu wa sheria! Sasa wale wanaotaka kujua ni mali gani ambazo Rais mtaafu aliorodhesha wana nafasi kwa mujibu wa taratibu kuweza kujua ni mali kiasi gani Rais wetu aliweza kulimbikiza akiwa madarakani.!
 
Kwa kuwa alikuwa Rais wa nchi yetu na ni sisi wananchi tuliompa mandate ya kutuongoza tunadai itangazwe hadharani mali alizokuwanazo wakati akiingia Ikulu kuwa Rais na mali alizokuwanazo wakati akitoka Ikulu baada ya kumaliza muda wake. Sekretariat ya Maadlili iwatangazie wananchi kuhusu hilo. Hata kama sheria haisemi hivyo wananchi wanapaswa kujulishwa ili utata huu uliojitokeza uweze kupata majibu na Mkapa astarehe kwa amani!
 
Back
Top Bottom